Babu Tale Amjia Juu Mrisho Mpoto Kisa Diamond

Meneja wa staa wa Bongo fleva Diamond Platnumz, Babu Tale amejikuta akimtolea Povu zito Msanii wa muziki Mrisho Mpoto Baada ya Msanii huyo kuhudhuria msiba wa Ruge Mutahaba.

Siku chache zilizopita Mrisho Mpoto alimtaka Diamond aweke tofauti zake pembeni na Marehemu Ruge na ahudhurie msiba Wake na Kupitia ukurasa wake wa Instagram, alimuandikia ujumbe mzito.

Siku ya jumamosi Ruge aliagwa na wasanii Mbali Mbali na viongozi wa serikali katika viwanja vya Karimjee Hall na Diamond na timu yake ya WCB walihudhuria hafla hiyo.

Baada ya Diamond kuhudhuria hafla hiyo Mrisho Mpoto alitumia ukurasa wake wa Instagram kumshukuru Diamond kwa kuenda kauli iliyomkera Babu Tale ambapo alimjia juu Diamond na kusema kuwa hakuenda kwenye msiba kwa sababu yeye alimwambia.

Meneja wa Diamond Kukata Rufaa Kesi yake Dhidi ya Shekhe Mbonde

Meneja wa msanii Diamond Platinumz , Babu tale amefunguka na kusema kuwa baada ya hukumu ya kesi hiyo kutoka wameomba kukata rufaa katika kesi hiyo ambayo kampuni ya Tip Top Imekuwa ikishatakiwa kufanya uradufishaji wa baadhi ya kanda bila ruhusa ya aliyekuwa akimiliki.

Babu take anasema kuwa kwa sababu hakuwa amelizika na hukumu ya kesi hiyo imekuwa jambo la khri sana walipoambiwa kuwa wanaweza kukata rufaa na kutaka kesi hiyo kurudiwa kwa sababu hiyo.

Hata hivyo meneja huyo anasema kuwa mpaka alipofikia hatua ya kwenda mahakamni , ilikuwa haiwezekani tena kukaa chii kama wao na kufanya mazungumzo.

Ikumbukwe kuwa kesi hiyo iliwahi kumpeleka Babu Tale magereza ambako alisota kwa zaidi ya wiki nzima.

Fid Q Awaomba Radhi WCB Baada Ya Mgogoro Wa Wasafi Festival na Fiesta

Mwanamuziki wa hop hop nchini Fid Q ameibuka na kumuandikia ujumbe wa kumuomba radhi meneja wa Diamond Platnumz, Babu Tale mara Baada ya mgogoro wao.

Sakata hilo kati ya Fid Q na Wasafi lilianza maraa Baada ya Fid Q kuamua kufanya shoo kwenye Fiesta ya Clouds na kukataa kufanya shoo Wasafi Festival siku ya jumamosi tarehe 24.

Baada ya kufikia uamuzi wa kufanya show Fiesta alifanya tangazo la Tigo Fiesta ambalo linasambaa mtandaoni akitafsirikiwa kwamba alitupa dongo kwa Wasafi Festival.

Kupitia video hiyo, Fid alisikika akisema “Yani nyinyi mnataka kusubiri watu wafanye halafu na nyie mfanye, kawambie acheni upumbavu ni moja kubwa” kauli ambayo ilitafsiriwa ni dongo kwa kwambi hiyo.

Baada ya sintofahamu hiyo Fid q aliamua kutoa kauli yake huku akiomba radhi wa WCB kama walimtafsiri vibaya kwani hakuwa na nia ya kuwarushia vidongo.

PART 1: Nimeonelea si vibaya nikifungua hiki kigazeti changu na sentensi hii—-.> “ Keki ya taifa ni kubwa sana na ina vipande vingi vya kuwatosha wachakarikaji wote wenye kuistahiki “

