“Amber Lulu Ananiendea Kwa Waganga Kuniloga”- Amber Rutty

Msanii wa Bongo fleva aliyejizolea umaarufu kwa video yake chafu ya ngono kwenye Mitandao ya kijamii Amber Rutty ameibuka na kudai kuwa msanii mwenzake Amber Lulu anamuendea kwa waganga.

Amber Rutty na Amber Lulu wamekuwa hawana maelewano kwa muda mrefu ambapo kisa kilikuwa Amber Lulu aliona kama Amber Rutty anamuiga swaga zake kuanzia kumuiga jina na hata kumuiga tattoo zake alizochora mwilini.

Kwenye mahojiano aliyofanya na kituo kimoja cha habari, Amber Rutty amemtolea povu zito Amber Lulu na kudai amamuendea kwa waganga wa kienyeji kwa majaribio ya kutaka kumloga.

Amber Lulu amedai kuwa hawezi kumpenda Lulu kwa sababu kwa muda mrefu amekuwa akijaribu kumshusha na kumharibia jina lake Lakini Baada ya kushindwa kwa njia hiyo sasa Hivi ameanza kumuendea kwa waganga wa kienyeji kwa lengo la kumloga asifanikiwe.

 

Upelelezi Wa Kesi Ya Amber Rutty na Mume Wake Wakamilika

Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, jijini Dar es Salaam imeambiwa kwamba upelelezi wa kesi inayomkabili Msanii wa video za wasanii, Rutyfiya Abubakary Amber Ruty umekamilika na wenzake wawili dhidi ya mashtaka mawili la kufanya mapenzi kinyume na maumbile.

Aidha kesi hiyo itaanza kusikilizwa maelezo ya awali Machi 7, mwaka huu. Awali kesi hiyo ilipangwa kutajwa mbele ya Hakimu Mkazi Mwandamizi, Augustine Rwizile.

Hata hivyo, Wakili wa Serikali Faraja Nguka alidai kuwa upelelezi wa kesi hiyo umekamilika na kuomba tarehe ya kuwasomea washtakiwa maelezo ya awali.

Hakimu Rwizile amesema washtakiwa watasomewa maelezo hayo Machi 7, mwaka huu na dhamana yao inaendelea ambapo amewataja washtakiwa wengine ni pamoja na Saidi Mtopali na James Charles Maarufu kama James Delicious.

Katika kesi ya msingi, ilidaiwa kuwa washtakiwa walifanya mapenzi kinyume na maumbile ambalo linamkabili Amber Ruty, inadaiwa alitenda kosa hilo kati ya ama baada ya Oktoba 25, 2018 ambapo alimruhusu Said Mtopali kumuingilia kinyume na maumbile, huku akijua ni kosa kisheria.

Ambe Rutty na Mumewe Wafunga Mtaa.

Mwanadada amber rutty amefunga mtaa huku jijini baada ya kutokea mitaa flani na kukutana na mtu ambae wamekuwa wakimtuhumu kila leo kuwa ndio aliuyewaharibia sana katika mitandao ya kijamii baada ya kuvijisha picha na video wakiwa faragha na mume wake.

Ambae Rutty na mume wake walipokutana na mwanaume huyo walikamata na kuanza kumpga huku baadhi ya watu wakiwa wanaangalia bila kutaka kuingilia ugomvi huo.

Ikumbukwe kuwa wawili hao bado wako na kesi mahakamani inayohusu kuvujisha kwa video ambayo iliwafanya kukaa rumande kwa muda mrefu kidogo na hata kesi hiyo kwenda mahakamani  mpaka sasa ambapo mara ya mwisho ilishindwa kusomwa kwa sababu mwanaume wa Amber Rutty alidondoka.

Hata hivyo wawili hao wanaweza kupatwa na kesi nyingine ya kuchukua sheria mkononi.

 

Mch.Mashimo Amcharukia Mama Amber Ruty

Mama wa msanii Amber rutty aliwahi kusema katika mitandao ya kijamii kuhusu swala la mchungaji mashimo kumtolea dhamana mwanadada Amber Ruty na kusema kuwa yeye ndio aliyekuwa mdhamini wa mwanae na wala sio mtu mwingine kama ambayo inasemwa katika mitandao ya kijamii.

