Baraka Avamiwa Studio na Mwanadada Aliyesema Amemtapeli

Siku chache zilizopita moja ya wadada wa mjini walifumuka na kusema kuwa wametapeliwa na msanii Baraka the prince shilingi milioni tano ambazo alimpa kama zawadi kutokana na kumpenda lakini pa kutaka kumsaidia katika muziki.

Wawili hao walitegemewa kuingia katika mapenzi endapo wangekubaliana ilhali tayari Baraka alikuwa amekwisha chukua kiasi cha pesa walizokubaliana lakini cha ajabu hakufanya chochote kwa dada huyo zaidi ya kutumia pesa hiyo kununua gari.

Siku ya jana , baraka alikuwa studia ya Clouds media akitambulisha wimbo wake mpya ndipo ghafa mwanadada huyo alipotokea studio hapo bila taarifa ya Baraka wala waaandishi wa habari waliokuwepo eneo hilo na kuanza kudai pesa yake.

Huku akiongea kwa jazba , dada huyo alisema kuwa Baraka ni tapeli na muongo na anamdai pesa yake zaidi ya milioni 5 ambayo aliitaka muda huo la sivyo aache gari.

Mwanadad huyo aliejulikana kama Sex Dina alitaka kujua muafaka wa pesa yake kwa sababu tangu alipomtoa Baraka polisi  na kukubaliana kurudishiana pesa hiyo lakini Baraka hukuwahi kuonana na dada huyo wala kutaka kuwasiliana nae tena.

 

Baraka The Prince Mbaroni kwa Utapeli Wa Mapenzi

Msaii wa bongo fleva Baraka The Prince ametiwa mbaroni baada ya kusemwa kuwa amemtapeli mwanadada mmoja ambae inasemekana akuwa alimpatia pesa kaisi cha shilingi milioni tano kwa ajili ya kuwa nae katika mahusiano lakini ilishindikana.

Tetesi zinadai kuwa mwanadada huyo aliamua kumpeleka baraka polisi baada ya kukubaliana kupatiana penzi kwa shilingi milioni tano lakini Baraka alishindwa kufanikisha hilo na ndipo walipofikishana polisi.

Hata hivyo tetesi zinasema kuwa baraka alipokea pesa hiyo lakini Alishindwa kutekeleza huku pesa hiyo akiamua kuinunulia gari.

Baraka :-Sishei Kitu na Mtu Kwenye Page Yangu , na Sitemegei Hivyo Kutoka Kwao

Msanii Baraka The Prince amesema kuwa yeye hawezi kukaa kutegemea msanii mwenzie amposti kwenye page yake huku akiweka wazi kuwa hashei kitu cha  msanii kwenye pegi yake.

Baraka amesema kuwa ukitegemea sana Support unafeli na hasa ukitegemea wasanii kwasababu akisema wao kama wana suppotiana ni unafki. “Sitakaa nikaitaji page ya artist kwasababu still ye wale mashabiki wake, mimi sishare kitu cha mtu kwenye page yangu kabisa na ukiona nimepost mtu jua kaniomba sana na mimi nikishare kitu chako other wise nimekipenda sana,” amesema Baraka.

Baraka anasema kuwa ukitegema kupewa sapoti na watu kila siku ipo siku utaikosa na utajikuta unaanguka vibaya sana, lakini pia anasema kuwa wasanii wengi wamekuwa waitaka kuzionyesha jamii kuwa wanapenana sapoti lakini ukwlei ni kwamba mioyoni mwao wanakuwa na kinyongo na mafanikio ya mtu.

Ukitegemea sana support watu tunafeli sana kwa kutegemea support , tusidanganyane kwamba maartist wote tunasupotiana huo ni unafki tunaionyesha jamii ile kwamba tunasapotiana lakini real na kwenye moyo kabisa hakuna kabisa mtu kabisa eti anamsapoti mtu kiroho safi na ndio maana mimi huwaga na tabia moja siwei kuanza kukwambia kuwa nimekutumia kitu siwezi kukupigia kwamba we ushee inafaa wewe kusuport utapost,” amesema Baracka kwenye kipindi cha The Playlist cha Times FM.

