Baba Diamond Kukatwa Miguu Kutokana na Kansa Ya Ngozi

Baba mzazi wa staa wa Bongo fleva Naseeb Abdul ‘Diamond Platnumz’, Abdul Juma amedaiwa kuwa katika hai mbaya itakayompelekea kukatwa miguu katika siku za usoni.

Baada ya kujionea baba Dia­mond akiwa anasumbuliwa na tatizo la kansa ya ngozi, Gazeti la Ijumaa Wikienda lilimpigia simu dak­tari Godfrey Charle wa jijini Dar alipoelezwa kuhusu tatizo hilo, alisema kuna mambo ya kufanya ili kumnusuru kwani tofauti na hapo basi huenda akalazimika kukatwa miguu.

Kwa baba Diamond sambam­ba na kutibiwa kansa anatakiwa atibiwe pia maambukizi mbalim­bali yanayojitokeza kwani hayo ndiyo yanasababisha mgonjwa kukatwa mguu au kiungo chochote kilichoathirika na siyo kansa.

Kwa kweli kwa hatua ile aliy­ofikia kupona kwake ni asilimia 50 tena kwa msaada wa ndugu yaani kama ndugu zake watam­saidia katika matibabu hivyo inategemea na msaada ataka­opata lakini vinginevyo asipopata msaada wa matibabu tena kwa haraka anaweza kukatwa miguu“.

Kwenye mahojiano aliyofanya na Gazeti la Ijumaa Wikienda, Baba Diamond alisema amepitia changamoto za muda mrefu kwa kusumbuliwa na miguu hiyo bila kupata matibabu hivyo ilifika wakati alikata tamaa ya maisha kabisa.

Kwa kweli miguu hii imen­isumbua kwa muda mrefu sana. Nimehangaika katika hospitali nyingi tu lakini kwa kweli nimeshindwa kujitibia kutokana na gharama kuwa kubwa”.

Baba Diamond alipoulizwa kama ame­shamwambia mwanaye amsai­die, baba Diamond hakutaka kumzungumzia lakini akasema anaamini kama ni tatizo hilo, Diamond atakuwa analifahamu vizuri maana lina muda mrefu.

Siwezi kumzungumzia sana lakini kikubwa mimi kwa sasa namshukuru Mungu kanikutani­sha na dada kutoka Uingereza anaitwa Zubeda Humphries ambaye amekuja na kuahidi kunisaidia ili niweze kutibiwa”.

 

 

Dada wa Diamond Amtaka Diamond Amsaidie Baba Yao Maana Ana Hali Mbaya

Mwanamke mmoja aliyejitambulisha kama Dada yake na staa wa Bongo fleva Diamond Platnumz, anayejulikana kwa jina la Zubeda amempigia magoti Diamond amsaidie baba yake ambaye anaumwa hoi.

Dada huyo ambaye wakati akiwasili nchini alipokelewa na Baba mzazi wa Diamond, mzee Abdul Juma, amesema hajui kipi kibaya ambacho baba alimkosea Diamond hadi kufika hatua ya kuwa mbali naye na kutomsaidia ilihali ni mgonjwa sana akisumbuliwa na tatizo la miguu kuvimba kwa muda mrefu.

Kwenye mahojiano aliyofanya na Global Publishers, Zubeda amemtaka Diamond akubali kuonana naye ili waongee na amwambie kwanini amemtelekeza baba yake kwani ni mgonjwa sana na anahitaji msaada wa hali na Mali.

Nimetoka London nimekuja Tanzania kuonana na Diamond na kumuuliza Mzee Abdul amemfanya nini Mpaka hutaki kumuona wala kumsaidia Baba yake kwani kiukweli Baba yake anaumwa sana anahitaji msaada”.

Lakini pia Mwanamama huyo amesema kuwa yupo tayari kusaidia kumaliza tofauti zilizopo kati ya Diamond na Baba yake.

