Hatimaye Ali Choki Arejea Stejini Baada Ya Kupona

Msanii mkongwe wa muziki wa Dansi nchini Ally Choki ametangaza kurudi mazoezini Baada ya Kuugua kwa miezi kadhaa.

Ali Choki ameanza mazoezi ya muziki katika bendi anayoifanyia kazi ya Super Kamanyola iliyopo jijini Mwanza.

Kwenye mazungumzo aliyofanya na gazeti la Ijumaa Wikienda, Ali Choki alisema alianza mazoezi rasmi wiki iliyopita ikiwa ni baada ya madaktari wake kumweleza kuwa kwa sasa amepona kwa asilimia 80 hivyo anamshukuru Mungu na Watanzania waliokuwa wakimwombea wakati akiwa hoi.

Tayari nimeshaanza rasmi mazoezi ya muziki ila kupanda jukwaani bado maana ninakula kwanza ugali wa kisukuma na sato nipate nguvu za kutosha na mwisho wa mwezi huu mambo yakiwa mazuri ndiyo nitaanza kupanda stejini kuwaburudisha mashabiki wangu“.

Ali Choki alikuwa akisumbuliwa na maradhi ya presha na maradhi mengine yaliyopelekea kupumzika kufanya muziki kwa muda.

Ali Choki- Afya Yangu Inazidi Kuwa Njema Zaidi

Msanii mkongwe wa muziki wa dansi nchini kutokea katika bendi Ali Choki amefunguka na kuweka wazi kuwa hivi sasa afya yake inazidi kuimarika zaidi tofauti na siku chache zilizopita.

Siku chache tu zilizopita Ali Choki alikuwa Alikuwa akisumbuliwa na ugonjwa wa kisukari, mapafu na presha hali iliyopelekea kulazwa hospitali.

Lakini Kwenye mahojiano yake na Risasi Vibes, Choki alisema kwa sasa anaendelea vizuri tofauti na ilivyokuwa mwanzo hivyo Mungu akipenda mwishoni mwa mwezi huu ataendelea na kazi ya muziki katika bendi anayoitumikia kwa sasa ya Super Kamanyola jijini Mwanza.

Nina furaha kwani kwa sasa naendelea vizuri, hali yangu inaimarika kila siku, Mungu akipenda mwishoni mwa mwezi huu nitapanda jukwaani kama kawaida kwa ajili ya kuwapagawisha mashabiki wangu“.