Anerlisa Adaiwa Kufuta Picha za Ben Pol

Msanii wa muziki wa kizazi kipya nchini Ben pol  amabae alikuwa katika mapenzi mazito na mwanadada anerlisa kutoka nchinu uganda inasemekana kuwa penzi lake na mwanadada huyo limeota mbawa hasa baada ya wawili hao kutokuonekana pamoja hivi karubuni na hata mwanadada huyo kufuta picha za msanii huyo katika ukursa wake.

Wawili hao ambao walifika mpaka katika hatua ya kutambulishana kwa wazazi wanasema kuwa inawezekana kwa sasa wako katika migogoro na ndio maana hata mwanadada hyo ameamaua kufuta picha aliwahi kupiga nae hasa zile za siku ya utambulisho.

Lakini pia mwanadada huyo anaonekana kum-block mwanamuziki huyo kutoka tanzania ingawa bado haijathibitika kama wako katika mtafaruku, wameachana au wana sababu zao binafsi za kufanya hivuo.

Ben pol Amenifanya kuupenda muziki wa injili :-Anerlisa

Mwanadada anerlisa ambae ni mke mtarajiwa wa mwanamuziki Ben pol amefunguka na kusema kuwa tangu ameanza kuwa na mahusiano na mwanamuziki huyo amejikuta akipenda sana kusikiliza nyimbo za dini kitu ambacho hakuwa nacho hapo awali.

Ben pol  na mwana dada huyo wameanza mahusiani mwaka uliopita na wamekuwa na mafanikio sana katika mahusiano kiasi cha kufikia hatua ya kutambulisha kwa wazazi.

Mwanadada anerlisa mabe kwa sasa yuko nchi Tanzania, amefurahi sana kupajua na kugika tanzania kwa mara ya kwanza lakini kubwa ni kwa sababu amepajua pale anapotoka mwanaume wa maisha yake.

Hata hivyo mwanadada huyo amekuwa akijivunia ben pol kutokana na kipaji chake cha kuimba na kumfa nya kupenda nyimbo za injili.

Ben Pol Ataka Kurusha Ngumi kwa Mwandishi.

Mwanamuziki Ben Pol ambae tumesikia kuwa hivi karibuni anategemea kufunga ndoa na mrembo kutoka nchini Uganda, ameshindwa kudumu katika interview na mwandishi kutoka millad ayo hasa baada ya mwandidshi huyo kumuuliza kuhusu mahusianoa yake ya sasa na yale yaliyopita,

Ben pol ambae alionekana kuwa na hasira na hata kutaka kurusha ngumi kwa mwandishi aliamua kumfukuza mwandishi na kukataa kujibu swali alilokuwa ameulizwa na kusema kuwa hataki kuzngumzia b=mada hizo.

Ben pol ambae hapo awali aliwahi kuwa na mpenzi alieahatika kupata mtoto nae mmoja , walikuja kuachana huku kukiwa hakuna sababu ya msingi iliyotolewa na wawili hao ambapo baada ya hapo zilikuwa tetesi kuwa amekuwa akitoka na ebitoke mpaka alipoamia kuhamisha majesho yake kwa anerlisa.

Wyse Amjibu Ebitoke kuhusu Ben kulelewa na Anerlisa

Msanii anaekuja kwa kuchipukia kwa sasa ambae amekuwa akisapotiwa na Ben pol amemkingia kifua bosi wake na kusema kuwa Ebitoke atakuwa na mapungufu ya akili  baada ya mwanandada huyo kufunguka na kusema kuwa  ben pol analelewa na mwanamke.

Wyse anasema kuwa  kuna watu wamekuwa wakionekana wakiongea vitu kuhusu watu wengine na kuaminika wakati hawajulikana hali zao za kiakili inawezekana wakawa na matatizo ya akili bila kujua.

mimi siamini katika hilo  wanalosema,  atakuwa tu labda aliteleza  na mimi naona kuwa hawa wanaosema watakuwa ni mapunguani  na wanaupungufu wa akili  watu hawamjui wanamuona ona tu  na unaanza kuongea ongea  ila mimi ninajua ben pol anafanya show na watu mnaona kabisa.