BarakaAomba Kisiwa cha Mbudya Kifungwe

Mwanamuziki Baraka The Prince amefunguka na kuishauri serikali kuwa kwa muda ambao yameshatokea matatizo mengi katika kisiwa cha Mbudya abasi ni bora kisiwa icho kingefungwa kwa muda mpaka pale kutakapo boreshwa na kuwekwa kwa huduma za msingi katika kisiwa icho.

Baraka anasema kuwa kisiwa icho kimekuwa kikiingiza pesa kwa sababu ya watu wengi wanaoenda huko hivyo uweoz wa kuweka maboresho unawezekana na kama haiwezekani basi ni bora kukifungwa kwanza.

Kisiwa hicho kimekuwa hatarishi kwa maisha ya binadamu na hata kupoteza maisha ya watu weng sana kutokana na mazingira yake kuwa hatarishi, hata hivyo wasaii wanazidi kuguswa na swala hilo kutokana na kuwa wamkuwa wakienda na kuona matukio ya vifo vya watu mara  nyingi  na hata hivi karibuni kupoteza producer Pancho Latino.

Malalamiko hayo yamekuwa yakitolewa na watu tofauti tofauti na sasa ni jukumu la serikali na uongzo wa kisiwa icho kurekebisha baadhi ya vitu vya muhimu ili kuokoa maisha ya watu.

Wasanii Tunafeli kwa Sababu ya Ujanja Ujanja Wetu :-Baraka The Prince

Msanii wa muziki wa bongo fleva Baraka the Prince ameamua kuwashauri wasanii wengine ambao kila siku wamekuwa wakilalamika kuhusu maonnvu ya Basata kuacha kulalamika na kufanya kitu cha maana kuokoa muziki wao na sio kukaa tu huku waksiema basata hawafanayi sawa.

Baraka anasema kuwa jambo muhimu la kufanya ni kufuata sheria na kanuni zinazohitajika kufuatwa na sio kufanya vitu amabavyo havina msingi na vinavyokatazwa na mamlaka kam ambavyo yeye anafanya amekuwa akifuata sheria na ndio maana amekuwa hasumbuliwi kila mara,

Baraka anashauri kuwa huu ni wakati wa wasanii kuandamana na kwenda Basata na kuwaiskiliza wanataka nini kwa kukaa chini na kuongea nao na wakishaambiwa cha kufanya wao pia wakae wawaombe Basata kuwa na wao wanaona hapa iwe hivi na hivi.

Bakara anasema kuwa wasanii wengi wamezea kufanya kazi kwa ujanja ujanja bila kujua kuwa kuna tofauti za nyakati kati ya enzi za Magufuli na sasa ni tofauti kabisa.

 

Baraka The Prince Amuangukia Mange Kimambi.

Mwanamuziki Baraka The Prince amemuangukia Mange Kimambi na kumuomba msamaha baada ya mwanadada huyo kutoa taarif za siri ambazo hazijawahi kusikika mahali popote kuhusu mwanamuziki huyo kuwa na mahusiano na mwanadada kutoka bongo movies.

Mange Kimambi ambae amkeuwa akitoa siri na kukosoa wasanii wengi kila kukicha siku ya jana alimuamkia Wema sepetu baada ya wema kuonekana kulivalia njuga swala la Hamisa kutaka kuiloga familia ya kina diamond kama voice notes iliyovuja ilivyokuwa ikisema.

Hata hivyo baada ya Mange kuamua kutoa siri za Wema moja kati ya vitu alivyoongea ilikuwa ni kwamba mwanadada Wema alishawahi kuwa na mahusiano ya kimapenzi na BARAKA lakini haikuwahi kufahamiaka hapo kabla.

