“Naj Hakujua Kama Nabadilisha Dini”- Barakah The Prince

Msanii wa muziki wa Bongo fleva Barakah The Prince ameibuka na kudai Mpenzi wake Naj hakuwa na taarifa kuwa amebadilisha dini.

Barakah amefunguka hayo Baada ya tetesi kusambaa kwenye mitandao ya kijamii kuwa Barakah amebadili dini kisa mpenzi wake Naj ambaye ni  Muislamu.

Katika mahojiano yake na mtandao wa Dizzim Online, Barakah ameweka wazi kuwa alipofikia uwamuzi wa kubadilisha dini hakumshirikisha mpenzi wake Naj mpaka zoezi lile lilipokamilika:

Ni kweli kabisa nimebadili dini kutoka ukristo na kuwa Muislamu na hivi sasa naitwa Abdulmalik na nilifanya kwa maamuzi yangu mwenyewe kwa sababu mimi sio wa kwanza, kuna ndugu zangu kibao kwenye familia yangu wamekwisha badilisha dini na Naj mwenyewe hakujua kama nimebadilisha dini mpaka alivyoona mtandaoni, nilimficha sikutaka ajue”.

Taarifa zilisambaa Kuwa huenda Barakah aliamua kubadilisha dini ili apate kufunga ndoa na mpenzi wake huyo ambaye anaishi majuu kwa sasa.

Barakah The Prince Adaiwa Kabadili Dini Kisa Mpenzi Wake Naj

Msanii wa muziki wa Bongo fleva Barakah The Prince amethibitisha taarifa za yeye kubadilisha dini lakini inadaiwa amebadilisha dini kwa ajili ya mpenzi wake Naj.

Barakah ambaye alikuwa muumini ya dini ya kikristo amesemekana kubadilisha dini na kuhamia katika imani ya Kiislamu kwa ajili ya mpenzi wake Naj ambaye ni muislamu pia.

Kwenye Interview aliyofanya hivi karibuni na kituo kimoja cha habari Barakah amethibitisha kuwa amebadilisha dini yake:

Ujue mambo ya dini bro ni imani, sio rahisi kama wengine wanavyochukulia hivyo mpaka unaikana imani unakua umeamua sana, umefatilia umejua faida na hasara zake“.

Ingawa Barakah hajaweka wazi sababu kabisa ya kubadilisha dini yake lakini inasemekana amefanya hivyo ili aweze kumuoa mpenzi wake Naj ambaye tayari ni muislamu.