Na kwakua Allah ndio mtoaji riziki, mimi kama mimi sina hayo mamlaka au hata hiyo roho mbaya ya kutamani wachakarikaji wenzangu mkwame ktk harakati zenu, ninasema hivi ni kwasababu siku zote huwa siamini kama nitapungukiwa kitu nyinyi mkifanikiwa, na siamini hivyo kwasababu ninajiamini mimi ni mchakarikaji na kipande changu cha KEKI bado kipo mezani kinaningojea ( cha muhimu ni PUMZI na DUA tu ).. ni ukweli tupo kwenye tasnia moja na kila mmoja wetu anajaribu kufanya lile alionalo sahihi ili kusogea mbele, na iko wazi mmeshafanya na mnaendelea kufanya mengi makubwa, nami bila kusita siku zote nimekua ni mtu wa kuwapongeza iwe kwa njia ya mitandao au tukutanapo ana kwa ana.. mie hufanya vile kiroho safi pasina chembe yoyote ya unafiki. ••••••••••••
Nimeyasema hayo hapo juu ili tu uweze au muweze kupata picha halisi ya kilichomo moyoni mwangu na pia kuwakumbusha ya kwamba mimi pia ninao uhuru wa kufanya shughuli zangu za sanaa na yeyote ambaye nimeridhia nae kimaslahi pasina kujali kama jicho la pembeni yangu linaiona faida iliyopo au laah.. sioni ni busara kwa nyie kuja na kujaribu kunipangia yupi nifanye nae au yupi nisifanye nae ili kuwaridhisha machoni/ mioyoni mwenu.. na kama mnaamini ni haki yenu ya msingi mimi kuyafuata hayo matakwa yenu basi naomba nikujuzeni ndugu zangu mtakua mmeonyesha UBINAFSI wa hali ya juu kwenye hili.. pia kumbukeni mimi pia nishawahi kuwa na matatizo na MJENGO.. lakini nilijikuta ninapambana peke yangu hadi UTULIVU uliporejea pasina msaada wa mtu yeyote.. na sikupambana peke yangu kwasababu hamkua na taarifa, taarifa mlikua nazo lakini ninafikiri mlikua mmetingwa na shughuli zenu za ujenzi wa taifa kiasi kwamba hamkuona kama kuniongezea nguvu ingesaidia lile zoezi kuisha haraka.. amini msiamini sijawahi kumuwekea mtu yeyote kinyongo kwenye hilo, na hiyo kitu ilinifunza sana juu ya suala zima la KUJIPAMBANIA MIE MWENYEWE kwenye situation yoyote ile na KUTOKUPIGANA VITA NISIYOIJUA au ISIYONIHUSU.

PART 2: Yote na yote.. Kiukweli yale maneno ya kwenye promo ya “MOJA KUBWA” sikutegemea kama yangekua na uzito huu uliopelekea ndugu yangu uchafukwe kiasi cha kunifungulia bomba la matusi humu insta.. kwanza sikumbuki hata kama niliyatamka kwa nia ya kuleta msigishano huu.. Lakini kama kweli nimewakwaza… Naomba mnisamehe kibinadamu kwa hilo ,naomba tumuache SHETANI apite na mwisho naomba nimalize kwa kusema.. BURUDANI sio VITA <hivyo ninawatakia kila la heri/ MAFANIKIO ya hali ya juu ktk MAPINDUZI YA BURUDANI huko MTWARA.. KEKI YA TAIFA NI KUBWA SANA NA INA VIPANDE VINGI VINAVYOTOSHA KUMFIKIA KILA ANAYESTAHIKI KWA KUDRA ZAKE MUWEZA WA VYOTE…. MAULID NJEMA ??”.

 

Hawa Atoa Shukrani Zake Kwa Diamond na WCB Baada Ya Kumaliza Matibabu

Msanii wa Bongo fleva Hawa Said maarufu kama Hawa ntarejea wa Diamond amevunja ukimya Mara Baada ya kumaliza matibabu nchini India na kumshukuru Diamond na WCB.

Msanii Diamond Platnumz na timu nzima ya WCB ndio ilisimamia matibabu yote ya Hawa mpaka anapiga kabisa Baada ya kuugua mpaka kutaka kufa miezi michache iliyopita.

Mrembo huyo amemshukuru Mungu pamoja na Watanzania kwa dua zao kwani mpaka sasa anaendelea vizuri na uvimbe wa tumbo umeondoka kwa asilimia kubwa.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Babu Tale ameweka wazi salamu kutoka kwa Hawa:

https://www.instagram.com/p/BqM4FSDlEiw/?utm_source=ig_share_sheet&igshid=1ex61xjcr1qbp

Awali msanii huyo wa kike aliripotiwa kuumwa ugonjwa wa ini lakini alipofanyiwa vipimo nchini India walimkuta na ugonjwa wa moyo.