Wyse na Ben pol wamekuwa wakifanya kazi pamoja kwa muda sasa na hata katika moja ya nyimbo yake ya BADO KIDOGO ambayo imefanya vizuri.

Ben Pol Nae Akimbilia Nchini Kenya.

Msanii wa muziki nchini, ben pol nae ameamua kufuata nyayo za wasanii wenzake baada ya kuamua kujihusisha na mapenzi na mwanamke kutoka kenya jama alivyofanya Diamond na Alikiba .

Wasanii wengi wa watanzania hasa wa kiue wamekuwa wakijiingiza na mahusiano na wasichana kutoka nje ya nchi hasa Kenya na Uganda huku wakiwaacha wasichana kutoka Tanzania wakiwa solemba.

Gumzo ili limekuwa la muda mregfu kuwa kwanini wasanii wa kiume kutoka tanzania wamekuwa kaitika mahusiano na wasichana kutoka nje ya tanzania huku kukiwa hakuna majibu kuhusu hilo, na zaidi sana ni kwamba mahusiano hayo yanakuwa ya uhakika mpaka kufikia hatua ya kufunga ndoa.

 

 

Monalisa Awatolea Povu Wanaomuita ‘Bibi’

Muigizaji mkongwe wa filamu za Bongo movie Ivyonne Cherry maarufu kama Mobalisa amewatolea Povu zito watu ambao walimuita bibi Baada ya kuonekana kwenye video ya msanii Ben Pol.

Mwezi uliopita Staa wa Bongo fleva Ben Pol aliachia video yake ya wimbo wake wa Ntala Nawe na ndani yake alimuweka Monalisa Kama Video Queen Wake uwamuzi uliozua hisia mbalimbali kutoka kwa mashabiki.

Kwenye mahojiano aliyofanya na kipindi cha Enews cha EATV, Monalisa amefunguka na kusema hakushangaa comments za mashabiki wa Ben Pol waliomuhoji kwanini hakuchukua Wasichana wadogo wa kuendana naye.

Kila mtu ana mtazamo Wake na kwangu Mimi hicho ni kitu cha kawaida  watu lazima tu wataongea midomo wameumbiwa ili kuongea ila poleni sana na itabidi tu muangalie video kwa sababu Ben Pol ndiye mtu ambaye amenichagua na ameona ninapendeza kwenye video yake”.

Lakini pia Monalisa ameweka wazi kuwa yeye ni shabiki namba moja muziki wa Ben Pol hivyo alipopata nafasi ya kuwa video queen alikuwa tayari hata kufanya bila malipo lakini Ben alimpa kiasi fulani cha pesa ambapo halukitaja hadharani.

 

Ben Pol Afungukia Mapenzi Yake Kwa Monalisa

Ben Msanii wa muziki wa RnB Bongo, Benard Paulomaarufu kama Ben Pol amefunguka na kuelezea jinsi anavuomkubali mwanamama Mkongwe katika tasnia ya Bongo Movie Ivyonne Cherry ‘Monalisa’.

Ben Pol ameweka wazi kuwa Monalisa ndiye mwanamke namba moja kwake kuliko wasanii wote wa kike wa muziki na filamu Bongo.

Monalisa ameonekana kama video queen katika video ya nyimbo mpya ya Ben Pol inayofanya vizuri hivi sasa ‘Ntala Nawe’.

Kwenye mahojiano na Global Publishers, Ben Pol amefunguka na kuweka wazi kuwa anamkubali sana Monalisa kutokana na kazi zake Lakini pia amekuwa akimuhamisha kufanya Muziki bila kiki.

Ananihamasisha kwa kweli kwa namna anavyojitunza, nimefarijika sana kugundua kwamba Monalisa pia anapenda muziki wangu same way mimi ninavyopenda kazi zake za filamu, nilikuwa na ndoto ya kufanya kazi naye siku moja, nashukuru Mungu leo imetimia, niwaombe mashabiki waingie kwa wingi kujionea kazi yangu mpya katika Mtandao wa Youtube niliyofanya naye inayoitwa Ntala Nawe”.

 

BASATA Wajenge Urafiki na Wasanii-Ben Pol

Msanii wa Muziki wa Bongo fleva Bernard Paul maarufu kama Ben Pol amewafungukia BAraza la sanaa Tanzania (BASATA) na kuwataka kujenge mazingira rafiki na wasanii.

