Bill Nas Ajitapa Kuwa Hajawahi Kuachwa na Mwanamke

Msanii wa muziki wa Bongo fleva anayefanya miondoko ya kurap Bill Nas ameibuka na kudai kuwa kwenye maisha yake yote hajawahi kuachwa na mwanamke kwenye mapenzi.

Kwenye mahojiano aliyofanya na kituo kimoja cha habari katika siku za Hivi karibuni Billnass amesema kuwa amedate na watu wengi sana huku akisema neno wengi linaanzia na mbili lakini hajawahi kuachwa.

Mimi sijawahi kuachwa kwenye mahusiano kama kuna dada ana prove amewahi kuniacha na nimedate na watu wengi kidogo sio wengi sana kwasababu wengi inaanzia na mbili sasa sikujua anamzungumzia dada gani lakini kwa bahati sijawahi kuachwa nikiona vitu haviendi naamua kufanya vitu vingine“.

Billnas alitengeneza headlines miezi michache iliyopita Baada ya video yake ya faragha na Mpenzi Wake Nandy kusambaa katika mitandao ya kijamii.

Billnas Afunguka Sababu Za Kumpotezea Nandy

Msanii wa Hip hop nchini William Lyimo maarufu kama BillNas amefunguka na kuweka wazi sababu zilizopelekea kumpotezea aliyekuwa Mpenzi Wake Faustina Charles ‘Nandy’ wikiend iliyopita.

Wikiendi iliyopita Msanii Nandy alifanya uzinduzi rasmi wa albamu yake ya ‘The African Princess’ na katika hafla hiyo Billnas alikuwepo ndipo Nandy alipomfuata Billnas kwa ajili ya kuimba wote lakini cha ajabu Billnas alimpotezea kabisa Nandy.

Baada ya sakata hilo BillNas amefunguka Kwenye mahojiano na kipindi cha Enews na kusema sio kila sehemu anaenda Kama msanii kuna sehemu nyingi anaenda Kama mtu wa kawaida tu na anakuwa hayuko tayari kuimba  na haikuwa lazima kushiriki kama msanii.

Sapoti niliyotoa ya kununua albamu na kufika pale ilitosha, sioni sababu ya kuendeleza uadui kati yangu Mimi na Nandy Mimi nilienda pale kumpa sapoti yangu ya kweli kama msanii mwenzangu na si vinginevyo, hivyo alivyonipa mic sikujuwa nifanye nini kwa muda ule kwa kuwa sikuwa tayari kuimba kabisa”.

Lakini pia Billnas amefunguka kuwa ni miezi Sita imepita tangu atoe nyimbo yake hivyo amewataka mashabiki wake wakae mkao wa kula kwani muda wowote anaachia mambo.

Bill Nas Aanika Majibu Yake Ya Ukimwi

Msanii wa muziki Bongo fleva William Nicholaus maarufu kwa Jina la usanii kama Bill Nas ameanika hadharani majibu yake ya virusi vya Ukimwi mara baada ya kupima.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Bill Nas avowals taarifa mashabiki zake kwa uwamuzi wake wa kwenda kupima afya yake na baada ya kupata matokeo yake aliyaanika pia.

Bill nas amewaasa mashabiki zake kwenda kupima ugonjwa huo na kuwaambia kuwa kila mmoja ni muhimu kujua hali ya afya yake.

Bill Nas ameungana na Listi ya wasanii wengi ambao siku za hivi karibuni wameonekana wakiwa wanapima Ukimwi na kisha kuyaachia majibu yao hadharani.

Bill Nas Akana Bifu na Dogo Janja Baada Ya Kumwagiana Povu Zito

Msanii wa Bongo fleva anayefanya miondoko ya kuchana William Lymo maarufu kama Bill Nas amefunguka na kuweka wazi kuwa yeye na msanii mwenzake Dogo Janja hawana bifu lolote.

Tetesi za Bill Nas na Dogo Janja kusemekana kuwa na bifu zilianza mara baada ya wawili hao kurushiana maneno ya kejeli Kwenye mitandao ya kijamii ambapo Dogo Janja alimtania Bill Nas kwa kuachwa na mwanamke wake kwa sababu ya mdomo  na Bill Nas alimchana kuwa ameolewa na Uwoya ili acheze na mtoto wake.

