“Siwezi Kutoka WCB, Diamond Ni Mtu Mmoja Poa Sana”-Mose Iyobo

Dansa maarufu kutoka WCB ambaye anafanya kazi kwa Msanii wa Bongo fleva Diamond Platnumz kwa muda mrefu, Mose Iyobo ameibuka na kudai kuwa bosi wake  huyo ni mtu poa sana.

Kwenye mahojiano aliyofanya na kipindi cha Refresh cha Wasafi Tv, Mose Iyobo amefunguka na kusema Bosi Wake Diamond ni mtu poa sana na ni bosi mzuri kufanya naye kazi.

Diamond ni mtu fulani ambaye yupo poa sana yaani Siwezi kusema nitoke pale (WCB) eti niende sehemu nyingine! Labda nikafungue kitu changu mwenyewe”.

Lakini pia Mose Iyobo ametupilia mbali Tetesi Za kuwa analelewa na mzazi mwenzake Aunty Ezekiel na kudai anatengeneza hela nzuri tu kama Dansa wa Diamond hivyo hahitaji kulelewa.

Nalelewaje wakati nafanya kazi kwa Diamond? Nikimwambia Diamond nataka gari Fulani yaani inachukua dakika chache tu”.

 

 

Aunty Ezekiel Ajibu Tetesi Za Kumwagana na Iyobo

Muigizaji wa Bongo movie mrembo Aunty Ezekiel amefungukia tetesi za Kumwagana na baba Watoto Wake ambaye ni mcheza shoo wa Diamond Platnumz, Mose Iyobo.

Katika siku za karibuni kumekuwa na uvumi mwingi ambao umekuwa ukisambaa kuwa wawili hao hawaonekani pamoja kama zamani kwa sababu Penzi Lao limefika ukingoni.

Kwenye mahojiano aliyofanya na Gazeti la DIMBA Jumatano, Aunty Ezekiel amesema kuwa hata ikitokea ameachana na Iyobo itabaki kuwa siri yao Lakini kwa sasa wapo vizuri tu.

Wapo wengi wanaamini sisi hatuwezi kudumu, lakini nataka niwathibitishie kuwa mapenzi yetu yapo salama sana, tumejiwekea mikakati yetu ili kuhakikisha tunaishi kama tunavyotaka na si kama wengine wanavyotaka na hata ikitokea tukiachana naamini itabaki siri ya sisi wawili“.

Aunty Ezekiel amesema moja ya mipango yake kwa sasa ni kuongeza mtoto kwa kuwa ni wakati sahihi kwake na mwenzake kufanya hivyo, kama ambayo walikuwa wamepanga toka awali.

“Mimi na Aunty Ni Wanandoa Bado Sherehe Tu”- Iyobo

Mpenzi wa Msanii wa filamu za Bongo movie Aunty Ezekiel, Mose Iyobo ameibuka na kuweka wazi kuwa yeye na mama Watoto Wake Aunty Ezekiel ni Kama wanandoa bado kufanya sherehe tu.

Mose Iyobo ambaye ni mcheza shoo wa Diamond Platnumz amesema kuwa watu wamekuwa wakimuuliza sana lina atafunga ndoa na Aunty Ezekiel Lakini yeye anaona wao wawili ni kama wanandoa tayari kilichobaki ni kufanya harusi tu.

Kwenye mahojiano aliyofanya na Global Publishers Mose Iyobo aliulizwa ni lini atafunga ndoa na Aunty ambaye tayari Ameshazaa naye Mtoto mmoja ambaye anaitwa Cookie:

Kwa jinsi tunavyoishi ni ndoa tayari kwa sababu tunakaa pamoja, Mungu ametujalia mtoto mzuri (Cookie), yaani sisi ni kama wanandoa bado sherehe tu ambayo muda wowote tutafanya wala haina haraka“.

Lakini pia Iyobo amekataa kabisa tetesi zilizosambaa kwenye Mitandao ya kijamii kuwa yeye na Aunty wameachana:

Mimi na Mama Cookie hatujawahi kuachana ila tumeshawahi kupishana kauli zaidi ya mara mbili na huwa tunamaliza tofauti zetu wenyewe na maisha yanaendelea“.

