Aunty Ezekiel Awatolea Povu Wanaosema Mwili Wake

STAA mwenye mvuto Bongo Muvi, Aunt Ezekiel amefungukia ‘tatuu’ aliyoichora pajani kuwa anashangaa watu wanavyoijadili alichoraje kwani kwake ni kitu cha kawaida tu.

Akizungumza na Za Motomoto, Aunt alisema kwanza hiyo tatuu siyo halisi ameichora kwa piko ila watu wanavyomjadili amewezaji kufunua paja kuchora na wakati kuna watu wanaochora sehemu tofauti na za kushangaza.

Aunty anasema kuwa kuchra mchoro kama huo ni kitu cha kawaida sana hivyo anaomba watu wampumzishe kwa sababu kuna watu wanafanya makubwa kuliko hata yale anayoyafanya yeye na hakuna wanaow-judge.

Nawashangaa sana wanaojadili paja langu sijui wanachotaka ni kitu gani, kwanza hapa nimejichora tu na piko lakini kingine wameona kujichora hivi kama kitu kisicho cha kawaida inashangaza kwa kweli waniache na maisha yangu,” alisema Aunt.

Aunty Ezekiel Afungukia Tattoo Yake Ya Paja

Muigizaji wa Bongo movie Aunty Ezekiel amefunguka na kumwaga povu zito kutokana na maswali ambayo amekuwa akipata baada ya kuanika tattoo yake mpya ya paja.

Siku chache zilizopita Aunty alivaa nguo fupi na Kujiweka kwenye Mitandao ya kijamii na kwenye paja lake la mguu wa Kulia alionekana akiwa na tattoo kubwa iliyozua maswali.

Kwenye mahojiano aliyofanya na Gazeti  La Ijumaa, Aunty alisema kwanza hiyo tatuu siyo halisi ameichora kwa piko ila watu wanavyomjadili amewezaji kufunua paja kuchora na wakati kuna watu wanaochora sehemu tofauti na za kushangaza.

Nawashangaa sana wanaojadili paja langu sijui wanachotaka ni kitu gani, kwanza hapa nimejichora tu na piko lakini kingine wameona kujichora hivi kama kitu kisicho cha kawaida inashangaza kwa kweli waniache na maisha yangu“.

 

 

Iyobo Nae Akanusha Kuachana na Aunty

Ikiwa ni siku chache sana zimepita tangu mwanadada Aunty Ezekeiel kuonga ktaika vymbo vya habari na kukanusha tetesi zinazosambaa juu yao kuhusu swala la kuachana na baba wa mtoto wake hatimaye pia baba huyo amefunguka na kuongea jambo kuhusu swala hilo.

Moze iyobo ambae ni mpenzi wa aunty ezekiel amefunguka na kusema kuwa hawajawahi kuachana na mwanamke wake ingawa kumekuwa na maneno mengi hapo katikati kutokana na wao kutokuwa wakionekana pamoja kwa sasa .

Hata hivyo Iyobo amefunguka na kusema kuwa kutoana na mfululizo wa matukio ya kazi imekuwa ngumukwao kuonekana pamoja lakini kamwe hawezi kuachana na mwanamke wake.

Mose anasema kuwa wataka wasubir sana kuona yeye akiachana na Mama Cookie kwa sasa wao bado wapo sana na hakuna wa kuwaachanaisha ingawa wamekuwa wakigomaba na kukwaruzana lakini hawzwezi kuachana hata mara moja.

kwa mujibu wa habari za kunyapia nyapia ni kwamba wawili hao walishindwa kuelewana baada ya aunty kukuta smsm za kimapenzi katika simu ya mzazi mwenzie, na imekuwa kitu kisichovumilika.

Aunty Ezekiel Ajibu Tetesi Za Kumwagana na Iyobo

Muigizaji wa Bongo movie mrembo Aunty Ezekiel amefungukia tetesi za Kumwagana na baba Watoto Wake ambaye ni mcheza shoo wa Diamond Platnumz, Mose Iyobo.

Katika siku za karibuni kumekuwa na uvumi mwingi ambao umekuwa ukisambaa kuwa wawili hao hawaonekani pamoja kama zamani kwa sababu Penzi Lao limefika ukingoni.

Kwenye mahojiano aliyofanya na Gazeti la DIMBA Jumatano, Aunty Ezekiel amesema kuwa hata ikitokea ameachana na Iyobo itabaki kuwa siri yao Lakini kwa sasa wapo vizuri tu.