Kwenye mahojiano na Enews ya East Africa Tv, Ben Pol ameweka wazi kuwa ni muhimu kwa BASATA kutengeneza urafiki na ukaribu na wasanii ili kuondoa ile dhana ya kuhofia pale wanaposikia wanaitwa BASATA.

Tangu Mwanzoni watu walikuwa wanaitwa BASATA kwa matatizo lakini ingekuwa kuna Ukaribu fulani yaani wangeanza hadi kuita wasanii kwa ajili ya mambo mazuri kama kupongeza wasanii kwa ajili ya kushinda tuzo ingekuwa vizuri.

Sasa hivi imekaa Kwenye akili za watu wengi kama ukiitwa BASATA basi ujue ni msala lakini wakijenga mazingira rafiki na wasanii basi kutakuwa na matokeo chanya katika sanaa na uhusia Mzuri”.

Siku za hivi karibuni Kumekuwa na mvutano mkubwa baina ya wasanii na BASATA hasa linapokuja suala la sheria mpya na maadili za nyimbo wanazotoa.

BASATA Inashusha Muziki Wa Bongo Fleva- Ben Paul

Msanii wa muziki wa Bongo fleva nchini anayefanya miondoko ya RnB, Bernard Paul jina la usanii Ben Pol ameitupia lawama BASATA kama chanzo cha kushuka kwa muziki wa Bongo fleva.

Ben Pol amedai muziki wa Bongo fleva unashuka kutokana na presha  kubwa ambayo wasanii wanapata kutoka kwa taasisi zinazosimamia muziki huu yaani BASATA.

Kwenye mahojiano na kipindi cha Kikaangoni cha East Africa Tv, Ben Pol amefunguka kama ifuatavyo:

Bongo Fleva na yenyewe kama imetetereka hapa katikati, naona kama kuna presha ya kutoa muziki mzuri, kuna presha ya kuwa relevant, kuna presha ya wasanii wachanga kutoka, kuna presha ya vyombo kama taasisi kumekuwa na presha ambao ndio walezi wetu.

BASATA ni chombo na chombo pia kinaongozwa na binadmu, hata tukikataa hatuwezi kujikataa kuwa sisi ni binadamu wote sisi ni binadamu. Kunaweza kuwa na makosa ya kibinadamu pia taasisi yoyote au chombo chochote kwa sababu kinaongozwa na binadamu kinaweza kikawa na makosa ya kibinadamu. Naheshimu namna ambavyo wanasimamia na wanapigania sanaa yetu lakini sote ni binadamu”.

Wasanii wengi wamekuwa wakiilaumu BASATA kwa kuwawekea vikwazo katika kutengeneza muziki mzuri kutokana na sheria mbali mbali.

Ben Pol Akana Kuwa Kwenye Penzi na Ebitoke

Msanii wa Muziki wa Bongo fleva Bernard Paul maarufu kama Ben Pol amekana kuwa Kwenye Mahusiano ya Kimapenzi na mchekeshaji kutoka Timamu Tv, Ebitoke.

Tetesi za Ben Pol na Ebitoke kuwa Kwenye Mahusiano zilianza kusikika Mara baada ya Ebitoke kukiri hadharani kuwa anampenda Ben Pol na kuwa angefurahi sana kuwa naye.

Kwenye mahojiano na Bongo 5, Ben Pol alikataa kukubali kuwa Kwenye Mahusiano na Ebitoke au hata kuwahi kuwa naye tofauti na Ebitoke ambaye ameshasema mara kwa mara kuwa wapo Kwenye Mahusiano:

Kuhusiana na mahusiano hayo its Complicated ingawa kila kitu nilishaongea ila kila kitu kilichoonekana kwenye vyombo vya habari ni sehemu ya maisha yangu”.

Lakini pia Ben Pol alifunguka na kuendelea kunena:

Vyovyote mtu atakavyohisi aendelee kuhisi ila mimi siwezi kutamka chochote ila muda ukifika kama kweli niko kwenye mahusiano ntaweka wazi na kama siko nae pia itafahamika”.

Imeshawahi kusemekana kuwa Ben Pol hajawahi hata kuwa Kwenye Mahusiano na Ebitoke bali ilikuwa ni kiki tu.

