Barnaba Akiri Bado Anampenda Mama Steve

Msanii wa muziki wa siku nyingi Barnaba amefunguka na kuandika ujumbe mrefu huku akisema kuwa katika maisha yake yote hawezi kuacha kumpenda mama wa mtoto wake ambae ndie aliekuwa mpenzi wake kwa miaka 9 aliokaa nae tangu alipoanza muziki alipopambana na hata kufikia hapo alipo.

Barnaba anasema kuwa katika maisha kuna mapenzi na mapendo lakini aliyonayo kwa mama steve ni mapenzi ambayo anaamini kuwa hayaweiz kuisha hata kitokeee nini kamwe haweiz kuacha kumpenda mama huyo.

Barnaba anasema kuwa yeye na mama steve watabaki kuwa ndugu tu kwa sababu ya mtoto wao anaewaunganisha na hata siku moja haweiz kumchukia mama wa mtoto wake, lakini pia barnaba amezungumzia swala la mpenzi wake wa sasa kuwa mjamaizto kwa kusema kuwa watoto wamekuwa baraka katika maisha ya kila siku hivyo hata yeye  hawezi kuliongelea hilo.

Ikumbukwe kuwa zuu ambae ni mama steve alianza kuonekana akiwa na mwanaume mwingine na ndipo ilipojulikana kuwa wawili hao wameachana pamoja na kwamba mara nyingi barnaba amekuwa akitunga nyimbo zinazoonyesha kuumizwa sana na kuachwa na Mama Steve.

 

Barnaba Awataja Wasanii Hasa wa Kike Kukaa Chonjo na Hamisa Mobeto

barnaba boy amefunguka na kuona kipaji kikubwa alichonacho mwanadada Hamisa Mobeto na kuanza kuwapa tahadhari wasanii wengne hasa wale wa kike kuwa hata siku moja wasije wakakaa wakabweteka kwa sababu  Hamisa atawapita muda so mrefu.

Hamisa Mobeto ambae ametoa wimbo mpya hivi karibuni na kuonekana kuwa wimbo huo utafanya vizuri kutokana na kupokelwa vizuri, nawasahasa wasanii kukaa chinjo na wanadada huyo kwa sasa.

Wimbo wa hamisa kwa sasa umekuwa habari ya mjini kwa sababu kila mtu amekuwa akizungumzia wimbo huo ambao ametoa ikiwa ni wimbo wake wa pili lakini amekuwa akiwatia moyo hata wale wanampa sapoti.

Ben Pol Akana Tetesi za Yeye Na Barnaba Kuunda Kundi Moja

Msanii wa Bongo fleva Bernard Paul maarufu kama Ben Pol amefunguka na kuzima tetesi zilizosambaa Kwenye mitandao ya kijamii na kudai kuwa yeye na Barnaba wanaenda kundi moja la muziki.

Barnaba na Ben Pol ni moja kati ya Wasanii Kwenye tasnia ya Bongo fleva ambao wana ukaribu sana na wameshafanya nyimbo kadhaa pamoja.

Siku za hivi karibuni waliwaambia mashabiki zao wanataka kuunda kundi moja na kufanya Muziki pamoja ambapo kundi hilo walipanga kuliita BEBA yaani kirefu ni Ben na Barnaba.

Kwenye mahojiano aliyofanya na Wasafi Tv, Ben Pol amekana taarifa na kusisitiza kuwa walivyosema hivyo ilikuwa ni utani lakini hawakumaanisha kama kweli walikuwa wana mpango wa kuwa kundi moja:

BEBA was a a joke tulisema kwa nini wasanii wanaungana wawili wawili hlafu wanakata vifupi vya majina yao kwanini na sisi tusifanye hivyo? Lakini ilikuwa kama utani ingawa tumesharekodi nyimbo kama mbili lakini hatifanya kama kundi bado lakini huwezi kujua huko mbele because we are family na tunasopitiana”.

Wasanii mbali mbali wamekuwa wakiungana na kuwa kundi moja mfano ni Rostam ambao ni Roma na Stamina na MoCo ambao ni Moni na Country Boy.

