Nina Nyumba USA na Ndipo Yatakapokuwa Makzi Yangu.:-AY

Msanii wa kitambo katika muziki na mpaka sasa amekuwa akifanya vizuri katika game AY, amefunguka na kusema kuwa ni kweli kuwa anamilikinyumba kwa sasa nchini marekani ambapo ameinunua hivi karibuni lakini anategemea kuwa huko ndipo yatakapokuwa makaiz yake.

akiwa kama mmoja ya wasanii weny mafanikio makubwa lakini hawakuwahi kutaka kuonyesha kwa kila mtu na hata katikia mitandoa y akijamii , AY kwa sasa anasema kuwa atakuwa na makzi nchini huko kwa sababu tu ameamua kukaa huko.

Aangu hapo awali kulikuwa na tetesi hizo kutokana na baadhi ya picha zilizowahi kusambaa zikimuonyesha msanii huyo akiwa ameseimama mbele ya jumba la kifahari na moja ya wadada wanaosemekana kuwa ni madalali wa nyumba huko USA.

Akiwa katika mhojiano ya kutambulisha ngoma yake mpya iliyokwenda kwa jina la SAFARI aliyomshirikisha king kiki, AY aliulizwa na B-Dozen kuhsu kumiliki nyuma nchi USA na alisema “ni kweli nimefanikiwa kupata nyumba huko na ndipo kwa sasa yatakuwa makazi yangu ”

Hata ni mafanikio makubwa kwa AY mabe kwa sasa amebahatika kupata mtoto mmoja na mkewe waliofunga nae ndoa mwaka uliopita.

AY Athibitisha Kumiliki Mjengo Calabasas, Marekani

Mwanamuziki mkongwe wa muziki wa Bongo fleva Ambwene Yesaya maarufu kama AY amethibitisha kumiliki mjengo wa kifahari nchini Marekani katika maeneo ya Calabasas.

Katika mahojiano aliyofanya na Global Publishers AY  amethibitisha kwamba akili yake inafikiri mbali zaidi nay eye ni wa anga za kimataifa, naye aka­nunua Mjengo maeneo ya Calabasas ingawa hajataka kufafanua gharama zake.

Ni kweli nimefanikiwa kupata nyumba Calaba­sas na ndipo yatakuwa makazi yangu, ninamiliki nyumba mbili ikiwemo hiyo ya Marekani na moja Tanzania,na pia ninamiliki magari manne“.

AY anakuwa Kama ametisha hivi kwani eneo ambalo amenunua mjengo Wake ni eneo wanalokaa washua na mastaa wakubwa wenye pesa zao Kama vile Kim Kardashian, Kanye West, Drake Justin Bieber na wengineo wengi.

 

Ay Amshauri Dudu Baya Kusajili Neno Konki ili Kujipatia Faida.

msanii wa muziki wa siku nyingi  Ambwen yesaya , Amefunguk na kutoa ushaur kwa msanii mwenzake Dudubaya kufanya mchakato wa kusajili neno KONKI ambalo kwa sasa hivi limekuwa habari ya mjini na kutumiwa na watu wengi.

Ay anasema kuwa kampuni nyingi wamekuwa wakidata maneno yanayotumiwa na watu mitaani kwa ajili ya kufanyia biashara bila kuwa na ruhusa ya mzalishaji wa nene hilo lakini kikubwa ni kuwa kuna kuwa hakuna hati miliki ya neno hilo na ndio maana inakuwa sio faida kwa wasanii baadhi.

Ay anasema kuwa Dudu baya afanye mchakato wa kusajili neneo hilo kabla halijadakwa na makampuni makubwa kibiashara.

Dudu baya akitaka kutisha bsi akasajili slogan yake maana si mnayajua makampuni makubwa  ya mawasiliano kwa kudandia misemo…PATA OFFER KONKI mfikishien ujumbe wangu -Aliandika AY

AY Afunguka Kuhusu Kuhamisha Makazi Marekani

Msanii mkongwe wa Muziki wa Bongo fleva Ambwene. Yesaya maarufu kama AY amefunguka na kuweka wazi kuwa amehmisha makazi yake kufika Tanzania kwenda Marekani.