Global Publishers lilimtafuta Billnass ili azungumzie ishu hiyo ambapo alisema hana bifu na Dogo Janja bali maneno hayo yalikuwa ni utani tu.

Sina bifu na Dogo Janja, hayo maneno tuliyokuwa tunaandikiana yalikuwa ni utani tu, sisi tumeshazoea kutaniana kwa hiyo nawaomba mashabiki zangu wasichukulie kwamba tuna tofauti”.

 

Billnas- Nipo Tayari Kufanya Kazi BASATA Ili Kuikoa Sanaa

Staa wa Bongo fleva na Hitmaker wa wimbo wa ‘Labda’ Billnas amefunguka na kuweka wazi kuwa Yupo Tayari kufanya kazi BASATA (Baraza la Sanaa Tanzania).

Billnas ambaye mbali na kuwa ni msanii mzuri lakini pia ni msomi kwani alihitimu elimu yake ya Chuo Kikuu mwaka jana.

Billnas amefunguka na kuweka wazi kuwa a naomba Kupitia elimu yake ya chuo kikuu apatiwe kazi BASATA ili aweze kutatua migogoro inayoendelea kati ya wasanii na BASATA.

Kwenye mahojiano na kipindi cha Refresh cha Wasafi Tv, Billnas amesisitiza kuwa wasanii wanahitaji mtu wa kuwawakilisha ili mawazo yao yafike katika uongozi:

Mimi natamani sana kufanya kazi pale BASATA ili niweze kushirikiana nao kutengeneza miundo mbinu sahihi ya kuweza kuwasaidia wasanii kuliko makatazo, masharti magumu, kuigandamiza sanaa nahisi wakinipa nafasi na vyeti vyangu kuna kitu tunaweza tukatengeneza”.

Lakini pia Billnas alisisitiza kuwa hataki hiyo kazi kwa ajili ya kupata mshahara mkubwa bali anajitoa ili kusaidia BASATA kufanya maamuzi yatakayo wafaidisha wasanii na kazi zao:

Sitaki hiyo nafasi kwa ajili ya kunufaika ila natafuta njia ili wasanii wote tuweze kunufaika na pia maprodyuza, waandishi, madancer na hata waigizaji kwa sababu sanaa sio kitu cha mchezo”.

 

Bill Nas Athibitisha Kuwa Yupo ‘Single’ Kwa Sasa

Msanii wa muziki wa Bongo fleva anayefanya vyema kabisa na hit single yake ya ‘Labda’ William Lymo maarufu kama Billnas ameweka wazi kuwa kwa sasa hana mpenzi yaani ni Single Boy.

Bill Nas amefunguka na kudai hivi sasa yupo single hana mwanamke Lakini pia kinacho mtatiza ni kwamba bado hajajua ni mwanamke gani ambaye anatakiwa kuwa naye Kwenye Mahusiano.

Kwenye mahojiano aliyofanya na Star Showbiz, Bill Nas amesema kwamba hahitaji kukurupuka, anachotamani ni kupata mtu sahihi ili aweze hata kufunga naye ndoa na si kuwa kwenye uhusiano ambao unaanza leo na kumalizika kesho.

Watu wanaweza wasiamini lakini ukweli ni kwamba kwa sasa sina uhusiano wa aina yoyote ile. Kinachonikwamisha kuingia ni kwamba sioni bado mwanamke sahihi wa mimi kuwa naye.

Ninasubiri pengine Mungu anionyeshe, huyo nitakayempata ndiye atakuwa mke wangu na sihitaji uhusiano wa kuanza leo na kuvunjika kesho”.

Bill Nas alishawahi kuwa Kwenye Mahusiano na msanii mwenzake Faustina Charles maarufu kama Nandy lakini wawili hao waliachana siku za nyuma kidogo.

Petit Man Hajahusika Kufuta Video Yangu Youtube- Billnas

Msanii wa muziki wa Bongo fleva anayetamba kwa miondoko yake ya kurap Billnas ameibuka na kumkingia kifua Petit Man Wakauache na kusema hajahusika katika kufuta video yake Youtube.

