Ray vanny, Vannesa Watusua Na Dili la Essence Marekani

Wasanii wawili  kutoka katika muziki wa Bongo Fleva waliotajwa  kutumbuiza kwenye tamasha kubwa la EssenceFestival nchini Marekani, wasanii hao ni Vanessa Mdee na Rayvanny.Tamasha hilo ambalo kila mwaka hufanyika huko New Orleans, Louisiana mwaka huu limepangwa
kufanyika kuanzia July 4 hadi 7 mwaka huu.

Wasanii wengine wa Afrika waliotajwa kutumbuiza ni pamoja na Sauti Sol kutokea Kenya, Davido
kutokea Nigeria pamoja na Nasty C wa Afrika Kusini.Wasanii wengine nje ya Afrika ni pamoja na Miss Elliot, Mary J.Blidge, Nas, H.E.R, Teyana
Taylor, Pharrell Williams na wengine.

Tamasha ya Essence fest lilianzishwa na jarida la Essence mwaka 1995 likiwa na lengo la kuwapa
nguvu wanawake wenye asili ya rangi nyeusi na kusherekea tamaduni na muziki wa watu wenye
asili ya Afrika nchini Marekani.

Shaddy Boo Amkubali Zaidi Zari Kuliko Hamisa

Mwanadada maarufu katika mitandao ya kijamii Shaddy boo amfunguka na kujibu swali aliloulizwa na moja ya mashabiki zake kuhusu ni nani anaweza kumchagua zaidi kati ya hamisa na zari kama ikitokea akaambiwa achague mmpj wapo.

Mwanadada huyo ambae aliwahi kum-attack Zari alipokuwa na mahusiano na Diamond na hata baadhi ya picha zake kusambaa katika mitandao akiwa na msanii huyo hivyo kuhisiwa kuwa mwanadada huyo anaweza kuwa na mahusiano na Diamond Platinumz.

Alipokuwa akijibu maswali hayo katika uwanja wa snapchat, Shaddy boo anasema zari ni mwanamke bora na mama bora zaidi kuliko Hamisa hivyo siku zote chaguo lake litakuwa kwa zari na sio Hamisa.

Mashabiki Wamtolea Povu Aliemshauri Diamond Kuhama Nchi.

Moja ya mashabiki wa Diamond alimshauri Diamond platinumz kuhama nchi mara baada ya taarifa kusambaa kuwa msanii huyo amefungiwa kwa muda usiojulikana kisa kuimba wimbo   ambao  ulisgakatazwa kutokana na sababu za kimaadili.

hata hivyo ,shabiki huyo alisema kuwa diamond amekuwa  moja ya wasanii wanaojitolea sana katika kufanya kila kitu kwa jamii lakini serikali haioni mchango wake hivyo, ni bora kuhama nchini na kuhamia kenya au uganda mabako atakuwa huru kufanya kila kitu anachoweza kufanya.

Alichoandika shabiki kumshauri diamond platinumz.

Baada ya maoni hayo , watu wengine walikuja juu na kusema haiwezekanai kwa sababu yeye amekuwa akisaidia jamii basi avunje sheria za nchi na huku watu wakimuangalia hivyo wamuogope kama mungu mtu.

 

Watanzania Kuwania Tuzo za Soundy City Nigeria, Diamond aongoza.

Tuzo za Soundy city awards nchini nigria imetoa majina lukuki ya wasanii watakao wania tuzo hioz kwa mwaka 2019, wakati huo wakitoa idad iyo ya wasanii jambo la kufurahisha ni kwamba kwa Tanzania muziki unazidi kukua na wasanii wanazidi kujulikana nje ya nchi.

Diamond Platnumz atawala nominations nchini Nigeria katika tuzo za Sound City Awards 2019 kwa jina lake kuonekana Mara 11 kwenye vipengele tofauti akiwa single na vya kushirikishwa. Diamond ametajwa kuwania tuzo ya msanii bora wa kiume wa mwaka, digital artist wa mwaka, msanii bora wa pop, msanii bora wa mwaka, etc. Maua Sama anawania msanii bora wa kike wa mwaka Africa akichuana na kina Tiwa Savage na Yemi Alade, .