Lakini mchungaji mashimo amefunguka na kuonyesha kukerwa na tabia hiyo na kusema kuwa yeye ndio aliyehusika na dhamana ya msanii huyo huku wakati mwingine hata akituma pesa ya matumizi kwa ajili ya  walengwa hao ingawa anahisi kabisa kuwa pesa hizo hazikuwa zikiwafikia walengwa.

Mchungaji huyo aliwahi kusema kuwa kufabya kwake hivyo hakumaanishi kuwafungwa sanii hao kuchana na imani yao lakini yeye alifanya kwa sababu alikuwa akiongozwa na mungu kufanya hivyo.

 

 

Amber Rutty ApangaKuanza Kuzaa Muda si Mrefu.

MSANII na Video Queen wa Bongo, Muscat Abubakary ‘Amber Rutty’ baada ya kufunga ndoa hivi karibuni ameweka wazi dhamira yake ya kumzalia mumewe, Said Mtopali na kwamba jambo hilo halitachukua muda mrefu.

Amber aliiambia Showbiz kuwa anatarajia kuzaa watoto wengi na mapema kabla ndoa yake haijaanza kuingia dosari na katika kulitimiza hilo, ameshaanza mchakato.

“Napenda watoto na nitamzalia watoto wengi mume wangu mpaka kizazi kitakapoisha, namuomba Mungu anijaalie kile ninachokipanga kiweze kutimia,” alisema Amber Rutty

Amber Rutty Aweka Wazi Changamoto Anazopitia Tangu Atoke Jela

Video vixen maarufu Muscat Abubakary maarufu kama Amber Rutty amefunguka na kuweka wazi magumu aliyokuwa anapitia tangu alipotoka jela Wiki chache zilizopita.

Kwenyr mahojiano aliyofanya na Gazeti la Risasi Jumamosi kwa njia ya simu, Amber Rutty alisema maisha ya jela siyo mazuri ndiyo maana tangu atoke kwa dhamana amekuwa na matatizo ya kiafya na kisaikolojia.

Aliendelea kusema kuwa kwa sasa hajawa sawa kwa ajili ya kuelezea kiundani kuhusu alichojifunza huko jela kwani hali yake bado haijatengamaa akirudi katika hali yake ya kawaida ataeleza mengi lakini kifupi watu watambue kuwa jela siyo mahali pazuri hivyo wawe makini.

“Kiukweli tangu nimetoka jela nimekuwa nikiumwa sana, yaani afya yangu siyo nzuri ndiyo maana sijaweza hata kuzungumza na vyombo vya habari kuhusiana na maswali yao wanayohitaji kujua kutoka kwangu. Pamoja na ukweli kuwa afya yangu siyo nzuri pia kisaikolojia siko sawa hivyo nikiwa vizuri ndiyo nitaongea mengi”.

Amber Rutty na mpenzi wake wanakabiliwa na mashtaka matatu yakiwemo ya kufanya mapenzi kinyume na maumbile na kusambaza picha za ngono kupitia mitandao ya kijamii ambapo kesi yao bado inaendelea kuunguruma katika Mahakama ya Hakimu Mkazi, Kisutu sasa wako nje kwa dhamana.Kabla ya dhamana hiyo, wawili hao walisota katika Gereza la Segerea kwa siku 25.

Amber Rutty , Mpenzi wake Wafika Mahakamani Kusilikza kesi Yao

Mwanadada Amber Ruty na mpenzi wake siku ya  December 11 walifika tena mahakamni kwa mara ya kwanza tngu waliotoka kwa dhamani ndani kwa ajili ya kusikiliza  kesi yao inayowakabili.

Mwanadada huyo na mpenzi wake walikabiliwa na kesi ya kusambaza na kurekodi picha na video za uchi huku wakifanya mapenzi kinyume na maumbile .

Wakiwa mahakamani hapo, wawili hao walisomewa mashtaka yao ambapo Amber Rutty alisomewa kosa la kumruhusu mpenzi wake kufanya nae mapenzi kinyume na maumbile, kosa ambalo alilikana,  lakini kosa lingine ni kuchapisha video hizo katika mitandao ya kijamii, lakini pia kusambaza video hzo katika mitandao ya whatsapp.