Kwa muda mrefu Petit Man alikuwa anasimamia kazi za Billnas mpaka pale alipohiondoa Kwenye Label hiyo mwaka jana mwishoni hivyo kuacha kumsimamia Billnas.

Siku ya juzi Billnas alilalamika kufutwa kwa video yake mpya ya wimbo wake ‘LAbda’ na watu wasio julikana na mara moja tetesi zilianza kutembea na Petit alinyoshewa vidole na kudaiwa kuhusika.

Lakini Kwenye Interview na kituo kimoja cha habari Billnas amemkingia kifua Petit Man na kudai sio yeye Lakini pia amesema sio mara ya kwanza anafanyiwa mchezo huo mchafu:

Sio mara ya kwanza watu kutoa video Yangu Youtube na sielewi kwanini wananifanyia hvyo maana mimi aio mtu wa kupiga views milioni 10, sijajua ni nani anafanya hivyo lakini sio Petit Man kama watu wanavyodai.

Naamini mtu anayenifanyia hivyo anataka kunikwamisha maana hakuna kingine anachofaidi akishanifanyia mimi hivyo”.

 

 

Billnas Adai Hawezi Kuwa na Mwanamke Anayejichubua

Staa wa muziki wa Bongo fleva anayefanya miondoko ya kuchana BillNas ameibuka na kuweka wazi kuwa hawezi kuwa kwenye mahusiano ya Kimapenzi na mwanamke anayejichubua.

Billnas ameweka wazi kuwa Kitendo Cha mwanamke kubadilisha rangi yake ya mwili kutoka Kwenye weusi asilia kuwa mweupe anakuwa kama amejikataa mwenyewe.

Kwenye mahojiano na kipindi cha Refresh cha Wasafi Tv, Billnas amekataa uhusiano na wanawake wanaotumia kitaulo (mkorogo):

Kujichubua au kubadilisha rangi ya mwili sio pia kabisa mimi mwanamke anayejichubua siwezi kuwa naye kimapenzi uaani sijui iweje.

Kujichubua ni kitu ambacho mimi niko tofauti nacho sana kwa sababu kwanza unakataa uhalisia wako vile ambavyo mwenyezi Mungu amekubariki na hii rangi yetu nyeusi ipo very unique.

Lakini pia kuna vitu vingi vinavyomfanya mtu kuwa mzuri na viko ndani yako na sio muonekano wako wa nje Fanya matendo mema mazuri watu watakupenda”.

Baada ya kuachia kibao chake kipya ‘Labda’ Bill Nas alitangaza kuwa video hiyo ilidukuliwa katika mtandao wa Youtube na kufutwa.

 

Lulu Diva Adaiwa Kufaidi Penzi La Bill Nas

Msanii wa Bongo fleva anayefanya vizuri na kibao chake cha ‘Ona’ Lulu Abbas maarufu kama Lulu Diva amesemekana kuwa Kwenye Mahusiano ya kimapenzi na msanii mwenzake Bill Nas.

Global Publishers wanaripoti kuwa wasanii hao wawili wamekuwa na ukaribu wa ajabu na wameonekana wakionyeshana Mahaba hadharani bila kujali macho ya watu.

Gazeti hilo linaripoti kuwa lilimpata mtu ambaye alitoa taarifa hiyo ambapo alifunguka:

Walianza kama masihara, tukajua labda Rich Mavoko ndiyo anakaa kwa Lulu kumbe ni Bill Nas bwana, juzi walikuwa tena pamoja wakielekea mkoani sijui mkoa gani lakini picha zao za kujibebisha zinamaanisha“.

Baada ya Tetesi hizo na kusindikizwa na picha kadhaa Kwenye mitandao ya kijamii zikionyesha ukaribu Global Publishers lilimsaka Lulu Diva ambaye alimwaga povu hili:

Hivi jamani mtu kuongozana na mwanaume ndiyo kutembea naye? Mbona mnataka kuniharibia kwa mtu wangu niliyekuwa naye?“Bill Nas ni mshikaji   wangu wa kawaida tu, juzi (Jumamosi iliyopita) tuliandaliwa shoo ya pamoja huko Iringa, tukiwa njiani tulikuwa tukipiga mapicha picha kama mtu na rafiki yake, nashangaa watu wanageu-zageuza maneno”.

