Baada ya kuacha matumizi ya madawa za kulevya, Chidi Benz apanga kuachia muziki

Kunauwezekano wa kuziskiza nyimbo za Chidi Benz tena ikiwa ni kweli ambacho walichosema wao hizi wake wapya walisema katika interview yao.

Kulingana na Bongo 5 ambao walinena na uongozi wake mpya, ni kweli kuwa Chidi Benz ameungana na Q Chief kuachia wimbo mpya ambao uataachiwa hivi karibuni.

Nyimbo hii imeandaliwa katika studio za Kill Record chini ya producer Mbezi.

“Wiki ijayo Chidi Benz anarudi upya kwenye game, ngoma ni kali sana bila shaka mashabiki walikuwa wanamsubiria Chidi yule wazamani,” alisema meneja huyo aitwae Shabaha. Mimi binafsi nje ya umeneja Chidi ni msanii ambaye namkubali sana toka kitambo, nilivyosikiliza hii kazi yake mpya akiwa amemshirikisha Chidi Benz nimeona kabisa hapa kuna kitu kipya. Unajua ngoma nyingi za Chidi ambazo amekuwa akizitoa hivi karibuni sio level zake, lakini alivyonisikilizisha huu wimbo nimeona kuna kitu cha ziada kipo. Kwahiyo mashabiki wakae mkao wa kula kuna jiwe linakuja,”

Shamsa Ford aeleza kwanini hawezi ruhusu mumewe kumuongezea mke mwenza

Muigizaji wa filamu za Bongo Shamsa Ford amefunguka kuhusu kinyongo alichonacho ikikuja kwa swala la mumewe kuoa mke wa pili.

Akiongea kwenye FNL, Shamsa alisema kwamba hataweza kukubali mume wake kuongeza mke wa pili kama hataweza kumpa sababu maalum.

Chidi Mapenzi na Shamsa Ford

Mrembo huyo aliyekua kwenye uhusiano wa kimapenzi na Nay wa Mitego kabla ya kuolewa na Rashidi Said ‘Chidi Mapenzi’ alieleza kuwa anaamini anamtosheleza mume wake kwa kila kitu na kuwa Rashidi hana sababu ya kutaka kuoa mke wa pili.

“Wivu nilionao siwezi kukubali kuongezewa mke wa pili hata mume wangu (Rashid) anajua kwa sababu yeye mwenyewe ana wivu sana na mimi. Ukweli kabisa nahisi ninaweza hata kufa kwa presha nikiongezewa mke wa pili. Inabidi kwanza kabisa kabla ya kuniomba aoe, anatakiwa anipe sababu za msingi kwannii anaamua kufanya hivyo na ikiwa sababu zinamashiko na mimi nikazielewa basi nitamruhusu kwa kuwa dini inasema hivyo kwa sababu pia ni ibada. Lakini kama hazina msingi siwezi kukubali kwa sababu naamini namtosheleza kwa kila mtu na sina kasoro yoyote,” Shamsa alisema.