Babu Tale Aweka Wazi Hali Ya Kiafya Ya Hawa Kwa Sasa

Meneja wa staa wa Bongo fleva nchini Diamond Platnumz, Babu Tale ameweka wazi kuwa Mwanadada Hawa Saidi ambaye alikuwa anatibiwa nchini India anaendelea vizuri.

Hawa alikuwa na tatizo la ini ila ni moyo ndio uliokua unapelekea mgonjwa kujaa maji mwilini na Babu Tale ndio alipewa jukumu la kusimamia matibabu yake nchini India kwa kuwa gharama zote za matibabu alizitoa Diamond Platnumz.

Hawa alikuwa na tatizo la ini ila ni moyo ndio uliokua unapelekea mgonjwa kujaa maji mwilini na Babu Tale ndio alipewa jukumu la kusimamia matibabu yake nchini India kwa kuwa gharama zote za matibabu alizitoa Diamond Platnumz.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Babu Tale amesema wazi kabisa kwa sasa Hali ya Hawa inaridhisha kabisa tofauti na siku chache zilizopita kabla ya kupata matibabu:

Diamond aliweka wazi kuwa ametumia zaidi ya milioni 490 kumtibia Hawa ambaye miezi michache iliyopita alikuwa hoi kitandani nchini Tanzania.

Babu Tale-Tumeshaanza Kuwasiliana na Uongozi Wa Ali Kiba

Meneja wa msanii wa Bongo fleva Diamond Platnumz, Babu Tale amefunguka na kuweka wazi mipango yao ya kumpata msanii wa Bongo fleva Ali Kiba ili aweze kuperfom kwenye tamasha la Wasafi Festival.

Siku ya Jana kwenye mkutano na waandishi wa Habari Mkurugenzi wa WCB, Diamond Platnumz aliweka wazi mipango yao  ya kumpata Ali Kiba ili aweze kuperfom kwenye shoo yao.

Lakini sasa Meneja wa Diamond Babu Tale anafunguka kuhusu jitihada zao za kuwasiliana na Kiba ambapo amekiri kuwa hana mawasiliano na Kiba lakini anaelewana sana na meneja wake anayeitwa Seven.

Siongeagi na Alikiba kivile, mimi naongeaga na meneja wake maana alishawahi kunisaidia sana, lakini kuhusu inshu ya Wasafi Festival Sallam ameshaanza kuwasiliana na uongozi wa Alikiba”.

Baby Tale ameweka wazi kuwa siku ya uzinduzi wa Wasafi festival pamoja na wasafi fm mbali ya kuwepo kwa mipango ya kumpata Ali Kiba lakini pjs atakuwepo msanii Konki konki konki master Dudu baya katika tamasha hilo ambalo limeandaliwa na Wasafi media.

Babu Tale Afunguka Baada Ya Tetesi Za Kumtelekeza Hawa India

Meneja wa staa wa Bongo fleva Diamond Platnumz, Babu Tale amefunguka baada ya maneno maneno kusemwa kuwa amemtelekza mrembo Hawa Said nchini India ambako anapata matibabu.

Wiki mbili zilizopita Babu Tale alimpeleka msanii Hawa kwa ajli ya matibabu nchini India baada ya kuifanyiwa vipimo na upasuaji mkubwa Babu Tale amerejea nchini siku chache zilizopita na kumuacha mgonjwa Nchini India.

.

Kwenye mahojiano aliyofanya na Global Publishers, Babu Tale alisema amerejea nchini na kumuacha Hawa India kwa kuwa msanii huyo anaendelea vizuri hivyo baada ya kushauriana na madaktari wake walimwambia asiwe na wasiwasi mgonjwa yupo sehemu salama hakuna ulazima wa yeye kuendelea kumsimamia muda wote.

Madaktari ndiyo walioniruhusu nirudi Bongo na wakanihakikishia hali ya mgonjwa wangu inaendelea vizuri baada ya kufanyiwa upasuaji mkubwa wa moyo hivyo hakuna ulazima wa mimi kuendelea kuwepo muda wote kama nitahitajika kwa lolote watanijusha.