 

Bill Nas Hawezi Kumfikia Ngwea- TID

Mkongwe wa Muziki wa Bongo fleva khalid Mohamed na maarufu kama TID ameibuka na kuweka wazi kuwa marehemu Ngwea alikuwa msanii mkali hata Bill Nas hawezi kumfikia.

Ikiwa ni siku chache tangu Ngwea atimize miaka kadhaa tangu Kifo chake TID ambaye alikuwa rafiki yake mkubwa ameweka wazi kuwa pengo lake halitaweza kuzibwa na msanii yoyote.

Kwenye mahojiano na kituo kimoja cha habari TID amesisitiza hata Bill Nas hajaweza kumfikia Ngwea kwa kipaji alichokuwa nacho enzi za uhai wake:

Hakuna msanii anayeweza kumfikia Ngwea that man was special Ngwea alikuwa blessed alafu umfananishe na nani? Bill Nas anaweza kuwa a half of it lakini hawezi kuwa kama Ngwea, Ngwea can rap Ngwea can sing Ngwea can give you melody halafu unataka kumfanisha na mtu? Hakuna wa kufanana naye”.

TID na Billnas walishawahi kuwa Kwenye bifu zito miaka ya nyuma lakini bifu hilo lilimalizika baada ya kutoa pamoja wimbo unaoitwa ‘Ligi Nzito’.

Bill Nas Adai Kuwa Video Ya Ngono Na Nandy Haikuathiri Mahusiano Yake

Staa wa muziki wa Bongo fleva Bill Nas amefunguka na kusema pamoja na kwamba video yake ya ngono na Nandy ilivuja lakini mahusiano yake hayajavunjika.

Miezi michache iliyopita Bill Nas na Nandy walikumbwa na masahibu mazito baada ya video yao ikiyowaonyesha wakiwa faragha kuvuja Kwenye mitandao ya kijamii.

Lakini Bill Nas anaiambia Bongo 5 kuwa pamoja na video hiyo chafu kuvuja na kuonekana na dunia nzima mpenzi wake hakumuacha bali alizidi kuwa katibu naye katika kipindi hiko:

Hapana sijaaachana na mpenzi wangu nipo naye hadi sasa na ndio mtu pekee nilikuwa nawasiliana naye kila saa. She is very clever anajielewa, alitazama kwanza, alijua, akaangalia ni kwa namna gani anaweza kujenga kuliko kuharibu zaidi”.

Lakini na kwa upande wa Nandy pia Hivi karibuni akiwa katika media tour nchini Kenya alisema kuwa Boyfriend wake amemkataza kuzungumzia suala hilo ila bado penzi lao linaendelea na hali kuvunjika kwa skendo ile.

Nandy na Billnas pia wamesisitiza kuwa wameendelea kuoa marafiki na kuweka skendo ile nyuma.

Bill Nas- Nandy ni Dada Yangu na Ninamuheshimu Sana

Msanii wa Bongo fleva aliyefanya vizuri na ngoma zake kama chafu pozi amefunguka na kusema Nandy ni dada yake na anamuheshimi sana.

Bill Nas na Nandy walishangaza watu wengi wiki chche zilizopita baadae ya kuitana dada na kaka huku Ikiwa wazi kabisa kuwa wawili hao walisha wahi kuwa Kwenye Mahusiano siku za nyuma.

Bill Nas ameiambia Enews ya EATV kuwa uamuzi wake wa kumuita Nandy dada unatokana na ukweli kuwa mapenzi yao yalipiita siku nyingi sana kwani baada ya kuachana na Nandy alikuwa Kwenye uhusiano na wasichana wengine wawili hivyo kwake sio Ex tena bali ni dada:

Kwa kweli kibusara Nandy ni dada yangu inaweza pia kiumri akawa dada yangu ingawa sina uhakika lakini ni dada kiheshima kwa sababu sijawahi kumvunjia heshima kwa namna yoyote ile ndio maana nikamuita dada lakini sio kindugu”.

