“Sijazaa na Diamond Pamoja Majizzo Kwa Ajili Ya Pesa”-Hamisa

Mwanamitindo na Msanii wa Bongo fleva Hamisa Mobetto amefunguka na kuweka wazi kuwa hajazaa na Msanii wa Bongo fleva Diamond Platnumz na CEO wa EFM kisa pesa kwani ana pesa zake binafsi.

Hamisa amesema watu wengi wakisikia amezaa na wanaume wenye uwezo kama hao basi moja kwa moja wanafikiri kuwa amefuata pesa Lakini hawajui kuwa pesa zake anatafuta mwenyewe kwa jasho lake.

Kwenye mahojiano aliyofanya na kituo kimoja cha habari, Hamisa amekana stori za kuwa amegeuza watoto wake mtaji kwa kuishi kutegemea matunzo atakayopewa kwa ajili ya Watoto Wake na Diamond pamoja na Majizzo.

Mimi ni mtu ambaye nilikuwa najiweza vizuri tu kabla ya kuzaa na ninataka wasichana wadogo wanaoniangalia wajue kuwa kuzaa ndio kutoka kimaisha hapana sio hivyo, Nataka watu wajue kuwa sio kwamba kwa sababu nimezaa na wanaume wenye pesa basi ndio nimejirahisishia maisha hapana kila kitu nilichokuwa nacho ni jasho langu mwenyewe na nguvu zangu nimetumia kuvipata”.

Siku za nyuma Hamisa ameshawahi kusemekana kupangishiwa jumba la kifahari na baba wa Mtoto Wake Diamond Platnumz na kabla ya kuhamia hapo anadaiwa kuwa alipangishiwa nyumba na Majizzo.

“Marafiki Wanamuharibu Hamisa”- Esma Platnumz

Dada wa staa wa Bongo fleva Diamond Platnumz, Esma Khan ‘Esma Platnumz’ ameibuka na kudai Hamisa ni rafiki mzuri sema watu wanatajwa kama marafiki zake ndio  wamemuharibu.

Esma amefunguka hayo kwenye ukurasa wake wa Instagram ambapo aliomba mashabiki zake wamuulie maswali yoyote na yeye angejibu na moja kati ya maswali aliyoulizwa yalimuhusu Hamisa.

Kama utakumbuka siku za nyuma Esma alishawahi kuwa na urafiki wa karibu na Hamisa Mobetto tena inasemekana alikuwa na urafiki na familia ya Diamond kwa miaka mingi.

Lakini urafiki huo uliingia shubiri baada ya Hamisa kuzaa na Diamond na kupelekea Bifu kubwa kati ya Hamisa na Familia nzima ya Diamond iliyopelekea urafiki wa Esma na Hamisa kuisha kabisa.

Swali la Kwanza:

Umemiss nini kutoka kwa Hamisa Mobetto alikuwa rafiki Yako sana?

Esma Akajibu:

Hamisa ni rafiki mzuri ila watu wanamuharibu tu”.

Swali la Pili:

Kwa nini hupendi Hamisa aolewe na Diamond?

Esma Akajibu:

Sijawahi kusema hivyo”.

Sakata la Hamisa na Esma lilichukua sura mpya Baada ya kumrushia tuhuma za uchawi dhidi ya kaka yake Diamond.

 

Pretty Kind Afurahia Kuvunjika Kwa Penzi La Mobetto na Diamond

Video vixen na Msanii wa Bongo fleva Suzan Michael maarufu kama Pretty Kind ameibuka na kuchekelea kuvunjika kwa mahusiano kati ya staa wa Bongo fleva Diamond Platnumz na Hamisa Mobetto.

Wiki chache zilizopita Mobetto aliweka wazi kuwa baada ya miaka kumi ya kuwa pamoja na Diamond na kuzaa mtoto mmoja wameachana rasmi na kila mmoja kuendelea na maisha yake.

Baada ya taarifa hizo za kuachana kwa Mobetto na Diamond Pretty Kind ameibuka na kudai amefurahishwa na Taarifa hizo kwa sababu yaliyotokea ni Mungu kaamua kumuumbua Mobeto kutokana na uchawi aliokuwa anamfanyia Diamond na hilo ni fundisho kwa wasichana wengi wanaoamini uchawi katika mapenzi.

Kwenye mahojiano na Global Publishers, Pretty Kind ametiririkia haya:

Kilichomtokea Mobeto ni fundisho kwa wasichana wengi na wanatakiwa kujua kwamba mapenzi hayalazimishwi na kamwe uchawi hauna nguvu katika mapenzi”.