Baada ya kupata kauli ya wataalamu hao nikaona nirudi nije kuendelea na mambo mengine huku nikiwasiliana nao kiukaribu zaidi”.

Hawa alipelekwa nchini India ambako walienda wakidhani ana ugonjwa wa ini lakini walikuta ana gonjwa wa moyo hii ni baada aliyekuwa mpenzi wake miaka ya nyuma msanii Diamond Platnumz kujitolea msaada huo.

Babu Tale Aweka Wazi Hali Ya Hawa Baada Ya Upasuaji Wa Moyo

Meneja wa staa wa Bongo fleva Diamond Platnumz, Babu Tale ambaye yupo nchini India kwa ajili ya kusimamia matibabu ya Msanii wa Hawa Said ameweka wazi kua anaendelea vyema baada ya upasuaji.

Hawa amefanyiwa upasuaji wa moyo chini ya madaktaru bingwa watano na sasa Babu Tale anasema Mrembo huyo amepata fahamu baada ya kufanyiwa upasuaji huo mkubwa.

Baada ya opersheni hiyo kufanyika Babu Tale ameandika:

 

Babu Tale Afungukia Matibabu Ya Hawa Nchini India na Ugonjwa Unaomsumbua

Meneja wa Msanii mkubwa wa Bongo fleva Diamond Platnumz, Babu Tale amefunguka na kutaja ugonjwa unaomsumbua Msama Hawa na kudai sio ini kama ilivyoaminika hapo Mwanzoni.

Wiki iliyopita Babu Tale aliondoka na Hawa kwa ajili ya kwenda kufanyiwa matibabu nchini India baada ya Diamond kujitolea msaada wa zaidi ya Milioni 450 kwa ajili ya matibabu yake.

Babu Tale ametoa taarifa kuwa  Hawa atafanyiwa upasuaji wa moyo jioni ya leo Lakini pia Wataalamu wameangalia kila kitu na hawajaona tatizo kwenye Ini kama iliyokuwa inaripotiwa awali.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram Babu Tale ameandika:

Asante Mungu tumefika salama India na tumefanya vipimo vyote upya salama na jibu lililotoka kwa wataalamu kwa asilimia 95% awajaona tatizo linalohusiana na ini kwa mgonjwa ila ni moyo ndio uliokua unapelekea mgonjwa kujaa maji mwilini ivyo basi kutaitajika kufanyika upasuaji mkubwa ambao utakua na uangalizi mkubwa wa wataamu then wametuakikishia baada ya hapo mgonjwa atapata nafuu na inawezekana izo 5% zilizobaki itakua poa na tatizo la ini alitokuwepo kikubwa tunaomba mtuombee dua na msiache kumuombea pia @diamondplatnumz apatenguvu ya kuendela kumsaidia kwa maana kutoa ni moyo. Kikubwa sana naomba tumuombee Hawa coz anaingia kwenye upasuaji mkubwa na hii ni atua ya yeye kua salama. Mungu tusimamie”.

 

Wasanii Wanaofanya Vizuri Tanzania Wanatoka WCB- Babu Tale

Meneja wa staa wa Bongo fleva na CEO wa WCB, Diamond Platnumz, Babu Tale amefunguka na kuweka wazi kuwa wasanii wote wanaofanya vizuri Kwenye gemu kwa sasa wanatoka WCB.

Kwenye mahojiano aliyofanya na Bongo 5, Babu Tale amedai hata watu wanune au waumie lakini ni ukweli usiopingika kuwa WCB ndio Label yenye wasanii wakali kwa sasa:

Wasanii wetu wote wanafanya vizuri,” alisema Babu Tale. “Wasanii wanaofanya vizuri nchini Tanzania kwa kipindi hichi wanatoka Wasafi iko wazi ukinuna ukiumia wasanii wanaofanya vizuri kwa kipindi hiki Wanatoka Wasafi”.

Babu Tale amepingana na vikali na baadhi ya maneno ambayo yamekuwa yakisemwa kuhusu mikataba ya WCB ambapo mapema wiki hii Mkurugenzi wa vipindi EFM, Sebo aliishauri kampuni hiyo kupitia upya mikataba ya wasanii wao kwani kitu ambacho kimetoka kwa msanii Rich Mavoko kwenda kulalamika BASATA hakikuleta picha nzuri kwa taasisi kubwa kama WCB.

