Rammy Galis Kumuingiza Mtoto Wa Masogange Kwenye Bongo Movie

Muigizaji wa Bongo movie nchini Rammy Galis ametangaza kumuingiza kwenye filamu Mtoto wa Marehemu Agness Masogange ajulikanaye Kama Sania.

Rammy alifunguka hayo alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari siku chache zilizopita jijini Dar es Salaam kuhusiana na uzinduzi wa filamu yake mpya aliyocheza na marehemu Agness Masogange, amesema kuwa amemshirikisha mtoto huyo kufatia kipaji kikubwa alichokiona ndani yake.

Nina mpango wa kumuingiza katika soko la filamu kwasababu mtoto wa Agness anakipaji kikubwa sana cha kuigiza na nitakua nae mwanzo hadi mwisho maana hata baba yake amekubaliana na suala hilo la mwanae kuingia kwenye sanaa”.

Lakini pia kupitia ukurasa wake wa Instagram, Rammy pia ameweka wazi kuwa Mtoto wa Masogange ndio ameomba kuingia kwenye filamu Kama mama yake:

Rammy ameweka wazi kuwa  filamu hiyo inayotarajiwa kuzinduliwa Desemba 15, mwaka huu katika ukumbi wa Citymall jijini Dar es Salaam itakwenda kwa jina la Hukumu ambayo aliamua kumshirikisha Masogange lengo likiwa ni kuhakikisha anamuhamishia katika upande wa uigizaji moja kwa moja.

Rammy Galis Kuzindua Filamu Yake na Marehemu Masogange

Muigizaji wa Bongo movie Rammy Galis amefunguka kuhusu uzinduzi wa Movie yake mpya aliyomshirikisha marehemu Agnes Masogange ambayo anatarajia kuizindua December 15, 2018.

Rammy Galis amefunguka na kuweka wazi kuwa moja ya jambo alilolitaja kwenye movie hiyo ni Marehemu Agnes Masogange kuigiza kuhusu madawa ya kulevya.

Kwenye mahojiano aliyofanya na waandishi wa Habari Rammy amefunguka haya kuhusu filamu hiyo:

Niliamua kumshirikisha Masogange kwenye filamu hii ya hukumu lengo langu likiwa ni kumuona anafanya kazi zake katika mpangilio nilimuona ameanza kupotea katika upande wa video queen hivyo nikaamua nimuhamishie kwenye sanaa ya filamu maana niliamini anaweza na alifanya vizuri”.

Rammy amesema filamu hiyo inayotarajiwa kuzinduliwa Desemba 15, mwaka huu katika ukumbi wa Citymall jijini Dar es Salaam itakwenda kwa jina la Hukumu,ambapo amefunguka kuwa aliamua kumshirikisha Masogange lengo likiwa ni kuhakikisha anamuhamishia katika upande wa uigizaji moja kwa moja.

 

 

Mtoto wa Masogange Atusua.

Mtoto wa marehemuAgness Masogange ametyusua mtihani wa darasa la saba na kuwapa walzi matumaini ya kuendelea na kidato cha kwanza.

Mtoto huyo ambae hapo awali alikuwa akisoma shule ya serikali aliktaaa kuhamishwa kwenda shule ya binafsi baada ya mama yakekufariki ikiwa ni moaja ya wazo la waliokuwa wakitaka kumsomesha.

Hata hivyo ikimbukwe kuwa kipindi cha msiba wa mama wa mtoto huyo walijitokeza wat wengi wakitaka kumsomesha mtoto huyo ikiwa kama moja ya kutaka kulipa fadhilia kwa marehemu kutokana na kuwa alikuwa akipenda na kufahamika sana na watu kupitia kazi zake.

Sonia ambae kwa sasa amekuwa akilelewa na baba yake mzazi anategemewa kuendeleavizuri na masomo yake ikiwa dalili za awali zinaonyesh kuwa ni mtoto mwenye kupenda kusoma na kuleta mafanikio.

 

Agnes Masogange: Sitaki Kujichanganya na Watu

Videi vixen maarufu Agnes Gerald maarufu kama Masogange amefunguka na kuweka wazi kuwa hivi sasa hataki kabisa masuala ya shobo na watu baada ya kesi yake badala yake anataka kuwa kivyake.

Wiki iliyopita Masogange aliponea chupu chupu kwenda jela baada ya kuhukumiwa miaka miwili au kulipa faini ya shilingi milioni 1.5 ambayo alifanikiwa kuilipa na kuepuka jela.

Kwenye mahojiano aliyofanya na Ijumaa Wikienda, Masogange alisema kuwa, kwa sasa anataka aishi maisha yake ya kawaida na wala hataki kujihusisha na mambo ya kwenye mitandao ya kijamii kama ilivyokuwa mwanzo maana anaona hayo ndiyo yaliyomu-ingiza kwenye misukosuko.

