Mbosso Afungukia Bifu Lake na Aslay

Msanii wa muziki wa Bongo fleva anayefanya vyema chini ya Label ya WCB amefunguka na kuweka wazi kuwa hali sio shwari kati yake na msanii mwenzake Aslay.

Mbosso ameweka wazi kwamba kwa sasa hayupo sawa na muimbaji mwenzake, Aslay ambaye awali alikuwa anafanya naye kazi katika bendi ya Yamoto Band.

Kwenye mahojiano aliyofanya na Azam, alisema kuwa awali alikuwa anamsupport Aslay katika kazi zake ambazo amekuwa akizitoa lakini yeye amedai alikuwa hasapotiwi na muimbaji huyo.

Baada ya kumsupport Aslay kwa muda mrefu watu wakawa wananimbia mbona wewe unam-support halafu yeye haku-support? umem-follow mwenzako ameku-unfollow. Jifunze kubalance shobo, nikasema kumbe na mimi naonekana namshobokea ngoja na mimi nim-unfollow. Kwa hiyo sasa hivi kila mtu hana urafiki na mwenzake”.

Aslay na Mbosso walikuwa katika Kundi moja la Yamoto Band kwa miaka mingi Lakini walikuja kutengana  kutokana na sababu za kimaslahi ambapo Mbosso alijiunga na Label ya WCB.

Aslay Achora Tattoo Ya Sura Ya Binti Yake

Msanii wa Bongo fleva anayeendelea kufanya vyema kabisa Isihaka Nasorro maarufu kama Aslay ameonyesha mapenzi ya hali ya juu baada ya kuchora tattoo ya sura ya binti yake Mozah kwenye mkono wake.

Siku ya jana Mtoto wa Aslay alikuwa anafikisha umri wa miaka mitatu baba yake mbali ya kushiriki na kusheherekea siku hii na binti yake Lakini pia amechora tattoo ya sura ya Mtoto Wake.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Aslay ameandika maneno haya kwa ajili ya binti yake:

https://www.instagram.com/p/BuD5USUFEZi/?utm_source=ig_share_sheet&igshid=a1a78c7dl370

Aslay ambaye ana umri wa miaka 23 alizaa Mtoto huyo na mrembo maarufu kwenye Mitandao ya kijamii Tessy Chocolate ambaye Hivi sasa hawapo kwenye mahusiano ya kimapenzi tena.

Mkubwa Fella Ashtushwa na Kuachana kwa Aslay na Tessy

Aliyekuwa meneja wa kundi la ya moto band mkubwa Fella, kundi  ambalo lilikuwa likiundwa na wasanii wanne chipukizi amefunguka na kuonyesha kushtushwa kwake na taarifa kuwa moja ya wasanii walikokuwa wakiunda kundi hilo amb ae ni aslay ameachana na aliyekuwa mpenzi wake a siku nyingi ambae pia ni mama wa mtoto wake mmoja.

Mkubwa Fella anasema kuwa taarifa hizo alikuwa haziamini hata kidogo na kwamba hakuona kama kuna umuhimu wa kuzifatilia kwa sababu zilikuwa zikisambaa katika mitandao ya kijamii tu.

Mkubwa fela anasema atakuwa tayari kufanya usuluhisho endapo wawili hao wataamua kutaka kumjulisha tatizo hilo na sio kubeba habari kutoka katika mitandao ya kijamii kwa sabab habariz hizo mara nyingine huwa sio za kweli.

 

Nandy Kupanda Steji Moja na Hamisa Mobetto

Msanii wa muziki wa Bongo fleva Faustina Charles maarufu kama Nandy ametangaza habari njema kwa mashabiki Wake wanaokaa nje ya nchi kwani anatarajiwa kupanda steji moja na Hamisa Mobetto.

Nandy ambaye anafanya vizuri na ngoma yake ya ‘Aibu’ ameweka wazi kuwa mwezi huu baadae anatarajia kuungana na Hamisa Mobetto kwa ajili ya your yake ya nchini Marekani.

Kwenye mahojiano aliyofanya na Gazeti la Ijumaa Wikienda, Nandy ameweka wazi kuwa yeye na msanii mwenzake Aslay wanatarajia kuungana na Hamisa Mobetto nchini Marekani.