Global Publishers wanaripoti kuwa AY ameweka makazi nchini humo baada ya kununua nyumba ya kifahari nchini humo Miezi michache iliyopita.

Kwenye mahojiano na Global Publishers  AY mwenye makazi katika Jiji la Calabasas, California amesema ilikuwa ni ndoto yake ya muda mrefu kwamba siku moja awe na makazi kwenye taifa hilo mbali na alipozaliwa Tanzania.

Siri ya kuja kuishi Marekani ni kwamba hii ilikuwa ndoto yangu ya muda mrefu niwe na makazi huku. Kwa hiyo kwa kufanikisha kununua mjengo Marekani kwangu nimetimiza jambo moja muhimu sana maishani mwangu na ninamshukuru Mungu”.

AY na mke wake Remmy walifanikiwa kuzaa mtoto wao wa kwanza siku ya jana ambapo mtoto huyo pia amezaliwa nchini Marekani.

Ay Kununua Mjengo Mkali katika Jiji la Florida .

Msanii mkubwa na wa siku nyingi Ambwene Yesaya inawezekana akawa na mjengo mkubwa nje ya nchi hii ikisemekana kuwa nyumba hiyo inapatikana katika jiji la Florida nchini Marekani.

Akiweka picha za moja ya jumba kubwa nchini humo Ay ambae kwa sasa yuko nchini Calabasasa ameweka picha za nyumba hiyo akiwa amesimama nje ya jumba hilo huku akiandika maneno ya kutia hamasa na yenye kuonyesha kuna kitu kinaendelea.

Ay aliandika “now let me welcom everybody  to the wild wild west,”    na kisha kumalizia na hashtag ya #CALIFORNIALOVE .

Hata hivyo aktika picha hizo alizotuma Ay aliweka akiwa amesimama na moja ya mwanadada ambae katika ukurasa wake pia aliweka picha hizo hizo huku mwanadada huyo akionekana kuwa kazi yake kubwa ni dalali wa majengo makubwa huko California.

 

Nilimjua Mke Wangu Tangu Akiwa Mdogo.-AY

Msanii wa muziki wa hip-hop ambwene yesaya maarufu kama AY, kwa mara ya  kwanza tangu kufunga ndoa amefunga ndoa na kuamua kushare na mashabiki wak maisha yake ya ndoa na ni vipi aliweza kukutana na mke wake ambae kwa sasa wanaishi pamoja.

AY anasema kuwa ameonana na mpenzi wake huyo kwa muda mrefu sana lakini kila kitu kinakuwa na muda wake na mud ukifika hakuna kinachoweza kuzuia watu kuwa pamoja kinachotakiwa kufanyika ni kuzungatia malengo tu,

AY anasema kuwa alimjua mke wake tangu akiwa mdogo lakini aliamuacha kwanza amalize shule na kutimiza malengo yake kwa sababu asingeweza kumuoa kama alikuwa bado mdogo hivyo ilibidi amsuburi.

Tulionana nikiwa Rwanda 2008, kwaio ni zamani kidogo kama miaka 9 hivi, na nilijua kuwa ni ke wangu ilitokea tu autoamticalyy unajikuta unafeel tu.Nilimjua tangu akiwa mdogo sana ila niliona nimwache kwanza asome nsipo niliposubiri hivyo kikubwa ni uvumilivu.Alikuwa mdogo sana hivyo nilimwacha kwanza atimize malengo yake.

AY alipoulizwa kuhusu mabadiliko aliyoyapata baada ya kufunga ndoa AY alisema kuwa yeye alikuwa tayari alishajianda kuishi maisha hayo tangu mwaka mmoja nyuma

mwaka mmoja nyuma nilikuwa yatari nilishaanza kujipanga kufunga ndoa hivyo nilianza kujiandaa kisaikolojia kwaio pamoja na kwamba nilebadilika lakisi sio asana ingawa hata maamuzi na jinsi ya kufikiri pia huwa inabadilika

Hata hvyo sio kila mmoja aliweza kufikiria kama AY angeweza kufunga ndoa na hivyo watu wengi walikuwa wakishangaa baada ya mamuzi yake na AY analiongelea hilo.