Vanessa Mdee anawania digital artist of the year pamoja na kina Davido, Diamond, Wizikid, Yemi Alade, Kwangaru ya Harmonize na African Beauty wa Diamond wanawania wimbo bora wa mwaka. Harmonize na boss wake Diamond wote wanachuana kutwaa msanii bora wa kiume Africa. Mboso anawania msanii bora mpya Africa

Kenya imepata nominations kupitia Sauti Sol, Kalgraph Jones , ambapo kwa upande wa mwaka 2018, khaligraphs jones amekuwa moja ya wasanii waliongoza sana Kenya kushinda tuzo mbalimbali ndani na nje ya kenya.

Tuzo hizo zinatarajiwa kutolewa mwakani huku tegemea kkubwa la wasanii hawa ni kura kutoka kwa mashabiki wenyewe.

Wasanii Waguswa na Kijana Aliyeibuliwa na Ugonjwa wa Kutisha

kuna baadhi ya picha na video zimekuwa zikisambaa katika mitandao ya kijamii zikimuonyesha mtoto wa kiume aliyekonda sana na kudhohofika kiasi kwamba anahitaji msaada wa kila kitu,

Mtoto huyo aliibuliwa na mwanadada floraj lauwo kutoka mwanza, huku akiomba watanzania wamsaidie ili aweze kupata pesa kwa ajili a matibabu yake nje ya nchi  na kuisaidia familia yake kwa ajili ya kupata  chakula bora na malezi mazuri kwa kipindi hiki anachoumwa.

Watu wengi wameguswa lakini  jamii inazidi kuwashukuru wasanii ambao wanamajina katika jamii kwa kuliona hili na kulitolea msaada kwa sababu hii imefanya watu wengine pia waguswe kupita wao.

Wasanii kama Wema Sepetu, Zari the Bossy, Riyama Ally, mwanadada Zamaradi Mketema, kaka Millard Ayo,Dogo janja na wengine wengi ambao waliweza hata kuhamasisha kupitia kurasa zao .

Naibu Waziri Awaonya Wanaopiga Picha za Uchi.

Naibu  Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe.Japhet Hasunga  amewashauri wasanii wanaopiga picha za utupu waache kupiga picha hizo badala yake watembelee Hifadhi za Taifa ili wakapige picha na simba, twiga chui pamoja na sokwe kwa ili  waweze kutangaza vivutio vya utalii vilivyopo nchini.

Pia amewataka wasanii wenye nia ya kutaka kutengeneza filamu  katika Hifadhi ya Taifa wawasaliane na Uongozi wa Hifadhi za Taifa au wawasiliane na  yeye mwenyewe moja kwa moja.

Ametoa rai hiyo wakati  akifunga tamasha  la utamaduni wa mtanzania inayowakilishwa na jamii za mkoa wa Lindi lililofanyika kwa muda wa siku nne katika  kijiji cha Makumbusho jijini Dar es salaam

Aidha, Ameiasa jamii iitumie mitandao ya kijamii kujipatia elimu badala ya kusambaza picha ambazo ni kinyume cha maadili ya Mtanzania.

Ameongeza kuwa Jamii iwakemee wasanii wenye tabia hiyo badala ya kusubilia Serikali ndo ichukue hatua.

Polepole Akutana na Wasanii Kuzungumzia Changamoto Zao.

katibu mwenezi wa chama  tawala nchini, Mh Humphrey Polepole amekutana na wasanii wa mzuki na miguzo nchini ikiwa ni kama mwakilishi wa serikali na kuongea nao mawili matatu yanayosumbua sanii nchini.

Wasanii wengi walijitokeza ikiwa ni kama wito wa serikali wa kutaka kukutana nao ili waweze kuzungumzia maswla yanayowahusu na kuona ni namna gani wanaweza kuayatatua ili kufanya sanaa ya tanzania iweze kuendelea mbele zaidi.