Wapo wengi wanaamini sisi hatuwezi kudumu, lakini nataka niwathibitishie kuwa mapenzi yetu yapo salama sana, tumejiwekea mikakati yetu ili kuhakikisha tunaishi kama tunavyotaka na si kama wengine wanavyotaka na hata ikitokea tukiachana naamini itabaki siri ya sisi wawili“.

Aunty Ezekiel amesema moja ya mipango yake kwa sasa ni kuongeza mtoto kwa kuwa ni wakati sahihi kwake na mwenzake kufanya hivyo, kama ambayo walikuwa wamepanga toka awali.

Warembo Wa Bongo Movie Wataja Siri Za Bata Za Dubai

Wasanii wanaosumbua katika tasnia ya Bongo movie warembo Aunty Ezekiel na Halima Yahaya maarufu kama Davina wamefunguka na kuanika Siri ya wao kula bata ndefu nchini Dubai.

Davina ameweka wazi kuwa siri kubwa ya wao kuweza kujihudumia na kula bata ndefu Dubai ni Faida za vikoba ambavyo wamekuwa wakijiwekea akiba kwa muda mrefu.

Kwenye mahojiano aliyofanya na Mtandao wa Global Publishers, Davina  alisema watu wasishtuke sana kwa bata hizo kwani Vikoba vyao vina mpango wa kuwapeleka wanachama wake sehemu mbalimbali duniani hivyo wao bata lao wamekwenda kulila Dubai.

Unajua watu wakituona tunakula bata kama hizi wanakimbilia kudhani tumewezeshwa na wanaume, hapana! Na hii naipigia mstari kwa sababu naujua ukweli, sisi tunawezeshwa na mfuko wetu wa Vikoba ambao una maendeleo makubwa na kwa mwaka huu watu wategemee makubwa kwani tuna filamu ambayo tutaicheza pia”.

Wasanii hao wametaja siri yao hiyo kutokana na tetesi zilizosambaa kwenye Mitandao ya kijamii kuwa kuna pedeshee mmoja ambaye amesimamia kuona warembo hao wanakula maisha.

“Nipo Tayari Kuzaa na Mtoto Mwingine”-Aunty Ezekiel

Muigizaji wa Bongo movie Aunty Ezekiel ameibuka na kuweka wazi mipango yake kuzaa Mtoto mwingine baada ya binti yake ambaye Hivi sasa ana umri wa miaka minne.

Aunty Ezekiel na Mpenzi wake ambaye ni mnenguaji kutoka label ya WCB, Mose Iyobo, amesema sasa ni wakati wake wa kuongeza mtoto mwingine endapo mipango ya Mungu itatimia.

Kwenye mahojiano aliyofanya na Gazeti la DIMBA, Aunty Ezekiel amesema kuwa anaona wakati umefika wa kuongeza mtoto wake wa pili:

Nadhani sasa ni wakati sahihi wa kupata mdogo wake Cookie, najua kila kitu ni mipango ya Mungu na hata hili litatimia kwa uwezo wake, nilipanga kuwa na watoto zaidi ya wawili na naamini inawezekana, kama mambo yatakwenda vizuri wakati wowote nitakuwa tayari kwa hilo“.

 

Nipo Tayari Kuzaa Watoto Wanne na Iyobo-Aunty Ezekiel

Muigizaji wa Bongo movie na Mfanyabiashara Aunty Ezekiel amefunguka na kuweka wazi mahusiano yake na Mpenzi Wake ambaye ni dansa wa WCB Mose Iyobo.

Aunty na Iyobo wamefanikiwa kuzaa Mtoto mmoja wa kike anayeitwa Cookie ambapo kwenye mahojiano yake na Global Publishers, Aunty ameweka wazi sababu za kumpa binti yake jina la Cookie.

Unajua maana ya Cookie ni vibiskuti vile vidogo, lakini vitamu sana, sasa nilipomzaa tu niliona nimepata kitu kitamu sana kuliko chochote hapa duniani, nikaamua tu kumpa mtoto wangu jina hilo kumuonesha kwamba yeye kuwa mwanangu ni utamu tosha kwangu”.

Lakini pia Aunty Ezekiel alisema Kama walivyokuwa wazazi wengi ana mipango mingi juu ya binti yake huyo hasa inapokuja Suala la elimu yake:

Nimepanga aje kuwa msomi huko mbeleni na ndiyo maana nimetenga pesa zake nyingi tu za kumsomesha sasa hivi mpaka darasa la saba bila bugudha yoyote alafu nyingine ya kuendelea na masomo ndiyo nimeanza kuweka sasa“.

