Kuna Muda Natamani ku-post Picha ya Mpeniz Wangu Nashindwa :-Dayna

Mwanadada Dayna Nyange amefunguka na kusema kuwa kwa kipindi hiki cha valentine ni muda wa kukumbushana kuwa wawili waliopo katika mapenzi ni kweli mmekuwa mkipenda na wala sio kitu kingine.

Hata hivyo dayna anasema kuwa kuna muda anakuwa akitamani sana kuweka picha ya mwanaume aliyenae katika mahusiano lakini anshindwa kwa sababu  ya mitandao hivyo anabaki akisita tu.

Wakati muda mwingine amekuwa akitamani asiweke post ya picha ya mtoto wake lakini anajikuta tayari amekwsha weka na hayo yote ni kwa sababu ya mapenzi tu na wala sio kingine.

Hata hivyo mwanadada huyo ni moya wa wasanii wa kike wasiri sana hasa iapokuja kwa swala la mahusiano na ni nani amekuwa nae katika mahusiano kiasi kwamba hata mtoto wake hakuna anejua baba wa mtoto huyo.

Dayna Nyange Awachana Wasanii Wa Kike

Msanii wa muziki wa Bongo fleva nchini Dayna Nyange amewajia juu wasanii wa kike wanaoingia kwenye tasnia ya Bongo fleva bila ya kuwa na kipaji chochote.

Dayna amewataka wasanii  hao watambue kuwa kama kazi zao hazitakuwa nzuri lazima zitafeli, licha ya pesa nyingi walizotumia kuwekeza katika harakati za kuingia kwenye Sanaa hiyo.

Kama kitu kizuri kitabaki, na kama kitu kibaya kitapotea, wengi wanaotumia pesa huwa wanatumia wakiamini watawapiku watu fulani kuwa watu fulani, lakini kazi kama sio nzuri haijiuzi unakuja kujikuta unaongeza tu mtaji, wengine wakiwa na nia na wakajifunza watabaki”.

Lakini pia Pia Dayna amewataka wasanii hao kuchukua muda kujifunza au kuomba msaada kwa wanaojua, ili kuweza kujitengeneza zaidi na wasipoteze pesa zao ambazo hazitarudi kutokana na kazi hizo.

Hivi karibuni mwanamitindo, Hamisa Mobetto kwa mara ya kwanza ameachia nyimbo zake mbili zinazojulikana kama ‘Madam Hero’ na ‘Tunaendana’ akifuatiwa na mwanadada mwingine maarufu katika mitandao ya kijamii, Irene Louis maarufu ‘officiallyyn’ ambaye ameachia nyimbo inayojulikana kwa jina la ‘Chafu’.

Dayna Nyange Ajutia Safari Yake Ya Ulaya

Msanii wa muziki wa Bongo fleva ambaye pia nddiye hit maker wa ‘Mafungu Ya Nyaya’ Dayna Nyange ameweka wazi kuwa kati ya vitu ambavyo anajutia ni kusafiri kwenda Ulaya.

Dayna ambaye alikuwa kimya kwa muda mrefu amebainisha kuwa kutokana na kuishi nje ya nchi kwa muda mrefu ilibidi asimamishe shughuli zake za kimuziki.

Kwenye mahojiano yake na Global Publishers, Dayna alisema, alipata nafasi ya kutembelea baadhi ya nchi ikiwemo Marekani na nchi nyingine za Afrika kidogo na kukaa huko kwa zaidi ya miezi miwili bila kujihusisha na muziki wake jambo lililomfanya kupata wakati mgumu kuanza tena gemu.

Nimejifunza mengi na najuta kutumia muda mrefu Ulaya, nimeachia Wimbo wa Salama lakini mapokezi yake si makubwa sana kama ilivyo nyimbo zangu nyingine na hii ni kwa sababu mashabiki walianza kunisahau“.

