Msiba Watengeneza Bifu Zito Kati Ya Isabela na Baby Madaha

Msanii wa muziki wa Bongo fleva Baby Madaha na msanii mwenzake wa Bongo movie Isabela wamedaiwa kuwa kwenye Bifu zito na kisa kinatajwa ni msiba.

Global Publishers wanaripoti kuwa wawili hao ambao walikuwa marafiki walioshibana kwa sasa wamekuwa maadui chanzo kikitajwa ni Baby Madaha kutohudhuria mazishi ya dada wa Isabela ambaye alifariki dunia hivi karibuni.

Katika mahojiano na GPL,  Isabela aliulizwa  kuhusiana na hilo alisema ni kweli hampendi Baby Madaha na urafiki wao umeshavunjika kwani alishindwa kumpa ushirikiano alipofiwa na dada yake jambo ambalo linamuumiza mpaka sasa.

Kitendo cha kutokuja kwenye msiba wa dada yangu kiliniuma sana na mpaka sasa naumia maana Baby Madaha ni rafiki yangu wa damu, aliniachia msiba nizike peke yangu na anajua fika kwamba yeye ndiye rafiki yangu mkubwa nimekasirika sana huo ndiyo ukweli“.

Lakini Baby madaha amesema kuwa hana Bifu na Isabela na yeye mwenyewe anajua kwanini hakuhudhuria mazishi ya dada yake kwani alikuwa nje ya nchi.

 

Baby Madaha- Napenda Sana Kufanya Tendo La Ndoa

Msanii wa muziki wa Bongo fleva aliyewahi kutamba na vibao vikali kama vile ‘Amore’ amefunguka na kudai anapendelea sana kufanya tendo la ndoa.

Baby Madaha ametoa kali hiyo ya mwaka na kuwashangaza wengi baada ya kusema starehe pekee anayoipenda ni kufanya tendo la ndoa na anaweza kufanya hata mara nne kwa wiki.

Kwenye mahojiano na Gazeti la Amani, Baby Madaha alisema tendo hilo huwa anapenda kulifanya mara nyingi zaidi pindi anapokuwa na fedha mfukoni.

Napenda kufanya nikiwa niko vizuri sana mfukoni, akili yangu yote iwe hapo tu yaani kwa wiki naweza kufanya hata zaidi ya mara nne”.

 

Baby Madaha Awatolea Uvivu Wanaume wa Kibongo

Msanii wa Bongo fleva Baby Madaha amewapa makavu ya Uso wanaume wa Dar na kudai ni Matapeli wa mapenzi.

Baby Madaha amefunguka na kuwatolea uvivu wanaume wa Kibongo huku akiweka wazi kuwa kutoka na wanaume hawa ni kujitia tu nuksi kwani huishia kukupotezea muda na kukutosa.

Kwenye mahojiano na Global Publishers ,Baby  Madaha alisema kuwa watu wengi hawamuelewi kwa nini hawajawahi kumuona na mwanaume au kumnadi mpenzi wake mitandaoni kwa sababu hapendi kabisa kutoka kimapenzi na Mbongo.

Watakuja kunisikia tu nimeolewa huko nje ndio watajua ninachomaanisha, sipendi kabisa kumpa penzi Mmbongo kwa sababu wengi wababaishaji na wanajua kutiana nuksi sana kwakweli“.

Wanaume wa Kibongo nao wamekuwa wakisema hayo hayo mambo kuhusu wanawake hadi wengine hasa mastaa wa kiume wameonekana wakienda kuoa nje ya nchi kwa kuwakimbia watoto wa kike wa kibongo.

Baby Madaha Adaiwa Kutimuliwa Kwenye Nyumba Ya Kupanga Baada Kushindwa Kulipa Kodi

Mwanamuziki wa Bongo fleva aliyewahi kutamba na wimbo wake wa ‘Amore’ Baby Madaha amefungukia tetesi za yeye kutimuliwa kwenye nyumba aliyokuwa amepanga baada ya kushindwa kulipa kodi ya nyumba hiyo.

Habari zimetapakaa mtandaoni kuwa Baby Madaha amefulia vibaya kiasi ya kwamba hajiwezi hata kulipa kodi ya nyumbani kwake alipopanga jambo lililomlazimu kuhamia kwa shoga yake Isabela Mpanda ‘Bela Fastaa’ maeneo ya Mbezi Beach.

Taarifa za chini ya kapeti za kimbea zaidi zimedai kuwa mambo yamemuendea kambo staa huyo hii ni kutokana na ukimya wake Kwenye muziki hasa kushindwa kutoa hit song na biashara zake zimebuma jambo linalompelekea kufulia kufika hadi hatua ya kukosa pesa.

Kwenye mahojiano aliyofanya na kituo kimoja cha habari Baby Madaha amekataa kata kata tuhuma hizo na kudai kuwa hazina ukweli wowote:

Hayo ni maneno tu ya watu waliokuwa na chuki na mimi si kweli kama nimefulia na ifahamike kuwa siku nyingi nakuwa niko Dubai nafanya shughuli zangu ninapokuja Tanzania na kufikia kwa Bella siyo tatizo”.

Lakini pia Baby Madaha amedai kuwa yeye haishi Dar kwa sasa kwaiyo haitaji nyumba hivyo akifikia kwa marafiki sio mbaya:

Nilirudi Bongo hivi karibuni kwa ajili ya harusi ya mdogo wangu na siishi hapa kwaiyo suala la kushindwa kulipa kodi na kuenda kuishi kwa Bela halina mshtuko”.