Mfahamu Mtoto wa Chuchu Hans Mwenye Kipaji Zaidi ya Mama Yake

Mtoto wa msanii chuhcu hans anaejulikana kama farihiya, anaonekana kuwa na kipaji kikubwa zaidi kuliko hata mama yake mzazi kutokana na picha anazoigiza huku akionekana kuwa mwenye hisia za kweli kila anapoigiza.

Baadhi ya directors waliowahi kufanya kazi na mtoto huyo wanamsifia sana  na kusema kuwa kama kipaji chake kinaweza kuendelezwa basi binti huyo anaweza kufanya kazi kubwa na nzuri sana.

Hata hivyo, mama wa mtoto huyo ambae ni Chuchu hans anasema kuwa anatamani kukikuza kipaji icho lakini anaomba sana kwa sasa mtoto wake huyo ajikite katika masomo na wala sio kitu kingine mpaka pale elimu yake itakapotosha.

 

Chuchu Hans Awatolea Mapovu Mashabiki

Mwanadada Chuchu Hans kutoka kiwanda cha bongo movies amefunguka na kuwatolea povu mashabiki kwa kuwaambia kuwa waekuwa wakikosoa movies kila siku bila kujua undani wa  vitu hivyo.

wikiendi hii kuna picha ilipostiwa katika page nyingi za udaku zikimuonyesha  mwanadada huyo akiwa katika moja ya sehemu ya filamu zake akifanya kazi huku akiwa katika jeneza lakini akiwa hajafumba macho , picha iliyowafanya mashabiki weng kuongea na kuponda sana thamani ya bongo movies.

Sio kila kitu mnakuwa tu mankosoa hapa hii picha tulikuwa hata hatujaanza kushoot, nadhani muangalie na muvi na ndio mkosoe.

katika movie hiyo ambayo ipo jikoni, inaitwa Laura na pia yupo mwanadada anaefanya vizuri Esha Buheti, lakini hakuna kitu walichokiona  ambacho wao wanakiponda sio kweli, na movie hii ni ya kitambo kidogo na hata picha zake ziliwahi kuonyeshwa katika swahili world kwa ajili ya kuitangaza movie na haina vitu mabavyo mashabiki wamevipond.

Chuchu Hans Awajibu Wanaomsema Vibaya Kukaa na Ray Mwezi Huu wa Ramadhan

Mwanadada kutoka bongo movies Chuchu Hans amefunguka na kuwataka wanaomsema vibaya katika kipindi hiki cha Ramadhan kumuacha kufatilia mambo yake kwa sababu maswala ya ndani ya ndoa wao hawawahusu.

Akijibu tuhuma wanazomzushia watu kuwa mwana dada huyo ambae yuko Afrika ya Kusini kwa ajili ya kushuti muvi kuhusu swala ya yeye kukaa chumba kimoja na mzazi mwenzie mwezi huu wa Ramadhani wakati katika dini hairuhusu kwa sababu hawajafunga ndoa , Chuchu anasema anaomba wamuache na mambo yake.

mimi ninachojua kuwa wa kumhukumu mtu ni mungu pekee, maana yeye ndio anajua kila kitu  na ukweli wote  kuhusu binadamu nawala sio mtu wa kawaida,ba hata nilivyo huku watu wanasema sana lakini mii sijali.

 

Chuchu Hans Amkingia Kifua Wema Sepetu Kuhusu Mtoto

Msanii wa bongo movies Chuchu Hans na msanii mwenzie Ray Kigosi waliamua kuonyesha sura ya mtoto wao wa kiume ambae jana alitimiza mwaka mmoja na  ndio ilikuwa ni kwa mara ya kwanza mtoto huyo kuonekana katika mitandao ya kijamii tangu azaliwe.

Hata hivyo baada ya kuonyesha sura ya mtoto huyo wasani wengine walivutiwa na muonekanao wa mtoto huyo hivyo wengi walimpost mtoto huyo katika page zao za instagram na ndicho alichokifanya Wema Sepetu lakini hali ilikuwa tofauti katika page hiyo ya mwanadada huyo kutokana na  mashabiki wengi kuanza kumshambulia mwanadada Wema Sepetu  kuhusu tatizo lake la kutopata mtoto huku wengi wakimtuhumu na kumtukana kuwa chanzo cha  kukosa mtoto  ni yeye mwenyewe.