Baba Diamond- Natamani Diamond Angenialika Tandale

Baba mzazi wa staa wa Bongo fleva Diamond Platnumz, Mzee Abdul Juma maarufu kama Baba Diamond ameibuka na kudai mwanaye hakumualika kujumuika naye Tandale wiki iliyopita.

Wiki iliyopita Diamond aliongozana na Familia yake yote akiwemo mama Yake na dada zake pamoja na Familia nzima ya WCB katika charity event aliyofanya maeneo ya Tandale Maguniani.

Kwenye mahojiano na Global Publishers, Baba Diamond amefunguka na kusema anatamani angekuwepo kama sehemu ya kukumbuka maisha yao waliyoyapitia miaka ya nyuma akiwa na mwanaye huyo kwani historia aliyoitoa Diamond ilimgusa.

I wish na mimi ningekuwepo pale. Nilitamani kushuhudia pia mambo mazuri aliyoyafanya mwanangu maana awali nilidhani ni jambo dogo, lakini baadaye nikaona ni jambo kubwa sana.

Nilipofuatilia kwenye TV nikaona mwanangu anatoa Bajaj, anatoa bima, anatoa mikopo kwa akina mama, pamoja na bodaboda kwa kweli moyo wangu ulifurahi sana.

Ile ishu ya kuuza mitumba aliyoizungumza, hata mimi niliuza. Pengine pia ningeweza na mimi kuwatia moyo mamia ya watu waliofurika pale.

Nilisikia alisema amepanga kufanya kila mwaka hivyo bado naamini Mungu akitujalia uzima, ishallah mwakani anaweza kunialika kwani hakuna tatizo kati yetu”.

Diamond amekuwa hana Mahusiano mazuri na Baba yake kwa miaka mingi hii ilitokana na Baba Diamond kumtelekeza Diamond wakati mdogo na hivyo kulelewa na mama yake ambaye yupo naye karibu zaidi.

Queen Darleen Amuomba Msamaha Baba Yake Ili Kukwepa Laana

Msanii wa Muziki wa Bongo fleva kutoka WCB, Mwanahamisi Abdul maarufu kama Queen Darleen amedaiwa kumuangukia kwa magoti Baba yake Mzee Abdul baada ya kuwa bifu la muda mrefu.

Sintofahamu kati ya Baba Diamond na mwanaye ilianza baada ya Queen Darleen kutoa kauli kuwa baba yake ni Diamond Platnumz na kudai Mzee Abdul sio Baba yake Tena.

Global Publishers wanaripoti ili kukwepa laana ya mzazi, hati­maye  Queen Darleen ametambua umuhimu wa wazazi na kuamua kumfuata na kumuomba msa­maha Baba yake.

Kwenye mahojiano na Global Publishers Baba Diamond amesema ni kweli awali ali­kuwa na ugomvi mkub­wa na Queen Darleen na ikafikia hatua mpaka ya kumtamkia maneno mazito kuwa hata akifa binti yake huyo asimzike ila anamshukuru Mungu kwamba mwanaye huyo ametambua makosa yake na kujirudi.

Haya ni mambo ya kawaida tu katika familia, ni kweli mimi na Queen Darleen tulikuwa na ugomvi mkubwa mpaka ikafikia hatua nikamtamkia maneno mabaya kwamba iki­tokea nimefariki dunia asije kunizika, jambo ambalo si zuri, lakini ameyatambua ma­kosa yake, akaja kuniomba msa­maha na mimi nikamsamehe kwa moyo mmoja”.

 

Baba Diamond Adaiwa Kukaata Mtoto Wake Wa Nje

Baba mzazi wa staa wa Bongo fleva Diamond Platnumz, Mzee Abdul Juma ametupiwa tuhuma nzito baada ya kudaiwa kutelekeza mtoto wake wa nje.

Global Publishers wanaripoti kuwa kijana aliyejitambulisha kwa Jina la Emmanuel alidai ni mtoto wa Baba Diamond na ametoka mkoani Kigoma kwa ajili ya kuja kuonana na Baba yake ambaye mama yake amemwambia alimtelekeza.