Baraka The Prince kupitia ukurasa wake aliamua kuandika barua ya wazi kwa Mange huku akimuomba asimuharibie muziki wake kwa kutangaza habari kama hizo ambazo hazina ukweli ndani yake.

Baraka anamuomba mange kuangalia upy vyanzo vyake huku akimuelezea kuwa amekuwa akiangaika sana kutengeneza jina lake na brand yake hivyo akimchafua kwa sasa anakuwa kama anamuharibia sana.

Baraka aliwaomba mashabiki wake msamha akwa kilichoandikwa katika page ya mwanadada huyo huku akiaknusha kuwa kuliwahi kuwa na ukaribu wa kiampenzi kati yake na Wema sepetu na kusema kuwa amekuwa akimheshimu sana Wema .

 

Baraka Atangaza Kuachana na Naj , Asema Yuko Single.

Msanii wa  bongo fleva kutoka katika lebel ya bana music , Baraka the prince amethibitisha kuachana na mpenzi wake wa siku nyingi Naj  Datan ambae muda mwingi amekuwa akiihsi nje ya nchini.

Katika ukurasa wake wa instagram, Baraka aliweka ujumbe wenye maana kuwa sasa hivi yuko single na hakuna mahusiano kati ayke na mwanamke yoyote kitu kinachofanya kupigia mstari kuwa hayuko katika mapenzi tena na naj.

Ikumbukwe kuwa hivi karibuni kulitokea teesi kuwa msanii huyo Baraka the prince alibadilisha dini ili kufuata dini ya mwanadada Naj, hivyo kama wameachana bado haijajulikana kama msanii huyo atabaki katika dini aliyobadilisha au atarudi katika dini yake.

“Ali Kiba ni Msanii Mkubwa na Amenifundisha Mambo Mengi Kwenye Muziki”-Barakah The Prince

Msanii wa muziki wa Bongo fleva Barakah The Prince amempa heshima msanii mkongwe wa Bongo fleva Ali Kiba na kudai ni msanii mwenye experience kubwa Kwenye Bongo fleva.

Barakah alikuwa chini ya Label ya Rockstar 4000 ambayo inaendeshwa na Ali Kiba lakini baada ya miaka michache ndani ya Label hiyo BAraka alitangaza kujitoa na kuanza kufanya Muziki wake mwenyewe.

Baada ya kutoka Rockstar Baraka aliwatuhumu kwa kufanya njema mbali mbali za kumrudisha nyuma kimuziki ikiwemo mapema mwaka huu aliwatuhumu kwa kufuta nyimbo zake Youtube.

Lakini sasa inaelekea Baraka amerudi katika nafasi nzuri na Ali Kiba kwani Kwenye Interview yake na kipindi cha refresh cha Wasafi Tv, Baraka amemtaja Ali Kiba kama mtu aliyemfundisha mambo mengi kwenye sanaa kutokana na experience yake;

Ali Kiba ni mkubwa na ana experience Kwenye Industry more than me kwaiyo muda ambao nilikuwa naye nilijifunza vitu vingi Kimuziki na kusema kweli nilikuwa niijua thamani yangu kama msanii na nilijua nini natakiwa kufanya ili kufanikiwa maana yeye ameshakula matunda ya Muziki wetu”.

Barakah amesema kwa sasa hana mpango wa kusainiwa chini ya label yoyote hapa Tanzania labda hapo baadae.

Baraka The Prince Amuumbua Rommy Jones

Msanii wa bongo fleva Baraka The Prince ameshindwa kuvumilia kwa muda mrefu kitedno alichokifanya rommy jones na kuamua kumuumbua katika mitandao ya kijamii.Ingawa barak the prince hakutaka moja kwa moja kusema kile alichokifanya rommy jones lakini siri ilikuja kuvuja na kusambaa katika mitandao ya kijamii.