Sasa hivi nataka kuishi maisha yangu ya kawaida kabisa, sitaki tena kujihusisha na mambo ya mitandao, nataka maisha yangu yawe ya kawaida kabisa“.

Agnes alikamatwa mwaka jana Kwa Tuhuma za kujihusisha na matumizi ya madawa ya kulevya na mkemia mkuu wa serikali alithibitisha hayo baada ya kumpima.

Masogange Alikwepa Gereza,.

Mwanadada Agness Masogange amelikimbia gereza baada ya kesi yake ambayo hukumu yake ilitolea siku ya tarehe o3 March mwaka huu kumtaka kutumikia kifungo cha miaka miwili jela baadaya kukutwa nahatia ya kutumia madawa ya kulevya au kutoa faini ya shiling milion 1.5 kama faini ya hukumu hiyo.

Hata hivyo, faini hiyo ambayo ilitakiwa kutolewa mara baada ya hukumu la sivyo agnes alitakiwa kusekwa gerezani ilipatukana na kutolewa papo kwa papo na kumfanya Agnes kuwa huru na kutolewa .

Agness amekuwa akifatilia kesi hiyo kwa kipindi cha mwaka sasa baada ya kukumbwa na sakata la utumiaji wa madawa ya kulevya , kampeni ambayo iliendeshwa  na mkuu wa mkoa wa Dar Es Salaam na wasanii wengi walikumbwa na mkasa huo.

Agnes Masogange Ahukumiwa Kwenda Jela Kwa Miaka 2

Muigizaji wa Bongo movie Agnes Gerald maarufu kama Masogange amekutwa na hatia na mahakama ya hakimu mkazi Kisutu na kuhukumiwa miaka miwili jela au kulipa faini ya shilingi milioni 1.5.

Agnes alifunguliwa kesi na Jamhuri mapema mwaka Jana baada ya kukamatwa nna kutumia madawa ya kulevya aina ya Heroin na ya pili ni kutumia madawa ya kulevya aina ya Oxazepam.

Hakimu wa mahakama ya hakimu mkazi Kisutu, Wilbard Mashauri ametoa hukumu hiyi Leo na kuieleza mahakama kuwa amekutwa na hatia katika makosa yote mawili.

Hivyo katika kosa la kwanza mahakama inamuhuqkumu kwenda jela kwa miaka miwili au kulipa faini ya shilingi milioni moja na kosa la pili amehukumiwa kwenda jela miezi kumi na mbili au kulipa faini ya shilingi laki tano”.

February 17 mwaka Jana Masogange alitiwa hatiani kwa tuhuma za kutumia madawa ya kulevya ambapo alienda kupimwa na mkemia mkuu Wa serikali.

Kesi ya Agnes Masogange Kusogezwa Mbele Tena

Kesi ya mwanamitindo na video vixen wa muda mrefu , Agness Masogange imesogezwa mbele tena baada ya wakili wake kuomba kuhairishwa kwa kesi kwa sababu  mwanadada huyo ni mgonjwa na amelazwa katika hospitali moja jijini Dar.

Agnes ambae amekuwa akifatilia kesi yake kwa muda mrefu sasa baada ya kuingizwa katika list ya watu maarufu nchini ambao walisadikika kutumia madawa ya kulevya.Kesi hiyo ambayo i ekuwa ikisikilizwa na kupangiwa tarehe mpya kila siku.

Hata hivyo kesi hiyo imepangwa kusikilizwa tena mwezi ujao (april 4) na kuangalia ili kujua hatma yake.

 

Agnes Masogange Awapa Kichambo Marafiki Zake Wanafki

Muuza nyago kwenye video au kwa lugha kimjini video queen maarufu Agnes Masogange aliyepata jina baada ya kutokea kwenye video ya msanii Belle 9 inayoitwa Masogange miaka michache nyuma lakini pia amepata umaarufu kutokana na umbo lake la kuvutia.

Kwa miaka kadhaa sasa mrembo huyu amekuwa akiandamwa na kashfa na hata kesi za kujihusisha kwa njia moja ama nyingine na uuzaji au matumizi ya madawa ya kulevya. Kama utakumbuka kipindi cha nyuma alipokuwa anaishi nchini South Africa alishakamatwa na madawa ya kulevya lakini aliachiwa hapo baadae.

Lakini hakuishia hapo kwani mwaka jana alijikuta tena kwenye mkumbo huo huo pale ambapo mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam alipopitisha msako wake wa wasanii wanaoutumia kuuza au kubeba madawa ya kulevya ambapo baada ya kukamatwa alifunguliwa kesi yake mahakamani.

