Tafadhali Kuwa na Subira, Ben Pol Amsihi Ebitoke

Mwanamuziki wa Bongo fleva Ben Pol amefunguka na kumsihi mchekeshaji Ebitoke awe na subira.

Mchekeshaji Ebitoke alikuwa wa kwanza kutangaza na kuweka wazi hisia zake juu ya Ben Pol lakini tangu hapo mengi yamekuwa yakitokea baina yao kwani wamekuwa wakipigana chenga na kila mtu kusema lake mara Ben Pol alilipwa kupiga picha na Ebitoke! Mara ooh wanatafuta kiki! Ilimradi tafrani.

download latest music    

Kwenye mahojiano aliyofanya na kituo cha televisheni cha East Africa kupitia kipindi cha Planet Bongo, Ben pol  ameweka wazi kuwa mpenzi wake huyo anaelewa mazingira ya kazi zake kama msanii hivyo hana budi kuvuta subira.

Mimi naamini anaelewa saa nyingine uko safarini hakuna mtandao, nafikiri tuwe na subira halafu vitu vingine vingi vitapata ufumbuzi wa kila kitu, unajua kila mtu ana mapungufu yake, unaweza ukakosea sehemu baadae mkaelewana mkaja kusahau”.

Hivi karibuni Ebitoke alisikika akilalamika kuwa ghafla msanii name mpenzi wake huyo amekuwa hapokei simu zake wala hajibu meseji zake, na kuomba watu wansaidie kumuuliza Ben Pol amekumbwa na mini mpaka kufikia hatua hiyo.

Ben Pol ambaye kwa sasa anatamba na ngoma yake ya ‘kidume’ inayofanya vizuri kwenye stesheni mbalimbali amesema yuko bize na tamasha la fiesta analofanya vizuri

About this writer:

Diana

I am a hard working young woman Aspiring writer with dreams larger than life itself, always living by the principle that live today like there is no tomorrow.