 

“Nipo Tayari Kuzaa na Mtoto Mwingine”-Aunty Ezekiel

Muigizaji wa Bongo movie Aunty Ezekiel ameibuka na kuweka wazi mipango yake kuzaa Mtoto mwingine baada ya binti yake ambaye Hivi sasa ana umri wa miaka minne.

Aunty Ezekiel na Mpenzi wake ambaye ni mnenguaji kutoka label ya WCB, Mose Iyobo, amesema sasa ni wakati wake wa kuongeza mtoto mwingine endapo mipango ya Mungu itatimia.

Kwenye mahojiano aliyofanya na Gazeti la DIMBA, Aunty Ezekiel amesema kuwa anaona wakati umefika wa kuongeza mtoto wake wa pili:

Nadhani sasa ni wakati sahihi wa kupata mdogo wake Cookie, najua kila kitu ni mipango ya Mungu na hata hili litatimia kwa uwezo wake, nilipanga kuwa na watoto zaidi ya wawili na naamini inawezekana, kama mambo yatakwenda vizuri wakati wowote nitakuwa tayari kwa hilo“.

 

Mose Iyobo Afungukia Mipango Ya Ndoa Na Aunty Ezekiel

Dansa maarufu wa staa Diamond Platnumz, Mose Iyobo ambaye pia ni Mpenzi na mzazi mwenzake ambaye pia ni staa wa Bongo movie nchini Aunty Ezekiel.

Iyobo amesema kuwa hana muda wa kukaa na kusikiliza watu wanasema nini kwenye mitandao ya kijamii kuhusu mapenzi yake na Aunty kwani anampenda na lazima atamuoa tu.

Kwenye mahojiano aliyofanya na Gazeti la Risasi Jumamosi, Iyobo alisema wapo watu wanaotamani siku moja waachane lakini anajua ni kitu ambacho hakiwezi kutokea kwa kuwa mizizi ya penzi lao imekwenda chini sana.

Mimi natarajia kumuoa Aunt kwani ana kila sifa ya kuwa mke wangu, na nitakuwa mfano bora kwa mastaa wote na kuondoa ile dhana kuwa mastaa hawadumu kwenye ndoa”.

Hivi karibuni kulikuwa na tetesi kuwa penzi la wawili hao limeingia doa Baada ya kutoonekana pamoja kwa muda mrefu na kusemekana kuwa wameachana.

Nipo Tayari Kuzaa Watoto Wanne na Iyobo-Aunty Ezekiel

Muigizaji wa Bongo movie na Mfanyabiashara Aunty Ezekiel amefunguka na kuweka wazi mahusiano yake na Mpenzi Wake ambaye ni dansa wa WCB Mose Iyobo.

Aunty na Iyobo wamefanikiwa kuzaa Mtoto mmoja wa kike anayeitwa Cookie ambapo kwenye mahojiano yake na Global Publishers, Aunty ameweka wazi sababu za kumpa binti yake jina la Cookie.

Unajua maana ya Cookie ni vibiskuti vile vidogo, lakini vitamu sana, sasa nilipomzaa tu niliona nimepata kitu kitamu sana kuliko chochote hapa duniani, nikaamua tu kumpa mtoto wangu jina hilo kumuonesha kwamba yeye kuwa mwanangu ni utamu tosha kwangu”.

Lakini pia Aunty Ezekiel alisema Kama walivyokuwa wazazi wengi ana mipango mingi juu ya binti yake huyo hasa inapokuja Suala la elimu yake:

Nimepanga aje kuwa msomi huko mbeleni na ndiyo maana nimetenga pesa zake nyingi tu za kumsomesha sasa hivi mpaka darasa la saba bila bugudha yoyote alafu nyingine ya kuendelea na masomo ndiyo nimeanza kuweka sasa“.

Alipoulizwa kuhusu kuongeza mtoto mwingine na baba watoto wake huyo Aunty aliweka wazi kuwa yupo tayari kuwa na watoto wengine watatu lakini endapo tu muda maalumu utafika:

Natamani sana, lakini bado kidogo, kuna vitu navikamilisha alafu ndiyo nifikirie kuzaa mtoto mwingine, siyo mmoja hata watatu kwa sababu mimi napenda sana watoto”.

 

Aunty Ezekiel na Mose Iyobo Wadaiwa Kutibuana Mtwara

Muigizaji wa Bongo movie na Mjasiriamali Aunty Ezekiel amedaiwa kutibuana na Mpenzi Wake ambaye pia ni baba Watoto Wake dansa kutoka WCB Moses Iyobo.