Katika ukurasa wake wa instagram, Baraka The Prince aliweka picha ya Rommy Jones na kuandika caption hii”unaonekana mwana kumbe pimbi tu,hata hilo vazi uliovaa pia unalitia aibu tu,shenzi typ soon  nakutia aibu jamaa..next post nakutia aibu wack wewe..

hata hivyo baada ya baraka kushindwa kuweka moja kwa moja kosa la rommy, dada yake na rommy anaejulikana kama ladynaha aliamua kuweka wazi picha za meseji ambazo rommy alikuwa akichat na najdattan akiwa anamtongoza.

Picha hizo ndizo zilizosambaa sana katika mitandao na kufanya siri kuvuja na kitu gani kilifanya baraka aandike maneno yale kwa Rommy.

Baraka the Prince:Nisingekuwa Msanii Ningekuwa Mwanajeshi.

Msanii wa muziki wa bongo fleva nchini Baraka the Prince amefunguka na kusema kuwa endapo hasingekuwa katika tasnia ya muziki basi angekuwa anafanya kazi ya uanajeshi kwa sababu anaona kabisa kuwa ni kazi anayoendana nayo na anahimili kuifanya.

Baraka ambae alikuwa akifanya mahojiano na kipindi cha Eight cha TVE, anasema kuwa anapenda kazi ya uanajeshi na kusema vitu vitano ambavyo vinamvutia sana kwa wanajeshi.

napenda sana mazoezi ya wanajeshi, napenda na ule mchaka mchaka  wao, lakini pia napenda hata mavazi yao , napenda attitude yao   na pia ni wakarimu sana nawapenda hapo lakini pia  napenda the way walivyo.

Baraka the Prince ambae kwa sasa anatamba na kibao cha sometimes anafanya kazi chini ya lebo yake mpya aliyotengeneza mwenyewe inayojulikana kama Bana Music baada ya kutoka katika uongozi wa Rockstar4000  ambapo walikuwa wakifanya kazi pamoja na Alikiba na ndipo alipo Ommy Dimpoz kwa sasa.

 

Baraka The Prince Awasili Kwa Tundu Lissu

Yawezekana Baraka akawa ndio msanii wa kwanza kwenda kumtembelea Mh.Tundu Lissu tangu alipokutwa na matukio ya kupigwa risasi nyingi na kuwa mahututi kwa kipindi cha zaidi ya miezi miwili sasa.Jana,kuanza kwa  mwaka 2018 umeanza vizuri kwa Baraka na kwa Mh.Tundu Lissu pia baada ya wawili hao kupata bahati ya kuonana kwa mara ya kwanza tangu amepata majanga hayo.

Wasanii wengi walihaidi kwenda kumuona  mwanaharakati huyo akiwemo Wema Sepetu kipindi bado hajahama kutoka CHADEMA  kwenda CCM, lakini ndoto hiyo ilikatika baada ya mwanadada huyo kuhamia tena CCM.

Baraka The Prince ametua Nairobi na kwenda moja kwa moja mpaka hospitali aliyolalazwa Tundu Lissu kwa ajili ya kwenda kumjulia hali alkini bado haijajulikana kama Baraka The Prince aliamua kufunga safari tu mpaka Nairobi kwa ajili ya kumuona tu mwanasiasa huyo au alikuwa na shoo nchini humo au kuna kitu cha ziada zaidi ya hicho.

Hata hivyo mashabiki wa Baraka na wanachama na watu wengi wamefurahishwa na kitendo cha msanii huyo kujitokeza kama msanii wa kwanza kwenda kumuona mwanasiasa huyo kwa sababu tangu amepata matatizo wapo wasanii wengi wanaoimba harakati lakini hawajapata bahati ya kwenda kumuona huku baadhi ya mashabiki wakihisi kuwa huo ndio mwanzo wa msanii huyo kuanza kujiingiza katika siasa.