Natarajia kusafiri siku ya tarehe 25 mwezi huu kuelekea Marekani kwa ajili yakufanya ziara nikiwa na msanii mwenzangu Aslay na Hamisa kisha nitarudi Bongo tarehe 10, Desemba tukiwa wote watatu, pia hii kwangu itakuwa ni mara ya kwanza kufika huko kwa sababu sijawahi kwenda kabisa”.

Hamisa Mobetto amekuwepo nchini Marekani kwa zaidi ya mwezi sasa ambapo ameonekana akiwa anafanya matamasha katika majimbo mbali mbali katik nchi hiyo.

Alichosema Aslay Baada ya Kuanguka Jukwaani Nchini Kenya

Msanii wa bongo fleva, Aslay amechukulia kitendo cha kuanguka kwake jukwaani ni kama moja ya changamoto wanayokutana nayo wasanii wakiwa stejini,Aslay anasema kuwa hilo linaweza kumtokea mtu yoyote mahali popote anachoshukuru ni kwamba hakuumia , kupitia ukurasa wake wa instagram, Aslay ameelezea juu ya ajali hiyo iliyompata akiwa Kisumu nchini Kenya kwa kuandika
It’s normal for celebrities and performers to encounter some challenging moments while on stage and mine came through yesterday, I slipped on stage but miraculously I wasn’t hurt, I came back on stage and gave one of the most electrifying performance, KISUMU  you guys are AMAZING the Energy was insane. Mwenyezi Mungu Awabariki !!!
Ambapo tasfiri yake ni kuwa “Ni Kawaida kwa Wasanii kupatana na changamoto jukwani, na Jana ilikuwa zamu yangu, yalitokea Haya punde tu nilipopanda jukwani kwa bahati nzuri sikuumia ,nilirejea jukwani na kuburudisha Mashabiki wangu wa Kisumu waliyojitokeza kwa wingi. Asanteni sana nyote Mwenyezi Mungu Awabariki!!!’ aliandika

Baada ya kuanguka kwa msanii huyo kulitokea maoni mengi sana katika mitandao huku baadhi ya waandishi na mashbiki walisema kuwa kuanguka kwa msanii huyo ni figisu zilizokuwa zikifanywa na baadhi ya watu hili kuondoa sifa nzuri ya kazi za wasanii wa kitanzania katika nchi za jrani , lakini alsya anasema kuwa maswala kama hayo huwa yanatokea  kial mahali.

Aslay Adaiwa Kuanguka Stegini Mjini Kisumu -Kenya.

Msanii wa muziki wa bongo fleva Aslay ameanguka jukwaani baada ya stegi ambayo ilijengwa kwa ajili ya perfomance  kuporomoka na kushindwa kuhimili mzigo ulokuwa umebeba.

Hata hivyo baadhi ya waandishi  wanadai kuwa hii inaweza kuwa ni mipangi kutoka kwa baadhi ya waandaaji au mtu yoyote ambae hakutaka kumuona Aslay akifanya vizuri katka tamasha hilo.

Matukio ya wasanii wa tanzania kuhariwa show wakiwa nchini kenya yameanza kuripoiwa kwa kushamili sana kiais kwamba inawezekana kuwa kuna figisu kubwa zinazoendelea kati ya wasanii wa Tanzania na waandaji au wasanii wa Kenya.

Aslay alionekana kuanguka mzima mzima katika jukwaa hilo huku akiacha mashabiki wake wakianga kilio kwa kile ambacho hawakutegemea kukiona lakii pia baada ya kukatishwa kwa show hiyo.

 

 

Nandy Amtaja Aslay Kama Msanii Alimtungia Nyimbo Kwa Ajili Ya Albamu Yake

Msanii wa muziki wa Bongo fleva nchini kutoka katika Nyumba ya vipaji Tanzania (THT) Faustina Charles maarufu kama Nandy amefungukia Albamu yake mpya.

Albamu mpya ya Nandy ambayo hivi sasa iko sokoni inaitwa ‘The African Princess” Kiowa ni albamu yake ya kwanza kuingiza sokoni tangu aanze Sanaa yake ya kimuziki.