 

Siwezi Date na Diamond ni Pasua Kichwa :-Dayna Nyange

Mwanadada Dayna Nyange amefunguka na kusema ukweli wake kuwa hawezi kuwa na mahusiano ya kimapenzi na msanii mwenzake Diamond Platinumz kwa sababu ni pasua kichwa na kama atadate nae basi anaweza kumfanya kuwa na stress sana kiasi kwamba atamkondesha.

Alipokuwa akijibu swala la moja ya mashabiki zake katika ukurasa wake wa instagram, dayna alisema  kuwa : pasua kichwa atanifanya nirudi kiportable kwa stress”

Hii inaweza kuwa ni kutokana na skendo nyingi za mapenzi na wanawake Diamond anazokumbana nazo ambazo zinawafanya baadhi ya wanawake kusema hivyo akiwemo Dayna.

 

 

TID Ajikanyaga Kutoa Majibu Kuhusu Ushirikina

Msanii mkongwe wa muziki wa Bongo fleva Khalid Mohamed maarufu kama Top In Dar, TID amejikuta akipata kigugumizi pale alipotandikwa maswali kuhusu mambo ya kishirikina.

Siku za hivi karibuni topic ambayo imekuwa ikitrend Kwenye mitandao ya kijamii ni suala zinasambaa la uchawi ambapo watu maarufu wamekuwa wakinyosheana vidole kuhusu ushirikina.

Kwenye mahojiano na kituo kimoja cha habari, TID alipoulizwa kuhusu uchawi alishindwa kutoa jibu la moja kwa moja na kuishia kupata kigugumizi na kudai haamini uwepo wa masuala ya ushirikina katika muziki hususani kwa wasanii, kwa sababu hajawahi kuona wala kuletewa ushahidi kuhusu mambo hayo.

Nikiulizwa swali kama hilo, mnanichanganya maana mimi sina utaalam wa hayo mambo. Nitafutieni ushahidi niufanyie upembuzi ili niweze kujua kama kweli washirikina wapo au laa”.

Lakini pia Msanii mwingine wa Bongo fleva Dayna Nyange alipotandikwa swali hilo hilo aliweka wazi kuwa uchawi upo kwa sababu hata kwenye vitabu vya dini imeandikwa hivyo.

Uchawi upo kiukweli, itabidi nimtafute TID ili niongee naye kwanini hajui masuala ya ushirikina”.

Siku mbili hizi zilizopita Hamisa Mobetto ametrend sana Kwenye mitandao ya kijamii kwa kutuhumiwa kuwa anafanya mambo ya kishirikina.

Dayna Nyange Asafisha Nyota na Wizkid Nigeria

Msanii wa Muziki wa Bongo fleva ambaye ni hitmaker wa Mafungu ya nyanya, Dayna Nyange amefunguka na kueleza jinsi alivyokutana na staa wa nchini Nigeria Wizkid.

Kwenye mahojiano aliyofanya na Global Publishers, Dayna amefunguka jinsi alivyokutana na Wizkid ambaye  alimpokea vizuri na hata sapoti kubwa aliipata kutoka kwa Wizkid.

Siwezi kusema kuwa nipo njiani kutoa naye wimbo, hiyo inabaki kimenejimenti kwa sasa lakini ninachotaka kushea na nyinyi, jamaa (Wizkid) ameweka heshima ya aina yake kwao, amekuwa ni mtu wa watu na hata nilivyokutana naye kila mmoja alikuwa akijiuliza huyu nani ametoka wapi, kumbe ni Mbongo mimi, haaa haaa.

Mbali na kukutana naye na kuzungumza naye mawili matatu, nilibahatika kutembelea redio zao, yaani karibu kila redio ni kama wameweka kautamaduni kao, kuna picha kubwa za wasanii wao wanaoiwakilisha nchi, kuna P Square, Wizkid, Davido, Yemi na wengine wengi tofauti na hapa Bongo kikubwa utakutana na saini za wanamuziki tu”.

