Siku Zote Mtu Utafuta Kile Kisichoonekana:-Shusho Aongea na Wasichana.

Mwanamuziki wa nyimbo za injili nchini, Christina Shusho amefunguka na kuwahasa wanawake hasa wasichana wa kileo ambao wamekuwa wakizoe kuweka miili yao wazi na kupiga picha zinazoonyesha maungo yao kuwa yako wazi kuwa hakuna mtu anaetamani  vitu hivyo.

Mwanamuziki huyo amesema kuwa wanatakiwa kujua kuwa kila siku kinachoafutwa ni kile kisichoonekana kwaio kama unaweka mwili wako wazi ni vigumu watu kuvutiwa nawe kwa sababu wanajua kila kitu kuhusu wewe.

Siri kubwa ninayotaka kuwaambia wadada ni kuwa siku zote unapoficha mwili wako ndio unazidi kuvutia,  na kufanya watu wakutamani.Maana siku zote mtu huwa anatafuta kile kischooneka na wala sio vilivyo wazi na unapovaa nguo za ajabu unaondoa thamani yako.Maana hakuna mwanaume anyeweza kuja tu na kuokota kimgomba ambacho kiko hapo tu , na hata kama atakuja atakuwa anakudanganya tu lakini in reality anaondoka na kutafuta yule anaejihifadhi.

 

 

Christina Shusho Akana Tuhuma Alizotupiwa na Kiben-10 Chake

Msanii wa nyimbo za Injili Christina Shusho amekana tuhuma zinazomkabili dhidi ya kijana mdogo (kiben-10) aliyedai kuwa Christina alimtaka kimapenzi kwa nguvu.

Siku chache zilizopita kijana mwenye asili ya Kenya aitwaye Nelson Tiger ambaye pia alikuwa ni director katika albamu yake ya ‘Ning’are’ alidai kuwa Christina Shusho alitumia nguvu za giza kumgombanisha na mpenzi wake ili atembee naye yeye.

Nelson Tiger alidai kuwa alikutana na Christina Shusho nchini Nairobi alipoenda kufanya video kadhaa za nyimbo zake na Nelson ndiye aliyekuwa ana direct video zake lakini alipogundua kuwa Nelson ana mpenzi alikasirika sana hasa alipokuja naye Tanzania.

Nelson alidai kuwa Christina alianza kutumia uchawi na nguvu za giza ili kuvunja uhusuano wake na girlfriend wake ili awe sugar mamii wake kwani alishasikia kuwa Christina Shusho anapendelea wanaume wenye umri mdogo kuliko yeye.

Lakini Christina mara moja amekana tuhuma hizo nzito ambazo yeye kama muimbaji wa nyimbo za dini skendo hizo zinakuwa zinamchafua sana hivyo kupitia ukurasa wake wa Instagram Christina aliandika ujumbe huu:

In life you will realize there is purpose for everyone you meet some are there to test you, some are there to teach you, some will use you, and some will bring the best out of you, Good morning”.

 

Shusho Aongelea Ishu Yake Na Mashabiki Wake Wa Kenya

Yeye ni mmoja wa wanamama wanaopendwa sana na mashabiki zake hasa kwa sababu ya nyimbo zake za injili zinazosaidia kutia moyo na kutoa faraja, Christina Shusho ambae alijizolea mashabiki wengi zaidi  nchini Kenya kuliko hata nchini Tanzania amefunguka na kuongelea ishu ya yeye kutukanwa na mashabiki wake wa nchini Kenya baada ya  kupost picha ya moja wa wagombea wa uraisi nchini Kenya huku akiporomosha maombi kwa mgombea huyo.

Christina Shusho alipost picha ya Uhuru Kenyata na kutoa maombi kwake kwa kipindi hiki cha uchaguzi , lakini kitu cha kustaabisha ni kwamba mashabiki wake kutoka Kenya walimvaa kwa matusi katika ukurasa wake wa instagram na kumwambia kuwa anachofanya ni kuwagawa mashabiki wake.

Akiongea na East Africa Television , msanii Shusho anaelezea alivyoyapokea matusi hayo na alichukuliaje swala hilo na ni kitu gani aliamua kufanya ili  kuwapoza mashabiki wake”unajua ile ni mihemuko tu inayokuwa iko miongoni mwa watu hasa katika kipindi kama hiki ambacho wakenya wanakipitia kwa sasa,mimi nilikuwa nafanya tu maombi nikasema sio shida nimuombee na raisi wa Kenya , basi wakanijia juu na kuanza kunitukana, wakawatafuta mpaka marafiki zangu wa kule wakaanza pia kuwatukana,ni kitendo ambacho kilinishtua sana nikaona basi isiwe tabu  acha tu nimpost na huyo mwingine ili  niweke usawa lakini naomba ndugu zangu wa kenya wajue kuwa sikuwa na nia yoyote ya kuwagawa au kuwa na upendeleo” alifunguka Christina Shusho

Christna Shusho ni mmoja wa wasanii   wa kike wa injili wenye ushawishi mkubwa sana katika mitandao ya kijamii na ni kwa sababu amekuwa na mashabiki wengi sana, inawezekana ni kweli kuwa  kitendo chake cha kupost mgombea wa upande mmoja kingefanya kupoteza baadhi ya mshabiki  zake kwa sababu   mashabiki wanaompenda ni watu wenye itikadi tofauti  tofauti hivyo kufanya hivyo ni kuweka upendeleo kwa wale wanaomwamini mgombea huyo huko akionyesha kama kuwatenga wale wa upande mwingine, lakini pia alifanya vizuri alipoamua kuweka usawa katika hilo.

Nchi ya Kenya wanategemea kurudia  kufanya uchaguzi wa uraisi tarehe 26 Oktoba.