Baby Madaha aendelea kumchana Vanessa Mdee

Muimbaji Baby Madaha ameonekana kuwa na uchungu na mwenzake, Vanessa Mdee. Hivi karibuni alisema kuwa Vmoney hana kipaji chat kuwa msanii ambaye anatajwa kuwania tuzo zozote za muziki.

Baby J
Baby Madaha

Hata hivyo Baby Madaha haonekani kujuta kwa kusema maneno haya. Hivi karibuni akiongea na Bongo 5 Baby Madaha alidai kuwa kuna wasanii wakali kumshinda mrembo huyu wa Jux . Kulingana na Madaha, Vmoney bado hajafikia kitengo cha kuwania tuzo za kimataifa Kama anavyofanya kwa sasa. Madaha alisema,

“Mimi si shabiki wa Vanessa hata muziki wake, hata nyimbo zake sizisikilizi kabasa,”

Aliendelea kusema kuwa yeye anawatambua wasanii Kama Lady Jaydee na wengi even ambao wameonyesha talanta zao za kuimba kupitia mziki mzuri ambao wameachana. Aliongeza,

“Kuna wasanii wakali hawapewi tu nafasi, mimi ni shabiki wa Lady Jaydee, akina Mwasiti kuna wasanii wengi wanafanya muziki nzuri,”

Hata hivyo alisema kuwa yeye hana wivu kwa Vanessa Mdee ila tu ni maoni yake.

Kuna nini Kati ya Vanessa Mdee na baby Madaha?

Msanii wa Bongo baby Madaha amedai kuwa kwenye industry ya bongo hakuna waimbaji wa kike ambao wanatalanta ya kuwafanya kuwania Tuzo za kimataifa.

Akizungumza na watangazaji wa Sibuka FM katika kipindi cha 180 Power, Byno na Joco, baby Madaha aliskika akimgusa Vanessa Mdee kwa kusema kuwa kunawaimbaji wa kike ambao hutajwa kuwania tuzo mbalimbali ilhali hawashindi hata moja.

Hata hivyo maneno yake yalionekana kumlenga vanessa ambaye nimsanii wa kike kutoka Tanzania ambaye amewania tuzo kadhaa. Baby Madaha alisema,

“Tunapeleka watu kuwania tuzo wengine hawana vigezo vya hizo tuzo, especially nazungumzia kwa madada kuna dada mmoja yaani kila tuzo anaendaga lakini ashindi kutokana na nini hana qualification za hizo tuzo,”