Baba Diamond Kukatwa Miguu Kutokana na Kansa Ya Ngozi

Baba mzazi wa staa wa Bongo fleva Naseeb Abdul ‘Diamond Platnumz’, Abdul Juma amedaiwa kuwa katika hai mbaya itakayompelekea kukatwa miguu katika siku za usoni.

Baada ya kujionea baba Dia­mond akiwa anasumbuliwa na tatizo la kansa ya ngozi, Gazeti la Ijumaa Wikienda lilimpigia simu dak­tari Godfrey Charle wa jijini Dar alipoelezwa kuhusu tatizo hilo, alisema kuna mambo ya kufanya ili kumnusuru kwani tofauti na hapo basi huenda akalazimika kukatwa miguu.

Kwa baba Diamond sambam­ba na kutibiwa kansa anatakiwa atibiwe pia maambukizi mbalim­bali yanayojitokeza kwani hayo ndiyo yanasababisha mgonjwa kukatwa mguu au kiungo chochote kilichoathirika na siyo kansa.

Kwa kweli kwa hatua ile aliy­ofikia kupona kwake ni asilimia 50 tena kwa msaada wa ndugu yaani kama ndugu zake watam­saidia katika matibabu hivyo inategemea na msaada ataka­opata lakini vinginevyo asipopata msaada wa matibabu tena kwa haraka anaweza kukatwa miguu“.

Kwenye mahojiano aliyofanya na Gazeti la Ijumaa Wikienda, Baba Diamond alisema amepitia changamoto za muda mrefu kwa kusumbuliwa na miguu hiyo bila kupata matibabu hivyo ilifika wakati alikata tamaa ya maisha kabisa.

Kwa kweli miguu hii imen­isumbua kwa muda mrefu sana. Nimehangaika katika hospitali nyingi tu lakini kwa kweli nimeshindwa kujitibia kutokana na gharama kuwa kubwa”.

Baba Diamond alipoulizwa kama ame­shamwambia mwanaye amsai­die, baba Diamond hakutaka kumzungumzia lakini akasema anaamini kama ni tatizo hilo, Diamond atakuwa analifahamu vizuri maana lina muda mrefu.

Siwezi kumzungumzia sana lakini kikubwa mimi kwa sasa namshukuru Mungu kanikutani­sha na dada kutoka Uingereza anaitwa Zubeda Humphries ambaye amekuja na kuahidi kunisaidia ili niweze kutibiwa”.

 

 

Christian Bella Awajia Juu Waliomposti Dimpoz Alipokuwa Mgonjwa Hoi Kitandani

Msanii maarufu wa muziki wa dansi nchini Christian Bella amewajia juu watu waliokuwa mstari wa mbele kumposti Ommy Dimpoz alipokuwa hoi kitandani lakini wakashindwa kumposti alipopona siku yake ya birthday.

Kwenye mahojiano aliyofanya na Gazeti la Ijumaa, Bella amesema alikuwepo wakati Dimpoz anaanza kuugua koo mpaka kufikia hatua ya kufanyiwa Upasuaji lakini amewalipua watu ambao walimposti Dimpoz wakati akiwa hoi kitandani na kumtakia apone haraka lakini alivyopona hawakufanya hivyo wala hawakuposti wimbo wake mpya aliouachia hivi karibuni.

Watu walikuwa na wasiwasi sana huenda chochote kikatokea kwa Dimpoz, walimposti sana wakimuombea apone, hadi wale ambao alikuwa haelewani nao walimposti. Baada ya hapo ikafika Birthday yake lakini hao watu hawakumposti, na hata juzi alivyotoa wimbo wake hawakumposti lakini angefariki wangemposti sana”

Ommy Dimpoz aliugua nusu ya kufa miezi Michache iliyopita mpaka kufikia hatua ya kupostiwa na kila Msanii akiwemo hasimu Wake namba moja Diamond Platnumz.

Kisa Pesa, Christian Bella Ashindwa Kufanya Shoo.

Mwanamuziki mkongwe wa muziki wa dansi Christian Bella amefunguka na kukiri kuwa kwa sasa hali imekuwa mbaya na pesa hakuna na ndio ababu inayomfanya shindwe kufanya shoo mara tatu au nne kama hapo awali na kupunguza idadi ya shoo kwa mwezi na kufanya moja tu.

