Uongo Wakwamisha Penzi la Ben Pol na Ebitoke.

Msanii wa muziki wa kizazi kipya ambaye ilisemekana yupo kwenye mahusiano ya kimapenzi na muigizaji wa vichekesho Ebitoke, ameweka wazi juu ya mahusiano yao kwamba walishindwa kuwa wapenzi kutokana na mmoja wao kutokuwa muwazi kwa mwenzake.

Ben Pol amebainisha hayo wakati alipokuwa anazungumza kwenye kipindi cha KIKAANGONI kinachorushwa mubashara kupitia ukurasa wa kijamii wa facebook wa EATV, baada ya miongoni mwa shabiki zake waliokuwa wakimfuatilia, alipotaka kufahamu undani wa mahusiano yake na Ebitoke.

“Kiukweli sijawahi kuwa na mahusiano na Ebitoke na wala ile haikuwa kiki. Kilichotokea ni kwamba hatukufanikiwa kuwa na mahusiano licha ya wananchi au mashabiki zangu wenyewe kumpitisha kuwa mpenzi wangu kabla ya mimi sijamuona na kumkubali”, amesema Ben Pol.

Pamoja na hayo, Ben Pol ameendelea kwa kusema “Ebitoke alikubarika hadi kwa wazazi wangu kutokana na yeye kuonekana kwenye vyombo vya habari akidai mimi ni mpenzi wake. Wazazi wakawa wanajua kwamba wameshapata mkwe wao. Hapakuwa na mapenzi ya kweli baina yetu ila tulikuwa tunafanya vile ili kuwaridhisha mashabiki zetu”.

Mbali na hilo, Ben Pol amesema chanzo cha mapenzi hayo kushindwa kuendelea ni kutokana na Ebitoke kuogopa kusema ukweli

Sitaki Kumsikia Ben pol Sasa Hivi:-

Mwanadada muigizaji na mchekeshaji maarufu nchini Ebitoke amefunguka kwa hasira na kusema kw ahataki kumsikia ben pola katika masikio yake kwa sababu Ben pol amekuwa hatokei katika nbaadhi ya matukio yake muhimu pamija na kwamba anakuwa amempa mwaliko wa sehemu hizo.

Akiongea usiku wa kutambulisha trailer ya filamu yao mpya ya Sema , Ebitoke amesema kuwa pamoja na kwamba yeye na ben wamekuwa pamoja na bado hawajaachana lakini anashangaa kwanini Ben pol ajatokea katika uzinduzi huo.

Yaan hapa tunaongelea sema habari za Ben Pol calm down kwanza,nilimpa kadi kabisa na ninaona hajafika  sijui ni sababu gani  na nimempigia simu hajampokea kwaio sitaki kumsikia kabsia ben pol hapa sasa hivi.mimi na ben pol hatuwezi kuwa basi bado tuko pamoja na tuna slay a king na queen lakini kwa sasa tuongele movies tu.

Wiki chache zilizopita mwanadada huyo alipofanya interview na  waandishi wa habari alisema kuwa amechoshwa na mambo ya Ben Pol hivyo anaona bora kuachana nae lakini wikiend hii anaongea tena na kusema kuna muda wanakwazana na kufikia hatu ya kuwa na hsira hata kuona bora waachane lakini bado anamuitaji sana ben pol.

 

Uhusiano Wa Ben Pol Na Ebitoke Wafikia Pabaya

Msanii wa kiume wa muziki wa Bongo Fleva nchini anaefanya vizuri katika muziki na katika jukwaa la fiesta, tamasha kubwa linaloendelea kwa sasa katika baadhi ya mikoa mbalimbali. Ben Pol , ambae pia mashabiki wengi wanamwita “king of RnB”, ambae pia  ilisemekana yeye  kuwa katika uhusiano wa kimapenzi na msanii chipukizi wa vichekesho nchini  anaejulikana kama Ebitoke wameingia katika vichwa vya habari tena baada ya mahusiano yao kuonekana kusuasua.

kwa kipindi kirefu cha nyuma wasanii hao walionekana kuwa pamoja baadhi ya maeneo na kukiri kuwepo kwa ukaribu kati yao.Ingwa mara nyingi msanii huyo wa kiume Ben Pol alikuwa akikiri kuwa ukaribu wake na msanii Ebitoke ni wa kikazi zaidi kwasababu Ebitoke bado ni msanii chipukizi hivyo anahitaji msaaada katika kazi zake ili aweze kujulikana katika kazi zake, ilhali wakati huo huo msanii huyo wa kike Ebitoke alikuwa akisema kuwa yeye na Ben Pol wana mahusiano ya kimapenzi na anampenda sana na Mungu akiwajalia basi watafunga ndoa na kutengeneza familia pamoja.