Ikumbukwe kuwa miezi michache nyuma  katibu mkuu wa chama icho alitangaza kuwa CCM haitawatumia wasanii tena katika shughuli za kichama hasa kampeni kwa uchaguzi utakao kuja kama ilivyokuwa kwa ule uliopita, jambo ambalo liliwafanya wasanii wengi kulalamika na hata kutuma salamu kwa Mh Rais kuangalia swala ilo.

Hata hivyo baada ya kikao icho kuisha hakuna kilichosemwa kuwa kimejadiliwa cha zaidi ya changamoto zinazokabili sanaa ya Tanzania , hivyo bado hakuna mrejesho wa swala hilo mpaka sasa.

Watanzania Walioshinda Tuzo za Africa Entertainment Awards USA 2018

Rayvanny amefanikiwa kuchykuwa tuzo katika kipengele cha Best vocalist of the year 2018

Diamond amefanikiwa kuchukua tuzo mbili ambazo ni  Best collaboration of the year katika wimbo wa  African beauty aliofanya na Omarion na nyingine ni msanii bora wa mwaka wa kiume.

Nandy pia amepata tuzo katika kipengele cha Best female artist of the year 2018

Dj wa msanii maarufu Diamond, anaejulkana kama Rommy Jones amepata Tuzo ya best Dj of the year

 

Miss Ubungo Awakumbuka Wanafunzi wa Umoja.

Aliyewahi kuwa Miss Ubungo mwaka 2014-2016 Diana Kato amewakumbuka wanafunzi wa shule ya umoja na kusherekea siku ya kunawa mikono Duniani pamoja shuleni hapo ikiwa kama moja ya njia ya kukumbuka na kuhamasisha mambo muhimu katika jamii kama ilivyo kwa walimbwende wa tanzania wanavyottumwa kufanya mambo yanayonufaisha jamii.

Diana Kato alifika shuleni hapo kwa lengo la kukutana na wanafaunzi wa shule hiyo na kuwaelismisha juu ya umuhimu wa siku hiyo duniani na kwao pia huko akishirikiana nao katika kufanya jambo hilo.

Diana Kato ambae tangu hapo nyuma amekuwa moja ya mabalozi wanaoshughulikia sana swala la upatikanaji wa maji mashuleni  ilikuwasaidia kujikinga na magonjwa yatokanayo na uchafu.

Hata hivo Diana amesikiliza changamoto mbalimbali zinazopatikana katka shule hiyo na kuahidi kushughulikia anayoweza kwa nafasi yake na kufikisha mengine sehemu zinazohusika.

Wanafunzi wa umoja wakiwa wameshika mabongo ya kuhasisha siku ya kunawa mikono Duniani.

Mikono ya wanafunziwa shue hiyo wakiwa wanafanya zoezi la kunawa mikono na sabuni.

Jinsi Watu Mbalimbali Walivyoguswa na Kupotea kwa Mo Dewji

Tangu kumesambaa na kuthibitika kwa taaarifa kuwa moja ya matajiri wakubwa duniani kutekwa nyara na watu wasiojulikana wasanii mbalimbali wameonekana kuguswa na habari hizo hivyo  kuamua kuonyesha hisia zako katika kurasa zao za instagram.

baadhi ya wasanii hao ni pamoja na

Flaviana Matata.

Mboni.

 Diamond platinumz.

Mwana Fa

Madam Ritha Paulsen

Wasanii Tanzania Watoka Kapa Tuzo za AFRIMMA.

Usiku wa kuamkia october 8 ilikuwa moja ya siku muhimu kutokana na ugawji wa tuzo za AFRIMMA nchi Marekani ambapo kwa upande wa waliokuwa wakiwania tuzo pia wasanii kutoka Tanzania walikuwepo baadhi yao.

Hata hivyo mwaka huu umekuwa tofauti kwa wasanii wa Tanzania kutokana na kwamba wale wote waliowekwa katika kategoria mbalimbali hawakuweza kufanikiwa kuchukua tuzo hizo huku wasanii kutoka Uganda na Kenya wakiinuka kidedea katika tuzo hizo.