Bella anasema kuwa kwasasa atakuwa akifanya shoo mara moja kila jumamosi ya mwisho wa mwezi sio kama zamani na shoo hiyo itakuwa ikifanyika mzalendo pub iliyopo Kijitonyama.

mashabiki wangu najua kuwa mnapenda tufanye makamuzi kila siku na mara kwa mara lakini  kutokana na kwamba vyuma vimekaza sasa naomba tuwe tnafanya kila mwisho wa mwezi siku ya jumamosi  katika kiwanja hiki, :-Alisikika Bella alipokuwa akiongea na mashabiki wake alipokuwa katika shoo katika pub hiyo ya mzaleno iliyopo kijitonyama.

Christian Bella Atoa Siri ya Kutoboa Kimuziki Bongo.

Msanii wa muziki wa dansi bongo mwenye asili ya kikongo Christain Bella amefunguka na kutoboa siri na tabia ya wakongo na kwanini yeye ameweza kufanya vizuri kimuziki bongo na sio wakongo wenzake huki nchini kwao.

Christian Bella anasema kuwa ukiwa nchini Kongo ni vigumu sana watu wa kule kukuelewa au kuelewa muziki wako kama unatumia lugha nyingine tofauti na ile ya kilingala.Christain Bella anasema kuwa ili uweze kutengeneza mashabiki wa muziki wako ni lazima uweze kufanya muziki kwa lugha wanayoilewa wao.

Kuna ugumu mkubwa wa lugha kwa sababu kule mara nyingi wanapenda sana kilingala,kuna sehemu wanaongea kiswahili na huko ndipo ngoima za bongo  zinakuwa zinahit pia.ugumu ni kwamba wao  ni wabishi sana mpaka wakupitishe na kukukubali na lugha unayoitumia ni wabishi sana.

Hata hivyo Christian ana sema kuwa kutoboa kwake bongo na nje ya nchi ni kwa sababu watanzania wamemuelewa na kuamua kumfanya kuwa msanii wa ndani na nje ya nchi  na ndio maana hata huko kwao ameweza kutangazika sana.

Kwa ugumu wote wa ngoma za kongo na kutumia kwangu kiswahili niliweza kupata  nafasi  kwa  sababu watanania waliweza kunikubali na kunipa nafasi pia, wengi wao walikuwa wanashindwa kujua kama mimi ni mkongo au ni mtanzania. unaweza kuwa unajua sana na bado wakakukataa lakini ukifanya kitu kizuri nje ya nchi ukirudi nchini kongo wanakupokea.

Christian Bella Akana Skendo Ya Kutumia Madawa Ya Kulevya Ayala Mwenye Ushahidi Apeleke

Mwanamuziki wa muziki wa Dansi nchini Christian Bella amerudi tena Kwenye vichwa vya habari kwa mara nyingine tena huku tuhuma za kutumia madawa ya kulevya zikizidi kumuandama.

Bella aliingia kwenye listi ya wasanii wanaosemekana kujihusisha na matumizi ya madawa ya kulevya na tetesi hizi zilianza mapema mwaka huu baada ya kushindwa kufika kufanya shoo ya mkesha wa mwaka mpya.

Kwenye mahojiano aliyofanya na Ijumaa Wikienda,  Christian Bella amekana tuhuma hizo na kusema yoyote ambaye ana ushaidi kuwa yeye anatumia madawa apeleke huo ushahidi:

Watu waendelee kunihusisha na matumizi ya madawa ya kulevya, hii ni kama mimba, wasubiri hadi nitakapoathirika na unga ndipo watapata majibu kama natumia ama la, kwa sasa siwezi kujibu ndiyo ama hapana.

Nikisema hapana au ndiyo hakuna mtu atakayeweza kuniamini, hakuna mtu anayejua na hakuna anayeweza kukubali hilo, watu wanaoniambia natumia madawa ya kulevya watoe vithibitisho, hawajui maisha ninayoishi.

Hakuna mtu anayejua aina ya maisha yangu ninayoishi, waendelee kuongea ni kawaida tu kama navuta ama sivuti Mungu ndiye anayejua, hivyo waache wazungumze mengi kuhusu mimi. Ninachoangalia ni maisha yangu yanaendaje na wala simfuatilii mtu”.

Christian Bella alipotakiwa kutoa ushauri kuhusu matumizi ya madawa ya kulevya alidai  kuwa hawezi kutoa ushauri kwa watu kama watumie au wasitumie madawa kwa kuwa kila mtu ana maamuzi yake na maisha yake.