Gazeti hilo lilimsaka Baba Diamond ili kujua ukweli wa tuhuma hizo ambapo alikiri kumpokea kijana huyo na kusema kwamba siyo mtoto wake kama mwenyewe anavyodai bali ni kijana tu ambaye alikuwa anatafuta njia ya kukutana na Diamond kwa hiyo akaona njia rahisi ya kumfikia ni kujifanya mtoto wake.

Nilikuwa katika pilikapilika zangu, mara nikapigiwa simu nikaambiwa kuwa kuna mgeni wangu nyumbani, nilipouliza ni nani nikaambiwa ni ndugu yake Diamond ambaye ni muimbaji pia katokea Kigoma.

Baada ya kumaliza pilika zangu nilirudi nyumbani na kweli nikamkuta kijana huyo lakini cha kushangaza alikuwa anatetereka sana kujibu maswali kwa sababu hata nilipomuuliza jina la baba yake alitaja lingine kabisa tofauti na langu.

Unajua huyu siyo kijana wa kwanza kuja na kudai kuwa mimi ni baba yao, wanatafutaga njia ya kutaka kuonana na Diamond lakini wanashindwa kutokana na mama yake kule ni mkali hawawezi kuingia, kwa hiyo wanataka waje kwangu kwa sababu wanajua nafika kwa Diamond.

Wanahisi wakidanganya hivyo itakuwa rahisi mimi kuwakutanisha kitu ambacho hakiwezekani, narudia tena mimi sina mtoto wa nje kwa sababu watoto wangu wote nawafahamu”.

 

Diamond Atapata Tabu Sana :- Baba Diamond

Baada ya siku kadhaa kupita baada ya Diamond kuweka picha ya baba yake na mama yake pamoja na yeye bado akiwa mdogo lakini bado baba huyo anasema kuwa Diamond anayafanya hayo anayoyafanya kwa sababu yeye yuko hai.

Diamond ambae inaonekana kuwa anamchukia baba yake na baba yake anakiri kulijua hilo , amasema kuwa anajua kabisa kuwa Diamond anamchukia lakini anajua kuwa siku akifa ndio atajua umuhimu wake na kwamba itampa tabu sana atakapo kufa yeye

Niliiona hiyo picha na niliiona ni vizuri na nilijisikia faraja pia,haina tatioz lolote lakini mimi ninajua kabisa kuwa diamond ananichukia lakini hata iweje mimi ni baba yake, na ananichukia kwa sasa lakini ipo siku nikifa atapata tabu sana.

Baba diamond anasema kuwa pamoja na kwamba yeye ni baba ya Diamond lakini hajawahi kusaidiwa kama anavyostahili kama mzazi.

“Nikifa Leo Mwanangu Asinizike Wala Asiguse Jeneza Langu”- Baba Diamond

Baba mzazi wa msanii wa Bongo fleva, Diamond Platnumz pamoja na dada yake staa mkongwe wa Bongo fleva anayejulikana kama Mzee Abdul Juma, ameibuka na kudai kuwa endapo akifa hata leo kesho basi mtoto wake asimzike wala asiguse jeneza lake.

Baba Diamond amekuwa hana uhusiano mzuri na watoto wake wote wawili yaani Diamond na Queen Darlene mara kwa mara amekuwa akuongea na vyombo vya habari kuhusuatatizo aliyonayo kwenye familia yake.

Hivi karibuni Queen Darlene alifanya mahojiano na kituo kimoja na katika maongezi yake kuhusu wifi yake Zari, alimuingiza baba yake mzazi Mzee Abdul ambapo alisema:

Zari ni wifi mzuri kwangu ana roho nzuri na ndiye mtu pekee aliyekuwa ananishauri kumjali baba yangu, japo baba mwenyewe kuumwa kwake kumekuwa kama mtoto kwa kweli kwa sasa siwezi kusema baba yangu ni Abdul baba yangu ni Naseeb”.