Dayna ambaye alikuwa kimya kwa muda mrefu ameachia ngoma yake mpya ya ‘Salama’ ambayo mpaka sasa inaendelea kufanya vizuri.

Dayna Nyange Afunguka Kuhusu Kuumizwa na Mapenzi

Msanii wa muziki wa Bongo fleva Dayna Nyange anayefanya vyema na wimbo wake wa ‘Salama’ amefunguka na kuzungumzia namna alivyotendwa na mwanaume ambaye alikuwa anatoka naye kimapenzi tukio lililomfanya aandike wimbo huo.

Kwenye mahojiano na Bongo 5, Dayna amefunguka na kueleza wimbo wake mpya umetokana na mambo aliyoyapitia kwenye mahusiano yake ya mwisho ambayo aliishia kuumizwa vibaya mno na mwanaume aliyekuwa naye;

Mapenzi yanazingua sana ndio maana nasema ni bora mtu kuwa single kuliko kudate na kitunguu kila siku unalia, nilinusurika kuposti kitu tu juzi sema malaika wa kheri akaniambia sio wewe Dayna hebu acha nikaona haya mambo na maumivu bora nikayamalize studio.

Nikaenda tu studio nikatoa machungu yangu kwenye wimbo wangu unaoitwa ”Salama” lakini mimi ni binti ambaye nikIwa kwenye mahusiano nakuwa kwenye mahusiano ya muda mrefu sana kuanzia miaka mitano na kuendelea”.

Lakini pia Dayna amedai kwa sasa amegundua kwanini baadhi ya wasichana wanatoka kimapenzi na wanaume wazee kwani bora kuliko kuumiza kichwa na vijana ambao wanaishia kuumiza moyo wako.

 

Dayna Nyange Afunguka Kukoshwa na Rayvanny

Mwanamuziki wa kike wa Bongo fleva Dayna Nyange anayefanya vizuri na ngoma yake ya Salesale amefunguka na kusema amefurahishwa kwa kiasi kikubwa na msanii mwenzake wa Bongo fleva kutoka WCB Rayvanny.

Dayna amesema amekoshwa na msanii mwenzake Rayvanny hii ikiwa ni baada ya kumtaja katika nyimbo yake inayofanya vizuri ndani na nje ya Bongo ‘Makulusa’ ambao amemshirikisha msanii kutoka South Africa anayejulikana kama Dj Maphorisa.

Kwenye wimbo huo wa Makulusa kuna kipande ambacho Rayvanny amemtaja Dayna Nyange ambapo mashairi yake yanaimba hivii “Kipotabo kama Dayna, ana shepu ya birika she got ice cream China, hips from America My baby she is finna”.

Kipotabo Dayna Nyange

Kwenye mahojiano aliyofanya na Times Fm Kupitia kipindi cha The playlist, Dayna alidai labda pengine Rayvanny alimtaja kutokana na vitu anavyovifanya kuendana na ngoma hiyo.

Unajua Dayna amekuwa Kipotabo kwa muda mrefu hajawahi kuongezeka kwaiyo naamini Rayvanny akaona ngoja nimuweke Dayna kwa sababu huyu baadae hawezi kuja kunipa shida , na mimi kwa upande wangu nilifurahi sana japo kila nilikuwa nje ya nchi na sikutegemea kama alikuwa anaweza kufanya kitu kama hicho kwa sababu sikuwa na ukaribu naye kihivyo so I was happy”.

 

Dayna:Nilipopta Mimba Nikajua Kuwa Nina Malaria.

Mwanadada ambae kwa sasa amekuja na project yake mpya ya wimbo wa salesale, amefunguka na kuelezea historia yake ya mimba yake ya kwanza ambapo mtoto huyo hivi sasa ana umri wa miaka 11.

