Brown Akanusha Kukimbia Mombasa Baada Ya Kuiba Mke Wa Mtu

Msanii wa muziki kutoka Mombasa Kenya, Brown Mauzo ameibuka na kukataa yuhuma zinazomkabili za kukimbia Mombasa na kuja Dar Es Salaam baada Ya kuiba mke wa mtu.

Tuhuma hizo za Brown kukimbia Mombasa zilitolewa na msanii mwenzake anayeitwa Kelechi ambaye alidai Msanii huyo alikimbilia Dar kutoka Mombasa baada ya kutembea na mke wa Meneja wake.

Kwenye mahojiano na Kipindi cha Enews cha East Africa Tv, Brown amekataa tuhuma hizo na kusema yeye na Meneja wake wapo vizuri kabisa na hajaiba mke wake wala hajakimbia Mombasa.

Yaani hakuna kitu kama hicho kama sio naweza kupiga simu hata saa hii kwa meneja wangu niongee naye, hayo ni maneno watu tu wanazungumza yaani hilo jambo ndio kwanza nalisikia sasa hivi”.

Lakini pia Brown amesisitiza kuwa yeye yupo hapa Dar kwa muda na nyumbani Kenya anaweza kurudi lakini sio kwamba amefukuzwa kwa sababu ya kuiba mke wa Meneja wake.

Brown Mauzo Yupo Tayari Kuwa Spea Tairi Kwa Wema Sepetu

Msanii maarufu kutoka Mombasa Kenya Brown Mauzo amefunguka na kudai ana mapenzi mazito kwa Muigizaji wa Bongo movie Supastaa Wema Sepetu.

Kwenye mahojiano yake na kipindi cha Enews cha East Africa Tv, Brown amesema kuwa amekuwa akivutiwa sana na Wema Sepetu na yupo tayari muda wowote kumuoa mrembo huyo hata kama ikibidi awe spea tairi.

Mimi namzimia sana Wema Sepetu kwa bahati mbaya sijawahi kuonana naye namzimiaga sana, kila mtu anasema ukweli kutoka moyoni kila shetani na mbuyu wake. Licha ya kwamba alikuwa na nani sijui na nani ila mimi nipo tayari kumuoa, na popote atakapokuwa namwambia mimi nampenda na nataka kumuoa.. hata kama akiwa na mtu mwingine mimi nipo tayari hata niwe spea tairi”.

Brown amemwagia Wema Misifa kibao huku akidai ni mwanamke ambaye amekaa na ameona anafaa kuwa mke wake wa ndoa.

Brown Hana Hadhi Ya Kutembea na Wema Sepetu- Kelechi

Msanii wa muziki anayefanya kazi zake  Mombasa Kenya, Kelechi amefunguka na kudai msanii mwenzake Brown Mauzo hawezi kuwa na uhusiano wa kimapenzi na Wema Sepetu.

Siku chache zilizopita Brown Mauzo aliibuka na kufunguka juu ya mapenzi yake kwa msanii wa filamu Tanzania Wema Sepetu na kudai anataka kumuoa jumla jumla.

Kwenye mahojiano na Enews ya East Africa Tv, Kelechi amefunguka na kudai Brown hawezi kumuoa Wema Sepetu wala hata kumuhudumia hawezi:

Huyu Brown ni mtoto mdogo sana hawezi kumpata Wema Sepetu alafu isitoshe ni Dogo sana kwa Wema na pia hana hata hadhi ya kuwa  naye kimapenzi”.

Lakini pia Kelechi amedai Brown amekimbia Mombasa na kurudi Tanzania baada ya kutembea na mke wa Meneja wake.