Wasanii kama Nandy, Alikiba, Ommy Dimpoz, Vannesa, Diamond Platnumz na pia Navy Kenzo walikuwa aktika kategorai mbalimbali,hata hivyo wasanii kutoka nchi za jirani kama Khaligarph Jones,  na Eddy Kenzo waliweza kuibuka kidedea.

Wafahamu wasanii Wanaotembea na alama za maumivu ya Wapenzi Wao.

Wasanii wengi wamekuwa wakijisahau kuwa kukutana na mtu kwa mara moja na kujiingiza nae kwenye mapezi kuna weza kuwa na mwisho mbaya ndani yake, hii inawafanya wanajikuta wanaingia katika mapenzi mazito na kufikia kuchora tatoo ambazo mwisho wa siku zinakuwa kama kovu katika miili yao juu ya watu ambao inawezekana wakati wa kuachana waliachana kwa chuki na maumivu sana.

wasanii wengi wamekuwa wakichora tatoo  na wanaendelea kuzichora wengi bla kujifunza kutoka kwa wenzao. hawa ni baadhi ambao mpaka sasa wanatembea na maumivi ya makovu hayo.

CASTO NA TUNDA.

Hawa walipoanza casto alikuwa akijiamini sana mpaka kufikia hatua ya kuchora tatoo , pamoja na kelel za watu kumshauri casto lakini hakutaka kumsikiliza mtu, mapenzi yao yanaonekana kufika mwisho inagwa wamekuwa wagumu kuthibitisha hilo.

BROWN  NA WOLPER.

Brown aliamua kuchora tattoo ya wolper kifuani kwa kuamini kuwa hiyo ni alama tosha ya mapenzi yao lakini kwa sasa imebaki kama alama na kovu kwa mwanaume huyo.

NUH MZIWANDA NA SHILOLEH.

hii ni moja ya couple iliyovuma sana kiasi kwamba kila mmoja aliamua kuchora tatoo katika mwili wake yenye jina la mwenzake, lakini baada ya kuachana , shiloleh alifuta na kuchora ua ambalo halikuwa na msingi sana zaidi ya kuficha makovu ana maumivu ya mapenzi ya nyuma.

lakini pia wapo wasanii waliaomaua kuchora tatoo kamaishara ya kuwaonyesha wale watu wa muhimu katika maisha yao na nini wanamaanisha katika maisha yao kwa mfano.

AUNTY EZEKIEL NA TATOO YA MTOTO WAKE.

Aunty aliamua kuweka historia ya mtoto wake wa kike katika bega lake kwa kuliandika jina la mtoto wake kama ishara ya mapenzi yak kwake, ni mtoto wake na siku zote hatakuwa katika maisha yake.

IRENE UWOYA NA TATTOO YA AGNESS.

Baada ya kifo cha rafiki yake mpenzi aliamua kuandika tatoo hii kuonyesha  kuendelea kumkumbuka na kumpenda siku zote katika maisha yake.

 

 

 

 

Mashabiki Waombwa Kumsaidia Hawa wa Nitarejea

Kama mwaka sasa umepita tangu mwanadada hawa alipowahi kutolewa katika vyombo vya habari kuwa alikuwa amekuwa kama teja kutokana na matumizi ya pombe za kienyeji zilizompelekea pia kuacha muziki na kujikuta akibaki nyumbani tu,

Baada ya hapo walimsaidia dada huyo na kwenda sober ambapo alipatiwa matibabu na kuanza kurudi katika hali yake ya kawaida lakini bado alikuwa akihitaji msaada wa hapa na pale ili kurudi kimuziki.

Sasa mapya ayameibuka kuhusu hali ya mwanadada huyu huku akionekana kuendelea kudhoofka kabisa  na hii yote ni kutokana na ukweli kuwa mwanadada huyo kwa sasa ni mgonjwa sana na amekuwa akisumbuliwa na ugonjwa wa ini unaoendelea kutafuna sana afya yake.

