Barnaba Akanusha Tuhuma Zinazomkabili Ruge

Msanii Barnaba amefunguka na kukanusha taarifa na tuhuma zinazosambaa katika mitandao ya kijamii hasa zinazotaka kuchafua jina la marehemu Ruge mutahaba  kuhusu swala la kutaka kuwasaiai na kuwainua wasanii huku baadhi ya watu wakisema kuwa alikuwa akiwanyonya.

Barnaba ambae ni moja ya zao kutoka THT na pia ni msanii alielelewa na Ruge kama mtoto amefunguka na kusema kuwa hakukuwa na swala kama hilo walipokuwa katika chuo icho cha muziki kwa sababu kila mtu alikuwa na uhuru wa kufanya kazi yake ilimradi kuwa na nidhamu.

Wasanii wengi sana wametoka katika jumba hilo na wamekuwa na mafaniki katika muziki na kila mara wamekuwa wakikumbuka fadhila za mhasisi huyo na ndio maana baranaba anapata nguvu ya kusimama na kutetea hilo.

Msanii dudubaya ambae alianza kwa kumskashifu Ruge tangu akiwa mgonjwa alindelea hata mauti yalipomkuta kwa kumpa shutuma kali zidi yake.

 

Barnaba Amuonyesha Mrithi wa Mama Steve

Msanii wa muziki wa kizazi kipya nchini Barnaba classic ameamua kuonyesha kuwa kwa sasa ameamua ku-move on na maisha yake ya mapenzi na kuachana na mwanamke ambae kila siku amekuwa akisema kuwa amekuwa akimpenda sana katika maisha yake ambae ndio alikuwa Mama Steve.

Barnaba amefanya hayo katika ukurasa wake wa istagram , baada  ya kuamua kuweka picha yake akiwa na mpenzi wak huyo mpya na kumtakia kheri ya kuongeza mwaka mwingine huku akisema kuwa anatamani sana kumvsha pete katika siku yake hiyo ya kuzaliwa.

Ikumbukwe kuwa barnaba alikuwa katika mahusinao na mwanadada mmoja na kukaa nae kwa muda sana tangu msanii huo akiwa hana kitu mpaka sasa amekuwa na mafanikio lakini wamekuja kuachana na kufanya msanii huyo kuimba nyingi za mapenzi akilalamika sana kuhusu kuumizwa.

 

 

Barnaba Akiri Ugomvi na Mama Steve Ulishusha Muziki Wake

Msanii wa muziki nchini barnaba classic amefunguka na kusema kuwa moja ya kitu ambacho kimeua sana muziki wake kwa kipindi kifupi cha nyuma ni kutokana na mamatuzo aliyoyapitia hasa kugombana na mama wa mtoto wake.

Hata hivyo, Barnaba anasema kuwa mama steve ni mwanamke aliewahi kuchukua sehemu kubwa sana katika maisha yake lakini kwa sasa anaamini kuwa  kila mtu anatakiwa kuendelea na maisha yake kwa sasa.

Ikumbukwe kuwa siku za hapa karibuni, msanii huyu alisema kuwa siku zote amekuwa akimpenda na hatokaa kumchukia kabisa mama steve kwa sababu ni mama wa mtoto wake na kla siku wataendelea kuwasiliana kwa sababu wana kitu kinawaunganisha  ambacho no mtoto.

Barnaba na mama steve waliweza kukaa katika mahusiano kwa zaidi ya miaka 10 pamoja na kufanikiwa kupata mtoto mmoja , lakini penzi hilo lilikuja kufa mwaka 2018 baada ya mwanadada huyo kuamua kujiingiza katika mahusiano na mwanaume mwingine.

 

Barnaba Atoa Sababu ya Kuimba Gospel

Msanii anaefanya vizuri na nyimbo zake barnaba classic amefunguka sababu kubwa ya kuachia album yake yenye nyimbo sita (6) huku  nyimbo hizo zote akiwa  ameimba gospel akimshirikisha Damian soul.

Barnaba amekuwa akizoeleka kuimba nyimbo za kulalamika sana kuonewa katika mapenzi lakini safari hii amekuja kwa utaofauti baada ya kuachia album hiyo yenye muonekano wa tofauti kidogo kutokana na uwepo wa nyimbo hiyo ya injili.

