Chid Benz Asakwa Usiku na Mchana

Katibu Mkuu wa Chama Cha Wamiliki wa Sober House Tanzania, Pilli Missanah ametangaza rasmi kumtafuta msanii maarufu Chid Benz kwa lengo la kutaka kumsaidia kutoka katika janga la utumiaji wa dawa za kulevya ili aweze kurudi katika maisha yake ya kawaida kama alivyokuwa awali.

Pilli ametangaza hilo kupitia kipindi cha eNewz inayorushwa na EATV baada ya Chid kurudi kwa mara nyingine tena kujihusisha na utumiaji wa dawa za kulevya mpaka kufikia hatu ya kupoteza muelekeo wa maisha yake huku marafiki, ndugu na baadhi ya jamaa kuonekana kama wamemtenga kwasababu ya mambo yake.

Mimi ndio mtu wa kwanza kumshauri Chid Benz aje Sober house, nimeshamfuatilia sana na hata sasa hivi bado naendelea kumfuatilia ili niweze kumsaidia kwasababu ni kijana bado tuna muhitaji. Kuna uwezekano mkubwa wa Chid kuacha vitu anavyo vitumia na kuwa mtu wa kawaida. Ila tatizo ni moja tu anapaswa akubali tatizo na wala asifiche fiche mambo“, amesema Pilli.

Pamoja na hayo, Pili ameendelea kwa kusema “Chid anahitaji huruma yetu sisi wala tusimnyanyapae, tusimseme vibaya wala kumnyoshea vidole. Kusaidiwa kwake ni kumchukua na kumpeleka kwenye tiba ndio msaada mkubwa anaohitaji kwa sasa. Mimi mpaka sasa hivi nimeshamuwekea ‘deffender’ mtaani yani akionekana tu akamatwe hata kwa nguvu ili wamlete kwangu”.

Chid Benz Akamatwa Tena na Madawa Ya Kulevya

Mkongwe wa Muziki wa Bongo fleva Rashidi Makwito maarufu kwa Jina la usanii kama Chid Benz amejikuta Tena mikononi mwa vyombo vya sheria baada ya kukamatwa na madawa ya kulevya.

Chid Benz ambaye amekuwa akikataa kutumia madawa ya kulevya na kudai ameacha tangu atoke sober house amekamatwa tena madawa kama ilivyokuwa mwaka jana.

Chid Benz amekamtwa na Jeshi la Polisi jijini Dodoma kwa tuhuma za kukutwa na mzigo wa bangi kiasi cha gramu tano.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma, Gilles Muroto amesema hayo leo Jumatatu, Juni 18, 2018 wakati akizungumza na wanahabari jijini humo baada ya kumtia mbaroni msanii huyo.

Hii ni mara ya pili kwa Chidi kukamatwa na madawa ya kulevya huku akidai kuwa alishaacha kutumia madawa hayo na anaendelea na matibabu Sober House.

Hii ni sehemu ya taarifa ya polisi kuhusu kukamatwa kwa watuhumiwa mbaliombali akiwemo Chidi.

Chid Benz Bado Hajajutia Kutumia Madawa Ya Kulevya

Msanii mkongwe wa Bongo fleva anayefanya miondoko ya hip hop, Chid Benz amesema pamoja na kwamba alijiingiza katika matumizi ya madawa ya kulevya lakini hajawahi kujuta.

Chid Benz ambaye amekuwa akitumia madawa ya Kulevya kwa miaka kadhaa sasa amefunguka na kudai kuwa hajawahi kujutia kitu chochote Kwenye maisha yake.

Chid Benz amefunguka hayo Kwenye mahojiano na Wasafi Tv ambapo ameweka wazi kuwa hajawahi kujutia kutumia madawa kwa sababu mashabiki wake wamekuwa nae bega kwa bega Kwenye kila jambo.

No! no!, tusiongelee mambo ya madawa maisha ndio yapo hivyo, hamna kitu ninachojutia. Siwezi kujutia nilikolabo na wasanii, siwezi kujutia yaliyonikuta, siwezi kujutia mabadiliko yangu, siwezi kujutia chochote kilichonipata.