Ni kama week imeyopita tu ambapo msanii Ebitoke alikuwa akihojiwa katika kituo cha televisheni cha EATV, alikuwa akilalamika kuwa  kwa muda sasa kumekuwa na mawasiliano yasiyo mazuri kati yake na msanii Ben Pol, akiendelea kuongea, Ebitoke alisema kuwa akimtumia Ben Pol sms hajibu wala akimpigia Ben Pol hapokei simu zake.Hata hivyo ebitoke aliendela kusema  na kusisitiza kuwa yeye bado anampenda sana Ben Pol na alitaka kujua kwanini Ben hapokei simu zake wakati walikuwa na mipango mingi, ikiwa ni pamoja na kusaidiana katika kazi zao.

Hata hivyo baada ya msanii Ben ol kutafutwa ili aweze kujibu tuhuma hizo Ben Pol alikuwa akionekana kukwepa swala ilo na kusema kuwa  issue za Ebitoke zinamkata stimu”sasa hivi niko busy sana, kwa sababu nafanya mazoezi ya show,lakini kiukweli habari za Ebitoke zinanikata stimu kabisa, so  nikitulia ninaweza kukucheki”alisema Ben Pol ambae kwa muda sasa amekuwa akikwepa maswali ya waandishi wa habari yanayomuhusu Ebitoke.

“Nampenda sana Ben Pol” afunguka Ebitoke

Bado akiwa katika umri mdogo na mgeni katika tasnia hii ya uchekeshaji  lakini amejitwalia umaarufu mkubwa ,mchekeshaji huyu   wa kike chipukizi Anna exavery anayejulikana  maarufu kama Ebitoke ameongelea muendelezo ya ukaribu wake na msanii wa muziki wa kizazi kipya Ben pol  na kusema kuwa bado  anampenda sana ben pol na amekuwa akisikia wivu sana anaposikia watu katika mitandao  wanasema kuwa ben pol ana wanawake wengine  wakati yeye lengo lake kubwa ni kujenga mahusiano mazuri na ben pol na hatimaye baadae  kufunga ndoa  na kuwa na  familia pamoja kwa uwezo wa mwenyezi mungu.

“lengo langu lipo pale pale   ni kumuomba Mungu  anisaidie nije kuolewa na Ben pol ,nampenda sana  naamini mambo yataenda vizuri na mipango’ anasema mchekeshaji huyo, akiongelea pia kuhusu swala ya yeye kuwa bado bikra E bitoke anasema kuwa  swala ilo huwa hapendi kuliongelea sana maana alishaliongea tayari kwa muda . hata hivyo tukirudi nyuma kidogo katika kulizungumzia swala hili msanii ben pol pia alipoulizwa katika usiku wa fiesta pale mkoani Arusha alikaririwa akisema kuwa ‘ Tuko karibu ,ni mtu poa mtu mzima anajiamini na ana malengo hivyo atafika mbali’ alipoulizwa kuhusu mahusiano yake na ebitoke kwa sasa  Ben pol alikataa kuongelea swala ilo kwa kudai kuwa wataaribu vibes za fiesta ivyo hawezi kuongelea swala hilo.

Kumekuwa na picha tofauti tofauti zinaowaonyesha wawili hao wakiwa pamoja sehemu mbalimbali ,ben pol amekuwa akisema yeye na ebitoke ni watani na  marafiki tu  na amekuwa nae karibu kwa sababu amemuomba  ili kumsaidia katika kutangaza kazi zake za kiusanii huko ebitoke akionekana kuwa serious na mahusiano .hata hivyo bado ni jamboi zuri kwa msanii mkubwa kama ben pol anapokua ameona kipaji cha msanii na mchekeshaji huyo na kukubali kufanya nae kazi ilik kuweza kumuinua katika kazi zake hii inaonyesha ni jinsi gani ambavyo wasanii wakubwa wapo tayari katika kusaidia wale ambao ndio wanachipukia katika game

Mchekeshaji Ebitoke afunguka kuhusu Ben Pol kushindwa kumuondoa ubikira

Mchekeshaji wa kike Ebitoke alipata umaarufu sana miezi michache zilizopita alipolia kwenye mahojiano kwa TV huku akitaka msanii Ben Pol afunge naye ndoa.

Ebitoke alisema anampenda sana Ben Pol na hata alitaka mwimbaji huyo amuondolee ubikira wake. Alisema alikua tayari kufanya lolote ili Ben Pol ampende.

Soma pia: Ben Pol amjibu mchekeshaji aliyelia na kumwomba amuoe

Ben Pol na Ebitoke hatimaye walikutana na kwa sasa inasemekana kuwa wawili hao ni wapenzi. Akiongea kwenye kipindi cha Friday Night Live (FNL) ya EATV, Ebitoke alisema kuwa Ben Pol hajafanikiwa ‘kufungua mlango wake’.

Ben Pol na Ebitoke

Mchekeshaji huyo alieleza kuwa bado hajawahi kulala na mwanaume yoyote yule katika maisha yake na alitaka Ben Pol ndo awe mwanaume wa kwanza kulala naye.

Hata hivyo kuna wale wanaodai kuwa Ben Pol na Ebitoke wanafanya tu utani ilhali wanazidi tu kujitangaza na kuzidi kupata kiki katika kazi zao.