Sakata kati ya wawili hao lilichukua nafasi mkoani Mtwara ambapo Aunty Ezekiel aliambatana na timu nzima ya WCB kwa ajili ya kufanya tamasha la Wasafi Festival.

Gazeti la Ijumaa Wikienda linaripoti kuwa Aunty Ezekiel na Iyobo walizua sintomfahamu baada ya kudaiwa kufikia hoteli tofauti na kuwa wanapishana bila kusalimiana. Kufuatia hali hiyo mmoja wa watu wa ndani wa Wasafi aliling’ata sikio Ijumaa Wikienda kuwa, wawili hao hawakuwa sawa kwani walikuwa wametibuana.

Hata hivyo, baada ya wawili hao kuwekwa chini na watu wazima waliokuwa kwenda msafara huo, wawili hao hatimaye walionekana pamoja katika mapozi ya kimahaba, hali iliyoonesha mambo kukaa sawa huku wakionekana wakiongea kwa muda mrefu.

Baada ya sakata hilo gazeti hilo lilimsaka Mose Iyobo kwa mahojiano zaidi ambapo alikana tuhuma hizo na kufunguka:

Nani amesema tumetibuana? Siwezi kuongelea hilo tafadhali ni mambo binafsi na yatabaki hivyo,”.

Aunty Ezekiel na Iyobo wamekuwa wakiandamwa na tetesi za kuachana kwa miezi kadhaa sasa juju chanzo kikisemekana kuwa Iyobo na michepuko nyingi.

 

Wanaosema Nimeachana na Iyobo Watasubiri Sana- Aunty Ezekiel

Msanii wa filamu za Bongo movie Aunty Ezekiel amefunguka kuhusu mahusiano yake na Mpenzi Wake ambaye ni dancer wa WCB Moses Iyobo.

Aunty Ezekiel amefunguka na kuweka wazi kuwa amekuwa akishangazwa na tetesi zinazosambaa kwenye mitandao ya kijamii hivi sasa kuwa yeye ameachana na Baba watoto wake Mose Iyobo.

Kwenye mahojiano aliyofanya na Gazeti la Ijumaa, Aunt alisema afikiri katika dunia hii hata kama unapenda na mtu kwa kiasi gani hamuwezi kuishi bila kutokea ugomvi wowote kwa sababu wao sio malaika lakini wanapogombana wanayamaliza na maisha yanaendelea kama kawaida lakini inavyoonekana kuna watu wanataka kuona penzi lao likisambaratika kabisa.

Nafikiri wanaosema tumeachana watasubiri sana kama kugombana hakuna wanaoishi kama malaika, kwa sababu wote ni binadamu lakini hatuna ugomvi endelevu, yule ni mzazi mwenzangu na wanaosubiri tuachane tutawaacha mbali sana”.

Tetesi za Aunty Ezekiel na Mose kuachana Zilianza mara Baada ya wawili hao kutoonekana kwenye mitandao ya kijamii pamoja na zilipamba moto zaidi Baada ya Aunty kumuacha Mose Tanzania alipoenda kusheherekea birthday yake Dubai.

Aunty Ezekiel Atamba Kuwa Hodari Wa Mapenzi

Muigizaji wa Bongo movie na mfanyabiashara Aunty Ezekiel amefunguka na kujitambia kuwa yeye ni hodari wa mapenzi na kujisifia kuwa anapokuwa na mwanaume basi anafanikiwa kabisa kumtuliza na kuwa wake peke yake.

Kwenye mahojiano aliyofanya na gazeti la Risasi JumamosiAunty alisema kuwa linapokuja suala la kumpenda mtu hata akiwa na nani atamuachia tu kwani anajijua ni hodari wa kuondoa wote waliokuwa kwenye himaya hiyo.

Siwezi kuanika moja kwa moja ninafanya nini na kwa nini wakiwa kwangu hawafurukuti, lakini najua wazi kuwa nina sifa hiyo na sijawahi kushindwa kwenye hilo”.

Hivi sasa Aunty yupo kwenye mahusiano na Baba watoto wake dancer Mose Iyobo ambaye ameshawahi kukiri kuwa siku za nyuma wakati wanaanza mahusiano alikuwa na wanawake kadhaa lakini tangu yuko naye ametulia na yeye peke yake.