Barnaba Akana Kuwa na Mpenzi kwa Sasa.

Mwanamuzki barnabas amefunguka na kusema kuwa kwa sasa hana mpenzi kama imekuwa ikizushwa katika mitandao ya kjamii na kwamba kama atapata mpenzi hivi karibuni atakuja kumtambulishwa kwa mashabiki zake siku atakapofunga naendoa au kumvalisha pete na wala sio vinginevyo.

Barnaba ameyasema hayo ikiwa ni siku kadhaa zimepita tangu kusambaa kwa baaadhi ya picha katika mtandao wa kijamii zikimuonyesha akiwa na moja ya warembo studio na maeneo tofauti ya kujivinjari huku mazingira yakiwaonyesha kama wapenzi lakini amekataa na kusema hana mahusiano na wanamke yoypote kwa sasa.

sijui chgochote kwa sasa,nilisema siku nitakayo muonyesha mwanamke wangu ni siku namuoa au namvalisha pete tu na sio vinginevyo , siwezi kuwa na mapenzi ya mtandao na mwanamke wangu  na kwa mtu nimpendae siwezi kumuweka katika mtandoa hata siku moja,

Picha ya Barnaba na Mpenzi Wake Mpya Yazua Gumzo Mitandaoni

Baada ya kuachwa na mzazi mwenzie , Barnaba kwa mara nyingine aliweka post yenye picha yake na mwanamke mwingine huku akiwaaminisha mashabaiki wake kuwa huyo ndio mpenzi wake mpya  baada ya zuu mela kumuacha ambae alibahatika kuzaa nae mtoto mmoja.

hata hivyo baada ya kuweka picha hiyo katika mitandao ya kijamii kulitokea kwa maoni ya watu na wadau mbalimbali  huku wegine wakimponda na wengine wakionyesha kumsifia, katika caption ya barnaba aliandika “DONE” Baada ya hapo alianza kupokea maoni kutoka kwa wasanii wa mashabiki zake

@harmonize_tz  kaka mbona kama umepania hivi kulipiza kisasi!!!!!

@barnabaclassic @harmonize_tz mdogo wangu kuku katoka bandani tuimbe kwa sauti ya seiya wa mivarooooo #UKIACHWAACHIKA

@auntyezekiel tena kwa hasira jamaniii…..@harmonize_tz

@jimmymafufu @barnabaclassic hapa basi pawe pa mwisho maana pamekufanyia amani.

Hata hivyo baada ya kuweka pich ahiyo, kurasa mbalimbali za udaku izlianza kumuandama mwanamke huyo na kumsema kwa maneno mabaya huku wengine wakisema kuwa mwanadada huyo ni mke wa mtu huko Dodoma.

Barnaba Amedai Yeye Sio Wa Kawaida Kawaida Ameajiri Bodyguard

Msanii wa Bongo fleva mkali wa voko toka longtime kitambo Barnaba Classic amefunguka nini hasa kilichomsukuma kukodi bodyguard ambaye anatembea naye kila sehemu.

Siku za hivi karibuni Barnaba amekuwa akionekana sehemu mbali mbali kama kwenye matamasha na club kwenye shoo akiwa na mlinzi wake binafsi almaarufu kwa jina la bodyguard.

Kwa Bongo msanii pekee ambaye Ana kawaida ya kuwa na bodyguard ni Diamond Platnumz ambaye mara kwa mara amekuwa akionekana na bodyguard wake ambaye hata husafiri naye kwenda sehemu mbali mbali.

Barnaba alikuwa mmoja kati ya wasanii wachache waliohudhuria tamasha liliondaliwa na East Africa TV la 5 select ambapo alienda kwenye tamasha hilo akiwa ameandamana na body guard wake na alifunguka sababu za kutafuta bodyguard kwa sasa:

Mimi kuwa na bodyguard ni ku-add  value kuongeza thamani kwenye kile ninachokifanya lakini pia nikatika kuhakikisjha usalama wangu binafsi na maisha yangu hasa kwenye kazi zangu of course sisi ni watu wa watu tunafanya kazi kwa ajili ya watu lakini kuna watu wanakujia sio kwa nia nzuri lakini hii pia nichachu ya kuonyesha thamani ya Barnaba sio mtu wa kawaida kumfikia kirahisi rahisi Lakini pia huyu mlinzi ananisaidia kulinda usalama wangu binafsi kwani mimi ni staa”.