 

Christian Bella na Msafiri Diof Ndani Ya Bifu Kali Kisa Mwanamke

Mwanamuziki wa muziki wa Dansi nchini Christian Bella amejikuta akipata skendo ya mwaka baada ya kudaiwa kuwa kwenye bifu kali na msanii mwenzake Msafiri Diof kisa tu wanagombania penzi la mwanamke.

Habari za kimbea zilizoenea kwa muda sasa zimedai Bella na Msafiri Diof aliyejipatia umaarufu kutokana na kuwa msanii kutoka Twanga Pepete, nusura watoane roho kisa mwanamke ambaye wote wawili walikuwa wanamtaka.

Kama kawaida Christian Bella alipoulizwa na Enews ya EATV kuhusiana na tuhuma hizo alipangua vibaya mno tuhuma hizo na kudai hajawahi kugombana na mtu yoyote kisa mwanamke.

Mimi siwezi kugombania mwanamke na mtu, sijawahi kugombana na mtu Tanzania hakuna mtu anayeweza sema ana ugomvi na Christian Bella hata siku moja”.

Pamoja na kukataa kuwa hana ugomvi wowote na Diof, Bella alikataa hata kutaja jina la Msafiri Diof na kusema hivyo ni vitu vya kijinga ambavyo hawezi hata kuongelea na pia alisema hawezi kumuongelea na kumpa kiki badala yake anataka kuongelea mziki wake na mambo yake binafsi.

“Sasa Nataka Kuurudisha Mziki Wa Dansi Kwenye Chati”- Christian Bella

Mwanamuziki mashughuli wa Dansi nchini Christian Bella ‘Obama’ ameweka wazi dhamira yake ya kutaka kuurudisha muziki wa Dansi juu kwenye chati ulipokuwepo miaka ya nyuma.

Baada ya muda mrefu kuweka kwa malalamiko kutoka kwa mashabiki wakidai muziki wa Dansi umepotea, sasa Christian Bella ana mpango wa kuurudisha mziki huu juu kwa kuacha kufanya mziki wenye ladha ya Bongo fleva na kujikita kwenye Rhumba.

Siku za nyuma Bella aliwahi kulalamikia muziki wa Bongo fleva na kudai ndio uliopelekea kuua kabisa soko la muziki wa Dansi nchini kwani Bongo fleva imeonekana kuzoa mshabiki wengi zaidi na kupelekea kuua soko la mziki wa Dansi.

 

Christian Bella alifunguka hayo Kwenye mahojiano aliyofanya na Enews ya East Africa Tv:

Mimi kijana wenu kijana wa kazi nataka kurudisha muziki wa bendi mashabiki walilalamika kuwa namix sana na Bongo fleva lakini sahivi nataka kuwarudishia muziki wa bendi, nimetoa wimbo mpya unaitwa ‘Rudi’ ili kurudisha mziki wa Rhumba”.

Christian Bella amehaidi kurudisha muziki wa Dansi kwenye zile Enzi ambazo walikuwa wanajaza shoo na mapedeshee kuwatunza stejini na kuwamwagia mahakama usiku Kocha.

Christian Bella Awatolea Povu Zito Wasanii Wenzake

Mwanamuziki mahari wa mziki wa dansi nchini Christian Bella amewatolea povu zito wasanii wenzake wa muziki wa dansi ambao wamekazana kumsema na kudai hana uwezo mkubwa wa kuimba bali anabebwa sana na vyombo vya habari.

Kwenye kila mapambano huwezi ukakosa watu ambao wataenda tofauti na wewe kwenye mapambano ya Christian Bella kuna baadhi ya wasanii wenzake wa Muziki wa dansi ambao wanampiga mawe na kusema uwezo wa Bella ni mdogo lakini amekuwa akibebwa sana na media kwa nyimbo zake kupewa upendeleo na kuchezwa zaidi.

Kwenye mahojiano aliyofanya na Enews ya East Africa Tv, Bella ameshindwa kuwavumiloa watu hao na ameishia kuwatolea povu zito kuonyesha kuwa amechoshwa na majungu ya wasanii wenzake ambapo amezidi kufunguka yafuatayo:

Wadau wa muziki wa bendi wanasema labda anabebwa labda nyimbo mbaya au labda ya kawaida sasa unataka nyimbo itoke mbinguni? hakuna kitu special ambacho hakijawahi kifanyika kila kitu kilichafanyika mziki ulishafanyika wahenga walishaimba lakini melody ndio tofauti. Yaani akisema Christian Bella anabebwa ni muongo sana Tena ana wivu wake binafsi alafu mimi sina mzunguko kwenye media mimi nikitoa wimbo nazunguka kwenye vyombo vya habari hakuna kitu kama hicho”.