Lakini pia Pretty Kind asihangaike sana kutangaza kuwa ameachana na Diamond huku akiwa bado anamuhitaji pia ajue kwamba hawezi kuolewa na msanii huyo bali yupo mke wa Diamond atakayeolewa hivi karibuni kwake yeye haiwezi kutokea.

Hamisa-Kuna Msururu Wa Wanaume Wanataka Kunioa

Msanii wa Bongo fleva na mwanamitindo maarufu Hamisa Mobetto amefunguka na kudai Mpaka sasa kuna msururu mkubwa wa wanaume waliopanga foleni kutaka ndoa naye.

Hamisa ambaye alizidi kujizolea umaarufu baada ya kuzaa na staa wa Bongo fleva Diamond Platnumz amedai ingawa kuna wanaume wengi wanataka kumposa amekuwa akikataa.

Kwenye Interview na kituo kimoja cha habari hivi karibuni Hamisa amefunguka haya kama sababu ya kukataa ndoa na wanaume waliotayari kumposa ni kukosa nao chemistry:

Wapo wengi tu ambao wamekuja kutaka kutoa posa lakini kuoana na mtu mnatakiwa muwe na chemistry moja. Mimi na Diamond tushakuwa na mtoto lakini nina mwingine pia kama alivyo yeye”.

Hamisa amekuwa Kwenye Mahusiano na Diamond kwa miaka zaidi ya kumi lakini hawajawahi kuanika mahusiano hayo hadharani kabisa mpaka leo hii.

Esma- Sina Ubaya na Hamisa Akitaka Tuongee Tutaongea

Dada wa Staa wa Bongo fleva Diamond Platnumz, Esma Platnumz amefunguka na kuweka wazi uhusiano wake na mzazi mwenzake na kaka yake Hamisa Mobetto.

Siku za nyuma Hamisa na Esma walikuwa mashoga wakubwa sana lakini urafiki huo uliingia doa mwaka jana baada ya Hamisa kumtangaza Diamonf kama Baba wa mtoto wake ndipo matatizo na Familia ya Diamond yalipoanzia hapo.

Mpaka leo hii kuna sintofahamu bado kati ya Hamisa na Familia ya Diamond lakini Esma anafunguka na kuweka wazi kuwa hana bifu na Hamisa na kama akitokea kutaka kuongea naye basi yeye kwake ruksaa moyo mweupe.

Kwenye mahojiano na Kipindi cha Refresh cha Wasafi Tv, Esma ameweka wazi kuhusu hali yake ya Mahusiano na Mobetto:

Hamisa alikuwa akikosea mimi nilikuwa namsema kwa sababu mimi sina ubaya na mtu na ninaongea na mtu yoyote na Hamisa akitaka tuongee tutaongea yaani mimi naongea na watu wote”.

Esma pia alifunguka kuhusu mtoto wa Hamisa Dylan ambaye amekuwa akionekana naye sana siku za hivi karibuni:

Sisi hatuna tatizo lolote na mtoto halafu yule ni mtoto halafu pia ni damu yetu kwaiyo tu nampenda”.

Lakini pia Esma amemtupia Dongo Hamisa kuhusiana na wimbo wake alioachia hivi karibuni wa Madam hero kudai ni wimbo wa kusikitisha sana na akiongia yeye studio atamtupa mbali.

 

Mobetto- Sina Ubaya na Wanawake Wanaomtaka Diamond

Mwanamitindo na msanii wa Bongo movie Hamisa Mobetto amefunguka na kuweka wazi kuwa hana ubaya na wanawake ambao wanamtaka Baba mtoto wake staa wa Bongo fleva Diamond Platnumz.

Hamisa na Diamond wamefanikiwa kuzaa pamoja mtoto mmoja wa mwaka mmoja anayeitwa Dylan wakat Diamond ana watoto wengine wawili na mwanamama Zarinah Hassan.

Kwenye mahojiano na Global Publishers Hamisa amefunguka wakati alipoulizwa kuhusu Msanii wa Bongo fleva Pretty Kind ambaye aliwahi kuweka wazi mapenzi yake kwa Diamond na baadaye kulalamika Hamisa kachukia hadi kamblock:

Hamisa amekana kumblock Pretty Kind na kudai yeye hana ubaya na mwanamke yoyote anayemtaka Diamond ambaye anasemekana kuwa ni mpenzi wake:

Kwanza kabisa nilikuwa simjui na hata kumsahau huyo mtu mwenyewe halafu sijamblock kwa sababu ya Diamond kwa sababu kuna wanawake kama milioni tano wote wanamtamani huyo huyo mtu mmoja sasa sasa kama ndio hivyo nitawablock watu wangapi Jamani?

Pretty Kind kuna Maneno machafu na mabaya aliyaongea kuhusu mimi alinichafua sana halafu mimi ni brand simjui nikaona huyu naye katokea wapi? Nikamblock Maisha Yangu yaendelee kwa amani wa Nini mtu anayenipa kero”.