Alipoulizwa kuhusu kuongeza mtoto mwingine na baba watoto wake huyo Aunty aliweka wazi kuwa yupo tayari kuwa na watoto wengine watatu lakini endapo tu muda maalumu utafika:

Natamani sana, lakini bado kidogo, kuna vitu navikamilisha alafu ndiyo nifikirie kuzaa mtoto mwingine, siyo mmoja hata watatu kwa sababu mimi napenda sana watoto”.

 

Aunty Ezekiel Afungukia Tetesi Za Kufungwa Kwa Pub Yake Kisa Kodi

Muigizaji wa Bongo movie na Mfanyabiashara maarufu Aunty Ezekiel amefungukia tetesi za kufungwa pub yake Baada ya kushindwa kulipia kodi.

Kumekuwa na tetesi kwenye Mitandao ya kijamii kuwa Pub ambayo ilikuwa inamilikiwa na Aunty Ezekiel iliyopo maeneo ya Kinondoni imefungwa kutokana na mwanamama huyo kukosa kodi.

Kwenye mahojiano aliyofanya na Gazeti la Risasi Jumamosi, Aunty alisema siyo kwanza amefunga Pub yake kwa sababu ya kudaiwa kodi bali eneo hilo anataka kufanya biashara nyingine na hiyo ya pub ataihamishia sehemu nyingine.

Kwa nini nidaiwe kodi wakati nina biashara nyingine nafanya na zinaenda vizuri? Watu huongea vitu ambavyo hawavijui kabisa, nafanya marekebisho ili niweke biashara nyingine na hii nitaihamishia sehemu nyingine”.

Mbali ya Aunty Ezekiel kumiliki Pub hiyo Lakini pia anamiliki sabuni ya Murua ambazo amesema zinauza vizuri sana.

 

Nisha Amfanyia MwanayeBonge La Party Nchini China

Muigizaji wa Bongo movie na Msanii wa Bongo fleva Salma Jabu maarufu Kama Nisha amekiri kumfanyia bonge la party nchini China binti yake mwenye umri a miaka 14.

Kwenye mahojiano aliyofanya na Global Publishers, Nisha amekiri kumfanyia party hiyo binti yake  huyo anayeitwa Ipsum kwa sababu ndiye kila kitu kwake kwani anaye huyo pekee hivyo anamfanyia kile kitu kinachomfurahisha maishani mwake ili afurahie uwepo wake.

Mwanangu nimemfanyia sherehe ya bethidei China ambayo imegharimu milioni nane, tumekuja kufanya huku maana ndipo alipopachagua nami kwa kuwa nampenda na ndiye mwanangu wa pekee nikamleta na amefurahi sana na anajivunia kuwa na mama kama mimi pia nafurahi kuwa na mtoto mkubwa hivi kwa sasa“.

Mastaa wengi wameonekana kwenda nje ya nchi na watoto wao na kufanya mambo ya kufuru ambapo Wiki chache zilizopita Aunty Ezekiel na yeye alimbeba binti yake Cookie na kwenda kufanya naye bonge la party nchini Dubai.

Wema- Aunty Ndiye Rafiki Pekee Ambaye Hanichoki

Muigizaji wa filamu za Bongo movie Wema Sepetu amedai rafiki yake Aunty Ezekiel ndiye rafiki pekee ambaye amekuwa naye bega kwa bega Bila kuchoka katika hiko kipindi kigumu anachopitia.

Wiki chache zilizopita Wema Aliibua gumzo zito mara Baada ya kuachia video za faragha akiwa na mpenzi wake kwenye mitandao ya kijamii jambo lililomuingiza katika matatizo.

 

Wema Sepetu amefunguka na kudai rafiki yake wa kweli ni  Aunt Ezekiel kwani hajawahi kumchoka na kumtenga kama wafanyavyo wengine na kusisitiza kuwa kuwa ana marafiki wengi lakini baadhi ni wanafiki ila Aunt ana upendo wa kweli kwake.

Nimegundua kuwa rafiki wa kweli kwangu ni Aunt, amenipa faraja ya kweli kipindi chote cha matatizo, naamini ana upendo na mimi”.

Baada ya kuingia katika sakata hilo wasanii kadhaa walimgeuka na kutaka apewe adhabu ambayo itamfanya asirudie makosa hayo huku wengine wakiwa Upande wake.

Aunty Ezekiel Atamba Kuwa Hodari Wa Mapenzi

Muigizaji wa Bongo movie na mfanyabiashara Aunty Ezekiel amefunguka na kujitambia kuwa yeye ni hodari wa mapenzi na kujisifia kuwa anapokuwa na mwanaume basi anafanikiwa kabisa kumtuliza na kuwa wake peke yake.