Chuchu Hans aliumiza na maneno yaliyokuwa yakimlenga Wema Sepetu hivyo alifunguka na kuwaomba mashabiki kumuacha Wema aishi kwa amani kwa sababu maumivu ya kutafuta mtoto na kukosa ni makubwa sana  hivyo wanavyokuwa wakiendelea kumtukana  na kumuandana wanakuwa wanamuumiza sana.

ninasikitika sana kuona watu wanaongea maneno kibao kwa wema tena inawezekana wengine hawajazaa bado na wengine wameshazaa,…naomba nitoe historia yangu kidogo.mimi jaden sio mtoto wangu wa kwanza lakini kabla sijampata jaden nilikuwa napata maumivu sana kwa sababu zilishaharibika mimba kama tatu na nilikuwa nasikia maumivu sana na ukumbuke kuwa hakuwa mtoto wangu wa kwanza….

Hata hivyo ChuchH hans amewataka watu wanaomshambulia Wema wakae na kufikia kama wao ndio wamngekuwa Wema ingekuwaje, anasema kuwa kabla hajazaa na Ray wengine walisema kuwa Ray hana kizazi na hawezi kuzalisha lakini leo wanamtoto tayari.

muwe mnavaa viatu vya mtu na wala mapungufu yake isiwe fimbo ya kumchapia.watu waliongea sana kuwa baba jaden hazai, na miungu watu waliongea sana lakini kwa Mungu kila kitu ni kidogo.

Kwa muda mrefu sana wema amekuwa akitafuta mtoto na hata kupata mimba  na zingine kutoka , lakini watu wamekuwa wakimsema vibaya  na kum-judge tofati bila kujua maumivu anayoyapata msanii huyo.

 

Chuchu Hans Awatahadharisha Wanaopiga Picha Za Utupu

Kumekuwa na tabia ya baadhi ya wasichana maarufu katika tasnia ya bongo fleva na bongo movies kupiga picha za utupu na kurusha katika mitandao ya kijamii,moja ya wasanii wa bongo movies aliyeanza muvi kwa muda mrefu na anasema kuwa picha za utupu hazikuwahi kumsaidia katika kutengeneza jina lake amefunguka na kuwaasa wale wadada waliopo katikia tasnia hii kuacha kupiga picha za uchi kwa sababu itafika sehemu watajuta kuwa wanapiga picha hizo.

Mwanadada Chuchu  Hans ambae amezaa na msanii mwenzie Ray Kigosi amesema kuwa wadada wengi wamezoea kupiga picha za uchi lakini kuna kipindi watakapotaka kutulia na kufanya maisha hata watu wa kuwaoa watakosa kwa sababu ya matendo yao ya nyuma yatakuwa yanawahabisha kabisa.

Ninawatahadharisha tu wasanii wenzangu hasa wa kike  waachane na hayo mambo jaman, wengine hata nguo hawavaa eti kisa wanataka kuwa na umaarufu.mwanamke ukiwa hivyo baadae sasa  ukija kushtuka unakuta kuwa umeshajiaribia kila kona , hata mwanaume wa kutulia nae unakosa kutokana na matendo yako ya nyuma.mimi nilipata umaarufu kutoka katika filamu ya roho sita wala sikufanya jitihada hizo za kupiga picha za utupu kufanikisha ndoto zako. -Alifunguka Chuchu Hans

Wasichana wengi katika tasnia ya sanaa wanaamini kuwa kuvaa nguo za nusu uchi na kupiga picha zinazoonyesha maungo yao ni njia bora ya kujipatia umaarufu kwa sababu ya kuwa wanaongelewa katika mitandao lakini ukwli ni kwamba wanakuwa wanaharibu sifa za mwanamke bora na pia kwa maadili yetu sio kitu cha kukikazia kukifanya.