Baada ya mzee Abdul kusikia kuhusiana na maneno aliyoongea binti yake alikasirishwa na kumwambia kuwa endapo akifa basi Queen Darlene asiguse jeneza lake wala hata asithubutu kumzika kwenye mahojiano na Global TV alifunguka yafuatayo:

Nimeumia sana kwani Queen Darlene yeye ni nani hata kunyanyuka na kusema maneno kama hayo kanichukulia mimi kama mtoto hata kama ni dharau sio hivyo kaka yake mwenyewe ambaye ametoka kimuziki na anafanya vizuri hata kama ananidharau hajawahi kunitamkia maneno kama hayo iweje leo hii Queen Darlene anitamkie maneno kama haya Queen Darlene ni binti yangu ambaye nimekaa naye kwa muda mrefu sana na mara nyingi amekuwa akija hapa nyumbani tunapika tunakula lakini leo hii inakuaje baada ya kutoka kimuziki anaanza kutoka kimuziki anaanza kunidharau mimi nimeumia sana sasa na mimi niseme nikifa hata leo na yeye asije kabisa assogelee jeneza langu wala asinizike yeye si kasema baba yake Naseeb basi na mimi sio baba yake “.

 

Aliyoyasema Baba Diamond Kuhusu Mimba ya Tunda

Baba mzazi wa msanii Diamond amefunguka na kuolengea mambo yanayoendelea katika mitandoa ya kijamii kuhusu mtoto wake huyo na mahusiano mapya ya kimapenzi yanayosemekana kuwepo katika yake na video queen maarufu bongo Tunda na kwamba mrembo huo saa hivi ni mjamzito na mimba  ni ya Diamond.

Baba huyo amesema kuwa kwa pande wake hana kinyongo chochote kuhusu mimba hiyo na kama yeye mwenyewe amekubali basi yeye hana shida kwa sababu binadamu hakataliwi hata siku moja.Hata hivyo baba huyo anasema kuwa hamjui kabisa mwanamke anaeitwa Tunda kwa sababu hata yeye hafatilii sana mitandoa ya kijamii.

Sijui habari zozte kuhusu Tunda, maana sio mtu wa kufutailia katika mitandao lakini watu ninaowajua alishawahi kutembea nao ni Wema Sepetu, Zari na Mobeto.Huyo Tunda simjui kabisa lakini kama itakuwa kweli yeye mwenyewe karidhika basi haina shida mimi sitakaa kuitwa babu ukubwa jalala.uwezi kukataa mtoto wa mtoto wako.

Hata hivyo Baba Diamond amesema kuwa ameona katika gazeti kuwa mtoto wake huyo kapanga nyumba , lakini hajafatilia kwa sababu ameona tu katika magazeti na hawezi kusema kama habari hizo zina ukweli au la.

Kuhusu swala la ,Mama Diamond kuolewa na mwanaume mwingine mzee huyo amesema kuwa yeye na Sandra kwa sasa ni kama dada na kaka na wamekuwa marafiki tu wamekuwa wakikutana nakusaidia ushauri kimaisha  lakini hawezi kumonea wivu kwa kuolewa kwa sababu walishaachana siki nyingi sana. Na kama ni kweli kuwa mama huyo ameolewa na ni mjamizto basi ni jambo la kheri na ana muombea dua ili aweze kufankiwa katika hilo lakini hana wivu kabisa.

Ilo la kusema kaolewa mimi wala sijakasirika kwa sabau tulishaachana siku nyingi sana,ingawa watu wanakuwa wanasema namuachia yeye anapanda ndege, ninachiamini mimi ni kuwa ndege yangu ipo na kuna siku nitaipanda tu.kikubwa tu ninamuombea mungu aweze kufanikisha katika ndoa yake na kama ni kweli kuwa ana mimba basi ninamuombea dua kwa hilo.-Alisema baba yake mzazi na Diamond.

 

Baba Diamond Kafunguka Ishu Ya Mama Diamond Kuolewa “Msiniingilie na Mama Diamond”

Baba mzazi wa Msanii Diamond Platnumz, Mzee Abdul Juma amefunguka kuhusiana na suala linalo kiki mjini kwa hivi sasa suala la Mama mzazi wa Diamond Bi. Sandrah kuolewa na kiben-10 anayejulikana kama Shamte.