Kwenye mahojiano aliyofanya na gazeti la Risasi JumamosiAunty alisema kuwa linapokuja suala la kumpenda mtu hata akiwa na nani atamuachia tu kwani anajijua ni hodari wa kuondoa wote waliokuwa kwenye himaya hiyo.

Siwezi kuanika moja kwa moja ninafanya nini na kwa nini wakiwa kwangu hawafurukuti, lakini najua wazi kuwa nina sifa hiyo na sijawahi kushindwa kwenye hilo”.

Hivi sasa Aunty yupo kwenye mahusiano na Baba watoto wake dancer Mose Iyobo ambaye ameshawahi kukiri kuwa siku za nyuma wakati wanaanza mahusiano alikuwa na wanawake kadhaa lakini tangu yuko naye ametulia na yeye peke yake.

 

Aunty Ezekiel Amwaga Mamilioni Kusheherekea Birthday Yake Dubai

Muigizaji wa Bongo movie mrembo Aunty Ezekiel anadaiwa kumwaga mamilioni ya pesa kwa ajli ya tu ya kuweza kusheherekea birthday yake nchini Dubai.

Global Publishers wanaripoti ya kwamba Aunty hakwenda peke yake Dubai bali aliambatana na mwanaye Cookie pamoja na ndugu zake watatu ambapo wameonekana wakiponda raha katika viwanja mbalimbali nchini humo.

Kwenye mahojiano na Gazeti la Risasi Mchanganyiko kwa njia ya simu kutoka Dubai, Aunty alianza kwa kusema kuwa, ameamua kufanya sherehe hiyo ya kuzaliwa nje ya nchi ikiwa ni moja ya kufurahia kutimiza miaka 30 akiwa tayari na mtoto wake.

Nilipenda hii iwe ya tofauti kidogo na nilihitaji kufurahi na familia pekee ndiyo maana niliondoka na vijana wangu wawili na mdogo wangu pamoja na mtoto wangu kwa kweli nimeifurahia sana.

Lakini kwa mahesabu ya haraka haraka nauli za watu wanne pamoja na mtoto wangu Cookie inakaribia shilingi milioni tano, gharama za hoteli ni shilingi milioni nne na ushee na kuhusu sherehe hiyo kwa maana ya vyakula na vinywaji  haikuwa kubwa sana ilikuwa  takriban shilingi milioni 2″.

Lakini pia Aunty alizima tetesi za kuwa ameachana na baba watoto wake Mose Iyobo ambaye hakuonekana kabisa kwenye safari hiyo na kupelekea tetesi za kuachana;

Watu wanasema sana kuona nimeenda peke yangu bila Iyobo lakini mbona inawezekana kabisa kitu hicho maana bado kuna vitu vingi tutakuwa pamoja tu”.

Aunty Ezekiel Ajibu Tuhuma Za Kumlipizia Kisasi Wema

Muigizaji wa Bongo movie Aunty Ezekiel amejibu tuhuma ambazo zinemuwndama baada ya kutoonekana katika sherehe ya shoga yake mkubwa Wema Sepetu.

Gazeti la zamani linaripoti kuwa watu wa karibu wa Aunty wamedai Msanii huyo hakufika Kwenye Sherehe kwa ajili kumlipizia kisasi Wema ambaye hakufika Kwenye hafla yake siku za nyuma na sio k amna nguo yake kiharibika kama alivyosema mwanzoni.

Hakuna cha nguo kuharibiwa wala nini sema Aunt kaamua kumlipizia kisasi Wema kwa sababu naye hakuenda kwenye uzinduzi wa filamu yake iitwayo Mama,” 

Baada ya Tuhuma hizo Aunty aliyafutwa na gazeti hilo na alifunguka na kusema:

Sikuwa na sababu yoyote ya kunifanya nishindwe kufika kwenye sherehe ya Wema kwani nimeshirikiana naye hatua zote lakini kilichonikuta ndiyo hicho cha nguo na wala sijamlipizia chochote.

Kwangu alichelewa tu na mwisho tulionana na picha alipiga, watu wanafananisha tukio la Idris ndiyo fundi alimharibia nguo Wema hakufanikiwa kufika”.

Wema alipotafutwa alifunguka na kusema anaamini Aunty hakufika kwa sababu ya dharura na sio kingine:

Aunt aliniambia kuwa hatoweza kufika kwa kuwa amepata dharura lakini tulishirikiana katika kila kitu sasa anilipizie kisasi kwani mimi nina tatizo naye jamani! Dharura ni kawaida kwa binadamu na nilimwelewa”.