Babu Tale amesisitiza kuwa Mikataba ya WCB ipo vizuri na wasanii wake wanaridhika na wanafanya kazi nzuri na ndio maaana wanatoa wasanii wakali na kazi zenye ubora:

Hatuna mpango wa kupitia mikataba wa wasanii wa WCB, mikataba ya wasanii wetu wote haina matatizo, kama unavyoona wasanii wetu wote wanafanya vizuri“.

 

Wanakamati Wengi Hawana Passport , Saizi Wamepanga Foleni NIDA ;-Babu Tale

Meneja wa msanii babu tale amefunguka na kusema kuwa pamoja na kwamba walitoa aahadi ya wasanii waliokuwa katika kamato  ya shughuli ya Zamaradi wanatakiwa kwenda afrika ya kusini kwa ajili ya party ya Tiffah lakini wanashindwa kwa sababu wasanii wengi waliokuwa katika mamati hawana passport za kusafiria.

Moja ya wasanii walijihakikishia uhakika wa safari ni pamoja na Shiloleh ambae yeye alisema kuwa tayari alishaombwa passport yake na daiamond na  tayari imekwisha shughulikiwa hivyo anasubiri safari.

Tatizo kinachokwamisha wanakati wengi hawana passport za kusafiria mpaka sasa wanapanga foleni NIDA wapate vitambulisho vya utaifa ili wakapate passport na nina wasiwasi hata Wema Sepetu passport hana.

Jux na Vanessa Wamewapa Changamoto Diamond na Wasafi Festival

Wasanii wa muziki wa Bongo fleva Juma Jux na Mpenzi wake Vanessa Mdee wamewapa changamoto kubwa Diamond na timu nzima ya WCB.

Jux na Vanessa ambao wamemaliza tour yao ya ‘In Love and Money’ ambayo imesemwa kufanya vizuri sana kuliko ilivyotegemewa wameonekana kuwapa changamoto WCB ambao nao wametangaza kuja na Tour yao ya Wasafi Festival.

Babu Tale ambaye ni Meneja wa Diamond na mratibu wa Wasafi Festival ameiambia Bongo 5, kwamba mafanikio makubwa na tamasha hilo ni changamoto kwa tamasha la Wasafi Festival ambayo litaanza kutimua vumbi miezi michache ijayo.

Hii ni ishara ya muziki unakuwa, nchi zilizoendelea kila mwisho wa wiki unajua kuna show kubwa, kwahiyo hii ni ishara nzuri ukiangalia Vanessa amejaza viwanja kibao. Mimi nikiwa kama kiongozi au mratibu wa Wasafi Festival inanipa changamoto naanza mkoa gani? sisi tunafanya show zaidi ya mikoa 12 na tunapiga na Dar es salaam inakuwa histori“.

Kutokana na mafanikio makubwa ya Tour ya Vanessa na Jux wasanii hao wametangaza kwenda nchini Rwanda, Burundi na Congo.

Babu Tale Ataja Mbadala wa Kazi Yake.

Meneja wa msanii diamond platinumz amefunguka na kuongelea kazi ambayo angeweza kuifanya endapo asingekuwa meneja wa diamond au kujihusisha na kiwanda cha muziki.

Babu tale ameyasema hayo alipokuwa akiongea na waandishinwa habari alipokuwa amehudhuri aktika show kali ya vannesa mdee na jux , tour iliyozunguka mikoani na kumalizawa na jijini Dar.Babu aleanasema kuwa yeye sio mtu wa kutoka sana usiku lakini leo ameona afanye hivyo kwa sababu ya vanesa na jux.

mimi sio mtu wa kutoka lakini nimefanya hivyo kwa ajili ya vanesa na jux, Baraza letu inabidi iangalie  wasanii wanapaswa kulaumiwa wapi au kurekebishwa wapi na kusimamiwa wapi kwa sababu ndio sehemu inayowapa pesa , hivu jiulize kwa mfano mimi nisingekuwa nasimamaia muziki si ningekuwa mganga wa kienyeji mkuyuni huko.

Babu tale amekuwa meneja wa Diamond kwa mudamrefu na kila siku msanii Diamond amekuwa akisema anajivunia sana uongozi wake kutokana na misingi mizuri wanayompa katika muziki na kazi zake.