Ben Pol Ajibu Tuhuma Za Kupotea Kimuziki na Mziki Mpya

Msanii wa muziki wa Bongo fleva anayefanya vizuri na mahadhi yake RnB, Bernard Paulo maarufu kama Ben Pol ametangaza kuja na staili mpya ya muziki baada ya Tetesi za kupoteza ladha katika mziki wake.

Mashabiki wa Ben Pol wamedaiwa kulalamika Msanii huyo kupoteza muelekeo katika hii miaka ya katibuni na kuishia kupoteza muziki ambao hauna ladha ya kuvutia kama ilivyokuwa zamani.

Kwenye mahojiano na Bongo 5, Ben Pol ameweka wazi kuwa yeye hajabadilika kama msanii bali somo ndio limebadilika pia amedai kuwa anataka kuwafurahisha hao wanaodai amepotea kwa mziki mpya:

Wanaosema hivyo ntawafurahisha very soon”.

Lakini mbali na kuzungumzia hilo ametaja kolabo zake alizofanya na wasanii kutoka nje mfano kolabo zake na wasanii wa Nigeria kuwa zimesaidia sana kwani zimemueka sehemu nzuri ambayo anafanya vizuri katika baadhi ya nchini za kiafrika hasa kwa upande wa Afrika mashariki na Afrika magharibi.

Ben Pol Kuweka Mkono Kwenye Kazi za Wasanii Kutoka Kenya

Msanii wa Muziki wa Bongo fleva Bernard Paul Maarufu kama Ben Pol amefunguka na kuweka wazi kuwa ana mpango wa kufanya kazi na wasanii zaidi ya watano kutoka nchini Kenya.

Ben Pol ambaye anafanya vyema kwa staili yake ya RnB amekuwa aking’aaa sana Kwenye nyimbo za wasanii mbali mbali ambapo amekuwa akifanya vizuri kama mshirikishwaji.

Kwenye mahojiano aliyofanya hivi karibuni na kituo kimoja kikubwa Cha habari nchini Kenya, Ben Pol aliwataja Naiboi na wanamuziki wa kikundi cha Elani kuwa ni kati ya Mastaa kutoka nchini humo walioko katika mazungumzo ya kushirikiana nao katika kazi za muziki.

Ben Pola anafanya vyema na Kolabo yake na Mayan sama Kwenye wimbo unaoitwa ‘Amen’.

 

Ben Pol- Muziki Wa RnB Unahitaji Uvumilivu Ili Kupata Mafanikio

Msanii wa muziki wa Bongo fleva anayetamba kwa miondoko ya muziki wake wa RnB Bernard Paul maarufu kama Ben Pol amekiri muziki huo haulipi na unahitaji uvumilivu.

Ben Pol ambaye ameshawahi kutengeneza hits songs kibao kwa miondoko yake ya RnB amekiri kuwa muziki aina hiyo ya muziki kutusua sio rahisi na kukiri msanii anahitaji uvumilivu wa hali ya juu ili kupata mafanikio.

Kwenye mahojiano na Kipindi cha The Dj Show cha Radio One, Ben Pol amefunguka haya:

RnB ni muziki ambao unahitaji mtu uwe na passion kwa sababu asilimia kubwa ya miziki ya RnB haifanyi biashara vizuri, haiuzi . Kwa hiyo wale wachache wanaofanya kwa moyo na kubadilisha kidogo na kuifanya Kitanzania, wanaimba kiswahili fasafa, unaona kina Jux, Rama Dee, Ben Pol wanaweza kufanikiwa kuwafikia watu.

Lakini wengine wanaingia kwa mkumbo kwa kujaribu ndio wanashindwa wanaingia kwenye miziki mingine ambayo ndio inaonekana unauza hapo hapo, hata hao wengine inadoda pia”.

 

Ben Pol Atoa Sababu ya Kutotoa Video ya Wimbo Wake na Chidma na Kiss Daniel

Msani wa muziki wa kizazi kipya Ben Pol amefunguka na kusema kuwa watu wamezoea kufanya muziki kwa mazoea lakini wanashindwa kujua kwamba kuna muda kunatakiwa kuwe na utofauti wa kufanya kazi kwa upekee.

