Mimi na Nandy Sio Kikundi Cha Muziki- Aslay

Mwanamuziki mkali wa Bongo fleva Aslay ameibuka na kuweka wazi kuwa yeye na Msani mwenzake Nandy sio wasanii wa kikundi kimoja cha muziki bali wanafanya tu kazi pamoja.

Siku za hivi karibuni Nandy na Aslay wameonekana wakifanya matamasha kadhaa pamoja Ikiwa ni pamoja na Tamasha lao kubwa la Valentine’s Day lilipfanyika mwezi February.

Aslay ameweka wazi kuwa yeye na Nandy sio kikundi ila tu wanaonekana wakifanya shoo kwa pamoja sababu ya nyimbo zao walizotoa kwa pamoja hasa nyimbo yao ya ‘Subalkheri Mpenzi’ inayofanya vizuri kwa hivi sasa.

Kwenye mahojiano aliyofanya na Bongo 5, Aslay ameeleza ukaribu wake na Nandy ni wakazi tu na sio kama wao ni kundi la muziki ila mashabiki wanavutiwa na ngoma walizofanya pamoja ambazo ni ‘Mahabuba ‘ na ‘Subalkheri Mpenzi’ ndio maana na wanaalikwa katika show pamoja.

Aslay na Nandy Wachapwa Faini ya Milioni 5 Kwa Wizi

Msanii wa Bongo fleva Aslay na msanii mwenzake Nandy wanaotamba hivi sasa na wimbo wao wa ‘Subalkheri Mpenzi’ wamejikuta wakichapwa faini ya shilingi milioni tano baada kutuhumiwa Kwa Wizi wa wimbo.

Aslay na Nandy wametawala chati zote za redio na televisheni kwa wimbo wao wa Subalkheri Mpenzi hata juzi juzi hapa walipiga bonge moja la shoo pale escape one lililoitwa Nandy Aslay pamoja na marafiki ambapo watu walijazana kwa ajili ya kwenda kujionea uwezo wa kuimba.

Lakini wiki iliyopita tuliweka habari ya wasanii hawa wawili kuimba wimbo huo bila ruhusa ya wenye wimbo ambao Subalkheri Mpenzi ni wimbo ulioimbwa na kikundi cha taarab asilia visiwani Zanzibar ambao walisema wanataka kuwashataki kwa kuimba wimbo wao bila ruhusa.

Kikundi hiko kilidhamiria kuwaburuza mahakamani wasanii hawa lakini baada ya mazungumzo ya pande zote mbili walifikia uamuzi wa kuwalipisha faini ambayo ni shilingi milioni tano.

Katibu mkuu wa kikundi cha utamaduni wa taarab asilia, Twaha  amefunguka na kusema kuwa licha ya wasanii hao kukiri kosa na kukubali kulipa faini lakini pia meneja wa Aslay ameomba kuingia mkataba na kikundi hicho na kufanya biashara ya kuziimba tena nyimbo zao za zamani ambapo amedai bado hawajakubali kuhusu hilo kwani walishapewa agizo na raisi mstaafu wa awamu ya tatu, Dk. Salmin Amour Juma kuwa wasikubali nyimbo zao za taarab asilia kubadilishwa na kuwa mziki wa kisasa.

Aslay na Nandy Kuburuzwa Mahakamani Kwa Tuhuma za Wizi

Mwanamuziki wa Bongo fleva anayefanya vizuri kwa hivi sasa Aslay pamoja na msanii wa kike mwenye sauti ya kipekee kutoka THT, Nandy wamejikuta katika wakati mgumu baada ya kutishiwa kuburuzwa mahakamani baada ya Luik a wimbo bila ruhusa.

Aslay na Nandy wanatamba hivi sasa na wimbo wao unaoitwa ‘Subalkheri Mpenzi’ ambao wanashika chati katika stesheni mbali mbali za redio na hata kukaa katika nafasi za mwanzoni katika mtandao wa nyimbo na video YouTube ambalo walishika nafasi ya kwanza kwa muda wa wiki nzima.

Kwenye ziara na vyombo vya habari waliyofanya   (media tour) katika jitihada za kutangaza nyimbo hiyo Aslay na Nandy waliwahakikishia mashabiki zao kuwa wamepata ruhusa kamili ya kurudiana kuuimba wimbo huo ambao ulishawahi kuimbwa siku za nyuma.

Sintofahamu imekuja kuzuka baada ya  mmiliki wa wimbo hu, kikundi cha Taarab asilia Visiwani Zanzibar (Culture Music club) kudai pesa zilizotolewa jumla ya shilingi 800,000 kama fidia ya wao kutumia kazi yao hawazitambui hivyo wanajipanga kuwapeleka mbele ya mahakama.

Kwenye mahojiano aliyofanya na kituo kimoja cha habari, Katibu mtendaji wa kikundi hiko Taimur Rakuni amedai kuwa wasanii hao kabla ya kuimba wimbo huo upya walitakiwa kuonana na uongozi huo ili kukubaliana jambo ambalo hawakufanya hivyo.

Kwa msanii Aslay hii ni mara ya kwanza kwake anakumbana na skendo hii ya kuiba wimbo wa wasanii wengine lakini kwa Nandy ametuhumiwa mara nyingi na wasanii wengine kwa kuiba nyimbo na kuzirudia bila ruhusa mfano ni Ray C ambaye alimjia juu na kudai kaiba wimbo wake na kuuimba bila ruhusa.

Mashabiki Wanataka Niwe na Nandy – Aslay

Mwanamuziki mkali wa Bongo fleva Aslay Amefunguka na kudai kuwa mashabiki zake wengi wanafurahia akifanya kazi na msanii mwenzake Nandy hivyo wanataka awe naye.

Aslay ambaye amekuwa akifanya vizuri kwenye ulimwengu huu wa muziki wa Bongo ambapo ni mara kwa mara amekuwa akishika chati ya juu kwa nyimbo zake. Aslay alitokea kwenye kundi la Yamoto band lakini tangu ameanza kufanya muziki kama solo artist amepata mafanikio zaidi.

Siku ya Jana Aslay na Nandy wameachia wimbo wao mpya unaoitwa ‘SubalKheri mpenzi’ wimbo huu ukiwa wa pili amemshirikisha Nandy Aslay amesema mashabiki zake wanawasababisha wafanye hivyo.

Kwenye mahojiano aliyofanya na Planet Bongo ya East Africa Radio, Aslay amesema kuwa mashabiki zake walifurahia pale alipofanya kazi ya kwanza na Nandy na ndipo walipoona ni vyema wakarudi tena studio kufanya kazi nyingine kwa ajili yao:

Ni pendekezo la mashabiki tumeona mashabiki zetu wakitaka kitu kingine kutoka kwetu baada ya kazi ya kwanza na Nandy inaelekea mashabiki wanapenda kuniona na Nandy hivyo tukaona tuingie jikoni tuwapikie kazi mpya”.

Aslay tangu awe solo artist ametoa jumla ya nyimbo kumi na sita ambazo amesema ilibidi atoe nyimbo nyingi kwa wakati mmoja ili aweze kupiga nyimbo zake mwenyewe kwenye shoo zake bila kutegemea nyimbo alizokuwa anaimba wakati yupo Yamoto.