Nandy ameweka wazi kuwa Albamu hiyo imemchukua Kama mwaka mzima kuiandaaa tu huku nyimbo zake akiandikiwa na msanii Kama Jay Melody na staa mkubwa wa Bongo fleva Aslay.

Kusema ukweli Albamu yangu imechukua muda mrefu kukamilika kwa sababu nimekuwa nikitungiwa nyimbo na wasanii Kama Aslay na Jay Melody”. 

Kwneye mahojino na kituo kimoja cha habari Nandy amefunguka haya kuhusu muziki wake na albamu yake hiyo:

Imenichukua mwaka mzima kutengeneza albamu yangu ili kupata Kitu kizuri hii imekuwa kwa sababu ya kusafiri kwa ajili ya kufanya shoo mbali mbali ambazo zimechukua muda wangu mwingi”.

 

Sijawahi Kulia Kisa Mapenzi :-Aslay

Msanii wa muziki wa kizazi kipya nchi Aslay amefunguka na kusema kuwa katika maisha yake  ya mahusiano hajawahi kulizwa na mwanamke kisa mahusiano hivyo mapenzi .

Aslay ambae alikuwa na mahusiano na mwanadada Tessy Chocolate kwa muda mrefu sana na kubahatika kupata mtoto mmoja laki ni walikuja kuachana bila kuwa na sababu bayana ya kufanya hivyo  na hata baadae kuanza kuwa na skendo za kuwa katika mahusiano na wanawake tofauti .

Mwanamuziki huyo anasema “sijawahi kulia kwa sababu ya mapenz lakini niliwahi kulia machozi kwa sababu  nilimpoteza mama yangu mzazi”

“Najisikia Vibaya Kushindanishwa na Aslay”- Mbosso

Msanii wa Muziki wa Bongo fleva kutoka WCB anayefanya vyema na ngoma yake ya ‘Hodari’ Mbosso amefunguka na kuweka wazi kuwa anachukia sana kupambanishwa na Aslay.

Mbosso na Aslay walikuwa pamoja katika kundi la Yamoto Band lakini baada ya kundi kuvunjika kila mmoja alienda njia yake lakini mashabiki wamekuwa wakiwapambanisha sana.

Mbosso amefunguka na kusema hakuna kitu kinachomsumbua na kumfanya ajisikie vibaya kama kuona anapambanishwa na Aslay kwa sababu anaona kabisa hawawezi kulingana kwa sababu Aslay ni kaka yake.

Hakuna kitu kinanifanya najisikia vibaya mara kwa mara kama nikaona nashindanishwa na Aslay, Mimi Aslay ni Braza angu, alafu isitoshe mimi nimeanza mziki kama Solo artist nina Miezi Tisa sasa lakini Aslay alianza muziki kama Solo artist tangu mwaka 2011 kwaiyo ni mkubwa sana kwangu mimi bado mchanga mno kwaiyo ukinifanisha naye unakuwa unamvunjia heshima yake na mimi sitaki iwe huvyo”.

 

Shuga Mamy wa Harmorapa Afunguka Mazito Kuhusu Aslay.

Mwanadada amanesemekana katika mitandao ya kijamii kuwa kwa sasa amemuweka ndani harmorapa na kumsaidia kwa kila kitu mpka afamilia  yake anajulikana kama khadija ziota kutoka mwanza amefunguka mambo makubwa na mazito kuhusu msanii anaefanya vizuri sana katika tasnia aslay.

Mwanadada huyo anaekiri kuwa aliwahikuwa na mahusiano na wasanii wengi sana na kuwa anawasaidia lakini baadae wanakuja kuachana nae , anasema kuwa aliwahi kuwa na mahusiano na aslay na kumsaidia sana lakini alikuja kumuacaha kwa sababu ya kuchoka kuwa anaombwa pesa kila siku.

Mimi na aslay tulishwahi kutembea, tulishakuwaga wapenzi,tulishafanya vitu vingi tu mbalimbali hata ile nyumba yake ghorofa mimi ndio niliemalizia ile nyumba.tulikuwa tunakutana sana Isamilo lodge na Gold crest, tumelala sana pale.

Alipoulizwa sababu ya kwanini aliachana na Aslay ,mwanadada huyo kwa dharau kabisa alisema kuwa alichoka kuombwa ela na aslay na ndipo alipomuakumuacha.