 

“Sijawahi Kufikiria Kuhusu Kufunga Ndoa na Iyobo”- Aunty Ezekiel

Muigizaji wa Bongo movie Aunty Ezekiel amefunguka na kudai hajawahi hata kuwaza Kuhusu kufunga ndoa na mpenzi wake Mose Iyobo.

Aunty Ezekiel amekuwa kwenye mahusiano ya kimepenzi na dancer wa Diamond Platnumz, Mose  Iyobo kwa miaka zaidi ya mitatu na kuzaa naye mtoto mmoja wa kike, Cookie.

Kwenye mahojiano na gazeti la Amani, Aunty amesema kuwa siyo kwamba mtu akifunga ndoa ndiyo anaweza kuishi vizuri na mwanaume wake, bali ni kwamba anachojua kuishi vizuri ni sifa moja kubwa ya kuendelea kuwa pamoja ni kupeana heshima na kila mmoja kutambua anachokifanya.

Mimi sitaki hata kukuficha wala sijawahi kufikiria kufunga ndoa na Iyobo leo wala kesho kikubwa tunaishi vizuri na tunalea mtoto wetu ipasavyo hilo ndilo ninalolitaka na si vinginevyo kwani kuolewa siyo ishu kikubwa malezi ya mtoto tu”.

Aunty Ezekiel ameshawahi kufunga ndoa miaka ya nyuma na mwanaume anayeitwa Demonte ambaye anasemekana mpaka sasa yupo jela kwa kuuza madawa ya kulevya.

Wema Alinifanya Nimjue Iyobo ;-Aunty Ezekiel

Mwanadada Aunty Ezekiel amefunguk na kueleze ajinsi alivyokuta na mzazi mwensie moze iyobo mabae mpaka sasa wapo wote na wamekuwa pamoja katika kujenga familia.

Aunty anasema kuwa katika watu wakiosababisha mahusiano yake na moze kuendelea ni wema sepetu kutokana na ukweli kuwa kama asingekuwa na urafiki na wema na akawa anenda kwa wema bai asingekutana kabisa na Iyobo.

Aunty anasimulia na kusema kuwa alianza kukutana na Moze siku moa alipowenda kumtembelea rafiki yake kipenzi wema ndipo awalipokuata na kubadilishana namba za simu.

miaka kadhaa iliyopita nilikwenda siku moja nyumbani kwa Wema na ndipo nilipokutana na kiana mmoa hivi, yes ndio Iyobo huyo.kwakweli sikujua kama tutakuwa wapenzi lakini tulibadilishana namba za siku na ndipo tulipoanza kuwasiliana.

kipindi icho sikuwa na mahusiano  na moze aliaribu kutupa ndoana na mimi nilikataa si unajua tena wanawake , lakini baadae tulikubaliana na nikapata ujauzito.

 

 

Aunty Ezekiel Afungukia Mipango Ya Ndoa na Iyobo

Muigizaji wa Bongo movie na mjasiriamali Aunty Ezekiel amefungukia mipango ya ndoa yake na mpenzi wake na Baba watoto wake Mose Iyobo.

Aunty ameweka wazi kuwa siri kubwa ya Mahusiano Yake na Mose Iyobo kudumu kwa muda mrefu ni kuheshimiana, kusikilizana na kutoleteana ustaa wanapokuwa nyumbani.

Kwenye mahojiano aliyofanya hivi karibuni na kituo kimoja cha habari, Aunty amefungukia mipango ya ndoa na Iyobo:

Mamboya ndoa mwanaume ndio anayeamua, Lakini pia kufunga ndoa ni makaratasi tu kikibwa ni jinsi gani unaishi na mpenzi wako na mna maelewano kwa kiasi gani”.

Lakini pia Aunty ameweka wazi kuwa pamoja na kwamba yeye na Iyobo wana uhusiano mzuri lakini wamepitia mambo magumu kwani ameshawahi kumfumania na mwanamke mwingine Lakini pia amekiri ameshawahi kukutwa na meseji za mwanaume mwingine.

Moze ni Upande Wangu Mwingine, Lazima Nimfatilie-Aunty Ezekiel.

