Msanii Barnaba Azimia Akimuaga Ruge (Picha)

Msanii wa muziki wa Bongo fleva Barnaba Boy ‘Classic’ amesababisha vilio Kutawala Baada ya kuzimia wakati akitoa hotuba fupi ya mazishi ya baba yake mlezi  Ruge Mutahaba.

Barnaba amesababisha vilio kutawala baada ya kushindwa kumalizia hotuba yake huku akiomba afunguliwe jeneza kumuona baba yake mlezi, Ruge Mutahaba.

Msanii huyo kutoka THT aliondolewa ukumbini akiwa amebebwa baada ya kuishiwa nguvu kutokana na uchungu mkali alio nao.

Kwenye hotuba yake Barnaba Alisema Ruge alikuwa kama baba kwake Baada ya kupoteza wazazi wake kwa kipindi kirefu Lakini pia Barnaba aligusia ugonjwa wa figo wa marehemu.

Kama shida ni figo ungeniambi nikupe yangu, wazazi wangu walifariki Ruge ndio alikuwa Baba na ndio mama, Watoto wengi unawaoona THT wametoka kwenye maisha ya shida, Ruge alikuwa ndio Baba yetu” .

 

Barnaba Awashukia Wanatumia Mitandao Ya Kijamii Vibaya

Staa wa muziki wa Bongo fleva anayefanya vyema kabisa na albamu yake ya ‘Gold’ amewajia juu watu ambao wamekuwa wakitumia vibaya mitandao ya kijamii.

Serikali imekuwa ikikemea vikali matumizi mabovu ya mitandao ya kijamii kwani Kumekuwa na watu wanaofanya uharibifu na mitandao hiyo ikiwemo kutoa kugha chafu za matusi na hata kuikashifu Serikali.

Mwezi uliopita Serikali Kupitia TCRA walitangaza kuwateua wasanii kama Barnaba, Hamisa Mobetto na wengineo kuwa mabalozi wa kuhakikisha kunakuwa na matumizi bora ya mitandao ya kijamii.

Kwenye interview na Ayo Tv, Barnaba Boy Classic ametoa Kauli yake  kuhusu harakati zake lakini kubwa zaidi ni kauli yake kwa watanzania ambao wanatumia vibaya mitandao ya kijamii na yeye  akiwa kama balozi wa mamlaka ya mawasiliano Tanzania (TCRA ).

Vijana wajitambue katika nafasi zao na sisi kama Serikali tupo macho na hatutamchekea yeyote anayetumia vibaya mitandao ya kijamii, hii hatuwaambii kwa kuwatisha ila tutawashughulikia”.

 

Barnaba Atoa Tamko Rasmi Kuhusu Mahusiano Yake

Mwanamuziki wa Bongo fleva anayefanya vizuri na albamu yake ya ‘Gold’ Barnaba Elias amefunguka na kuwataka mashabiki zake waache kuhoji kuhusu Mahusiano Yake.

Maisha binafsi ya Mahusiano ya Barnaba yalitwala mitandao ya kijamii baada wanawake watatu tofauti tofauti Kulilia Penzi la staa huyo huku kila mmoja akidai ni mpenzi wake.

Kwenye mahojiano aliyofanya na gazeti la Dimba, Barnaba alisema amekuwa akikutana na majibizano mengi kumhusu yeye na maisha yake ya mapenzi huku akisema hayo ni mambo yake binafsi hivyo watu wasiyahoji.

Watanzania wananidai muziki mzuri na kazi yangu ni kuwapa kile wanachokipenda..sasa siwezi kuchanganya na maisha yangu mengine..hayo yatabaki kuwa siri”.

Barnaba ameongeza kuwa anachofahamu kwa sasa anatakiwa kuutengeneza muziki wake ufike mbali zaidi kwa kuwa bado ana deni kubwa kwa mashabiki zake.

Barnaba Aachia Albamu Yake Ya Gold Adai Imemgharimu Mil.140

Msanii wa muziki wa Bongo fleva anayetamba kwa vocals kali Barnaba Boy ‘Classic’ ameachia albamu yake rasmi na ameweka wazi kuwa imemgharimu jumla ya milioni 140.

Siku ya jana Barnaba alifanya uzinduzi wa Albamu Yake katika hoteli ya Sea Cliff ambapo hafla hiyo ilihudhuriwa na wasanii mbali mbali wa Bongo fleva na Bongo Movie Lakini pia  na wadau.

Kwenye mahojiano na Bongo 5, Barnaba amefunguka kuhusu maandalizi ya Albamu hiyo yaliyomchukua miaka mitatu na fedha takribani milioni 140:

Hii Albamu imenitesa sana nimeiandaa kwa miaka mitatu na nimetunia pesa nyingi sana nikiongea kwa haraka haraka imenigharimu kama milioni mia na arobaini hivyo naomba mashabiki, vijana wenzangu waweze kunisapoti ili pesa yangu iweze kurudi”.