Mapenzi yapo kila sehemu , ukiwaona hata hao wakina Fid Q wanajifanya ma-hardcore lakini wanalegeaga sana tu hao , ila unapaswa kujua tu kwamba kila mtu ana mtu wake.-Alisema AY alipokwa akifanya mahojiano na Shadee wa Clouds E

 

Baadhi ya Watu Maarufu Waliompongez AY kwa Kufunga Ndoa.

Wikiend hii katika mitandao ya kijamii kulisambaa kwa picha zikionyesha matukio ya msanii wa muziki nchini ambwene yesaya alieamua kuuacha ukapela na kufunga ndoa na mwanamke aliyekuwa nae katika mahusiano kwa muda mrefu aliejulikana kama Remy.Mwanamke huyo aliacha gumzo kubwa katika ktandoa ya kijamii kutokana na uuzri wake alikuwanao lakini pia ni mwanamke msomi kutoka nchini rwanda,

Ingawa ilikuwa ni jambo la ghafla kwa macho ya watanzania kwa sababu ya ukimya wa AY lakini limekuwa ni jambo lakheri kwa msanii huyu  na watu wake wa karibu kutokana na uzito wa jambo lenyewe.wasanii mbalimbali na watu maarufu wamempongeza msanii huyo kwa kumuandikia.

PROFFESA JAY ALIANDIKA;

hongera sana mdogo wangu @aytanzania na mkeo @remyrwanda  kwa hatua hii ya kufunga pingu za maisha mungu awatangulie na kwabariki sana , muwe na maisha mema yenye baraka na furaha tele.

MWANA FA

brother @aytanzania  karibu katika hili chama la watu wazima  wenzio.. mungu awabariki sana wewe na shemeji wa taifa @remyrwanda kwenye muunganiko huu.Goodspeed my G...

DIAMOND PLATINUMZ

Congrats legend ..mwenyezi mungu awajalie maisha mema yenye baraka , furaha na amani tele. @aytanzania.

JOKATE MWEGELO.

hongera sana kwake the legendary hustler,kwa hatua hii muhimu sana katika maisha ya mwanadamu.

 

Ay Akiri Kuteswa Na Bifu Lilikowepo Kati Ya Fa Na Jay Dee

Msanii mkongwe kutoka nchini Ambwene Yesaya ambae kwa jina la muziki anajulikana kama Ay, amefunguka na kuongelea jinsi ambavyo bifu la wasanii wenzie Mwana Fa na Lady Jay Dee kukaa muda mrefu bila kuelewana wala kufanya kazi pamoja  ilivykuwa ikimpa ugumu wa kushirikiana nao wote wawili ilhali wote walikuwa ni watu wake wa karibu.

Akiongea wikiend hii msanii huyo anasema kuwa pamoja na kwamba kitu hicho kilikuwa kikimsumbua kwa sababu wote walikuwa ni watu wake wa karibu hivyo ilikuwa ikimpa muda mgumu sana lakini alikuwa akiamini kuwa ipo siku watu hao watakuja jupatana ingwa walikuwa hawaongei kabisa.

“Ilikuwani ngumu kwa sabau wote walikuwa hawaongei alafu kwangu wote washikaji kwaiyo ukiongea ukamletea za huyu anakwambia haaaa hayo mambo yaache, lakini ikafika time wakwa wakiuliziana e bhana huyo vipi.. nikasema basi mambo yatakuwa sawa tu”  alifunguka Ay.

Akiongea katika kituo cha East Africa Television, Mwana Fa pia alifunguka na kusema kuwa ” Tupo kwenye ground nzuri,jide ni mshikaji wangu na hata hdugu pia huwa wanakosana , na kila mtu anajua, ila kilichotokea kilishatokea tunaviacha vipite tu, tumefika mahali sasa hivi tunaongea vitu vya kawaida kabisa”

Mwana Fa, Ay na Fid Q wamekuja na project mpya wa kuimba pamoja wimbo wao mpya unaojulikana kama upo hapo, hivyo kwa sasa wasanii hao wanategemea kuwa karibu na kuonekana pamoja katika baadhi ya kazi.Hivyo pia Fid Q alipata nafasi ya kuongelea  mahusiano mapya ya  Mwana Fa na Lady Jay Dee.