Dhamana Ya Amber Rutty Yaibua Mazito

Wiki chache zilizopita Msanii Amber Rutty na Mpenzi Wake Said Mtopali waliwekwa ndani kufuatia kesi yao ya kufanya mapenzi kinyume na maumbile na kisha kusambaza kwenye mitandao ya kijamii.

Amber Rutty alifanikiwa kupata dhamana Novemba 27, mwaka huu na kuonekana ameambatana na Mchungaji Daudi Mashimo mahakamani hapo, watu wengi waliamini kwamba mchungaji huyo ndiye aliyemuwekea dhamana.

Lakini Baada ya Gazeti la Amani kuzungumza na mama yake mkubwa Amber Rutty aitwaye Asha Seif ambaye alisema mbali na watu kuamini hivyo, alimshangaa Mchungaji Mashimo kuendelea kuwaamisha watu hivyo wakati si kweli.

Mimi nashangaa, huyu mchungaji alikuja siku ile pale mahakamani akakuta mimi pamoja na wifi yangu tumeshakamilisha taratibu za dhamana, akaja huyo Mashimo, akaniambia anaomba anisaidie kumtoa nje Amber Rutty maana kuna fujo ya waandishi wa habari.

Kwa kuwa mimi nilikuwa sijui sana mambo ya mahakamani, nikamkubalia kweli akafanya hivyo. Sasa baada ya kunisaidia, nikashangaa mara ooh sijui anampeleka kanisani, sijui mara atambadilisha dini, kwa kweli amenisikitisha sana”.

Mchungaji Mashimo mchungaji huyo ameeleza ukweli wake kuwa yeye alimuwekea dhamana jamaa wake Amber Rutty, Said MtopalI na  sio Amber Rutty:

Mimi nilimuwekea dhamana Mtopali japo nilikuwa na lengo la kuwawekea wote wawili lakini bahati nzuri mama yake amemuwekea dhamana Amber Rutty basi mimi nikamuwekea Mtopali”.

Lakini pia Mchungaji Mashimo aifunguka kuhusu suala la kujitangaza kumbadili dini Amber Rutty ambapo alisema ishu hiyo haina ukweli wowote kwani yeye alimkaribisha kwenye maombi na si kumbadili dini.

Amber rutty , Mpenzi Wake Kuamua Kuokoka.

Mchungaji, Daudi Mashimo amesema kuwa  msanii Rutyfiya Abubakary maarufu kama ‘Amber Rutty’ na mpenzi wake Said Bakary baada ya kumdhamini msanii huyo yeye na mpenzi wake wamekubali kuishi maisha ya kumpendeza Mungu.

Mchungaji Mashimo akizungumza EATV, amesema kuwa Amber Rutty na mpenzi wake  wameamua kabisa kufanya hivyo kutokana na yale waliyoyapitia lakini pia wamegundua kuwa maisha yao ya hapo awal hayakuwa  ya mupnendeza mungu hata  kidogo, alizungumzia   swala hilo kwaajili ya maisha yajayo ya wasanii ha mchungaji anasema;-

“Kama mimi mchungaji mtumishi wa Mungu nimezungumza nao mambo mengi kwaajili ya maisha yajayo na hali iliyokuwepo ni watu ambao kweli kweli ni watu ambao mioyo yao imekunjuka na kufunguka na ni watu ambao wamekubali kuishi maisha ya kumpendeza Mungu,”alisema Mchungaji Mashimo.

Novemba 2, 2018 walifikishwa Mahakamani kwa kosa la kufanya mapenzi kinyume na maumbile  , kesi ambayo walikosa kabisa watu wa kuwadhamini na ndipo mchungaji huyo ambae alisema kuwa yeye ametumwa na Mungu atafanya kazi hiyo kama alivyoagizwa kiimani.

Mchungaji Aliyemtoa Amber Rutty Aongea Sababu ya Kufanya Hivyo.

Mchungaji Daudi Mashimo amefunguka na kutoa sababu kubwa ya yeye kuamua kumtolea dhamana video vixen Amber Rutty ni baada ya kuona kuwa kila mtu alikuwa kimya na hawakutaka kujitokeza kwa ajili ya kumnusu mwanadada huyo.