Christian Bella amesisitiza kuwa sababu pekee nyimbo zake zinapigwa ni kwa sababu ya mziki mzuri anaofanya lakini hatumii nguvu nyingi kama wasanii wengine na hivyo wasanii wa dansi wanaomsema anapendelewa ni wana wivu naye.

Christian Bella Amekana Kwa Nguvu Skendo Ya Kutumia Madawa Ya Kulevya

Msanii mkongwe wa Dansi nchini Christian Bella ‘Obama’ amekataa na kutupilia mbali skendo iliyomkumba hivi karibuni ya kwamba ni mtumiaji wa madawa ya kulevya.

Kuanzia mapema wiki hii kuna habari nyingi zilisambaa kwenye mitandao ya kijamii kutoka kwa wasamaria wema waliodai ni watu wanamfahamu Christian Bella walisema kuwa wana taarifa za kumshuhudia msanii huyo anatumia unga/ madawa ya kulevya.

Taarifa hizo zilienea Kama njugu mawe lakini haraka haraka Christiana Bella alizitupilia mbali tuhuma hizo na kudai kuwa hazina mashiko yoyote na habari hizo zimrsambazwa na watu wasiomtakia mema na hakuna lingine lolote lakini pamoja na hayo amedai hawezi kumlaumu mtu aliyesambaza habari hizo.

Kwenye Interview aliyofanya na kituo kimoja cha habari Christian Bella amesena hawezi kujiingiza kwenye anasa ya kutumia madawa ya kulevya kwani anajua mwisho wake na yeye anajielewa majukumu yake:

Mimi ni baba nina familia kubwa sana na majukumu Mengi siwezi nikajiingiza huko kwenye starehe za vijana japo mimi pia ni kijana, najua ni watu wenye chuki na mimi ndio wanasambaza uzushi huo lakini siwezi kumlaumu wala kuumia kwani najua nilipotoka nilikatishwa Sana tamaa mpaka leo nimefika hapa na ninajua nuna maadui Mengi hivyo sijashtushwa na habari hiyo”.

Bella amewahakikishia mashabiki zake kuwa kamwe hawezi kujiingiza kwenye matumizi ya madawa ya kulevya na sababu alikosa kufanya show mbili ni alikuwa anaumwa na walasio uteja kama ilivyozushwa.

 

 

 

Muziki Wa Dansi Haujafanya Vizuri Mwaka 2017 Kwasababu Umefunikwa na Bongo Fleva- Christian Bella

Mkali wa muziki wa Dansi nchini Christian Bella Obama ameibuja na kudai kuwa muziki wa  dansi haukufanya vuzuri kabisa kwa mwaka huu wa 2017 kwa saabu mziki wa Bongo fleva umeuzima kabisa.

Christian Bella sio msanii wa kwanza kulalamika kuwa mziki wa aina nyingine zaidi ya Bongo fleva haukufanya vizuri ni siku chache tu zilizopita mkali wa mziki wa Taarabu nchini Khadija Kopa alidai kuwa mziki wa Taarab haukufanya vizuri kwa mwaka huu kwa sababu ya sheria ya Makonda ya mziki mwisho saa sita.

Lakini pia msanii wa Hip hop Kala Jeremiah amekiri kuwa mwaka 2017 haukuwa mwaka mzuri kwa mziki wa hip hop kwani haukuvuma kabisa, pia Msaga Sugu mkali wa Singeli alikiri pia mziki huo ulidoda kwa mwaka huu wa 2017.

Christian Bella aliongelea mziki wa Dansi ambao hufanya vizuri kila msimu lakini amedai kwa mwaka huu umedoda kwa sababu ya nafasi kubwa ya mashabiki wameegemea zaidi kwenye mziki wa Bongo fleva.

Kwenye mahojiano aliofanya na East Africa TV Bella amekiri pia sababu nyingine iliyozima mziki wa dansi kwa mwaka huu ni wasanii wa dansi kutopendana.