Baba Diamond na Mama Diamond inasemekana kuwa waliachana miaka mingi iliyopita baada ya kumuacha na kumtelekeza na mtoto mdogo lakini kutokana na maelezo yake inaelekea hata kama baba Diamond hana uhusiano mzuri na mwanaye Diamond lakini anaelewana na mzazi mwenziye Bi Sandra.

Kwenye mahojiano aliyoyafanya na Millard Ayo Mzee Abdul alionyesha kukasirishwa na maswali aliokuwa anaulizwa kuhusu ndoa iliyofungwa kati ya Bi. Sandrah na Shamte:

Kwanza naomba niseme kuwa sijapenda na wala sipendi kuulizwa maswali hayo yanayo muhusu Mama Nasibu kwani mimi ninavyoona kuwa yule ni mama na mwanamke mwenye nguvu zake na uwezo wake na mwenyezi Mungu kampa pumzi kaamua na kajisikia mwenyewe kuwa anahitaji mume na ana uwezo wa kumudu kuwa na mume mimi naona hakuna matatizo yoyote ila naomba niseme na niwaambie watu wote kuwa wasipende sana kuniingilia maswala yangu na mimi na Mama Nasibu mimi naona kama wana maswali wanataka kumuuliza basi wamfuate tu wenyewe wakamuulize na kama wana maswali kwa Nasibu wawafuate wenewe wawaulize kuliko kunifuata mimi kuniuliza mambo yao wanayofanya mimi sijui”.

Baba Diamond amesisistiza kuwa yeye na Mama Diamond wanaelewana kama wazazi tu ila kwa sasa wamebaki kama dada na kaka tu ambao wanasaidiana kifikra na kimawazo na pia kimaisha lakini wanaelewana vizuri.

Baba Diamond Amshauri Zari Amvumilie Diamond Kwa Mapungufu yake

Baba mzazi wa Mwanamuziki Diamond Platnumz Mzee Abdul ameibuka na kumshauri Zari aendelee tu kumvumilia Diamond kwa makosa aliyoyafanya.

Katika mahojiano aliyoyafanya na Mllard Ayo Baba Diamond alipoulizwa akikutana na Zari atamshauri nini kuhusu mtoto wake ndipo aliposema kuwa atamshauri awe mvumilivu.

Baba Diamond amesema;

“Kwanza awe mvumilivu kwani mtoto wa kiume anakua mtu wa kudanganywa, mpotofu na ilimradi kashaambiwa kuna mke mwenzie basi awe mvumilivu ila kikubwa tu kuwe na heshima na adabu Zari kama Zari na Hamisa kama Hamisa waheshimiane wawe pamoja waangalie maisha tu yanaenda kama kawaida”.

Pia Mzee Abdul aliendelea kusema:

“Zari mi namwambia asipende kuwasikiliza waswahili ilimradi aangalie yake yanamwendea vizuri na Hamisa naye asipende kusikiliza ya Waswahili akae aangalie yake aendelee vizuri maana sisi waswahili kila neno linakuwa baya kwetu hamna neno zuri na mara nyingi tunakuwa hatupendani kupendeana mema mtu anapenda mwengine haaribikiwe asemwe tu, ila wakae pamoja tu waangalie haya maisha leo tupo kesho hatupo”.

Baba Diamond pia alimuomba Zari kama kuna uwezekano basi apewe nafasi awaone wajukuu zake akimaanisha Latiffah na Nilllan ambao amekiri hajawahi kuwaona kutokana na kutokuwa na  uhusiano mbovu na mtoto wake Diamond.

Baba Diamond aliongeza;

“Mi napenda kumwambia Zari nikiwa mimi kama mimi Baba Diamond aniletee wajukuu zangu kwanza niwaone au sio lazima nianiletee anaweza hata akaniambia sehemu gani naweza niweze kuenda kuwaona wajukuu zangu”.