Kwenye uzinduzi wa Albamu hiyo Msanii wa Bongo movie Jacqueline Wolper alikuwa kivutio baada ya kununua albamu moja kwa dola za kimarekani 3000$ ambayo ni sawa na milioni Sita na laki nane.

Mobetto, Barnaba na Shilole Wala Shavu Kampeni Ya Be Smart

Wasanii wa muziki wa Bongo fleva Barnaba Boy Classic na Shilole pamoja na mwanamitindo maarufu Hamisa Mobetto wamekula Shavu baada ya kuteuliwa mabalozi wa TCRA.

Wasanii hao wameteuliwa na Baraza la ushauri la watumiaji wa huduma za mawasiliano (TCRA CCC) kuwa mabalozi wa kampeni ya Be smart inayojihusisha na kuelimisha vijana kuondokana na matumizi mabaya ya mitandao ya kijamii mashuleni.

Kwenye mkutano na waandishi wa habari wasanii hao wamefunguka kupata shavu hilo nono Lakini pia nafasi watakayo cheza kama mabalozi:

https://www.instagram.com/p/BnGMZYTlrt8/?utm_source=ig_share_sheet&igshid=13yt54nc81jzx

Barnaba Awataka Mashabiki Wafatilie Mziki Wake Badala Ya Maisha Yake Binafsi

Msanii wa muziki wa Bongo fleva Barnaba amemfungukia skendo zinasambaa Kwenye mitandao ya kijamii na kusema anataka mashabiki zake wasikilize miziki yake badala ya skendo zake.

Wanawake wawili wamekuwa Kwenye vita ya mitandao ya kijamii dhidi ya penzi la Barnaba ambapo amekuwa Kwenye Mahusiano na wanawake hao kwa wakati mmoja.

Kwenye mahojiano na Kipindi cha Enews cha EATV Barnaba amekataa skendo hizo na kudai hazina ukweli wowote na kuwataka mashabiki zake wasizitilie maanani:

Hizo skendo mimi nazisikia tu kama wewe kwa maana hazina ukweli Kwanza mimi sio mtu wa kuanika mahusiano yangu mitandaoni kwaiyo tafadhali mashabiki zangu msisikilize kelele za watu hao. Bali naombeni msikilize mziki wangu na kazi zangu”.

Lakini pia Barnaba anafanya vyema na  wimbo wake mpya unaoitwa Tuachane mdogo mdogo.

Zubeda Akana Kurudisha Penzi Kwa Barnaba

Mzazi mwenza wa staa wa Bongo fleva anayefanya vyema na ngoma yake ya ‘Chausiku’ Barnaba Boy Classic, Zubeda amekataa kabisa Kurudisha Penzi kwa Baba watoto wake huyo.

Zubeda na Barnaba walikuwa Kwenye Mahusiano ya Kimapenzi kwa miaka mingi na hata kujaaliwa kuzaa mtoto mmoja wa kiume lakini penzi lao lilivunjika na kila mmoja kushika njia yake.

Siku chache zilizopita kulikuwa kuna tetesi kuwa wawili hao wameweka tofauti zao pembeni na kuamua kuwa pamoja tetesi ambazo Zubeda amezikataa na kudai hawezi kurudi kwa mzazi mwenziye kwa sababu kila mtu ana maisha yake mengine.

Kwenye mahojiano na Global Publishers, Zubeda alisema kila mtu kwa sasa yuko kwenye uhusiano wa kimapenzi na wanaheshimiana katika hilo kilichobaki kwao kubaki kama wazazi na hakuna lingine zaidi ya hilo kwa sababu tangu wametengana ni muda mrefu sasa.

Watu wanadai tu kuwa nimerudi kwa Barnaba, lakini sio kweli kabisa yule ni mzazi mwenzagu tu na ataendelea kuwa hivyo na si kitu kingine kwa sababu nina mtu wangu na yeye ana mtu wake kilichobaki ni heshima tu ya mzazi mwenzangu”.

 

Mama Yangu Ndio Mwanamke Pekee Aliyenipa Sapoti Kwenye MuzIli- Barnaba

Msanii wa muziki wa Bongo fleva anayeendelea kufanya vyema na wimbo wake mpya aliomshiriksha Vanessa Mdee ‘Chausiku’ Barnaba Boy amefunguka na kuweka wazi mapenzi yake kwa mama yake.

Barnaba amefunguka na kuongea mambo mazito kuhusu mama yake mzazi ambaye alifariki miaka michache ya nyuma na kudai ndiye mwanamke pekee ambaye ni wa Shoka kwake.