Dansi haijafanya vizuri na sio kwamba wasanii hawapo ila nahisi ni upepo tu haujakaa vizuri tujitahidi tu kujituma lakini mara nyingi kwenye kundi la watu kumi ishirini kuna kuchukiana na ninasema hivyo kwa sababu nimetokea kwenye kundi chuki za kuchekeana machoni Lakini moyoni tumejaza chuki”.

Kuna watu wengi waliongelea suala la ushindani na bifu la Diamond na Alikiba kuwa limetawala sekta ya muziki na sio tu limezima a in a nyingine ya miziki kusikiliza bali hata hump hump kwenye Bongo flea kuna wasanii hawasikiki kwasababu ya ushindani wa Diamond na Alikiba.

 

Christian Bella: Mimi na Alikiba ni Wahenga Ila Diamond ni Digitali

Msanii wa bongo fleva anayefanya mziki wa dansi nchini, Christian Bella amefunguka na kudai kuwa yeye na msanii mwenzake Alikiba ni wahenga lakini Diamond ni msanii wadigitali.

Hivi karibuni kwenye mahojiano na kituo cha televisheni cha East Africa Christian alidai kuwa yeye na Alikiba ni wasanii wazuri lakini hawawezi kupambanishwa katika kitengo kimoja kwani wanafanya mziki Mkubwa.

Christian Bella amepiga stori na Bongo 5 na amefunguka na  kuzungumzia ukongwe wake kwenye muziki bila kutetereka na kumsifia msanii mwenzake Alikiba na kudai kuwa Diamond  ni msanii wa digitali sio msanii wa zamani kama yeye na Alikiba.

Kwenye mahojiano hayo alifunguka yafuatayo:

Unajua wasanii kama Diamond, Belle 9 na wengineo walioingia kwenye gemu kuanzia mwaka 2010 ni wasanii wa digitali, lakini  mimi nampa sana saluti msanii mwenzangu Alikiba ambaye naweza sema ni mhenga kama mimi au msanii wa analogi mwenzangu maanaalianza kuhit kitambo sana yaani amevuka kutoka kwenye analogies mpaka sasa bado yupo anapambana na vijana wa kwenye digitali alafu mimi nakuja Tanzania  2005 namkuta Alikiba tayari ana-hit yaani supastaa ana ngoma nyingi zinapendwa kwaiyo ni artist mkongwe kwenye gemu kama mimi “.

Lakini Christian Bella amekiri kuwa Diamond ni moja kati ya wasanii waliokuza mziki wa bongo fleva tangu aingie kwenye gemu miaka ya 2010 kwani katika kipindi hicho mziki wa dansi ulikuwa umeitoa Bongo fleva kwenye ramani na hivyo Diamond aliurudisha mziki wa Bongo fleva kwenye chati na kuua mziki wa dansi.

Christian Bella Ampa Shavu Diamond, Amtaja Micheal Jackson

Mwanamuziki anaefanya vizuri sasa hivi na kibao chake cha Pambe amefunguka na kumsifia msanii mwenzake diamond platinumz kwa hatua kubwa anazokuwa anapiga katika muziki gasa katika kuukuza muziki huo.bella anasema kuwa diamond amekuwa akifanya vitu vizuri na vkubwa ambavyo mara ya kwanza vilikuwa vikiwa vya kushangaza watu lakini kadri siku zinavyozidi kwenda vinaanza kuonekana ni vya kawaida tu,

Diamond namu-apprecite sana amekuwa akifanya vitu vikubwa na vizuri sana, anafanya vitu ambavyo sio vya kuhadithiwa pembeni ila kila mtu amekuwa akiona, kwa mimi leo hata mtu akinimbia Diamond ameimba wimbo na Michael Jackson sitashangaa aisee kwa sababu kashafanya kolabo nyingi na wasanii wa Afrika na sasa kaamua kuhamia Marekani. Aliongea Christian Bella.

Kwaio imeshaanza kuwa ni kawaida  kwa sababu keshathubutu kufanya vitu ambavyo mwanzoni watu tulikuwa tunashangaa  lakini leo tunaona kuwa ni kawaida tu  na kwa mtu kama yeye ambae ameshafika huko kushushwa ni kazi sana.

Bela ameamua kusema maneno hayo baada ya kuona jinsi msanii huyo ambavyo amekuwa akijitahidi kupenyeza kimataifa na wasanii wakubwa Duniani katika kufanya muziki wa Tanzania kujulikana nje ya nchi.Hivi karibuni Diamond amefanya nyimbo za kolabo na wasanii wakubwa kama Morgan Heritage na Rick Ross.