Msanii wa bongo fleva na mjasiliamali Aunty eEzekiel amefunguka  na kutoa sababu kubwa inayomfanya awe anafatilia kila kinachosemwa katika mitandao ya kijamii kuhusu moze iyobo ambae ni baba wa mtoto wake wa kike.Aunty anasema kuwa Moze ni boyfriend wake na upande wake wa pili hivyo ni lazima afatilie kwa sababu kuna baadhi ya vitu vinaweza kutokea na kumuathiri hata yeye pia.

Mose ni boyfriend wangu , ni mtu ambae naishi nae ,so lolote linaweza kutokea katika mitandao siku yoyote na kwa sababu ni upande wangu mwingine ninaweza kusema, na kila kinachotokea inakuwa kinanihusu hata mimi pia so ishu yoyote hata mimi inanihusu.

Pia Aunty amezungumzia swala la yeye kutoa movie yake mpya hivi karibuni inayokwenda kwa jina la mama ambayo amecheza na mwane wa kike Cookie ambapo amecheza kama mtoto wake.

Aunty anasema kuwa kutokana na hadhi ayke katika tasnia ameona ni bora kucheza short film hiyo kwa sababu sasa hivi yeye ni mama hivyo anataka kuwaonyesha watu matatizo wamama wanapiatia hasa katika mazingira magumu.Hivi karibuni kulisambaa picha za aunty akiwa na mtoto wake mgongoni , na kusemekana kuwa wanatoa movie mpya hivyo yeye mwenyewe amethibitisha hilo.

 

Tunda Amuomba Msamaha Aunty Ezekiel Baada Ya Kumtukana Mtoto Wake

Video vixen na Socialite maarufu Tunda Sebastian amefunguka na kumuomba radhi msanii wa Bongo movie Aunty Ezekiel baada ya kumtukana mtoto wake na Mose Iyobo, Cookie.

Miezi michache iliyopita kulizuka bonge valangati baada ya Aunty Ezekiel kumuashia dude Tunda ambapo alienda kwenye ukurasa wake instagram na kumdai pesa yake aliyomkopesha pombe dukani kwake.

Baada ya hapo walianza kurushiana maneno ya kejeli na matusi hata Tunda alifikia hatua ya kumtukana mtoto wa Aunty Ezekiel ambapo alimuita mtoto wake kuwa ni mtoto mbaya dunia nzima.

Wikiendi iliyopita Tunda amemuomba msamaha Aunty Ezekiel kwa kumtukania mtoto wake na kudai kuwa zilikuwa ni hasira tu na hakupanga kumtukana mtoto wao.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram Tunda alimuandikia Aunty ujumbe huu:

 

Kwa kipindi kirefu Kumekuwa na tetesi kuwa Tunda ni mjamzito na alithibitisha kuwa ni mjamzito kwa kuandika “Naomba msamaha kama mwanamke ambaye nitaitwa mama pia soon”. 

Kwa habari za chini ya kapeti zinadai kuwa ujauzito huo ni wa miezi mitatu na inasemekana kuwa baba wa mtoto huyo ni mtangazaji za Clouds Tv Casto Dickson ambaye ni Baba mtoto wa Munalove ambaye ni rafiki wa Tunda.

SHILAWADU Wachezea Kipigo Kitakatifu Kutoka Kwa Mose Iyobo

Shirika la Wambe Duniani (SHILAWADU) ni kipindi kinachorushwa na kituo cha televisheni cha Clouds TV ambacho kinaongelea habari za kimbea kuhusiana na mastaa mbali mbali wa Bongo.

Kipindi hiko kina watangazaji wawili ambao ni Soudy Brown na qwisar. Vijana hao wawili usiku wa Jana walijikuta katika wakati mgumu baada ya kuambulia kipondo kitakatifu kutoka kwa mcheza shoo kutoka WCB Mose Iyobo.

Siku chache zilizopita Tunda na Aunty Ezekiel pamoja na Iyobo waliingia kwenye vita ya maneno baada ya kudaiana chupa ya pombe ya iliyokuwa ina thamani ya tshilingi laki moja. Inadaiwa kuwa Tunda alikopa chupa hiyo na kushindwa kuilipa kwa wakati halo iliyosababisha Aunty Ezekiel kumwashia moto Instagram.