Tuliachana kwa sababu mapenzi yana mwanzo na mwisho,yaani sikumbuki lini ila anaomba sana ela, unajua mtu ukiombwa saa ela unachoka nikamwamcha.

 

Aslay Kumsaidia Enock Bella Kimuziki Kwa Kolabo

Msanii wa Muziki wa Bongo fleva Aslay Isihaka amefunguka na kuweka wazi kuwa ana mpango wa kumshika mkono na kumsaidia Msanii mwenzake kutoka Yamoto Band Enock Bella.

Aslay alikuwa mmoja wa wasanii waliounda kundi la Yamoto Band lakini baada ya kundi hilo kuvunjika miaka michache iliyopita kila msanii alishika njia yake.

Baada ya kila msanii kuendelea na kazi zake binafsi Aslay alionekana kupata mafanikio makubwa zaidi lakini pamoja na Beka Flavor ambaye pia amekuwa anafanya vyema na Mbosso aliyesainiwa WCB amekuwa anafanya vizuri pia.

Lakini Enock Bella aliyekuwa maarufu kwa kuimba bezi kwenye Yamoto amekuwa akisuasua tofauti kabisa na wenzake kwani ameshatoa nyimbo kadhaa ambazo hazijafanya vizuri kabisa.

Kwenye mahojiano na kipindi cha Kikaangoni cha EATV, Aslay amefunguka na kukiri kuwa kuna jitihada anafanya kwa ajili ya kumsaidia msanii mwenzake Ikiwa ni pamoja na kolabo hivi karibuni:

Ndio Enock Bella yupo na ninaongea naye na pia Bado Yupo Kwenye grupu moja kwaiyo bado tuna ukaribu na kuna jitihada tunafanya kwaiyo inshallah siku is nyingi mashabiki wataona kitu kutoka kwetu ingawa siwezi nikakiongelea sana”.

Enock Bella alitangaza kusainiwa kwenye label iliyopo nchini Uganda mwaka jana mwishoni lakini baada ya muda mfupi akatangaza kujitoa.

Aslay Adai Uongo Wa Wanawake Umesababisha Kuyachukia Mapenzi

Staa wa Muziki wa Bongo fleva anayefanya vyema na ngoma yake ya ‘Totoa’ Aslay Isihaka amefunguka na kuweka wazi kuwa hana Mpango wa kuwa Kwenye Mahusiano ya Kimapenzi kwa sasa.

Aslay ambaye mwezi uliopita alitangaza kuachana na aliyekuwa mpenzi wake na mama watoto wake Tessy Chocolate bila kuweka wazi sababu ya wawili hao kuachana.

Tangu Aslay  ameachana na Tessy amedaiwa kuwa kimapenzi na Muigizaji Diana Kimary jambo ambalo hata yeye alithibitisha Lakini hivi sasa Msanii huyo anafai hayataki Tena mapenzi.

Kwenye mahojiano aliyofanya na kituo kimoja cha habari Aslay amefunguka na kuweka wazi kuwa kwa saaa hajali kuhusu kuwa na mwanamke kwani wengi wao ni waongo wanaangalia pesa tu:

Katika vitu ambavyo Sivipi kipaumbele kwa sasa ni Mahusiano na wanawake maana wengi wao hawana mapenzi ya kweli, hawajali maisha ya mtu au hawaamini kuwa fulani amepata leo pesa au amekosa”.

Hivi karibuni kulikuwa na tetesi kuwa Aslay amerudiana na aliyekuwa mpenzi wake Amber Lulu taarifa ambazo Aslay amezikataa na kusisitiza kuwa hana mpenzi kwa sasa na wala hahitaji.

Amber Lulu Akana Tetesi Za Kurudiana na Aslay

Video vixen maarufu ambaye pia ni msanii wa Muziki wa Bongo fleva anayetamba na kibao chake cha ‘Jini kisirani’ Amber Lulu amefunguka na kukamatwa kurudiana na msanii mwenzake Aslay.

Miezi michache nyuma Amber Lulu aliyoa siri ambayo haikujulikana kwa watu wengi kuwa yeye na Aslay walishawahi kuwa wapenzi siku za nyuma kabla hajawa maarufu.