Baraka Aendelea Kuwatuhumu Uongozi Wa Alikiba

Msanii anaefanya vizuri na kibao chake cha Sometimes Baraka the Prince, amefunguka na kusema kuwa kuna kipindi uongozi wa msanii alikiba walikuwa wakimfanyia figisu kwa ma-DJ ili wasicheze nyimbo zake katika media mbalimbali ili kuweza kumdidimiza.Hata hivyo msanii huyo anasema kuwa pamoja na kwamba walikuwa wakifanya kwa siri lakini alikuwa akiambiwa na baadhi ya watu hao kwa sababu alikuwa akiongea nao vizuri na walikuwa hawapendezwi na kitu hicho.

Kuna baadhi ya DJ’s walikuwa wakiambiwa wasicheze nyimbo zangu wengine mpaka walikuwa wakipewa ela kwa ajili tu ya kutokupiga nyimbo zangu lakini ndo hivyo unakuta Dj anakufata  anakwambia unajua nimeambiwa nisipige nyimbo zako na ela nimepewa kabisa .

Kwaio hicho ni kitu cha kushukuru kwa sababu watu wangekuwa hawanipendi na siongei nao vizuri kama inavyoenezwa sidhani kama kuna mtu angewza kunifuata na kuthubutu kuniambia  taarifa kama hizo kabisa .This means napendwa na watu na tayari nina Empire yangu tayari.

Baraka the Prince amekuwa akisema kuwa uongozi uluipita wa Rock400 umekuwa ukimfanyia michezo mibaya mara tu baada ya kuondoka katika uongozi huo huku wakitaka afe kimuziki, hii sio mara ya kwanza kwa baraka kutoa lawama kwa uongozi huo na baadhi ya watu maarufu katika kiwanda cha muziki kuhusu kumrudisha nyuma katika muziki.

Baraka the Prince na Alikiba walikuwa katika menejiment moja ya Rock400 inayopatikana nchi south afrika lakini msani Baraka the Prince aliamua kujiondoa huko na kufanya kazi zake.Hata hivyo baada ya kuamua kufanya kazi mwenyewe alijikuta akiingia katika migogoro na baadhi ya watu katika muziki huku akimtuhumu kila aliyehisi ni mbaya wake kwa kuhususha muziki wake.

 

 

Mx Carter:Baraka The Prince Anahitaji Msaada,Ana Stress.

Moja ya mameneja wakubwa  nchini Mx Carter ambae kwa sasa amekuwa akimliki Shetta na Aslay , amefunguka na kuongelea tuhuma ambazo Baraka The Prince amekuwa akiwatupia wasanii wenzie kuhusu kuchezewa kwa acount yake ya you tube na kushusha idadi ya mashabiki kama alivyokuwa akilalamika mwenyewe.

Mx Carter ambae ni mmoja wa wakala ya youtube Tanzania kupitia kampuni yake ya Ngoma amesema kuwa Baraka alimfuata mwenyewe na kumwambia kuwa anataka kufuta account yake ya you tube kwa sababu hawaamini sana wasanii wenzie aliokuwa akifanya nao kazi huko na kuomba atengenezewe account mpya.Meneja huyo amesema kuwa anahisi kabisa Baraka kwa sasa atakuwa na stress hivyo  anahitaji mtu wa kuongea nae kwa msaada zaidi kwa sababu mambo anayofanya yanashangaza watu.

Baraka haeleweki , alinifuata akaniomba nifute hiyo account, lakini cha kushangaza anafanya interview  kila media anaongea tofauti,hata ukiangalia comments za watu wengi baada ya interview wamekuwa wakishangazwa na wanashindwa kumuelewa kitu gani kinachokuwa kinamchanganya.Ananiomba msamaha  ya kwamba amenikosea kwani alikuwa hajui kitu anakifanya, nafikiri  ana stress tunaweza kukaa chini tukamshauri ili kumsaidia.– Alifunguka Mx Carter

Akiongea na eNews ya EATV,Mx Carter anasema kuwa hata hivyo balaa hilo la account yake ya youtube kwa sasa limehamia mpaka kwa msanii mwingine akimtaja shilole  akisema kuwa ndie aliemwambia kuwa Mx Carter ndie alikuwa akichezea account yake hiyo na kusababisha hayo yote.