Zaidi naona nikijutia mashabiki wangu wataona Chidi vipi why wewe hujutie wakati sisi tunaendelea kukupenda hadi leo. Ukitangaza show TMK unajaza, Morogoro, Singida unajaza, unajutia nini”.

Chid Benz ameshapelekwa rehab mara kadhaa ili aweze kuachana na matumizi ya madawa hayo lakini imekuwa ngumu kwani amesharudi Kwenye matumizi hayo mara zote.

 

Siumii Wala Sichanganyikiwi na Maneno ya Mitandaoni:-Chid Benz

Msanii mkongwe Tanzania Chid Benz amefunguka na kusema kuwa yeye sio mtu wa kuwa anaumia katika mitandao ya kijamii kwa sababu anajua kabisa kuwa mengi yanayoandika kuhusu yeye hayana ukweli woowte hivyo roho yake huwa aina shida na manno hayo.

Huku baadhi ya wasanii wakisema kuwa maneno ya mitandaoni huwavunja moya na hata kuwafanya walie wanapojiona katika mitandao ya kijamii au katika kurasa za udaku za magezeti .

Akiongea na waaandishi wa habari, SIUMII WALA KUCHANGANYIKIWA NA MANENO KATIKA MITANDAO YA KIJAMII KWA SABABU SIO YA KWELI.”

“Mama Yangu Haniulizi Kama Natumia Madawa Ya Kulevya”- Chid Benz

Msanii wa Bongo fleva Rashid Makwiro maarufu kama chidi Benz amefunguka na kudai hawezi kuongelea suala lake la kitukia madawa ya kulevya kwa sababu hata mama yake mzazi hamuulizi mambo hayo na hawezi kumjibu.

Chidi Benz amekuwa muhanga mkubwa kutokana na kushindwa kujimudu kwa sasa katika muziki kutokana na athari alizozipata za madawa.
Chid kabla ya kujiingiza kwenye matumizi hayo, alifanikiwa kuwa miongoni mwa wasanii wakubwa hapa nchini na kufanya vyema katika gemu la muziki.

Chid aliwahi kukiri kujiingiza katika matumizi ya madawa ya kulevya kupitia kituo kimoja cha redio hapa nchini katika siku za nyuma kwa kuomba msaada kwa ajili ya kujiondoa katika matumizi hayo jambo ambalo lilifanyika baada ya Babu Tale na mwanamuziki Nasibu Abdul ‘Diamond’ kujitolea kumsaidia kwa kumpeleka katika Sober House ya Bagamoyo inayoitwa Life and Hope ambapo alikaa kidogo.

Kwenye mahojiano aliyofanya na Gazeti la Championi Chidi Benz aligoma kabisa kuongelea husu matumizi yake ya madawa ya kulevya na kudai kuwa hata mama yake mzazi hamuulizi :

Sitaki kuongelea kuhusu madawa ya kulevya kwa sasa, hata mama yangu mzazi haniulizi swali hilo kipindi hiki kwa sababu sitaki kusikia.

Hata aje mtangazaji kutoka BBC siwezi kumjibu swali hilo, kila siku unataka mimi niongelee kuhusu madawa ya kulevya, mambo ya madawa ya kulevya ni mabaya.

Naomba mniache mkae kimya kama mnavyokaa kimya kwa wasanii wengine ambao wanatumia madawa lakini hamuwaulizi.

Kama navuta ama sivuti niacheni mwenyewe. Nipo tayari kutoa ushirikiano katika kazi ya muziki, kwa sasa ninaendelea na kazi yangu ya muziki, nawaandalia mashabiki wangu nyimbo ambazo zitakwenda na wakati uliopo.”

Chid Benz Kufanya Ngoma na Jay -Z

Msanii mkonge wa miondoko ya hip-hop nchini, Chid Benz amefunguka na kusema kuwa mara nyingi amekuwa akisema vitu na watu wanashindwa kumuamini huku wengi wakisema kuwa anatumia madawa ya kulevya na ndio maana anakuwa anaongea vitu visivyokuwa na maana.