Tangu kesi yake ianze kusikilizwa mwaka jana mara kwa mara Agnes amekuwa akiuambia umma ni jinsi gani alivyopoteza watu aliodhani ni marafiki zake ambao walimkimbia badala ya kumpa sapoti. Siku ya jana kupitia ukurasa wake wa Instagram Masogange aliwatolea povu zito wale wote alidai wanamfanyia unafki ambapo aliandika:

Pata tatizo ujue rafiki wa ukweli ujue ndugu wa ukweli uwajue hawa tunaowaita dada zetu wa mjini yaani tena watajifanya wako busy na mambo yao lakini ni wepesi kusahau utasikia wanakwambia pliz saidia kushare pliz i beg! yaani usumbufu sitaki mnajijua wanafki wakubwa nyie msione nacheka na nyie nawachora tu”.

Haikujulikana moja kwa moja maneno hayo alimlenga mtu gani lakini Agnes alikiri tangu apate kesi yake ya madawa ya kulevya ambayo bado inaendelea kisikilizwa watu wengi aliodhani ni marafiki zake walimtenga.

Agnes Masogange Aulaani Mwaka 2017

Mrembo na video vixen anayetikisa hapa bongo kwa umbo lake matata Agnes Gerlad aliye maarufu kama Agnes Masogange amefunguka na kuulani mwaka huu wa 2017 kwa mambo yote yaliyomkuta.

Agnes  amefunguka na kudai kiwa anauchukia sana mwaka 2017 kutokana na mambo magumu yaliyompata  akiri kuusubiri kwa hamu mwaka 2018. Agnes Masogange ambaye amjipatia umaarufu baada ya kutokea kwenye video ya wimbo wa Belle 9 ‘masogange’ miaka michache iliyopita amekiri kuwa mwaka huu ulikuwa mgumu sana kwake hadi kupelekea kuuchukia.

Mapema mwaka huu Agnes akiungana na wasanii wenzake mbali mbali kama Wema Sepetu, Rommy Jones, Petit Man Wakuache walikamatwa  na kifikishwa kituo cha polisi baada ya kituhumiwa kwa kujihusisha na matumizi ya madawa ya kulevya.

Ingawa baada ya tuhuma hizo na kukaa rumande kwa siku chache na uchunguzi kufanyika wengi wao waliachiwa huru lakini Masogange alikuwa mmoja wa watuhumiwa waliofunguliwa mashtaka mahakamani na hivyo kupelekea Agnes kuwa  na kipindi kigumu.

Kwenye mahojiano aliyofanya na Ijumaa Wikienda, Agnes Masogange amekiri kuwa tuhuma hizo zimemfanya mambo yake yamesimama pia amedai biashara zake nyingi zimesimama kwa mwaka huu kutokana na kukosa muda wa kwenda kufatilia kutokana na kuhitajika mahakamani mara kwa mara.

Bora mwaka 2017 uishe na mambo mengine yaendelee  ulikuwa ni mwaka mgumu sana kwangu kwa kila kitu hasa kwa sababu ya kesi inayonikabili ya matumizi ya madawa ya kulevya labda mwaka mpya ukianza na mambo mengine yataenda vizuri”.

 

Agnes Masogange apewa onyo na Hakimu Mkuu baada ya kuchelewa kuwasili Mahakamani wakati unaotakiwa

Agnes Masogange ni mmoja wa Video vixen ambao wanajulikana sana Afrika Mashariki. Ameweza kufeature katika video kadhaa nchini Tanzania lakini hivi sasa yuko matatani na Mahakama baada ya kudaiwa kuwa mmoja wa watu maarafu anayetumia madawa ya kulevya.

Mwezi Februari aliweza kufikishwa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu ambapo aliposomewa mashitaka yake kwa mara ya kwanza na kama wengi alikana na mahakama ikabidi kuhairisha kesi yake hadi, March 21, ili kuwapa polisi mda wa kutosha kufanya upelelezi wao.

Video vixen huyu anakabiliwa na mashitaka ya kutumia dawa za kulevya aina ya Heroin na Oxazepam.

Hata hivyo Jumanne hii mrembo huyu hakuwa mahakamani kuskiza kesi yake baada ya kuchelewa na Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, ilibidi kutaja kesi hiyo ingawa hakuwa.

Wakili wa Masogange, Nictogen Itege, aliweza kumtetea Masogange huku akisema kuwa yuko njiani. Masogange alipowasili Hakimu Mashauri alimtaka mshitakiwa kutii sheria anazopewa na Mahakama huku kesi yake ikihairishwa hadi Aprili 20, mwaka huu kwa kutajwa.