Mchungaji Mashimo anasema kuwa aliamua kufanya hivyo baada ya kutokea mtu na kumtuma kuhsuu uamuzi huo na kwamba aliemtuma ni mwenyezi Mungu.

Ni kweli nilihusika kuwatoa na hata magereza ni mimi ndio nilienda, jambo la msingi mnatakiwa kujua kuwa Amber Rutty ni mtoto wa mungu  na nisipotumika kwa watu kama hawa sitakuwa mtumishi wa Mungu,  ila kweli natumiwa na ninatumwa na Mungu.

Mchungaji Mashimo anasema ana mengi ya kuzungumza kuhusu Amber Rutty , mpenzi wake na hata Wema Sepetu lakini muda muafaka ukifika atazungumza na sio sasa.

Amber Rutty Mpenzi Wake Hoi Gerezani

Msanii Amber Rutty  na mpenzi wake ambae wanasota gerezani mpaka sasa kwa kukosa dhamana baada ya kuingizwa selo wakiwa na kosa la kuvujisha video walizojirekodi kinyume na kanuni na hata kuizfanya zikasambaa katika mitandao ya kijamii.

kwa chanzo kinachotoa habari za wawili hao zinasema kuwa wawili hao kwa sasa wameanza kuonekana kudhoofika sana huku sababu kubwa ikihisiwa kuwa wawili hao walikuwa na ugonjwa  wa kifua kikuu.

Moja ya ndugu wa karibu wa Amber Rutty anasema kuwa wawili hao walikuwa wakiumwa ugonjwa huo kabla ya matatzio haya kuwakuta na waliwahi kuzidiwa sana hata kusafirishwa kutoa jijini mpaka rifiji ambapo ni nyumbani kwa mwanaumekwa ajili ya kuuguzwa huko.

Hata hivyo baada ya kupata nafuu walirudi mjini kuendelea na shughuli zao, ndugu  huyu anasema kuwa hivi karibuni walikwenda kuwaangalia hali zao wakiwa huko gerezani na ndipo walipowakuta wameanza tena kudhofika sana.

Ndugu huyo anasema kuwa wamekuwa wakifanya mchakato kwa ajili ya kupata dhamna ili kunususru hali za ndugu zao.

Baada ya hapo waandishi wa habari walipata kuzngumza na kiongozi mmoja wa kituoni hapo na yeye alisema kuwa hajapata taarifa za ugonjwa wao lakini pia kama kweli ni wagonjwa basi kunataratibu huwa zinafuatwa na kupata matibabu lakini hawezi kutoa taarifza za mgonjwa au mahabusu.

Amber Rutty Apata Mtu wa Kumtolea Dhamana.

Mwanadada Amber Rutty ambae alikuwa katikakesi na mpenzi wake baaada ya kukutwa na hatia ya kurekodi na kusambaza video zilizokuwa zikiwaonyesha wakifanya mapenzi kinyume na maumbile amepata mdamini wa kumdhamini baada ya kusota rumande kwa muda mrefu kwa kukosa dhamana.

Amber Rutty ambae ni msanii na pia video vixen alikutwa na kashfa hiyo ya kufanya mapenzi kinyume na maumbile akiwa na mpezi wake huyo na kisha kujirekodi na  kuvujisha picha hizo wamesota rumande kwa muda mrefu na hatimaye yeye kupata dhamana huku akimwacha mpenzi wake akiwa bado anasota rumande.

Mwanaume huyo ambae mpaka sasa hajajulikana ana mahusiano gani na mwanadada huyo amjitokeza na kumtolea dhamana hivyo kuwa huru kwa dhamana.

 

Amber Rutyy na Mpenzi Wake Bado Wasota Rumande.

Msanii na video vixen Amber Rutyy na mpenzi wake bado wanaonekna akusota sana rumande kutokana na kukosekaa kwa watu ambao wanaweza kuwapa dhamana kutokana na kesi yao ya kusambaza video chafu na pia kosa la kufanya mapenzi kinyume na maumbile.