Sasa kama anagombana na watu kwa style hii hata akija na shida tena siwezi kumsaidia kwa 100% , hapa ninapokwambia kashaanzisha mtiti sehemu nyingine ,amesema kuwa Shilole ndie aliemsababishia yeye aseme hivyo,kwaio sasa hivi hapatani na Shilole kwa mantiki hiyo Shilole hawezi kumpostia video yake tena. -Aliongeza meneja huyo

Akiwa kama mmoja wa wataalamu wa mitandao Mx Carter amesema kuwa kitendo cha mtu kupunguza mashbaiki katika account yako ya youtube ina maana mtu huyo anakuwa ameingia katika server za youtube na ni kitu ambacho akiwezekani.

Hivi karibuni Baraka amekuwa akitapatapa na kutuhumu watu kadhaa akisema kuwa ndio wanaofanya muziki wake ushuke thamani youtube baada ya kuachia ngoma yake mpya ya Sometimes ,huku akituhumu watu hao kuwa ndio wanaochezea account yake.

Baraka The Prince Kusajiliwa Wasafi

Msanii wa muziki kutoka nchini  Tanzania ambae hivi karibuni amekuja na wimbo mpya unaojulikana  kwa jina la Sometimes,Baraka the prince  amesadikika kusajiliwa na lebel kubwa nchini ya  Wasafi (WCB) baada ya kutoka katika lebel ya kwanza alikuwepo ambayo pia alikuwa akifanya kazi na msanii mwingine mkubwa Tanzania  Alikiba ambae kwa sasa  anaefanya vizuri na kibao chake cha Seduce me.

Wakithibitisha taarifa hizi  katika ukurasa wao wa instagram ,  lebel ya Wasafi waliweka picha ya msanii huyo  Baraka the Prince na kuandika “welcome to the family @barakatheprince -can you tag his fans please” k ikiwa kama njia ya kuthibitisha na  kuwaambia mashabiki kuwa Baraka the Prince yuko Wasafi kwa sasa.

Kwa kipindi cha nyuma kidogo Baraka the Prince alikuwa akionekana kuwa karibu na Alikiba na kusemekana  kuwa wote  wawili walikuwa wasanii  wanaofanya kazi chini ya menejimenti moja yenye jina kubwa duniani inayojulikana kama lebel  ya  Rock Star4000, lakini baadae haikujulikana kimetokea nini lakini tetesi zilisema kuwa Baraka the Prince ameshatoka katika  lebel iyohuku sababu ya kutoka katika lebel iyo ikiwa haijajulikana.

Baada ya tetesi za kutoka katika lebel hiyo kusambaa, kulikuwa na sintofahamu ya maelewano kati ya alikiba na baraka ambao walikuwa wakifanya kazi chini ya menejiment moja , bifu ambalo pia ommy dimpozi alihusishwa kwa sababu kipindi hicho ommy dimpozi pia alikuwa amesajiliwa katika lebel hiyo, ilhali wao wenyewe hakuna hata mmoja aliyetaka kuthibitisha tetesi hizo zaidi ya kukataa na kusema kuwa wao hawana ugomvi wowote.

Ujio wa nyimbo mpya ya Baraka the Prince pamoja na kuhamia wcb inathibitisha kuwa kweli Baraka hayupo tena katika lebel moja na Alikiba lakini je, swali la kujiuliza ni kwamba Wcb ni lebel iliyopo chini ya Diamond Platinumz ilihali Baraka alikuwa akifanya kazi katika lebel moja na Alikiba, je hakuna lolote linalohusisha ugomvi wa team hizo mbili uliopelekea msanii huyo kuhamia huko.

 

 

“Tulimpunguza Baraka” Ben Pol aeleza chanzo cha bifu yake na Baraka The Prince

Baraka the Prince ana bifu kubwa na Ben Pol na Jux. Ben Pol ameeleza chanzo cha kilochosababisha wao kutoelewana na walikua marafiki awali.