Akiongea na Clouds Tv, Chid Benz anasema kwa muda ule aliokuwa akiongea alikuwa hajalewa wala hajatumia kitu chochote ila anatoa taarifa kuwa anataka kuanza kufanya kazi na wasanii wakubwa wa nje kama Jay-z, Jada Pink, na hata 50 cent.

Mnaweza kusema eti  nimelewa pale niliposema kuwa nataka kufanya kazi na 2-pac, lakini ukweli ni kwamba hata ukiniangalia machoni ninaongea hapa waa sijalewa ila nina ngoma na jada pink,nina ngoma na 50 Cent, nimefanya ngoma na 2-Pac na nina ngoma na Jay Z pia.

Chid benz ambae bado masabiki wake wengi wamekuwa hawamwamini kutokana na ukweli kuwa wanahisi bado anatumia madawa amekuwa akitumia nguvu nyingi sana kuwa hakikishia kuwa hatumii madawa kwa sasa.

Chid Benz Kauza Mjengo Aliokuwa Anaishi na Kuhamia Kwa Mama Yake

Mwanamuziki wa Bongo fleva Chid Benz ameendelea kukaa kwenye headlines baada ya kupata skendo mpya ambapo inadaiwa kuwa ameuza nyumba yake na kuhamia kwa mama yake.

Kwa kipindi kirefu sasa Chid Benz amekuwa akiandamwa na skendo ya kutumia madawa ya kulevya ameshapelekwa Rehab lakini imeshindikana kuacha kutumia madawa.

East Africa Tv wanaripoti kuwa Chid Benz ameuza mjengo wa ghorofa aliokuwa anamiliki maeneo ya Ilala ambapo ndio ilikuwa makazi yake na hata ofisini kwake ambapo alikuwa na kundi lake la La familia.

Inadaiwa kuwa Chid ameuza mjengo huo na kufikia hatua ya kukosa makazi na hivyo kuamua kurudi kuishi nyumbani kwa mama yake.

Nimeuza nyumba yangu ya ghorofa na wala sio ya kwanza kuiuza, nimeuza nyumba nyingi na sasa ninaishi kwa mama yangu mzazi ambayo ni nyumba nimejenga mimi. Nimeuza ghorofa na nimeuza nyumba nyingi ambazo nilikuwa nazimilik na nitaendelea kuuza”.

Mapema mwaka huu jeshi la polisi mkoani Dodoma lilimshikilia msanii huyu baada ya kukamatwa na madawa ya kulevya aina ya heroin ambapo sio mara ya kwanza Chid kukamatwa na madawa ambayo ameshindwa kuyaacha.

Chid Benz:Mashabiki Wanaosema Nimewachosha Hao Sio Mashabiki Wangu.

Chidi benz kwa sasa yupo uraiani  tangu alipokuwa amekamatwa tena mkoani Dodoma kwa tuhuma za kukutwa na madawa ya kulevya na kukaa rumande kwa siku 40 na kuachiwa huku kesi hiyo ikiwa bado haijaisha  na kusemekana kuwa wanafatilia swala la upelelezi wa kesi hiyo.

Hata hivyo Chid Benz amefunguka na kusema kuwa watu wengi katika mitandao ambao wamekuwa wanasema kuwa wao ni mashabiki wake, na  wamekuwa  wakisema kuwa wamechoshwa kusikia na habari zake za madawa ya kulevya kila siku lakini kwa upande wake anaamini kuwa shabiki wa kweli hawezi kumchoka msanii wake zaidi ya kumpa maneno ya kumfariji tu na kama wapo hivyo hao sio mashabiki wake.

Haijalishi Chid anaua anachinja au anafanya nini lakini unapaswa kupenda muziki wake, sometimes unasikia eti tumechoshwa na  habari zake kila siku laki i ukweli ni kwamba hao ni mashabiki wa wasanii wengine wala sio mashabiki wangu maana mashabiki wangu wasingechoka.

Akiongelea swala la kumalizika kwa kesi yake , Chid anasema kuwa kwa sasa bado kuna uchunguzi uaendelea lakini wanachoshukuru Mungu ni kwamba pamelegea sio kama pale ambapo walipokuwa mwanzoni.