Akiongea sababu kubwa ya kuamua kuimba ivyo, barnaba anasema  aliguswa sana na historia ya mpiga picha MXCartr baada ya kuwekwa jela kwa siku kadhaa.

Mtu alitetoa wazo hili kuu ni Mxcarter baada ya kupata matatizo na kuwekwa ndani kwa siku 8 pale Central kwaio wimbo huu ni kama shukrani kwa kuyapita hayo

Hata hivyo barnaba anasema kuwa uwepo wa album hiyo haimaanishi kuwa amecaha kuimba Bongo fleva maana kuna album inaitwa Washa inakuja.

Barnaba Amkabidhi Mh Kingwangala Album ya Gold Wodini MOI.

Msanii wa muziki wa bongo fleva nchini, Barnaba classic amekwenda kumtembelea  Waziri wa Maliasili na Utalii Mh Hamis kigwangala hospitalini MOI  ambako alilaza tangu August 4 mwaka huu ambako alikuwa akipatiwa matibabu ya mkono uliovunjika kwa ajali aliyoipata alipokuwa kazini.

Ukiacaha na kwenda kumjulia hali, lakini pia Barnaba ahakusita kumkabithi waziri huyo album yake mpya ya Gold ambayo imetoka hivi karibuni na imekuwa ikipatikana katika maduka ya  mitandaoni .

Hata hivyo mh Kigwangala amemshukuru sana Barnaba na kumwambia kuwa alipata mwaliko wake wa uzinduzi wa album hiyo lakini hakuweza kuhudhuria kutokana na  hali yake aliyokuwa nayo lakini anampongeza sana kwa hatua aliyoweza kuifikia na anamuombea afanikiwe zaidi.

Nilipata mwaliko wako lakini sikuweza kuja kutokana na ajali,lakini ninaendelea vizuri na ninashukuru kwa kufika na kuja kuniona.natambua wasanii pia ni nguzo katika kukuza utalii wetu hasa wanapotmia mashairi na ndio maana mwezi septemba tuna tamasha la urithi festival ambalo pia wasanii wamepewa nafasi ya pekee.

Kwa upande wa Barnaba pia amemshukuru sana dk hamis kwa kupokea album hiyo lakini pia amempa pole kwa ajali .

Barnaba Agoma Kumhusisha Mama Steve na Nyimbo Zake za Mapenzi.

Mwanamuziki mwenye kipaji cha kuimba nyimbo za mapenzi na za kulalamika Barnaba Classic amefunguka na kusema kuwa watu wamekuwa wakihusisha sana nyimbo zake na  maumivu aliyowahi kuyapata ya kuachana na mwanamke aliyemzalia mtoto, mama steve kitu ambacho kwake sio cha kweli.

Barnaba ambae kwa sasa ametoa wimbo wa tuachane mdogo mdogo, anasema kuwa kuimba nyimbo za mapenzi ni kipaji chake kila siku  wala haihusiani na kitu chochote cha kuumizwa na mamsteve hivyo watu wasiwe wanahusisha muziki na kitu icho.

Tangu barnaba ameachana na mama wa mtoto wake, barnaba ameshaimba baadhi ya nyimbo zenye kuonyesha kulalamika kuumizwa na mapenzi kitu kinachowafanya mashabiki kuisi kuwa labda bado anakumbuka mapenzi ya mwanamke huyo.

siwezi kuzungumzia mzazi mwenzangu ulshawahi kuona wapi mtu anamzungumzia mtu mmoja kla siku,mimi ninawaimbia watanzania.Watu walishanza kumjua barnaba kabla ya kuingia katika mahusiano, sijaanza kuimba mapenzi leo, nafanya kazi kwa ajili ya watanzania walionipa dhamana na walioniweka hapa.

 

 

Barnaba Ampiga Vijembe Mama Watoto Wake.

Baada ya kuachana kwa muda mrefu na kila mtu kujiingiza katika mahusiano mapya yaliyosababisha kila mmoja kuendelea na maisha yake , hivi karibuni Barnaba classic alimtupia kijembe mama watoto wake anaejulikana kwa jina la Zuu mela kwa kumwambai kuwa anamuona kama amezeeka kwa sasa.

