Babu Seya na Familia Yake Watinga Bungeni.

Mwanamuziki nguli na mkongwe nchini Babu Seya na familia yake ya Viking leo siku ya juma tano wamtinga bungeni ambapo siku ya kesho wanatarajia kufanya sho yao kwa mara ya kwanza katika mkoa wa Dodoma.

Wasanii hao ambao wamealikwa bungeni na mbunge mariam ditopile wakipofika bungeni walishangiliwa na bunge zima baaada ya kutambulishwa na spika wa bunge Mh Job Ndugai baada ya kipindi cha kwanza cha maswali na majibu.

Kama itakumbukwa wasanii wao ni miongoni mwa wafungwa waliotoka kwa msamaha wa Raisi Decemba mwaka jana baada ya kutumikia kifungo chao kwa miaka 14 ambapo kifungo chao kilikuwa ni kifungo cha maisha.

 

Papii Kocha na Babu Seya Kupiga Bonge la Show ‘Vikings Night’

Wasanii wakongwe wa muziki wa Bongo fleva waliowahi kutamba na kibao chao cha ‘Seya’ Nguza Viking ‘Babu Seya’ na mwanaye Papii Kocha wanampango wa kufanya bonge moja la show itakayoitwa ‘The Vikings Night’.

Wasanii hao Baba na mwana waliokuwa jela kwa miaka zaidi ya 10 kwa mashtaka ya kubaka, ambapo walifanikiwa kuonja ladha ya uraiani mapema mwaka jana siku ya uhuru 9 disemba ambapo walitoka jela kwa msamaha wa raisi.

Tangu warudi uraiani miezi mitatu iliyopita wasanii hawa wanatarajiwa kufanya Show yao kubwa ya kwanza baada ya kuachiwa huru ingawa wameshafanya shoo chache hasa visiwani Zanzibar shoo hii inatarajiwa kuwa kubwa zaidi.

Shoo hiyo inatarajiwa kufanyika siku ya Jumamosi tarehe 10 machi katika ukumbi wa King Solomon Hall. Papii Kocha ameshatoa wimbo wake mpya unaoenda kwa jina la Waambie ambao Mpaka sasa tayari unafanya vizuri sana.

Msamaha wa Babu Seya na Mwanae Waibuka Tena Bungeni.

Desemba 9 mwaka 2017 Mh Raisi Magufuli alitoa msamaha wa rais kwa baaadhi ya wafungwa kwa kuzingatia vigezo mbalimbali na kati ya wafy=ungwa waliopewa msamaha wa Raisi ni pamoja na Babu Seya na Papii Kocha ambao walikaa jela kwa zaidi ya miaka 10 sasa.

Siku ya jana , moja ya wabunge kutoka chama cha upinzani CUF , aliibuka na kuhoji juu ya msamaha huo na kusema kuwa kwanini wasanii hao walisamehewa ilhali walikuwa wamekutwa na hatia ya kubaka na kulwiti watoto wadogo, hivyo walipaswa kubaki jela kuendelea kutumikia kifungi chao cha kosa walilofanya.

Mtolewa amesema kuwa kitendo alichofanya Raisi cha kukuvali msamaha wa wafungwa hao na kuwapaheshima ya kuwasapoti na kuwapandisha katika majukwaa makubwa nchini ikiwa ni pamoja na kuwasaidia kusimama tena kimuziki haileti picha nzuri kwa jamii hasa ukizingatia na kosa walilokuwa wamefanya.

kwenye maadhimisho ya uhuru kulitoka kwa msamaha wa wafungwa wakiwemo babu seya na wenzake,ambapo pasipo shaka mahakama ilithibitisha kuwa hawa watu ni wabakaji.sasa tunapotoa msamaha kwa wabakaji tunaweka wapi ulinzi wa watoto wetu.tunawapandisha kwenye majukwaa wafanye show yaani tunawaona nao ni kioo cha jamii  je wanafundisha nini?

Mbunge huyo aliongezea kwa kusema kuwa serikali inawaharibu wa toto kwa sababu mwisho wa siku utataka kuwa uliza watoto unandoto za kuwa kama nani katika nchi hii na mtoto hatosita kujibu nataka kuwa mbakaji.