Wawili hao walikamatwa kwa kosa la kusambaza picha lakini pia kufanya mapenzi kunyume na maumbile ikichache zilizopita na hata kesi yao kuonekana ipo wazi kwa dhamana lakini hakuna aliyejitokeza kwa ajili ya kuwapa dhaman.

November 12 mwaka huu wawili hao walifikishwa tena mahakanami huku kukiwa na mategemeoa makubwa ya kupata  wadhamini lakini wadhamini hao walipotelea mitini na hawakuonekana.

Hivyo wawili hao wamerudishwa tena rumande mpaka pale watakapopata wadhamini huku kesi hiyo ikitarajiwa kusomwa tena november 24 mwaka huu.

Serikali inasema kuwa haitakaa kuvumilia watu wanaofanya uchafu kama Amber Rutty kwa sababu , kufanya mapenzi kinyume na maumbile ni swala silislokubalika lakini pia ni kinyume na sheria na misingi ya taifa na dini zote pia.

Tulirekodi Video, Niliona Jambo la Kawaida ;-Mpenzi wa Ambaer Rutty

Mwanaume aliyejitambulisha kuwa yeye ndie mpenzi wa Amber Rutty ambae alionekana katika video mbalimbali chafu zilizokusambaa mtandaoni wiki iliyopita amefunguka na kukiri kosa lake na kusema kuwa ni kweli kuwa walikuwa wakirekodi uchafu huo na mpenzi wake Amber Rutty lakini hakuwahi kuwaza kama inaweza kutokea kama ilivyotokea.

Mwanaume huyo anasema kuwa wakati wanarekodi alikuwa akiona kuwa ni jambo la kawaida ukizinatia kuwa simu ilikuwa ya kwake na hakuna ambae angeweza kusihika lakini kwa bagat mbaya alipotez simu wiki chache zilizopita na kusababisha yote hayo.

ni kweli tulirekodi video, lakini nilijua ninkawaida tu , tulikuwa tunachukulia poa kwa sababu sisi ni wapenzi na simu yangu hakuna mtu anaishika.ila wiki hizi mbili tautu kuna sehemu nilikuwa ninaenda nikaangusha simu kweny bodaboda na nahisi huyo aliokota simu yangu ndio anavujisha picha na video hizi.ninaomba radhi kwa sababu sikujua yote haya.

Wiki iliyopita baada ya kuvuja kwa picha hzio mtu wa kwanza kuulizwa aliuwa Amber Rutty ambae pia alisema kuwa hakujua kama jambo hilo litatokea na ni kweli vidoe zile walikuwa wakijirekodi yeye na mpenzi wake.

Amber Rutyy Akanusha Kuvujisha Video Zake Chafu.

Kumekuwa na wimbi la video na picha chafu katika mitandao ya kijamii zikionyesha waziwazi maumbile ya wanaohusika katika video hizo bila kujali kuwa ni nani anaweza kuona au zitakuwa katika mitandao kwa muda gani na kwa kiasi gani zinaweza kuharibu maisha yao.

Ilianza Wema , ikaja ya Gigy money akiwa uchi na sasa mwanadada Amber Ruty pia amekumbwa na skendo hiyo ya kuvujisha video za uchi kwa musa mchache wa siku mbili mfululizo.

Moja ya watangazaji wa ki-indi cha umbea kutoka clouds media aliguswa na tukio la Amber Ruttty hivyo aliamua kumtafauta  na kumuuliza imekuwaje kuweka video mbaya katika mitandao ya kijamii akiwa na mwanaume wake wakiwa wanafanya mapenzi.

Kwa njia ya sms , wawili hao walikuwa wakijibizana kwa smsm, na mwanadada huyo alikataa na kusema kuwa hajui chochote kuhusu video hiyo na hata mwezi wake hajui chochote kwa sababu mwanaume huyo ni mpenzi wake wa siku nyingi.

Hata hivyo kwa kujitetea zaidi mwanadada huyo anasema kuwa anahisi kuwa vidoe hiyo ilivujishwa na watu  waliookota smu ya mweiz wake ambayo ilipotea wiki iliyopita kwenye bodaboda.

Hili ni swala ambalo kila siku limekuwa likitakazwa lakini linazidi kuibuka kwa kasi na wanaofanya hivyo wengi ni wasanii mabao tunasema ndio kioo cha jamii .