Lakini pia Barnaba ameelezea vitisho anavyopokea kila siku vimemsukuma yeye kutafuta mtu wa kuangalia usalama wake.

Barnaba:Nahitaji Wasanii Wa Kike Sana

Msanii wa muziki wa bongo fleva Barnaba Elias maarufu kama Barnaba classic ambae kwa sasa ana lebel yake na anafanya production ya muziki amefunguka na kusema kuwa kwa sasa ataanza kusadia wasanii wengine wachanga lakini anahitaji wasanii wa kike sana kuliko wa kiume katika kufanya nao kazi.Barnaba ambae ataanza kufanya kazi na wasanii wachanga ifikapo mwakani anategemea kuanza na wasani wa kike watatu kwanza ili kuangalia upepo unavyokwenda pia.

Mimi lebel yangu ni changa na hata mwaka jana nilisema kabisa kuwa  nitawatambulisha na kuwatoa wasanii mwakani nikianza na mula, na baada ya hapo nitaanza kuchukua na chapa nyingine , in fact nimesema ninahitaji wasanii wa kike sana ninahitaji wa kike watatu. –Alifunguka Barnaba

Barnaba alipoulizwa sababu ya kuchagua wasanii wa kike tu na sio wanaume alisema kuwa wasanii wengi wa kike hawapati nafasi ya kuingia katika game na ukiangalia katika industry ya muziki wasichana ni wachache kuliko wanaume.Hivyo anataka kuibua wanawake pia, lakini pia Barnaba anaamini kuwa kwa sababu yeye pia ni mtunzi na nyimbo zake nyingi zinahusu mapenzi na ziznendana sana na wasichana basi hii itakuwa ni nafasi nzuri kufanya kazi na watu hao.

kwaiyo kwa upande wa kiume atabaki mula peke yake, na sababu yangu ni ya msingi sana kwa sababu wanaume tupo wengi sana ktiak game,na kitu kingin mimi pia ni mwandishi na nyimbo zangu nyingi huwa zinzendana na wasichana  na nimeamua kuwa hivyo na am sure mtu kama Diamond alishasaidia sana.- Alimalizia Barnaba.

Akiwa kama mtu aliesaidiwa mpaka kufikia hatua yakusimama na kufikia level aliyofikia barnaba hana budi kusaidia wengienwalopo mtaani ambao pia wana kipaji cha kufanya vizuri kama yeye.

Barnaba ni moja ya wasanii wakubwa wanoweza kutajwa katika list ya wasanii walioanza toka chini kabisa na kuweza kufika pazuri sana alipofika leo, ni mwalimu wa muziki kwa watu wengine lakini pia amekuwa mwandishi mzuri wa nyimbo zake na za watu wengine pia.

 

Barnaba Awaongelea Wasanii Wanaofeli THT .

Msanii mwenye kipaji ambacho akijawahi kushuka tangu aanze muziki wa Bongo Fleva Barnaba Elias anaejulikana kwa jina  la Barnaba Classic amefunguka na kuwaongelea baadhi ya wasanii ambao walikulia kimuziki katika jumba la sanaa la THT na kushindwa kuendelea kimuziki.Barnaba akiwa kama mmoja wa wasanii waliolelewa na kukua katika jumba la sanaa la THT amekuwa ni mmoja wa wasanii wa kuigwa kutokana na mafanikio yake aliyonayo mpaka saivi katika muziki.

Barnaba ambae amekuwa maarufu kwa uandishi wa baadhi kwa nyimbo za wasanii wengine wengi kwa sasa amekuwa msanii mwenye mafanikio mpaka kufikia hatua ya kufungua studio yake mwenyewe inayojulikana kama High Table Sound akiwa producer mwenyewe.