Ukiachana na kufanya kolabo nyingi nje lakini pia Diamond amekuwa ni msanii aliyejitoa sana ili kuwasaidia wasanii wengine kuweza kuendelea kimuziki kwa kuwatoa katika lebo ya ke ya WCB.

 

Christian Bella: Mimi ni Namba Moja Nisifananishwe na Alikiba

Mwanamuziki na mkali wa mziki wa dansi nchini, Christian Bella ameibuka na kudai kuwa yeye ni mwanamuziki namba moja na asifananishwe wala kupambanishwa na mkali mwenzie Ali Kiba.

Baada ya kipindi cha ‘cheche’ kuingia mtaani na kuhoji watu ili kuuliza watu nani mkali wa ‘vocal’ kati ya Ali Kiba na Christian Bella na majibu kurudi huku watu wengi wakimpigia kura Ali Kiba kuwa ni mkali kuliko Christian Bella na kuibuka mshindi kitendo ambacho Bella alionesha kutokuridhika na kusema Kiba ni mkubwa katika mziki wake wa Bongo fleva lakini na yeye mkubwa kwenye mziki wake wa dansi.

Kwenye mahojiano aliyofanya na kituo cha televisheni cha East Africa, Christian Bella alifunguka haya kuhusiana na ushindindani huo dhidi ya Kiba.

Unajua huo ni mtazamo wa shabiki waliyemhoji huyo walimhoji anamkubali msanii wake kila msanii ana mashabiki wake na mimi najua watu mliowahoji wanaweza wakawa mashabiki wanaompenda Alikiba na mimi sijawahi kusema kuwa Alikiba sio msanii mzuri kwaiyo mtu akisema kuwa ni msanii mzuri siyo vibaya kwanza sijawahi kujali sijui umsifie mtu zaidi yangu eti nione vibaya?Noo ila kama mlipiga kura mkaona Kiba ni zaidi sio vibaya siwezi kukataa maoni ya wale ila ukweli wangu hata ukimhoji Kiba hawezi kusema kuwa ananishinda mimi hats siku moja never! Alafu Ali hawezi kunizidi mimi na mimi siwezi kumzidi yeye hata siku moja”.

Pia Bella amekiri kuwa ni vigumu kumshindanisha yeye na Alikiba kwa sababu wanafanya aina mbili za mziki zilizo tofauti kabisa na hivyo hawawezi kupambanishwa kwani Kiba anafanya Bongo fleva na yeye anafanya mziki wa Dansi na kila mmoja ni mkali katika kitengo chake.

Christian Bella Amefungukia Ishu Ya Hamisa na Diamond

Mwanamuziki maarufu wa dansi, Christian Bella ameongelea habari ambayo bado inashika vichwa vya habari, uhusiano kati ya Hamisa Mobetto na mzazi mwenziye Diamond Platnumz.

Christian Bella aliyetumbuiza kwenye sherehe ya mtoto wa Hamisa, Kwenye mahojiano na Bongo 5 Bella ameongelea mawazo yake juu ya kinachoendelea kati ya Diamond na Hamisa:

Hamisa kwangu mimi ni mwanadada anayejituma ni model si unaona mpaka anapata tunzo za nje ya nchi, mi namuona ni mtu mzuri tu ambaye hana tatizo na piano suala la Hamisa na diamond kupelekana mahakamani mi sidhani kama Diamond anaweza kushindwa au anaweza kukataa kumlea mtoto wake ilimradi ameshakubali kuwa mtoto ni wa kwake”.

Pia Christian Bella hakuishia hapo aliendelea kuweka maneno:

Mi naona umefika wakati wawili hawa wakae chini wayaongee tu kistaarabu kwani Naseeb hawezi akashindwa au akamletea roho mbaya kwa sababu yule ni mtoto wake alafu isitoshe Naseeb mwenyewe kapitia maisha magumu kakulia Tandale kwaiyo anaelewa ugumu na Kama kweli hajatoa mi naaminmawa na misunderstanding hivyo wakae wayaongee mi naamini hapatatokea makelele yoyote”.

Kuhusu suala la kupelekana mahakamani Hamisa alielezea kuwa Diamond ndio aliyetaka iwe vile, yaani atafute mwanasheria na afungue kesi mahakamani ili wapate mwongozo wa kisheria wa jinsi Diamond ataweza kumtunza mtoto bila tatizo lolote.