 

Aunty Ezekiel Awataka Wanawake Waangalie Mapenzi Ya Kweli na Sio Pesa

Muigizaji wa Bongo movie na mfanyabiashara maarufu Aunty Ezekiel amefunguka na kuwaombea wanawake juu ya tabia ya kupenda kuwa na wanaume wenye pesa bila ya kijamii kipimo cha mapenzi na upendo wao.

Aunty Ezekiel amewashauri wanawake wenzie wenye tabia ya kuangalia kipato cha mwanaume au aina ya kazi kwa mwanaume kabla ya kujiingiza kwenye mahusiano, waache tabia hiyo na badala yake waangalie zaidi mapenzi ya dhati.

Akiongea kwenye usiku wa fainali ya Jibebe Challenge, Aunty amesema kwenye mapenzi hakuna haja ya kuangalia pesa wala kazi na ndio maana hata yeye akaamua kuolewa na Mose Iyobo.

Aunty Ezekiel ameongea hayo kutokana na kupitia mambo hayo kwani miaka ya nyuma alikuwa Kwenye Mahusiano na Jack Pemba ambaye ni mfanyabiashara tajiri sana lakini alishindwa kukaa Kwenye Mahusiano kutokana na kipigo alichokuwa anapata mpaka kupelekea ujauzito kuharibika.

Baada ya kuachana na Jack Pemba ambaye yupo nchini Uganda kwa sasa Aunty amejikuta Kwenye Penzi la Mose zito o ambaye ni dancer wa Diamond Platnumz.

Aunty Ezekiel Ataja Sababu Ya Kutoenda Kwenye Sherehe Ya Wema

Muigizaji wa Bongo movie Aunty Ezekiel ameweka wazi sababu ya kutoonekana Kwenye Birthday party ya rafiki yake kipenzi Wema Sepetu iliyofanyika siku chache zilizopita.

Siku ya Jumapili kulikuwa kuna bonge la party ya Birthday ya Wema Sepetu ambayo ilihudhuriwa na mastaa kibao lakini kati ya watu hao mtu ambaye alikosekana ni rafiki kipenzi wa Wema ambaye ni Aunty Ezekiel.

Aunty kutohudhuria kulizua maneno mengi ikiwemo watu kufikiri labda wawili hao hawana maelewano.

Kwenye mahojiano yake na waandishi wa habari Katika usiku wa Jibebe Challenge, Aunty amefunguka na kusema sababu iliyomfanya asihudhurie ni kukosa nguo ya kuvaa.

Kilichotokea ni kwamba kila kitu ambacho kilifanyika tulishirikiana kuanzia mwanzo hadi mwisho yaani kuanzia kutoa kadi mpaka mwisho Lakini pia mwishoni fundi akaharibu nguo yangu ikabidi nilale nyumbani hamna kingine”.

Aunty Ezekiel amekana tetesi za kuwa hajahudhuria sherehw ya Wema kwa sababu amemlipizia kwa sababu kama utakumbuka siku za nyuma Kwenye uzinduzi wa movie ya Aunty ya ‘Mama’ Wema naye hakuhudhuria uzinduzi huo Mlimani City akasema nguo yake iliharibiwa na fundi.

“Sijawahi Kufikiria Kuhusu Kufunga Ndoa na Iyobo”- Aunty Ezekiel

Muigizaji wa Bongo movie Aunty Ezekiel amefunguka na kudai hajawahi hata kuwaza Kuhusu kufunga ndoa na mpenzi wake Mose Iyobo.

Aunty Ezekiel amekuwa kwenye mahusiano ya kimepenzi na dancer wa Diamond Platnumz, Mose  Iyobo kwa miaka zaidi ya mitatu na kuzaa naye mtoto mmoja wa kike, Cookie.

Kwenye mahojiano na gazeti la Amani, Aunty amesema kuwa siyo kwamba mtu akifunga ndoa ndiyo anaweza kuishi vizuri na mwanaume wake, bali ni kwamba anachojua kuishi vizuri ni sifa moja kubwa ya kuendelea kuwa pamoja ni kupeana heshima na kila mmoja kutambua anachokifanya.

Mimi sitaki hata kukuficha wala sijawahi kufikiria kufunga ndoa na Iyobo leo wala kesho kikubwa tunaishi vizuri na tunalea mtoto wetu ipasavyo hilo ndilo ninalolitaka na si vinginevyo kwani kuolewa siyo ishu kikubwa malezi ya mtoto tu”.

Aunty Ezekiel ameshawahi kufunga ndoa miaka ya nyuma na mwanaume anayeitwa Demonte ambaye anasemekana mpaka sasa yupo jela kwa kuuza madawa ya kulevya.