Bill Nas na Nandy walizua gumzo mwezi uliopita baada ya video yao ya ngono kuvuja Kwenye mitandao ya kijamii.

Bill Nas: Sio Lazima Kila Mtu Ajue Mahusiano Yangu

Mwanamuziki wa Bongo fleva anayetamba kwa hivi sasa na ngoma yake ya ‘Tagi bovu’ amefunguka na kusema yeye sio msururu sana lakini anaona kuna baadhi ya vitu ambavyo anaona hamna umuhimu kuvianika na kila mtu ajue.

Bill Nas ametengeneza sana headlines kwenye mitandao ya kijamii wiki mbili tatu tangu atoke ngoma yake lakini kama kawaida kilichokuwa kinamfanya aongelewe sana ni mahusiano yake ya kimapenzi.

Kuna tetesi zilizosambaa toka mwaka jana na kudai kuwa Bill Nas ana Mahusiano ya kimapenzi na msanii mwenzake kutoka THT Nandy habari ambazo siku zote wawili hao wamezikataa na kusema wao ni marafiki.

Kwenye Interview aliyofanya na Dizzim Online, Bill Nas amekataa taarifa zilizodai kuwa yeye ni msiri sana hasa linapokuja suala la mahusiano yake na mpenzi wake ambapo Bill Nas amekiri hapendelei kuanika Mahusiano Yake hadharani:

Kusema ukweli mimi sio kwamba ni msiri sana ila hivi ndivyo nilivyo sio lazima kila kitu kila mtu ajue ama wafahamu kuna vitu watu wanapaswa kama binadamu waheshimu privacy yako na kuna vitu unatakiwa ubaki navyo mwenyewe au watu wako wa karibu”.

Bill Nas amekiri kuwa ana mpenzi wake lakini hayupo tayari kumuweka wazi kwa sasa na hizi skendo za yeye kutoka na wasanii wenzake zinakuwa kama zinamuharibia mapenzi yake.

 

Petit Man: Bill Nas Sipo Naye Tena

Petit Man Wakuache anayejulikana kwa ukaribu na kufanya kazi na mwanadada Wema Sepetu amefunguka kuhusu kuacha kumsimamia mwanamuziki wa Bongo fleva Bill Nas anayefanya vizuri na ngoma yake ya Sina jambo.

Petit Man alikuwa anawasimamia Bill Nas na Country Boy kupitia kampuni yake ya usimamizi/ management company inayoitwa ‘Living Fast Living Good’ (LFLG).

Petit Mama amevunja ukimya na kudai kuwa ameamua kujitoa LFLG na sababu ya kujitoa kwenye kundi hilo ni kuwa amedai anataka kuanzisha kundi/ label yake binafsi licha ya watu kudai kuwa Petit man na Bill Nas walichana kwa uhasama Mkubwa.

Inasemekana kuwa Petit ameondoka LFLG kwa sababu ya ugomvi uliotokea na kutokana na kwamba LFLG kulikuwa na mameneja wawili yeye Petit na Mchafu hivyo alivyoondoka aliosepa na Country boy na Mchafu akabaki na Bill Nas.

Kwenye interview aliyofanya na Enews ya East Africa TV Petit amefunguka haya kuhusu sababu za kutengana na msanii wake Bill Nas:

Mimi nimejiengua LFLG sipo tena LFLG panini sio kwamba nimejitoa kwa matatizo au kwa ubaya na ugomvi hapana ile itabaki kuwa ni familia yangu na mchafu ni braza wangu na pia Bill Nas bado mshikaji wangu kiroho safi kabisa maskani kama kawaida panini sahivi niko na Rooftop ambao nimeingia nao share ambapo nawasimamia baadhi ya wasanii akiwemo Country Boy”.

Lakini pia Petit amekiri kuwa pamoja na kwamba Bill Nas ni msanii mzuri na amefanya naye kazi kwa zaidi ya miaka mine lqkini anaamini ulifika wakati wa kila mtu kwenda upande wake ingawa hawana ugomvi na bado anamsapoti kwenye kazi zake.