Hata kama uchunguzi utakamilika na tukakutwa hatuna hatia basi tutashukuru mungu tu lakini hatuwezi kuishitaki serikali kwa sababu no one trust you chid, kwaio tunakaa tunasubiri tu tunaamini kuwa yataisha.

Lakini pia akitoa neno lake kuhusu kufungiwa kwa  Nay wa Mitego, Chid Benz anasema kuwa Nay wa Mitego inabidi anabilishe mfumo wake wa kuandika mashairi kwa sababu itafika sehemu watamkariri na kila kosa atakuwa anapewa yeye hata kama nyimbo zake zina mashairi mazuri.

 

Chid Benz Amshauri Ney wa Mitego Kufanya Aina Nyingine ya Muziki

Msanii mkongwe wa muziki ambae amekuwa akikumbwa sana na kashfa za matumizi ya madawa ya kulevya na kuwa anachezea kichapo cha kulala ndani kila iitwapo leo kutokana na kukamatwa kwa tuhuma hizo hizo kila siku ingawa yeye mwenye amekuwa akikanusha kuwa kwa sasa ameshaacha matumizi ya madawa hayo Chid Benz amefunguka na kumtaka msani mwenzie Ney wa Mitego kuachana muziki anaofanya sasa ka kutafuta aina nyingine ya muziki  wa kufanya.

Chid Benz ameamua kumchana Ney wa Mitego na kumwambia kuwa muda wake wa kufanya mzuiki guo ulishahisha na sasa styke ya muziki anayoifanya anatakiwa kuwaachia wakina Billnass wafanye na yeye kukaa pembeni kufanya muziki huo.

kwa sisi wakongwe ni lazima tujue kuwa inafika muda na wakati wetu unapita,na sasa kiki inabidi tuwaachie  madogo kina #billnass  huku kina juma nature, afande sele na  nimshauri tu @naythetrueboy  kufanya aina nyingine ya muziki.

Nay wa Mitego ambae ni msanii wa hip-hop amekuwa ni mmoja wa wasanii walioingia katika list ya wasanii ambao wanatakiwa kubadlisha aina ya muziki na kuacha kuimba nyimbo za matusi kama ambavyo nyimbo zake za awali zilivyokuwa.

Chid Benz Afungukia Skendo Yake na Madawa Ya Kulevya

Mwanamuziki mkongwe wa Bongo fleva Chid Benz amefunguka na kuongelea skendo yake ambayo imekuwa ikimzunguka kwa miaka kadhaa sasa ya kutumia madawa ya kulevya aina ya cocaine na heroine.

Chid Benz ameongelewa sana kwa miaka hii ya karibuni kutokana na matumizi yake ya madawa ya kulevya na imperial Miezi michache tangu akamatwe mkoani Dodoma na jeshi la polisi akiwa amebeba madawa aina ya Heroine.

Kwenye Interview aliyofanya hivi karibuni na kitu kimoja cha habari Chid Benzi aliulizwa kuhusu mipango yake ya kuacha kutumia madawa ya kulevya na kama ilivyo kwa muathirika yoyote wa madawa alitafuta visingizio:

Kuna muda ambao umefika siwezi kusema kuwa naacha madawa ya kulevya! Nataka kusema mimi nyie mniambie Chid leta ngoma sio nikikaa huko mnasema navuta tu sio sawa”.

Lakini pia Chid Benz alimpa maneno msanii mwenzake Ney wa Mitego na kumtaka atafute aina nyingine ya mziki wa kufanya na huu anaofanya sahivi wa kutafuta kiki awaachie madogo kama Billnas.

Dito Awatolea Povu Watu Wanaombeza Chid Benz

Mwanamuziki wa Bongo fleva kutoka THT nyumba ya vipaji, Dito aliyetamba na wimbo wake wa ‘Wapo’ amewatolea povu Kali wale watu wote wanaomsema na kumbeza msanii wa rap ya Bongo fleva Chid Benz.

Wiki chache zilizopita Chid Benz alikamatwa kwa mara nyingine mjini Dodoma ambapo alikuwa amebeba madawa ya kulevya aina ya ‘heroin’. Hii siyo mara ya kwanza kwa chid Benz kuwekwa hatiani amekuwa akitumia madawa hayo kwa muda mrefu sasa.