Inadaiwa baada ya sakata hili Shilawadu walifika Dukani kwa Aunty Ezekiel ili wamhoji lakini waliambulia kipigo, Mange Kimambi kaandika taarifa hiyo kama ifuatavyo:

Mose Iyobo kawapa kichapo Shilawadu unaambiwa bonge la ugomvi fujo hapo Dukani kwa Aunty Kinondoni, watu ndio wakaja kuamua na wakashindwa kumhohi Iyobo unaambiwa Qwisar kala vichwa viwili vya kijeshi, Soudy kala mtama double double alikuwa anageukia hewani, basi Shilawadu walijua wanaenda dukani wakamhoji Aunty kumbe yupo China”.

Baada ya sakata hilo time nzmia ya Shilawadu imeachia ujumbe huh kwenye mitando ya kijamii kuhusu kizaazaa hiko;

Kazi yetu ina changamoto kubwa sana, asilimia kubwa ya mastaa wanatuunga mkono, kwa kufanya maamuzi wanayoyataka kulingana na moods wanazokuwa nazo tunapowafata bila kutudhuru. Usiku wa leo tulipokuwa kazini mwagwa damu na mtu tuliyeenda kufanya naye mahojiano kati yetu kuna walioumia mikono, viuno n.k kuna uharibifu wa vifaa vyetu vya kazi umetokea wenzetu wanaendelea na matibabu Mungu ni mwema na hili nalo litapita, bado tuna wasiwasi Kama mhusika atakuwa anaendelea kututafuta atudhuru zaidi. Tunasikitishwa na matumizi makubwa ya nguvu dhidi yetu sisi wanyonge wa Shilawadu”.

Mose Iyobo na Tunda Warushiana Maneno Kisa Pombe

Dancer maarufu kutoka keen he label ya WCB, Mose Iyobo ameingia kwenye vita ya maneno na matusi na mrembo Tunda baada ya kutuhumiwa kuzulumu shilingi laki moja ya pombe ya Belaire.

Siku ya jana Aunty Ezekiel alianzisha kizaazaa na Tunda baada ya kuingia kwenye ukurasa wake wa Instagram na  kumdai pesa taslimu shilingi laki moja ambayo alimkopeshea pombe anzouza aina ya Beleire.

Lakini baada ya kudaiwa pesa hizo mara kadhaa Tunda alidai kuwa alipoenda kuilipia chupa hiyo Dukani kwao Aunty Ezekiel hakuwepo hivyo mtu aliyekuwepo alikuwa ni Iyobo ambaye ndiye aliyemkabidhi pesa hizo lakini alishangaa alipokutana na Aunty juzi akamdai wakati alishampa mumewe Iyobo.

Baada ya kuambiwa maneno hayo Iyobo aling’aka vibaya mno na kukana tuhuma hizo na kusisitiza kuwa hakupewa pesa hizo ndipo alipomtolea povu zito Tunda ambapo kupitia ukurasa wake wa Instagram aliandika maneno haya:

Ujinga nikubishana na mtu ambaye ameshafanya mambo yote ambayo wewe unafanya leo kama marudio unachotakiwa useme ni sina hiyo hela ntalipa siku fulani na sio kuanza kuongea ushamba  hawezi kutafuta kiki kwako ana mtoto maarufu kushinda wewe alafu kingine benten ni baba yako aliyekuzaa akashindwa kukupeleka shule umeishia kufumuliwa free unakosa laki ya kununulia pombe”.

Baada ya kutolewa povu hilo na Iyobo na Tunda naye alifunguka yaliyo moyoni mwake na kumjibu ambapo alimwandikia ujumbe huu :

Alafu na wewe Mose unakaa chini unaandika upuuzi kama huo kama ni kweli ni wewe umeandika basi huna Uso wa haya! Sasa nakuuliza swali moja tu kwa nini ulinoblock kukupigia kipindi Aunty ameanza kuniuliza kuhsu hela? Sikilizeni nyie hebu nitoleeni upuuzi wenu watu wazima mliokosa busara na akili kabisa yaani mimi nigombane na nyie Kisa laki moja? Kiukweli hata kama ningekuwa sina pesa siwezi kukosa laki “.

Lakini unakumbuka pale ambapo Mose aliposema mwanangu Cookie maarufu kuliko we we? Basi Funds alifika mbali katika ugomvi huo na kumuingiza mtoto wao kwa kumuita mtoto mbaya Tanzania nzima.