Ben Pol and Baraka wamewai kushirikiana kuachia wimbo unaoitwa ‘Mwambie’. Hata hivyo wiki mbili zilizopita Baraka alimkashifu Ben Pol alipowachia wimbo wake mpya ‘Tatu’.

Soma pia: “Ni upumbavu tu!” Baraka Da Prince atoa kauli yake kuhusu wimbo mpya ya Ben Pol

Baraka the Prince na Ben Pol

Ben Pol sasa ameeleza nini ilitokea kati yake na Baraka the Prince; katika mahojiano na Ayo TV, Ben Pol alisema Baraka alianza kuwa na chuki nay eye na Jux baada ya wao kumpuguza kimuziki kwa kushirikiana kufanya shows pamoja na tours.

“Mimi napenda sana kukoselewa, napenda kupokea maoni lakini ina matter sana maoni yanatoka kwa mtu gani au wewe na huyu mtu mko kwenye situation gani. Baraka maoni yake yanaweza yakawa mazuri, yanaweza yakawa ni ya kuboresha, yanaweza yakawa ya kujenga, kukosoa. Lakini mimi nawaza status yangu na Baraka ilivyo sasa sahi alafu nahusianisha na yale maoni yake, naona kuna msuguano. Baraka ana hali ya chuki na mimi, especially mimi na Jux, wote wawili sisi ana matatizo na sisi, ana chuki. Ata last time tulikutana naye alikua hataki kutusalamia akageuza mgongo kabisa…muda mrefu kama wiki tatu…Hataki kutusalamia ameweka mgongo hivi. Tumeenda kumsalamia Baraka, ‘Baraka tumekuona, umependeza na tumekumiss’, lakini alikua hataki kuongea na sisi, alikua na chuki.

“Sasa mtu ambaye ana chuki, ana tatizo na wewe akitoa maoni kuhusu kitu chako unakua na mashaka kidogo kwamba ni honest opinion au kwasababu ya misunderstanding ambayo munayo. Na Baraka hii source ya kutuchukia mimi na Jux sababu tulimpunguza kwenye umoja ambayo tulikua tumeuanzisha kufanya shows, kufanya tours…tulimpunguza. Hatukuwai kusema, hatukuwai kumuaibisha kwenye media kusema kwamba tumempunguza au nini… Ni mdogo wetu tumesema tumlindie heshima, tumempunguza lakini hatutasema hivyo kwenye redio au kwenye mtendao…kwenye sehemu yoyote. Lakini kumbe yeye alikua na kinyongo, kwanzia hapo ukimtumia post, ukimwambia kitu akusaidie kushare anakuwekea hivi ‘hapana, no’, si support’. Kwa hivyo twasema kwamba ana chuki. Na kumpunguza ilikua lazima tumpunguze kwasababu ya discipline, kukosa nidhamu. Ilikua lazima tumpunguze.” Ben Pol alisema.

Tazama mahojiano hayo kwenye video hapo chini:

 

Baraka the Prince azua uvumi baada ya kufanya hili

Uvumi umezuka katika mitendao ya kijamii baada ya mwimbaji Baraka the Prince kuonekana na meneja wake Diamond – Babu Tale.

Baraka ameongelewa sana baada ya kupost picha kwenye mtandao wake wa Instagram kama yuko na Babu Tale.

Wengi wa mashabike wake Baraka the Prince wanadhani staa huyo anajiunga na kambi la Diamond Platnumz – Wasafi Records WCB.

Baadhi ya mashabiki wamekuwa wakicomment kwenye picha hiyo wakisema kuwa Babu Tale anamshawishi Baraka kujiunga na Wasafi.

Kuna wale pia wanaodhani Babu Tale anataka Baraka the Prince aweke wimbo zake katika tovuti la wasafi kama wasanii wengi (wasio sajiliwa na Wasafi) walivyofanya.