Msanii Dito amewajia juu wale wote waliokuwa marafiki na washkaji wa Chid Benz ambao kwa sasa wanamsema vibaya na kumbeza msanii huyo kutokana na matatizo yake ya muda mrefu, Dito amedai sio vyema kumsema kwani hawatibu ugonjwa kwa kumsema.

Kwenye Interview aliyofanya na Enews ya East Africa TV Dito amewasihi watu wanaombeza Chid Benz waache tabia hiyo mara moja:

Kwanza haya ni matatizo yaayoweza kumkuta mtu  yoyote ni tatizo ambalo mtu yoyote anaweza akalipata yaani ukiteleza ukanguka inategemea ni utelezi gani kuna wengine wanahitaji msaada Mkubwa sana na ndio maana kuna siku nilisema sisi kama jamii tunakosea kushughulikia hili tatizo kwa sababu kwa upande mwingine tunakuwa tunazodoa, tunashambulia hawa waathirika wa madawa hatuwachukulii kama ni wagonjw lakini tungechukulia hivyo basi tungetafuta njia bora zaidi ya kuwapa tiba na wale watu wanaombeza hawamsaidii bali ndio wanamzidishia maumivu kwaiyo busara lazima itumike katika hili”.

Tangu Chid Benz ajiingize katika matumizi hayo ya madawa ya kulevya jitihada mbali mbali za kumsaidia zimefanywa na watu kadhaa bilamafanikio yoyotr mara ya mwisho Babu Tale alimpeleka Chid Benz sober house Bagamoyo lakini aliondoka baada ya muda mfupi kisha kurudia tena madawa ya kulevya.

Chid Benz Akamatwa Tena Kwa Madawa ya Kulevya

Msanii mkongwe wa kizazi kipya Chid Benz, amekamatwa tena  kwa mara nyingine  mkoani Dodoma akiwa na mke wake kwa tuhuma za kukutwa na madawa ya kulevya aina ya Heroine.

Sio mara ya Kwanza kwa msani Chid Benz kukamatwa na madawa ya kulevya lakini pia msanii huyo kwa zaidi ya miaka mitatu sasa amekuwa akipelekwa katika vituo mbalimbali kwa ajili ya kutibu watu waliathirika na madawa ya kulevya.

Mkuu wa kituo cha polisi mkoani Dodoma amethibitishwa kukamatwa kwa msanii huyo  tangu tarehe 30 Desemba mwaka 2017, lakini mpaka sasa wapo mahabusu.

Chid Benz ambae amekuwa akisaidia na watu mbalimbali katika tasnia ya muziki ili aweze kuinuka na kurudi tena kwenye muziki ili aweze kujikwamua katika tatizo hilo lakini jitihada hizo zimeonekana kukwama kabisa.

Chid Benz: T.I.D Ananiita Mimi Teja Mwambieni Aache Unafki

Mwanamuziki wa Bongo fleva Chid benz na  msanii mwenzie T.I.D wameingia katika bifu zito baada ya kauli aliyoitoa  T.I.D alipoulizwa kuhusu Chid benz kwenye mahojiano  aliyoyafanya.

Chid Benz amekuwa katika skendo ya kutumia madawa ya kulevya kwa muda mrefu ambapo mapema mwaka huu alipelekwa ‘rehab’ na Babu Tale lakini baada ya muda mfupi aliondoka na kusema kwamba ameacha kutumia madawa ya kulevya na kurudi kwenye muziki lakini baada ya muda mfupi ilisemekana amerudia tena kutumia madawa. Kwenye mahojiano aliyoyafanya hivi karibuni T.I.D aliulizwa anashauri ni vipi Chid Benz asaidiwe ili aache kutumia madawa ya kulevya T.I.D alijibu:

“Ukiniuliza mimi kabisa kabisa kutoka katika moyo wangu kabisa apelekwe detention thats the best we can do kwa sababu mkimuacha nje atarudia kufanya yaleyale, mpeleke detention piga pingu akitulia ndo mnamtoa pingu mpaka akili yake ikae sawa ndo mnamwambia akafanye mziki wake, Mimi sina urafiki na Chid mimi sio kaka yake, baba yake wala ndugu yake kwaiyo sijali wala nini”.

