T.I.D Kuingia Kwenye Siasa Mwaka 2020

Msanii mkongwe wa bongo fleva nchini  Mohamed Khalid mwenye jina la umaarufu kama T.I.D amefunguka na kusema kuwa kwa sasa anafikiria kuingia katika siasa na mwaka ujao wa uchaguzi anampango wa kugombea ubunge.

Msanii huyo amesema kuwa mwaka 2020 anampango wa kugombea ubunge katika jimbo la Kinondoni, jimbo ambalo kwa sasa linaongozwa na Maulid Mtulia.Hata hivyo  akiongelea sababu za yeye kutaka kugombea ubunge msanii huyo alisema kuwa kitu cha kwanza ni kwamba yeye ni mzawa wa jimbo hilo la Kinondoni hivyo amekuwa akijua matatizo yanayotokea na yanayoendelea kutokea jimboni hapo.

download latest music    

Hata hivyo T.I.D anasema kuwa msukumo mkubwa wa yeye kugombea ni kwa sababu anaona kabisa kuwa mbunge aliepo sasa hajaweza kutimiza na kutatua matatizo ya wananchi,T.I.D  anasema kuwa atakapogombea na akashinda  anaamini kabisa kuwa atatimiza na kutatua matatizo ya wananchi wa jimbo ilo.

T.I.D alipokuwa akiongea na chombo kimoja cha habari alisema kuwa moja ya tatizo linalomfanya awe na hamsa ya kugombea ubunge ni tatizo la vijana kujiingiza katika madawa ya kulevya, tatizo analoliona kuwa ni sugu na anatamani kuliondoa.Msanii huyo ambae pia  kwa muda mrefu alikuwa kimya katika muziki kwa sababu ya matumizi ya madawa ya kulevya alikuja  kuachana nayo   baada ya kukubali kupata msaada kutoka kwa mkuu wa mkoa wa Dar Es Salaam aliyeanzisha vita ya kutokomeza madawa ya kulevya, hivyo kwa msanii kama yeye ambae alipitia huko na akatoka na  anaona vijana wengine wanavyoendelea kuharibika ni dhahiri kuwa anaumia na ana nia ya kusaidia wengine.

Wasanii wengi sasa wamekuwa wakijitokeza kujiingiza katika siasa na wamefanya vizuri katika swala hilo, wasanii kama Joseph Mbilinyi mbunge wa Mbeya Mjini na Joseph Haule mbunge wa Mikumi wamekuwa chachu na amasa kwa vijana hasa wasanii ambao pamoja na kuwa katika tasnia ya muziki lakini pia wanaweza kufanya vizuri katika siasa. Hivi karibuni , msanii Nikki wa Pili kutoka kundi la Weusi pia alisikika akitangaza kuhusu nia yake ya kugombea ubunge kwa mwaka ujao wa uchaguzi, hii inaonyesha ni jinsi gani vijana wamekuwa na chachu ya maendeleo

 

About this writer:

Expedicto Lilian

#Godseeker, I am what i ought to be and always i will be, but am not what i used to be.