Siku za hivi karibuni baada ya Amber kutangaza kuachana na aliyekuwa mpenzi wake Prezzo na kudai yupo single amesemekana kurudiana na Aslay ambaye pia ameachana na mama watoto wake.

Kwenye mahojiano aliyofanya na Bongo 5, Amber amekana kurudiana na Aslay lakini alionekana kugoma kabisa kuiongelea ishu hiyo:

Mimi sina mahusiano yoyote na Aslay”.

Mapema mwaka huu Kwenye Interview moja aliyofanya Amber alidai katika wanaume Wote aliowahi kuwa nao Aslay ndio amewahi kumridhisha zaidi.

Mashabiki Wamjia Juu Aslay,ni Baada ya Kupata Mwingine Baada ya Tessy

Mashabiki wamemtolea maneno ya kashfa msanii wa muziki wa kizazi kipya anaefanya vizuri na kipaji chake bwana Aslay baada ya kusambaazakatika mitandao ya kijamii picha za mwanamke wake mpya ikidaiwa kuwa wawili hao kwa sasa ni wapenzi.

Mwanadada huyo ambae ametokea bongo movies anaonekana kujiamini kutokana na kuanikwa sana katika mitandao na mwanaume huyo  na kusahau kuwa aslya tatyri alishawahi kuwa na mahusiano na mwanadada mwingine na kupata nae mtoto.

Hata hivyo, mashabiki wameonekena kuchukizwa na maamuzi ya alsya ya kumtangaza mwanamke wake mpya hadharani huku hata mwezi haujapita tangu alipoachana na mama mtoto wake na kumwambia kuwa atapata tabu sana kwa sababu Tessy na diana ni wawili tofauti na watakuja kushindwana tu.

Aslay na Tessy wamedumu katika mahusiano kwa muda mrefu na kubahatka kupata mtoto mmoja na sasa kugombana bila wao wenyewe kuwa wazi ni nini chanzo cha ugomvi huo.

Aslay Ndani Ya Penzi Zito na Mrembo Mwingine

Staa wa muziki wa Bongo fleva anayefanya vizuri na ngoma yake ya ‘Nibebe’ Aslay Isihaka ameweka wazi penzi lake zito na Mrembo ambaye ni Muigizaji wa Bongo movie Diana Kimary.

Wiki chache zilizopita Aslay alithibitisha kuachana na aliyekuwa mpenzi wake Tessy Chocolate  ambaye pia ni mama wa mtoto wake mmoja wa kike anayeitwa Moza.

Aslay na Tessy hawa kuweka wazi sababu za kuachana lakini kila mmoja alisisitiza wameachana kwa wema na hawana chuki baina yao.

Siku ya jana Aslay amemuanika Rasmi mpenzi wake Mrembo Diana Kimary Kupitia ukurasa wake wa Instagram ambapo amemposti mara mbili huku akionyesha wazi kuwa wana Mahusiano zaidi ya urafiki.

Kwenye picha hizo Aslay alisindikiza kwa maneno kama “Mashallah” na “Sasa ndio nini Mke wangu”.

Aslay- Muziki Unanifanya Nakuwa Bize

Staa wa muziki wa Bongo fleva Aslay Isihaka amefunguka na kusema anajiona kama mtu anayeishi kama roboti kutokana na kufanya kazi mfululizo.

Aslay ambaye amekuwa kwenye chati toka aondoke Kwenye kundi lake la Yamoto Band ameendelea kufanya vizuri na nyimbo zake kama Nibebe, Natamba na nyinginezo.

Kwenye mahojiano na Global Publishers, Aslay amefunguka kuwa anaamini muda wa kupumzika kwa mwanadamu ni pale anapoondoka duniani, kwa hiyo kila siku yupo studio, kama siyo studio yupo lokesheni anafanya video na kama siyo lokesheni basi yupo kwenye shoo majukwaani.

Sina muda wa kupumzika, kwa maana ninaamini mtu kupumzika ni pale anapofariki dunia, nafanya kazi kila siku ili kuhakikisha nasonga mbele kwenye maisha yangu”.

Aslay anategemewa kupanda stejini moja na mkali kutoka NIgeria Davido pale next door Arena siku ya tarehe 16 Kwenye 30 Billion concert.