Chid Benz ambaye aliumizwa na maneno hayo aliyoyasema T.I.D aliyedai ni rafiki yake alimwaga povu hili:

“Kama T.I.D amesema  mimi sio mtu wake wa karibu kwa hilo mi naweza kumwambia ni mnafki mkubwa sana kwasababu kila mtu anajua ni mtu wangu wa karibu sana yaani mshkaji wangu sana nilishawahi kumuachia mpaka gari yangu atumie ilikuwa starlet ya kawaida mi nikawa natumia BMW alikuwa mtu ambaye hana gari nikamwambia we huna gari tumia hiyo starlet na alishakuja kwangu mara kadhaa akalala kwangu so ni mtu wangu wa karibu so kama kasema hivyo alikuwa kachanganyikiwa  au keshapata vitu vingine kichwani vimemfanya aongee uongo “.

Wasanii hao wote wawili wapo kwenye skendo za kutumia madawa ya kulevya lakini wakiulizwa kila mmoja hukataa na kumnyoshea kidole mwenzie. T.I.D alikamatwa mapema mwaka huu na kufikishwa mahakamani kwa kosa la kutumia na kuuza madawa ya kulevya baadae alikiri na kuhaidi kuacha lakini bado watu wanamshuku kuwa kutokana na tabia zake hajaacha kutumia madawa ya kulevya.

Q-Chillah Aingilia Ugomvi Wa T. I.D na Chid Benz.

Msanii mkongwe wa Bongo Fleva Q-Chillah ameingilia ugomvi unaoendelea kati ya msanii Chid Benz na msanii mwenzyie T.I.D.Wawili hao walijikuta wakiwa katika marubano mazito baada ya msanii T.I.D  kumtuhumu Chid Benz kuwa hafai kusaidiwa,  na tabia yake ya utumiaji wa madawa ya kulevya haiwezi kuisha. Wiki  iliyopita T.I.D alipokuwa anahojiwa katika eNews ya Clouds tv alisema kuwa  ili Chid Benz  aweze kusaidika basi inabidi apelekwe dentention akiwa amefungwa pingu akitulia afunguliwe  akaendelee na muziki wake.

Katika kujibu maneno ya T.I.D , Chid Benz alisema kuwa maneno aliyoyasema T.I.D  ni unafiki kwa sababu yeye anachojua T.I.D ni rafiki yake na kama ameweza kuongea maneno hayo basi T.I.D  ni mnafiki.Kwa mujibu wa Chid Benz yeye ni T.I.D ni marafiki walishafikia hatua ya kushare mpaka magari na T.I.D alikuwa akilala nyumbani kwao .

Akiwa kama rafiki wa karibu wa wasanii wote wawili ,msanii Q-Chillah  ameamua kuongea kuhusu ugomvi huo na kusema “Chid na T.I.D wapo kwenye same situation,wote wanahitaji msaada,tofauti ya Chid na T.I.D ni kwamba Chid anafanya open sana  alafu T.I.D haonekani,kwaiyo wote waache kurushiana maneno wanahitaji msaada”

“Hayo wanayoyafanya ni mambo ya kike,kurudishana maneno ya kwenye khanga” ameongezea Q-Chillah

Katika mahojiano hayo yaliyofanywa na kituo cha Clouds Tv kipindi cha eNews , Q-Chillah amesema kuwa hata alipojitolea kumsaidia kuna baadhi ya watu walisema na yeye anarudi kulekule “Nilijitoa kumsaidia  Chid Benz,lakini baadhi ya watu wakasema na mimi narudi kulekule, nilimsaidia kwa sababu nilihisi kuna siku na yeye atanisaidia mimi. nilijitolea kama kaka,kama rafiki, na ipo siku na yeye atasaidia wengine ”

Kwa muda sasa kumekuwa na kurushiana kwa maneno kati ya wasanii hao   huku T.I.D akionekana kama kuponda Chid Benz, hata hivyo kwa muda sasa Chid amerudi katika game la musiki na kutoa wimbo wake aliomshirikisha Q-Chillah unaojulikana kwa jina la “Muda” ambao pia umekuwa ukifanya vizuri katika vituo mbalimbali  vya Tv na Radio.