Barnaba ameweka wazi kuwa kinachomuumiza zaidi ni kuwa mama yake alifariki wakati ndio anaanza kupata mafanikio Kwenye muziki na hivyo mama yake hakuweza Kula matunda:

Mwanamke wangu wa shoka ni mama yangu ndio mwanamke pekee ambaye niliweza kumwambia hata yanayoniuma moyoni ambayo siwezi kumwambia girlfriend wangu.

Mama yangu alikuwa ananipa sapoti Kwenye muziki wangu wakati mafanikio ya Muziki yanaanza kuja Mungu akamvhukua”.

 

Barnaba Adai Anaogopa Kupiga Picha na Wasichana

Msanii wa muziki wa Bongo fleva anayefanya vizuri na kibao chake cha ‘Chausiku’ Barnaba Boy amefunguka na kuweka wazi kuwa hivi sasa anahofia sana kupiga picha na wasichana kwa kuhofia uzushi.

Barnaba amefunguka hayo baada ya kuulizwa kuhusu picha zake na wasichana kadhaa ambazo zimekuwa zikionekana Kwenye mitandao ya kijamii na kudaiwa kubadilisha badilisha wasichana.

Kwenye mahojiano na Enews ya East Africa Tv, Barnaba ameweka wazi kuwa wasichana wengine ni mashabiki zake akikutana nao wanaomba picha lakini baadae anasingiziwa ni wanawake wake:

Sio siri siku hizi nimekuwa muoga wa kupiga picha na watoto wa kike na Kuposti Kwenye mitandao ya kijamii naona kama itAleta maneno maneno kuwa ni wapenzi wangu wakati wengi ni mashabiki tu”.

Lakini pia Barnaba alikataa taarifa kuwa tangu ameachana na mama watoto wake MAma Steve amekuwa na wanawake wengi:

Mimi sina mahusiano na wasichana wengi ila nina mashabiki wa kike wengi sana na hata marafiki zangu wengi ni wa kike sio wanaume halafu watoto wa kike wananipenda sana kwa sababu mimi ni mtu ambaye ni mcheshi mtani na mtu wa stori.

Barnaba- Nikikutana na Vanessa Tunatengeneza Mziki Mzuri

Msanii wa muziki wa Bongo fleva Barnabas Elias ‘Barnaba Boy Classic’ amefunguka na kuweka wazi kuwa kila akikutana na msanii mwenzake Vanessa Mdee basi wanatengeza hits tu.

Barnaba anayefanya vizuri na ngoma yake ya ‘Chausiku’ aliyomshirikisha Vanessa Mdee amedai yeye na Vanessa wana chemistry fulani Inayovutana mpaka kutengeneza nyimbo kali.

Barnaba alifunguka hayo Kwenye mahojiano aliyofanya na Bongo 5, amedai kuwa mashabiki zao wenyewe wanafahamu wakikutana yeye na Vanessa nini kitatokea ndio maana wanafanya vizuri:

Mashabiki wanajua mimi nikikutana na Vanessa kuna mambo mazuri yanakuja, sisi tuna chemistry ya pamoja, sauti zetu zimekuwa zikikutana pamoja kuna mambo mazuri yanatokea”.

Lakini pia Barnaba ameweka wazi kuwa kwa sasa mashabiki wameshachoshwa na kelele wanataka mziki mzuri:

Hii inaonyesha kazi ni nzuri watu wanapenda muziki mzuri, watu wamechoshwa na makelele wanahitaji muziki mzuri, na ukweli kazi na sio maneno maneno”.

 

Barnaba- Mwanamke Anahitaji Kutunzwa Usipofanya Hivyo Wenzako Watakusaidia

Mwanamuziki wa Bongo fleva anayefanya vizuri na ngoma yake mpya ya ‘Chausiku’ Barnabas Elias maarufu kama Barnaba Boy Classic ameweka wazi umuhimu wa kumtunza mwanamke.

Kwenye mahojiano aliyofanya na Wasafi TV, Barnaba amesisitiza matunzo kwa mwanamke ambapo amesema mwanaume kumpatia mwanamke fedha ni sawa na kumwagilia maua.

Nahonga sana kaka na mpaka sasa nahonga, nawachukia wanaume wenzangu wanaosema kuhonga. Mwanamke ukimpa kitu, pesa au talanta yoyote yenye thamani haiitwi kuonga, mwanamke unamzawadia.

Mwanamke ni pambo ambalo linatakiwa kumwagiliwa, ukimpa mpenzi wako pesa umemwagilia ua lako, ume-protect tunda lako, mwanamke anahitaji kutunzwa, usimpomtunza mwenzako watakutunzia”.

Barnaba aliachana na mpenzi wake wa siku nyingi ambaye pia ni mama wa mtoto wake mmoja Steve, Mama Steve Lakini hivi sasa amekuwa akionekana na mwanamke mwingine ambaye ameweka wazi kuwa ni mpenzi wake.