Barnaba anasema kuwa anawashangaa wasanii ambao walikuwa wote katika tasnia ya muziki na walikuwa wote katika malezi ya kimuziki THT lakini kwa sasa wameshindwa kabisa kuendeleza sanaa iyo tangu watoke THT. kwake yeye anaamini kuwa waliotoka THT kwa mbinde ndio walioshindwa kuendelea kimuziki kwa sababu wameondoka kwa wivu na kisirani hivyo hawataweza kufanikiwa kwa sababu wameshindwa kukumbuka shukrani ya vitu walivyokuwa wakipewa katika jumba ilo.

Akiongea na eNews ya televisheni ya EATV Barnaba anasema “wapo wajanja waliovuna tunda la THT , THT ni tunda,  na ni msingi ambao mpaka saivi bado unaendelea kuleta watu wastaarabu ,wapo wengi walioondoka kwa jealous,upumbavu na kutokuthamini shukrani   wametoka  THT na wakashindwa kuendeleza sanaa wamepotea ” anasema Barnaba.Hata hivyo Barnaba ametaja wasanii wenzie wa THT ambao wanafanya vizuri katika muziki wakiwa nje ya THT ni pamoja na Estelina Sanga”linah”, Mwasiti, Amini

Akiwa kama mmoja wa wasanii waliosota sana kimuziki mpaka kufika pale walipofikia Barnaba ambae saivi hana menejementi na ametoka THT anafanya vizuri na nyimbo zake mpya alizotoa hivi karibu  wa “tunafanana” na  “mapenzi jeneza”, ukiachana na muziki Barnaba amebahatika kuwa na mtoto mmoja aliyezaa na mwanamke aliyekuwa nae kwa muda tangu anaanza muziki lakini walikuja kuachana hivi karibuni na kuamua kutengana na mwanamke huyo.

Mwanamuziki Barnaba aongelea uhusiano wake na mama wa watoto wake na sio mzuri

Mwanamuziki Barnaba amejitokeza na kuzungumza mara ya kwanza kuhusu uhusiano wake na mzazi mwenzake ambaye wamefanikiwa kupata mtoto mmoja na hii ni baada ya ripoti kutokea ya kwamba waliachana.

Akiongea kwenye kipindi cha XXL cha Clouds FM, hitmaker huyo wa Lover Boy amesema, “Kwa sasa siko kwenye maelewano mazuri na mama watoto wangu. Sio kwamba tumeachana au tumetengana sitaki kusema hivyo.”

“Siwezi kusema simpendi mwanamke niliyepata nae mtoto [mama Steve],yule ameshakua kama ndugu yangu.Namrespect sana mama Steve ila kila mtu anaendelea na maisha yake na hatutaki kutengeneza picha mbaya kwa mwanetu,” ameongeza.

Hilo swali liliulizwa baada ya kuzindua wimbo wake mpya lonely.

 

Msanii Barnaba adai kuwa ni bora fedha zao za muziki ziibiwe na Diamond

Hitmaker  wa ‘Lover Boy’ anadai kuwa ni bora wasanii waibiwe na Diamond Platnumz kuliko kuibiwa na mtu binafsi ambaye si mwanamziki.

Barnaba amemsifu Diamond kwa kuanzisha tovuti yake ya kuuza muziki ya Wasafi.com. Msanii huyu alikutana na Diamond alipomtembelea katika ofisini kwake.

Barnaba na Diamond

“Tumeibiwa sana wasanii, tumedhulumiwa sana. Mungu anisamehe kidogo, bora atuibie msanii mwenzetu, tunajua msanii mwenzetu anakula yupo kwenye soko letu kuliko atuibie mtu binafsi.”

““Na yeye akiwa kama CEO [Diamond] alichukua uamuzi wa busara kama heshima kutupigia simu wasanii wenzake mwenyewe kuliko kuwatuma menejimenti. Mimi naona jambo zuri la bahati alilolifanya na nilienda nikachukuwa contract yangu na kiukweli nimeusaini lakini bado kuurudisha,” Barnaba aliambia Dizzim Online.