Babu seya na papii kocha walitolewa kwa msamaha wa raisi baada ya kukituumikia kifungo kwa takribani miaka kumi baada ya kukutwa na hatia ya kubaka na kulawiti watoto.Hata hivyo  tangu wametoka serikali kupitia wizara ya utamaduni  na sanaa wamekuwa mstari wa mbele kuwasaidia na kuhakikisha wasanii hao wanarudi katika mstari wa sanaa.

Babu Seya, Papii Kocha na Familia Watinga Ikulu Kumuangukia Raisi Magufuli

Mwanamuziki wa muziki wa dansi, Nguza Viking au maarufu kama Babu Seya pamoja na watoto wake Johndon Nguza ‘Pappii Kocha’, Francis Nguza na Michael Nguza ambao waliwasili Ikulu leo tarehe 02 January kwa ajili ya kumshukuru kwa msamaha alioutoa kwao dhidi ya kifungo cha maisha walichokuwa wanatumikia.

Nguza Viking ‘Babu Seya’ na mwanae Papii Kocha walihukumiwa kifungo cha maisha miaka kumi na nne + iliyopita lakini baada ya kutumikia kifungo chao cha maisha kwa miaka kumi na nne mapema mwaka huu kwenye sherehe za Uhuru Raisi Magufuli aliwatangazia msamaha kutoka katika kifungo chao cha maisha na kuachiwa huru.

Siku ya leo familia nzima ya Nguza Viking wameongozana na kutinga Ikulu ambapo wameweka wazi kuwa wameenda pale kwa ajili ya kumshukuru Raisi kwa msamaha aliowapa na kuwaacha huru na pia wameenda Ikulu kwa ajili ya kuomba ruhusa na kupata baraka ya kuendelea na kazi.

Baada ya kumaliza makutano yao na Raisi Magufuli Babu Seya alifunguka yafuatayo kuhusu makutano yao na Raisi:

Yaani sijui niseme nini hapa nilipo nina furaha sana moyoni mwangu, nilikuwa naomba tangu muda mrefu nikutane na Raisi Magufuli, nimeomba sana mpaka leo nimefanikiwa kukutana naye na nimemwambia namshukuru sana kwa kutusamehe na hivi sasa nipo tayari kuchapa kazi, hapa kazi tu”.

 

 

 

 

Baada Ya Kutoka Gerezani,Babu Seya Kufungua Kanisa

Kila mmoja anakuwa na imani yake na njia yake ya kumshukuru Mungu kwa yale yalimkuta na kumuepusha katika maisha yake, swala la shukurani kwa Mungu linakuwa la kiimani zaidi.Hii pia inatokea kwa wasanii maarufu na waliokuwa wanapendwa sana miaka ya nyuma kutokana na kazi zao za muziki walizokuwa wakifanya, hapa tunawazungumza Babu Seya na mtoto wake Nguza Viking ambao wameachiwa huru December 9 mwaka huu.

Wasanii hao ambao walifungwa mwaka 2004 kwa tuhuma za kulawiti watoto ni mtu na mtoto wake na wamekaa gerezani kwa zaidi ya miaka 12 huku wakiwa na hawana tumaini la kutoka gerezani humo lakini  Mh.rais wa Tanzania aliamua kuwakumbuka na kuona kuwa kifungo walichokitumikia kitakuwa tayari kimewafunza kitu.

Wengi wamekuwa wakitoa ushauri kuwa wasanii hao bado wanahitajika sana katika jamii na katika soko la muziki huku mashabiki wakionyesha kiu zao za kuwataka kuwasikia tena katika muziki wakifanya vizuri kama mwanzo,lakini hata baada ya kutoka wasanii hao wamekuwa kimya kwa muda na hawakutaka kuongelea chochote kuhusu swala hilo.

Jana katika ukurasa wa Twitter unaosemekana kuwa ni wa kwao wasanii hao walithubutu kusema kuwa njia rahisi walioichagua ya kuamua kumtukuza Mungu na kumuonyesha shukrani kwa Mungu wo ni kuamua kufungua kanisa ikiwa ni jambo walilokuwa wamepanga siku nyingi tangu wakiwa gerezani endapo wangepata nafasi ya kutoka humo.

Mwaka mmoja kabla ya kuipata hii neema ya msamaha kunipata kuna mfungwa mwenza alipata kuniuliza  ukitoka utaendelea kuimba, nilichomjibu ni kua nikitoka ntafungua kanisa nimtukuze Mungu  naaam hata sasa nitafungua kanisa.

