Tessy Chocolate Athibitisha Kumfutilia Mbali Aslay

Aliyekuwa Mpenzi wa Staa wa Bongo fleva Aslay Isihaka maarufu kama Aslay, Tessy Chocolate amethibitisha kumfutilia mbali staa huyo tangu Penzi lao  lilipoisha.

Miezi michache Baada ya Penzi hilo kufika mwisho Tessy Chocolate Amedai kwamba kwa sasa hapotezi muda wake kumu­waza mwanaume huyo, kwani ame­shamsahau na sasa ana maisha yake mengine.

Kwenye mahojiano aliyofanya na Global Publishers, Tessy alisema kuwa alipata shida mwanzoni lakini tangu agundue kwamba msanii huyo hakuwa chaguo lake alia­mua kuishi maisha yake.

Nilipata shida sana mwanzo­ni, kila mtu alikuwa ananishauri anavyojua yeye, lakini nashuku­ru Mungu siku zilienda na sasa hivi nimesham­sahau kabisa.

Kilichobaki kati yetu ni kumlea tu binti yetu Moza basi, pia sidhani kama naweza nikarudi tena kwake nina maisha yangu na ninayafu­rahia”.

Aslay na Tessy walikuwa kwenye mahusiano ya kimapenzi kwa miaka mingi na wakafanikiwa kupata Mtoto mmoja wa kike anayejulikana Kama Mozah.

Aslay Achora Tattoo Ya Sura Ya Binti Yake

Msanii wa Bongo fleva anayeendelea kufanya vyema kabisa Isihaka Nasorro maarufu kama Aslay ameonyesha mapenzi ya hali ya juu baada ya kuchora tattoo ya sura ya binti yake Mozah kwenye mkono wake.

Siku ya jana Mtoto wa Aslay alikuwa anafikisha umri wa miaka mitatu baba yake mbali ya kushiriki na kusheherekea siku hii na binti yake Lakini pia amechora tattoo ya sura ya Mtoto Wake.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Aslay ameandika maneno haya kwa ajili ya binti yake:

https://www.instagram.com/p/BuD5USUFEZi/?utm_source=ig_share_sheet&igshid=a1a78c7dl370

Aslay ambaye ana umri wa miaka 23 alizaa Mtoto huyo na mrembo maarufu kwenye Mitandao ya kijamii Tessy Chocolate ambaye Hivi sasa hawapo kwenye mahusiano ya kimapenzi tena.

Tessy Chocolate Afungukia Tetesi za Aslay Kutomuhudumia Mtoto Wao

Mzazi mwenzake na Staa wa Bongo fleva Aslay Isihaka, Tessy Chocolate amefungukia tetesi zinazodai kuwa baba wa Mtoto wake huyo amegoma kumuhudumia mtoto wao baada ya wao kuachana.

Kumekuwa kuna tetesi kwenye mitandao ya kijamii kuwa tangu walipoachana miezi michache iliyopita Aslay amemsahau kabisa binti yake Moza na kuwa busy na wanawake wengine kiasi ya kwamba hakumbuki hata kutoa pesa ya matumizi.

Lakini Mama Watoto Wake anayejulikana Kama Tessy Chocolate amekana tetesi hizo na kusema Askay ni baba mzuri sana kwa binti yao na anashukuru amekuwa akimuhudumia Mtoto wao.

Kwenye mahojiano aliyofanya na Millard Ayo, Tessy Chocolate alifunguka haya kuhusu uhusiano Wake na Baba Watoto Wake huyo:

Hizo stori hazina ukweli wowote kusema ukweli mimi nashukuru kuwa Aslay anatimiza majukumu yake kama baba anavyotakiwa na kama unamfatilia utaona anamposti sana mtandaoni angekuwa amuhudumii nisingeweza kumruhusu amposti lakini namshukuru kila siku kwa kuwa baba bora kwa binti yake”.

Lakini pia Tessy Chocolate ameweka wazi kuwa hana Bifu na Baba Mtoto Wake hivyo hata akiwa na wapenzi wengine yeye hana neno kwa sababu kila mtu ana maisha yake kwa sasa.Aslay

Aslay Akiri Kuumia Moyo Baada Ya Kumwagana na Mama Watoto Wake

Msanii wa muziki wa Bongo fleva Aslay Isihaka amefunguka na kuweka wazi kuwa Kitendo Cha kuachana na kama watoto wake bado kinamuumiza mpaka leo.

Miezi michache iliyopita Aslay alikiri kuachana Rasmi na aliyekuwa na mpenzi wake kwa muda mrefu Tessy Chocolate ambaye pia amezaa naye mtoto mmoja.

Kwenye mahojiano na gazeti la Mwanaspoti, Aslay ameweka wazi kuwa hapendelei sana kuongelea kuachana kwake na Tessy lakini hawapo pamoja:

Huwa sipendi kulizungumzia hili suala kwa sababu linaniumiza sana, ila ukweli ndio huo kama ulivyosikia nimeachana na mama Moza.

Ni mambo ya familia na kilichobaki kwa sasa ni uhusiano wa wazazi wenye mtoto, ambaye anahitaji uangalizi wa pande zote. Unajua kuna baadhi ya watu wanadhani kuwa hii ni kiki, lakini mimi sio mtu wa kiki kabisa na ninazungumza hapa ni ukweli mtupu”.

Aslay amedaiwa kuwa Kwenye Mahusiano na Muigizaji wa Bongo movie Diana KImario na pia Tessy ametajwa kuwa Kwenye Mahusiano na mwanaume mwingine ambaye ni Kigogo fulani mjini.