Soudy Brown wa kipindi cha shilawadu kutoa Clouds Media amethibitisha ilo baada ya kwenda  kumtembea mwanadada huyo huku akionekana kudhoofika sana na hali yake aliyonayo kwa sasa.

Mwanadada huyo anaomba msaada kwa watu mbalimbali kwa chochcote kwa sababu ya matibabu na pia hata familia yao pia haina uwezo kwa kutoa huduma ya kila kitu.

Davista Afurahishwa na Ukaribu wa Jux na Diamond.

Msanii mpya katika game la muziki ambae ameachia ngoma inayokwenda kwa jina la super woman amefunguka na kusema kuwa amekuwa akifurahishwa sana na ukaribu wa Diamond na Jux kwa sasa na ana imani wanaweza kufanya kazi pamoja.

Davista anasema kuwa mara nyingi katika mitandao ya kijamii wamekuwa wakiwashindanisha wasanii hawa katika mavazi na kuimba nyingi zenye kuibua hisia kitu ambacho kiliwafanya wasanii hawa kuonekana kama wana bifu lakini kumbe sio.

Akiongea na meda, msanii huyo anaefananshwa sana na tkno kutoka Nigeria anasema pia anapongeza sana swala la WCB kuleta jibebe challenge ambayo anaona kuwa itasaidia kuwafichua vijana wenye vipaji waliopo mtaani lakini pia anaomba kusapotiwa katika kazi zake za muziki.

Wasanii wa Bongo Waaswa Kuacha Unafiki na Uoga.

Moja ya wanasiasa nchini, Peter msigwa amewaomba wasanii wa Tanzania kuacha kuwa wanafiki na waoga katika kutetea mambo ambayo yanakuwa na mnufaa kwa jamii hasa pale wanapoamua kufanya kwa ajili ya jamii.

Akiandika katika ukurasa wake, Peter msigwa anasema kuwa  ameona katika mitandao ya kijamii wasanii baadhi yao wakiungana na wasanii wa Uganda katika kampeni yao ya kuishinikiza serikali kumuachia mwanasiasa aliwahi kuwa msanii nchini humu Bob wine.

nimeona baadhi ya wasanii Tanzania wanaandika FREE BOBI WINE , jambo ambalo ni zuri lakini alipoonewa Sugu,Lissu ,Mawazzo ,Saanane,Azori  hapa Tanzania wamekaa kimya , Injustice  to one is injustice to all” Tuache unafiki  na UWOGA , Museveni Free BOBI wine, Magufuli FREE DEMEOCRACY.

 

Ray C, Koletha Mstari wa Mbele Kumshabiki Zari.

Sio kila mmoja anawez akukuchukia vile anaweza kukuchukilia mwingine  vile kundi kubwa la watu wanvayoweza kukuchukulia wewe.pamoja na kwamba mwanadada Zari the bossy amekuwa akipata upinzani mkali sana instagram ahasa katika page mbalimbali za udaku lakini kuna watu bado wanampenda na wanamsifia kila kukicha.

Mwanadada Ray c amekuwa moja ya watu hao wanaomsifia na kumpongeza kila kukicha na kila anapofanya jambo zuri, wikiendi iliyopita mwanadada zari aliweka picha nyingi zinazomuonyesha akiwa katika mashindano ya u-miss huko nchini kwao, wapo waliomponda sana kuwa hajapendeza na gauni alilovaa lakini iemkuwa tofauti kwa mwanadada Ray c na Koletha akutoka bongo movies.

Wasanii hawa wawili wameonekana kutokuwa na team  zamitandao na kumpongeza zri kwa kupendeza huko, wa upande wa Rayc pia amekuwa moja ya watu wanaopenda sana kukosoa kila anapoona mtu mmoja anaingiliwa na kushambuliwa sana katika mitandao ya kijamii , kwa mfano aliwahi kumttetea na hata kumkosoa hamisa kutokana na mambo tofauti tofauti.