AY Ajivunia Kuwa Moja ya Wasanii Waaminifu Sana

Msanii wa siku nyingi katika game ya muziki Ambwene Yesaya mabe siku zote amekuwa na mafanikio lakini anatajwa kuwa moja ya wasanii ambao wanaweza kutao msaada na sapoti kwa msanii mwingine na wala asitake kujulikana kwa kile alichokifanya amefunguka na kusema kuwa anajivunia kuwa moja ya wasanii wanaoweza kusemwa kuwa na uaminifi mkubwa sana.

Ay anasema kuwa siku zot yeye hajawahi kufanya manejement ya msanii yoyote lakini inapotokea msanii anataka usaidizi kwa nchi au msanii anaemjua ufanya kile anachoweza ili kufanikisha swala hilo.

Akitolea mfano, AY anasema kuwa aliwahi kuwasaidia wasanii kutoa Nigeria P-Square  kwenda nchi ambayo hawakuwahi kwenda lakini aliwatafutai watu anaowajua katika nchi hiyo na hata kufanya show yao na kupewa pesa yao na kutengeneza mashabiki katika nchi hiyo.

niliwahi kuwapa mchongo p-square walikuwa na show burundi lakini hawakuwa na mwenyeji , kwaiyo mimi nikawaunganisha na mtu akasimamia kila kitu, kwaio mimi nilikuwa kama bask stage na jamaa wakafanya show na wakapewa mzigo wao.

 

Shaffie Werru Afunguka Kuhusu Ndoa Ya AY na RemmyRwanda

                                         

Msanii mkongwe wa muziki bongo Ambwene Yesaya  amefunga ndoa wikiendi  hii na mpenzi wake wa siku nyingi remmy kutoka rwanda na kufanya harusi fupi iliyokuwa ya siri na kuarikwa watu wachache wa karibu  na familia hizo.habari hizo zilianza kuvuja katika mitandao kipindi ambacho harusi hiyo ikiwa imeshafanyika na kuonekana ni watu wachache tu kutoka Tanzania na nchi rafiki waliohudhuria harusi hiyo.

Moja ya wahalikwa katika harusi ya msanii AY ni mtangazaji maarufu wa radio nchini Kenya Shaffie Werru ambae alitoa siri ya kualikwa kwake katika sherehe hiyo ya msanii huyo  mkongwe.Shaffie anasema kuwa tangu mwanzo alishajulishwa kuwa msanii AY alitaka ndoa yake iwe ya siri na isiwe na watu wengi hivyo waliamua kuweka wageni wachache tu na yeye akiwepo.

nimemfahamu AY kwa zaidi ya miaka kumi sasa kupitiakazi yangu hii ya utangazaji,tumekuwa tukifanya kazi pamoja kwa muda mrefu sasa,tumefanya biashara pamoja na hata kusafiri mara nyingi.AY amenisaidia kunitambulisha sana nchini mwao na mimi nimekuwa nikimtambulisha na kumtangaza sana nchi kwetu kwa muda mrefu sasa na hii ni sababu kubwa sana ya yeye kunialika mimi katika ndoa yake kama mmoja wa wanafamilia.

Katika harusi hiyo  wawakilishi wachache walioonekana kutoka Tanzania ni pamoja na rafiki wa karibu wa msanii AY ,  ni Mwana Fa, B-Dozen na rafiki wengne kutoka nchi mbalimbali.Wasanii mbalimbali walimpongeza AY kwa tukio hilo la kuchukua jiko akiwepo Profesa Jay, Diamond Platinumz na Jokate Mwegelo.