Nini tasfiri ya Barnaba kwa mama watoto wake, ni kwamba Barnaba anaona kama Zuu alikuwa akionekana kijana kipindi wako nae ila kwa sasa kwa sababu yuko nje ya mahusiano yao anaona kama ameshaanza kuzeka kitu ambacho pia zuu aliamua kumjibu na kumwambia inawezekana ametumwa.

Katika picha ya mwanadada huyo barnaba aliandika “macho yangu au laaha, naona unazeeka mama watoto?’   Zuu nae aliamua kumjibu katika uwanja huo wa maoni na kumjibu “utakuwa umetumwa wewe sio bure kabisa, wakati moyoni unasema zuu kawa mcharo.”

Wawili hao waliishi kwa muda mrefu na kufanikiwa kupata mtoto mmoja wa kike lakini penzi lao lilikuja kuyeyuka bila kuweka wazi chanzo cha mahusiano hayo kufa.

 

Barnaba Atangaza Ujio Wa Albamu Yake Mpya

Mwanamuziki wa muziki wa Bongo fleva Barnaba Elias maarufu kama Barnaba Classic ameweka wazi kuwa anategemea kutoka na albamu yake mpya hivi karibuni.

Barnaba anayefanya vizuri na ngoma yake ya ‘Chausiku’ aliyomshirikisha Vanessa Mdee amesema kuwa Albamu Yake inatarajia kutoka hivi karibuni aliyoipa jina la ‘Gold’.

Albamu ya muimbaji huyo ambayo inakwenda kwa jina la Gold itakuwa na nyimbo zipatazo 18. Kupitia ukurasa wake wa Instagram ndipo ameeleza kukamilika kwa albamu hiyo.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Barnaba amesema:

Narudia tena kusema hii ni Gold na mgodi umebeba dhaabu ambazo zimepikwa muda mrefu sana, sitaki kusema mengi I can’t wait kwa kweli“.

Hapo mwanzoni  albamu hiyo ilipangwa kutoka February 2018 lakini ikahairishwa hadi July 2018 kutokana na kile Barnaba alichoeleza kuwa wadhamini wake wakuu watatu walipendelea hivyo.

Wasanii waliotajwa kuwepo katika albamu hiyo ni pamoja na Juliana Kanyomozi na Jose Chameleon kutoka Uganda. Kutoka Bongo kuna Vanessa Mdee, G Nako, Ben Pol, Aslay, Barakah The Prince, Linex na Joh Makini.

Ben Pol- Nilikuwa Chawa wa Barnaba

Mwanamuziki wa Bongo fleva Bernard Paul maarufu kama Ben Pol amefunguka na kukiri kuwa siku za nyuma alishawahi kuwa chawa wa msanii mwenzake Barnaba Boy Classic.

Ben Pol amewataka mashabiki kuacha kushangaa urafiki wake na Barnaba umeanzia wapi kwani ukifatilia historia ya muziki wake alishawahi kuwa chawa wa Barnaba.

Ben Pol amefunguka hayo Kwenye mahojiano aliyofanya na Enews ya East Africa Tv:

Kwanza watu wengi watakuwa hawafahamu urafiki wetu na Barnaba umeanza siku nyingi sana nilikuwa najiweka kwake kwa sababu nilikuwa naona anaimba vizuri na pia nakumbuka nilikuwa hata namsindikiza studio kwa Allan Mapigo.

Siku hizi hao watu wanawaita hao watu chawa kwaiyo mimi ndio nilikuwa chawa wake yaani namsindikiza lakini uchawa unasaidia hasa uchawa wenye malengo ambao hata mimi ni nao sahivi nina chawa wangu ambao wananifuata kila sehemu”.

Ben Pol amekiri kuwa kupitia kuwa chawa wa Barnaba alijifunza vitu vingi anavyojua leo hii kuhusu mziki kwaiyo uchawa wake ulikuwa wa faida.

Barnaba Adaiwa Kuchepuka Kwa Miaka 5 Wakati Yupo na Mkewe

Mwanamuziki wa Bongo fleva Barnaba Classic amerudi tena katika headlines baada ya kurushiwa tuhuma kuwa amechepuka na msichana mwingine kwa kipindi kirefu wakati yuko na mzazi mwenzie Zuwena.