Dayna ameyaongea hayo jana alipokuwa Clouds Radio katika kipindi cha XXL cha Clouds Tv,Dayna anasema hayo alipokuwa amekwenda kwa ajili ya kutambulisha wimbo wake mpya unaokwenda kwa jina la salesale ambao ameuachia siku hiyo.

Dayna pia akijibu tetesi zinazoendelea kuhusu yeye kuwa mjamzito alisikika akisema kuwa kwa sasa yeey sio mjamzito ila tu picha aliyotuma  ikimuonyesha ana kitumbo kikubwa na kuzua mjadala wa yeye kuwa na mimba ilikuwa ni shibe tu na sio kingine.

Hata hivyo Dayna ansema kuwa kitu anachokumbuka kuhusu ujauzito ni katika mimba yake ya kwanza ambayo aliiata akiwa na umri wa miaka 18 huko miaka ya nyuma ambapo alipokuwa akiumwa alihisi kuwa ni malaria na nyumbani kwao walimwambia kuwa inabidi aende kupima malaria na ndipo alipokwenda na kurudisha majibu nyumbani.

nilipopata mimba sikuwa hata najua juu ya hilo, nilihisi ninaumwa malaria hivyo niliambiwa kuwa nikapim hospitali, na ile karatsai ya majibu niliyopewa nikaambiwa niipeleke nyumbani ndipo nilipoenda na kumpa dada yangu na kumbe nilikwa nina ujauzito.

Dayna anasema kuwa anatamani san amtoto wake afike mbali kielimu kwa sababu yeye hakubahatika kupata elimu ya sekondari.

 

Dayna nyange Aweka Wazi Tetesi za Kuwa Mjamzito na Baba Kijacho WakeN

Msanii wa kike  muziki wa bongo fleva Dayna Nyange amefunguka na kuwekawazi kwa tetesi zilizokuwa zikisambaa katika mitandoa ya kijamii kuhusu kuwa mjamzito.Dayna anasema kuwa kwa muda amekuwa akisikia kuwa watu wamekuwa wakisema kuwa yeye ni mjamzito lakini ukweli ni kwamba yeye sio mjamzito na wanaomzushia wanatakiwa wajue hilo.

Akiongea na mwandishi wa habari wa Clouds Tv, Tei .Dayna Nyange anasema kuwa siku ya Valentine alipost picha ikimuonyeshe kuwa anakitumbo kikubwa na kuwatakiwa watu Valentine njema lakini kitu cha ajabu ni kwamba baada ya post hiyo watu walianza kusambaza picha hiyo na kumtamkia kuwa yeye ni mjamzito.

Dayna anasema kuwa siku hiyo alikuwa tu ameshiba na kuamua kuweka picha hiyo katika mtandao lakini kitu cha ajabu anakuja kuona ilishasambaa na walishamtafuta hadi baba wa mtoto huyo wakati sio kweli.

kuna vitu sio lazima uweke wazi moja kwa moja,ikifika muda wa kujulikana basi itajulikana tu.mimi nilikuwa nimekula zangu maharage nimeshiba  nikapost lakini baada ya hapo watu wakaanza kusema kuwa  nina mimba na nini na nini.-Alifunguka Dayna.

Hata hivuo mwandishi alitaka kujua neno lake la mwisho kuhusu hali hiyo ambayo watu wamekuwa wakimtangazia katika  mitandao ya kijamii na Dayna Nyange kwa kigugumizi kizito alisikika akisema.

no comment kwakweli kuhusu hilo, siwezi kusema kama ipo au haipo.

Hata hivyo mwandishi aliamua kumuuliza kuhusu tetesi za kuwa mimba hiyo ya dayna ni ya producer kutoka nchi Kenya William Tuva,ambapo wiki iliyopita kupitia kipindi cha Shilawadu habari hzio ndipo zilipoanza kusambaa.

binafis sijui kwanini watu waliamua kumzushia tuvva,kwa sababu mimi sijawahi kuweka mahusiano yangu wazi, kwaio hata sijui kwanini.