Ingawa wamejitokeza watu wengi hasa mapromota wakitaka kufanya kazi na watu hao lakini bado wao hawajatoa msimamo wao kabisa kuwa baada ya hapo wanataka kufanya nini.Wasanii hao walitamba sana enzi zao na kibao cha baba na mwana.

 

Baada Ya Babu Seya na Papii Kocha Kuachiwa Huru Hili Ndio Jambo La Kwanza Walifanya

Siku ya Jumamosi 9 Desemba ilikuwa ni siku kubwa ya kihistoria sio tu kwa sababu ilikuwa ni siku ya kusheherekea miaka 56 ya Uhuru wa Tanzania bali pia Watanzania walipata kitu kingine cha kuwapa furaha baada ya Babu Seya na mwanaye Papii Kocha kuachiwa huru kwa msamaha wa raisi.

Juni 25, 2004, Hakimu mkuu mkazi wa Mahakama ya hakimu mkazi Kisutu, Addy Lyamuya aliwahukumu aliwahukumu kifungo cha maisha gerezani Babu Seya au Nguza Viking na Papii Kocha katika gereza la Ukonga baada ya kukutwa na hatia ya kubaka na kunajisi watoto kumi.

Siku ya Uhuru 9 Desemba, Raisi Wa Jamhuri ya Muungano John Pombe Magufuli alitangaza katika hotuba yake alipokuwa anawahutubia wananchi kuwa ameamua kuwasamehe:

Kutokana na hiyo hiyo Ibara ya  45 kuwasamehe familia ya Nguza Viking jina jingine anaitwa Babu Seya pamoja na ndugu Johnson Nguza au kwa jina jingine pia ni Papii Kocha hivyo nao waachiwe huru kuanzia Leo”.

Baada ya Raisi kutangaza habari hizo ukumbi mzima ulilipuka kwa shangwe na vifijo lakini pia kwenye mitandao ya kijamii watu wote walifurahi na wananchi kwa ujumla waligubikwa kwa furaha.

Jioni ile baada ya kutangazwa kusamehewa Babu Seya na Papii Kocha waliachiwa huru kutoka katika gereza la Ukonga ambapo walipokelewa na nyomi la wananchi waliowazingira kila kona huku waandishi wa habari wakiwapiga picha.

Lakini mara tu walipopata Uhuru Babu Seya na Papii Kocha walielekea katika kanisa la Life Christian (Zoe) walipoenda kuonana na Mchungaji kwa ajili ya kupata maombi baada ya ombi Lao la kutoka jela kujibiwa.

 

 

 

Huu Ndio Ujumbe Wa Babu Seya Kwa Raisi Magufuli

Mwanamuziki Nguza Vicking au maarufu kama Babu Seya na watoto wake walifungwa jela miaka michache iliyopita amefunguka na kumwandikia barua Raisi Magufuli.

Babu Seya aliyefungwa kifungo cha maisha jela bila matumaini yoyote ya kutoka amefunguka na kumuangukia Raisi kwani ndio tumaini lake la mwisho.

Katika barua hiyo Babu seya aliandika;

“Naomba mwambieni Raisi Magufuli juhudi zake nazisikia, Mungu azidi kumpa maarifa azidi kuliongoza vyema jahazi la Watanzania. Raisi huyu nimependa hekima zake nami namfananisha na mwandishi wa makala za kitabu cha Mithali na Mhubiri. Mwambieni raisi nimeweka akiba yangu ya tumaini langu la mwisho kwake. Mungu ndio mfalme wangu Wa kwanza awezae kumaliza msiba wangu huu wa kuishi kwenye kuta za gereza”.

Aliendelea kumlilia Raisi;

“Wa pili ni yeye John Joseph awezae kunitenganisha mimi na maisha ya gerezani, siipendi ndoto yangu ya kufia gerezani, naichukia Kama tawala ya herode pale Galilaya, Naumwa na huku hakuna makaburi mazuri ya kuzikia wafu wetu. Mwambie aje anisaidie nije nifie mikononi mwa Mama yangu. Siku ntakayotoka ndio siku ntakapolivaa joho la uchungaji na nitapita mitaani kulihubiri neno la Mungu mpaka jasho langu ligeuke damu…NATUMAI KATIKA MKONO WA BWANA NA NINATUMAI KATIKA MKONO WA RAISI JOHN JOSEPH halleluyah tutaonana madhabahuni”.