Barnaba aliweka wazi uhusiano wake na Zuwena ambaye alidumu naye kwenye mahusiano kwa mipia ni mama watoto wake aliyezaa naye mtoto mmoja anayejulikana kama Steven. Uhusiano wake na Zuu uliisha hapo nyuma kidogo kwa sababu ambazo hazikujulikana.

Mwezi uliopita ilikuwa ni sherehe ya kumbu kumbu ya kuzaliwa kwa Zuwena na Barnaba alimuandikia mzazi mwenzake huyo ujumbe mzito akimtakia heri ya kuzaliwa lakini ilionekana wazi kuwa bado ana mapenzi kwa mkewe wa zamani kitendo kilichowagusa wengi.

Siku chache zilizopita mrembo mmoja anejulikana kama  Raya Sykes alifanya mahojiano na EATV katika kipindi cha NFL na alidai kuwa amekuwa kwenye uhusiano na Barnaba kwa miaka 5 kitu kilichowashangaza wengi kwa sababu kipindi chote hicho alikuwa kwenye uhusiano na Zuwena:

Kwenye mahojiano hayo Raya Sykes alifunguka na kudai kuwa yeye na Barnaba ni wapenzi mpaka hivi sasa  na wamekuwa kwenye uhusiano kwa moaka mitano na kukiri kuwa alikuwa mchepuko wake kwa miaka zaidi ya mitano tangia kipindi akiwa  na mkewe Zuwena hata alipokuwa mjamzito.

Barnaba Aweka Wazi Siri Ya Sauti Yake

Akiwa kama mmoja wa wasanii wanaofanya vizuri sana katika kazi zake zz musiki na sasa hivi anatamba na kibao chake cha mapenzi jeneza,msanii Barnaba Elias Maarufu kama Barnaba  Classic kipaji kikubwa kutokaTHT  amefunguka na kuongelea moja ya siri zake kubwa katika kutunza sauti yake ambayo imekuwa adimu sana katika muziki wake.

akiongea katika Clouds E ya Clouds Tv alipokutwa katika mazoezi ya kujitayarisha kwa ajili ya kufanya mazoezi ya kuperfom katika shoo ya mwisho ya tamasha la Fiesta, Barnaba amesema kuwa  kila anapojua kuwa anatarajia kufanya shoo sehemu amekuwa akijitahidi sana kutunza sauti yake ili aweze kufanya vizuri katika  shoo zake.

Barnaba ambae ni msanii anaesifika kwa kuweza kufanya live band kwa muda mrefu na mara nyingi zaidi katika show zake anasema kuwa amekuwa akifanya mazoezi, amekuwa akijitahidi kupumzika sana na hata kupunguza swala la kufanya mapenzi ili kuweza kumtain nguvu zake.

litu kikubwa uwa nazingatia kupumzika muda mwingi na kuwahi kulala,nalala muda mwingi sana hili kupumzika kwa sababu show ninayoenda kuifanya ni kubwa sana, lakini pia najitahidi kutokula vyakula vya wanga kama mahindi, maharage, mtama maana hivyo ni vyakula vinavyoweza kuacha mabaka kooni na kusababisha sauti kutoka kwa shida na kukuumiza koo, lakini pia najitahidi sana kunywa maji mengi na kwa wingi zaidi ya kawaida.Kitu kikubwa pia nazingatia sana katika kufanya mazoezi ya mwili kama kukimbia na kupiga push-up kwa sababu ya kutafuta pumzi maana kuimba muda mrefu kunahitaji pumzi sana.Lakini katika vyote ninaweza nisifanye mapenzi hii wiki nzima mpaka show ipite.Wasanii kutunza sauti jukwaani ni kama wachezaji wa mpira tu.

Barnaba na wasanii wengine wanategema kukonga nyoyo za watu novemba 25 , katika jukwaa la Fiesta katika uwanja wa Leaders Club jijini Dar Es Salaam baada ya tamasha hilo kuzunguka kwa zaidi ya mikoa 16 na kuamua kumalizikia jijini hapo.