 

Mke wa Babu Tale Afungukia Wivu wa Kimapenzi

Mke wa Babu Tale Shamira, ambaye ni Meneja wa staa wa Bongo fleva Diamond Platnumz amefungukia wivu wa mapenzi alionao kwa mume wake.

Mke wa Babu Tale amefunguka na kuongelea wivu wa mapenzi juu ya mume wake ambaye muda mwingi anakuwa na Diamond ambapo wanakuwa wanazungukwa na wanawake warembo.

Kwenye mahojiano na Bongo 5, Mke wa Babu Tale na aliulizwa anajisikiaje pale anapomuona mume wake akipiga picha na warembo mbalimbali wakati akiwa kwenye shughuli zake za kikazi.

Wivu upo lakini unategemea upo kwa kiwango gani na wivu ukiuendekeza mtakwama”.

Kwa upande wa Babu Tale alidai kwa kuwa yupo kwenye tasnia ya burudani kwa muda mrefu amejifunza hawezi tembea na mke wake kila sehemu ila mkiwa mnaaminiana inakuwa jambo jema zaidi.

Nina Wivu Sana kwa Mume wangu Hasa Akitoka Bila Mimi :-Mke wa Babu Tale

Mke  wa bosi wa Diamond Platinumz , Babu Tale amefunguka na kusema kuwa ana kuwa anaona wivu sana pale mume wake anapotoka nyumbani bila kuambatana nae tena hasa anapojua kabisa kuwa mtoko anaotoka sio wa kikazi zaidi.

Maneno hayo aliyaongea mwanadada huyo alipokuwa akihojiwa wikiend hii alipokuwa ameambatana na mume wake katika sherehe nyumbani kwa zamaradi huko Bunju jijini Dar, ambapo mwandishi laimuuliza kuwa je mwanadada huyo huwa anajisikiaje pale anapoona mume wake akiwa anapiga picha na warembo wengine na picha hzio zikawekwa katika mitandao ya kijamii.

mwanadada huyo alisema kuwa wivu unakuwepo lakini haweiz kuendekeza kitu hicho maana anajua atharibu kazi “wivu upo lakini ndo inategemea upo kwa kiwango gani, na ukiendekeza wivu unakwama

Na hata Babu tale alipoulizwa kuhusu kuambatana na mke mkewe baadhi ya sehemu alisema kuwa siku hiyo aliambatana nae kwa sababu hiyo ni sherehe ya kifamilia na wala sio ya kikazi.

Almas Mzambele Afunguka na Kudai Babu Tale Ataiua WCB

Almas Mzambele ambaye alikuwa mfanyakazi wa WCB kwa miaka mingi kabla hajaonekana amefunguka na kudai mtu pekee ambaye ataiua WCB ni Meneja Babu Tale.

Almasi Mzambele alikuwa mtu ambaye alikuwa anashughulikia mambo ya mitandao ya kijamii WCB amefunguka kwa mara ya kwanza tangu ameondoka kwenye Label hiyo.

Kwenye mahojiano na Bongo 5, Almas amefunguka mazito juu ya uongozi wa kampuni hiyo ambao ndio amedai una matatizo zaidi na unaweza kuua Label hiyo.

Tatizo pale lipo  kwenye uongozi wa WCB ambapo mwenye matatizo zaidi ni Babu Tale anayejiita meneja namba moja yaani anavuruga watu mpaka wanaacha kazi sio mchezo.

Babu Tale ndio mtu anayepelekea kuiua WCB kuna vitu vingi anakuwa anavifanya nyuma ya pazia ambavyo kama watu wangevifahamu sidhani kama wangetamani kumuona yeye anaendelea kuwa na Diamond kwa sababu naamini huko mbeleni sidhani kama tutaendelea kumuona Diamond huyu tunayemuona sasahivi”.

Lakini pia Almas aliendelea kutaja maovu ya Babu Tale:

Yaani kifupi tu Babu Tale ni mbinafsi na ni mmwinyi anapenda yeye ndio aonekane msemaji wa mwisho k a sababu ndio ametangulia kufahamiana na Diamond kwaiyo mkitofautiana mtazamo tu basi yeye anaanza kuleta visa vyake”.