Akijibu swali aliloulizwa kuhusu kwanini nyimbo zake mbili alizotoa na wasanii Chidma na Kiss Daniel , Ben Pol anasema kuwa aliamua kufanya hivyo ili kuonyesha utofauti wake na wasanii wengine na sio kufanya kazi za mazoea.

Kila kitu ni mipiango tu na nina fanya muziki kwa kuangalia vile ninataka kuufanya muziki wangu, lakini watu wanataka tufanye katika mazoea, usishangae kuona natoa video ya wimbo huo mwakani huko.sasa hivi nimekuwa nikitoa nyimbo kupitia paltform tofauti tofauti kwaio watu wakae waone huyu Ben Pol anaenda wapi sasa hivi.

Ben pol anawaomb mashabiki wake kukaa na kusubiria muda ukifika kila kitu kitakuwa sawa tu maana kila kitu kinahitaji muda sio vinginevyo.

 

 

Ben Pol Akana Tetesi za Yeye Na Barnaba Kuunda Kundi Moja

Msanii wa Bongo fleva Bernard Paul maarufu kama Ben Pol amefunguka na kuzima tetesi zilizosambaa Kwenye mitandao ya kijamii na kudai kuwa yeye na Barnaba wanaenda kundi moja la muziki.

Barnaba na Ben Pol ni moja kati ya Wasanii Kwenye tasnia ya Bongo fleva ambao wana ukaribu sana na wameshafanya nyimbo kadhaa pamoja.

Siku za hivi karibuni waliwaambia mashabiki zao wanataka kuunda kundi moja na kufanya Muziki pamoja ambapo kundi hilo walipanga kuliita BEBA yaani kirefu ni Ben na Barnaba.

Kwenye mahojiano aliyofanya na Wasafi Tv, Ben Pol amekana taarifa na kusisitiza kuwa walivyosema hivyo ilikuwa ni utani lakini hawakumaanisha kama kweli walikuwa wana mpango wa kuwa kundi moja:

BEBA was a a joke tulisema kwa nini wasanii wanaungana wawili wawili hlafu wanakata vifupi vya majina yao kwanini na sisi tusifanye hivyo? Lakini ilikuwa kama utani ingawa tumesharekodi nyimbo kama mbili lakini hatifanya kama kundi bado lakini huwezi kujua huko mbele because we are family na tunasopitiana”.

Wasanii mbali mbali wamekuwa wakiungana na kuwa kundi moja mfano ni Rostam ambao ni Roma na Stamina na MoCo ambao ni Moni na Country Boy.

Ben Pol- Tetesi Za Darassa Kutumia Madawa Ya Kulevya Sio Za Kweli

Mwanamuziki wa Bongo fleva Darassa alibamba sana siku za nyuma na kibao chake cha ‘Muziki’ ambacho kilikuwa ni kikali balaa lakini siku za hivi karibuni sifa hiyo njema aliyokuwa nayo imekumbwa na wingu baya.

Tetesi za Darassa kujiingiza Kwenye matumizi ya madawa ya kulevya zilisambaa kama moto wa kifuu baada ya picha yake tata kusambaa Kwenye mitandao ya kijamii na kuzua sintofahamu.

Ben Pol ni moja kati ya watu wa karibu wa Darassa na hata amefanya naye kolabo mbili ambazo ni Muziki na sikati Tamaa.

Kwenye Interview ambayo Ben Pol amefanya na Clouds Tv, amesema hamsini taarifa hizo kwani anawasiliana naye karibia kila siku.

Kusema kweli siamini, sina element yoyote inayonifanya niamini chochote kuhusiana na hizo tetesi kwa sababu ili mtu uweze kusema kitu lazima uwe na element ambazo umeziona lakini mimi hamna element.

Mimi tunaongea masaa mawili, saa zima kwenye simu, video call sometime kwa hiyo sioni kuna element ya hicho kitu”.

Wasanii wengi walikuwa wanafanya vizuri tumeona jinsi wanavyoteketea kisa matumizi ya madawa ya kulevya ambayo kwa kiasi kikubwa yameathiri maisha yao mfano mzuri ni Q Chillah,Ray C na Chid Benz na wengineo.