Yathibitika ,Dyana Nyange ni Mjamzito.

Msanii wa muziki wa bongo fleva Mwanaisha  Said maarufu Dayna Nyange ameonekana kuwa kimya sana kimuziki lakini kumbe sababu kubwa ya kukaa kwake kimya ni kutokana na hali ya uzazi aliyo nayo sasa hivi.dayna nyange inasemekana kuwa ni mjamzito na tumbo lake limeshaanza kuonekana na hali hiyo imekuwa ikimpeleka mputa mputa kiasi kwamba anashindwa kufanya kazi zak vizuri.

Watu wa karibu wa Dayna Nyange wanasema kuwa kwa hali aliyonayo Dayna kwa sasa ni mbaya kwa sababu ujauzito huo umekuwa ukimuendesha sana na amekuwa akijitahidi kujificha ili watu wasijue kuwa yuko nahali hiyo.

si unajua kuwa dayna nyange alipta mpenzi wa kizungu kwaio nadhani sasa wameamua kuzaa,na hataki kabisa kumtaja baba kijacho wake kwa sababu hata sisi marafiki zake  ametuficha.

siku ya wapendanao, Dayna Nyange aliweka moja ya picha yake katika ukurasa wake wa instagram ikimuonyesha akiwa ameshika tumbo linaloonekanakuwa kubwa na yupo katika hali ya ujauzito , hali hiyo iliwafanya mashabiki kumpongeza lakini wengine kuwa na shauku ya kutaka kujua baba kijacho.Alipotafutwa Dayna kuelezea hali yake aliwajibu waandishi wa habari kwa kusema:

sitaki kuzungumzia ujauzito wangu au baba kijacho wangu kwa sababu hayo ni maisha yangu binafsi.

Siku za nyuma, zilisikika tetesi kuwa Dayna Dyange amekuwa katika mahusiano ya kimapenzi na mwanamitindo maarufu duniani Dax Cruz.

Dayna Awalaani Wanaoenda Kudanga Nje ya Nchi

Mwanadada Mwanaisha Said maarufu kama Dayna amefunguka na kuwalaani wasanii wa kike ambao wamekuwa wakienda nje ya nchi tena hasa Marekani na kufanya kazi za kudanga na kuwafanya watu wa nchi hizo kuamini kuwa wasanii kutoka bongo wapo kwa ajili ya kufanya kazi hizo wanapoenda nje ya nchi.

Ilikiwisha wahi kuripotiwa kuwa wasanii wengi wa kike wamekuwa wakienda Marekani na kufanya biashara za ngono kitu ambacho kimekuwa kikiwaharibia soko wasanii wengine wanaokwenda kwa ajili ya kufanya kazi za musiki nchi humo.

Dayna amesema kuwa hata hivyo kwa muda mrefu amekuwa nchini Marekani kwa ajili ya kuangaika na kazi zake lakini itu cha kushabgaza ni kwamba kuna baadhi ya watu wamekuwa wakimjadili kuwa yupo huko kwa ajili ya biashara ya ngono kitu ambacho sio cha kweli hata kidogo.

Najua wapo wasanii wachache ambao wametuharibia kabisa  soko hasa tunapoenda nje ya nchi na hasa marekani,kuna nchini zingine watu wakituona wanaanza kutufikiria kuwa tumeenda kwa ajili ya kufanya biashara ya ngono wakati ilo sio kweli kwa mfano  kama mimi nilikuwa marekani kwa ajili ya kufatilia kazi zangu za muziki. Alifunguka Dayna.

Malalamiko ya Dayna yanaenda sambamba na tabia za wasichana wengi wa bongo hasa wasanii ambao wamekuwa natabia ya kwenda kudanga na kufanya biashra za ufuksa huku wakisambaza sifa mbaya kwa wasanii wengine kutoka Afrika.