‘i tink watu wamezoea kusema keep the good music alive lakini mimi nasema yeye kuwa rafiki na jide tena ni keep tha positive music alive” alisema Fid Q

Mwana Fa na Lady Jay Dee walikuwa katika ugomvi wa muda mrefu na walikuwa hawafanyi kazi tena kama zamani, lakini hivi karibuni wawili hao wameoneana kumaliza tofauti zao na kuona kuna umuhimu wa kufanya kazi pamoja kama zamani, hii ilidhihirika baada ya Mwana Fa aliposapoti wimbo wa mwanadada huyo kwa kuweka katika ukurasa wake wa instagram

 

AY na MwanaFA tayari kulipwa bilioni 2.1 baada ya kushinda kesi dhidi ya Tigo

Kampuni ya mawasiliano ya Tigo imepata pigo baada ya mahakama kutupilia mbali rufaa waliokata katika kesi yao dhidi ya wanamuziki AY na MwanaFA.

Mwaka jana mahakama Wilaya ya Ilala ilikua iliamuru kampuni hio kuwafidia AY na MwanaFA bilioni 2.1 kwa kutumia nyimbo zao bila kuwalipa.

AY na MwanaFA

Tigo ilikata rufaa katika mahakama kuu ya Tanzania kupinga agizo la mahakama wilaya ya Ilala iliyowaagiza walipe AY na MwanaFA bilioni 2.1.

“Ni haki yao kulipwa kwa sababu ni kazi zao ambazo zinalindwa kisheria,” Albert Msando, wakili wa wasanii hao wawili, alisema baada ya uamuzi huo wa koti.

 

AY amwomba mpenzi wake Remy afunge naye ndoa

Ambwene Allen Yessayah maarufu kama AY sasa huyo tayari kuingia kwa ndoa. Rapa huyo amepropose kwa penzi wake Remy.

AY alijulisha watu nia yake ya kufunga ndoa na Remy wakati alihudhuria harusi ya Professor Jay. Nduguwe Jay alisema kuwa AY alimwambia anataka kumoa Remy.

Remy na AY wakiwa kwa harusi ya Professor Jay

“Muda uliopita nilikuwa naongea na AY hapa akawa ananiambia na yeye soon anafunga ndoa na mpenzi wake. Kwa hiyo mimi naweza kusema kila kitu kinakuja kwa wakati,” Black Rhyno aliambia Bongo5.

AY alimwomba Remy afunge naye ndoa siku chache baada ya harusi ya Professor Jay. Tazama video hapo chini:

Picha 7 za AY na mpenzi wake ambaye anataka kufunga na yeye ndoa

Wambeya wanasema kuwa safari ya AY kuingia kwenye maisha ya ndoa yaanza kunukia. Hit maker huyo wa ‘Zigo’ alionekana kwa harusi ya Professor Jay akiwa na mpenzi wake huyo.

Black Rhyno – ndugu mdogo wa Professor Jay, alisema kuwa AY alimwambia wakiwa kwa harusi ya Jay kuwa anataka kufunga ndoa na mpenzi wake

“Muda uliopita nilikuwa naongea na AY hapa akawa ananiambia na yeye soon anafunga ndoa na mpenzi wake. Kwa hiyo mimi naweza kusema kila kitu kinakuja kwa wakati,” Black Rhyno aliambia Bongo5.

Tazama picha za AY na mrembo wake hapo chini:

Diamond, Victor Wanyama wamtakia AY heri ya siku ya kuzaliwa

Rapa Ambwene Allen Yessayah maarufu kama AY anasherekea siku ya kuzaliwa kwake leo Julai 2017. AY amefikisha miaka 36 leo.

Mastaa wengi wamemtakia AY heri ya siku ya kuzaliwa kwake, rafiki wake wa karibu Victor Wanyama alikua miongoni mwa wale waliomtumia jumbe mapema.

AY na Victor Wanyama

“Happy bday big boss @aytanzania have a good one bro,” Victor Wanyama aliandika.

Diamond na Rayvanny pia walimtumia AY jumbe:

“Big Birthday wish to Msoja wange @jahprayzah and my Legend Brother @aytanzania …. Long Life!!” Diamond Platnumz

“HAPPY BIRTHDAY KAKA LAO @aytanzania Mungu Akupe maisha marefu yenye Mafanikio zaidi,” Rayvanny