Dudu Baya amsifia Chidi Benz

Msanii mkongwe katika  style ya ku-rap nchini Tanzania  tangu miaka ya 90’s mpaka sasa  na msanii ambaye ukitaja  wasanii wakubwa wakongwe  waliosaidia kukuza na kuinua muziki wa Tanzania basi huwezi kumuacha msanii huyu, si mwingine ni Dudu baya,Dudu baya ni msanii wa Bongo Fleva  ambae amepitia mengi  mpaka kufikia hapa alipo katika muziki.

Akiongea katika interview aliyoifanya hivi karibuni kupitia kipindi cha eNews cha EATV Dudu baya ameonekana kumsifia msanii mwenzie ambae pia ni mkongwe katika fani hii ya muziki Chid Benz,pamoja na kwamba katika kumbukumbu inaonyesha kuwa Dudu baya ni moja kati ya wasanii ambao waliongea vibaya kuhusu maisha ya msanii Chid Benz hapo awali na kumponda huku wakisema kuwa hawezi kubadilika tabia yake ya kutumia madawa ya kulevya na wala hatoweza kusikiliza watu wanachomwambia. lakini leo ameamua kubadilika na kumsifia Chid Benz, na anaamini kuwa Chid amebadilika .

“Nampa big up, amerecover ,namsifia sana ,sina doubt na yeye na namkubali sana “,  pia alimpa ushauri Chid “ni kama mdogo wangu, mimi ni kaka yake, sitaki arudi tena kwenye madawa ya kulevya,Mungu amuinue,Mungu amsamehe,na Roho Mtakatifu amsaidie  “aliongeza Dudu baya huku akimuombea pia.

Alipoulizwa kwanini mara ya kwanza alikuwa akimponda na sasa hivi anaonekena kumsifia ,Dudu baya alijibu” baada ya kuona anaelekea ninapopata…na tulishakutana mara mbili namuona yuko fresh.. kwenye mic namkubali, ana pumzi…hakuna Dar Es Salaam bila KingKong’ aliongezea Dudu baya.

Hata hivyo Dudu baya alisema kuwa “Mungu alisema tuombeane, mimi ninamuombea,shetani yule aliyemkamata kipindi kile asimrudie tena”

Chid Benz pia ni msanii mkongwe wa Bongo Fleva ambae alikumbwa na kashfa ya utumiaji wa madawa ya kulevya, ambapo matumizi hayo yalimpelekea kushuka kimuziki na kupotea katika ramani ya sanaa, lakini kwa sasa Chid amerudi tena huku bado akisuasua kidogo, hivyo Dudu Baya kama msanii mkongwe pia aliamua kumuongelea msanii mwenzie na kumpa moyo ili aendelee kufanya vizuri katika kazi zake.

Alikiba amtetea Chid Benz

Alikiba amepinga shinikozo za kufungwa kwa msanii Chid Benz ambaye alikamatwa na dawa ya kulevya ya aina ya heroin.

Akiongea na eNews ya EATV, Kiba alimtetea Chid Benz kwa kusema kuwa anapofungwa mtumiaji wa dawa za kulevya ni kumtesa bali anapaswa kupelekwa katika vituo vya afya ili aweze kupatiwa tiba mbadala.

Chid Benz

“Unapomfunga mtu ambaye ni mtumiaji wa dawa za kulevya ni mateso makubwa kwa kuwa mtu huyo anapaswa apelekwe kitengo maalum ili apatiwe dawa za kuzuia kutamani vitu vya aina hivyo, pia yeye mwenyewe tunapaswa tumshauri ili aweze kushinda nafsi yake. Ujue vitu kama hivyo ni kuishinda tu nafsi katika kuamua na akae navyo mbali. Kama ametoka ‘Rehab’ hivi karibuni halafu inasemekana amejihusisha tena na hivyo vitu ni makosa makubwa kwa sababu tayari umetoka katika kupata tiba halafu unayakaribia tena hiyo haifai kabisa,” alisema Alikiba.