Pretty Kind alifunguka kuwa kama akitaka kutoka kimapenzi na Diamond anaweza akampata kwa sababu yeye ni mzuri na ana vigezo vyote vya kutokataliwa na Diamond.

Hamisa Mobetto Hana Kipingamizi Cha Ndoa na Diamond

Mwanamitindo na mfanyabiashara Hamisa Mobetto amefungukia mipango ya ndoa na Staa wa Bongo fleva Diamond Platnumz na kuweka wazi kuwa Yupo Tayari Kuolewa naye.

Kwenye mahojiano na Gazeti la Amani, Mobetto alipoulizwa kuhusu utayari wa kufunga ndoa  na Diamond alikubali na kusema Yupo Tayari kufunga naye ndoa:

NDIYO NITAKUBALI, Ingawa Wapo wanaume wengi tu ambao wamekuja kutaka kutoa posa lakini kuoana na mtu mnatakiwa muwe na ‘chemistry’ moja, mimi na Diamond tushakuwa na mtoto, lakini nina mwingine pia kama alivyo yeye”.

Lakini pia Mobetto aliulizwa kuhusu maovu yote ambayo Diamond amekuwa akionekana akifanya na wanawake mbali mbali na Hamisa alifunguka:

Makosa yapo lakini hayo naweza kuyaangalia mbele lakini siyo kwa sasa, kama ni mtu mwenye nia njema na mimi ataonekana”.

Diamond ambaye amewahi kukiri kuwa Kwenye Mahusiano na Hamisa kwa zaidi ya miaka 10 kwa siri, amesemekana kuwa Kwenye Mahusiano na Hamisa tangu alipoachana na Zari mapema mwaka huu.

 

Jumba La Mobetto Alilozawadiwa na Diamond Lagubikwa na Utata

Wiki iliyopita habari zilienea Kwenye mitandao ya kijamii kuwa Diamond amemnunulia mjengo wa fahari mama mtoto wake na Hamisa Mobetto ambapo Mama Mobetto alithibitisha taarifa hizo.

Lakini hivi sasa Global Publishers wanaripoti kuwa Habari hiyo siyo ya kweli kwani kwa taarifa waliyokuwa nazo ni kuwa nyumba ile haijanunuliwa bali imepangishwa tu kwa muda.

Baada ya Tetesi hizo gazeti hilo lilienda kufanya uchunguzi ambapo Jirani mmoja wa Mobeto aliyeomba hifadhi ya jina, alipoibukiwa na wanahabari wetu, aliweka wazi kuwa nyumba hiyo hajanunuliwa na ameshangazwa na habari kwamba amenunuliwa.

Kwa kweli nimeamini hawa mastaa wanapenda kujikweza, yaani nyumba hii tumeona mchakato wote na mwenye nyumba tunamjua lakini mitandaoni tunaona mama Mobeto anasema Diamond kawanunulia”.

Lakini baada ya taarifa hizo gazeti hilo lilimsaka mmiliki wa mjengo huo ili aweze kuthibitisha taarifa hizo ndipo ndugu wa mmiliki alipofunguka:

Mimi mwenyewe niliona kwenye mtandao kwamba wamenunua, nikashtuka sana ikabidi niende kumuonesha babu (mmiliki), akasema si kweli ndipo wakapuuza tu maana“.

Mama mzazi wa Mobetto anayejulikana kama Shufaa Rutiginga aliweka wazi Kwenye mahojiano na Wasafi Tv kuwa Diamond alinunua mjengo huo maalumu kwa ajili ya mtoto wake Dyalan.

Diamond Athibitisha Kumnunulia Mjengo Hamisa

Staa wa muziki wa Bongo fleva Diamond Platnumz amethibitisha tetesi zilizokuwa zinasambaa mtandaoni kuwa amemnunulia mjengo kama watoto wake Hamisa.

Baada ya Diamond kuachana na Zari na Kurudisha majeshi kwa Hamisa imekuwa ikisemekana kuwa Hamisa amehama alipokuwa anaishi na kuhamia kwenye mjengo mpya kabisa na mtoto wake Dylan na Fantasy.

Taarifa zilisambaa kuwa mjengo wenyewe ni ghorofa  ambalo ni bonge wa mjumba ambao upo maeneo ya Mbezi Beach, Bahari Beach.

Diamond amethibitisha taarifa baada ya kuandika Instagram na Hamisa kujibu kwa kumshukuru kwa nyumba hiyo:

 

Hii sio mara ya kwanza kwa Diamond kununua Nyumba kwa ajili ya wanafamilia wake kama utakumbuka ameshawahi kumnunulia nyumba mama yake mzazi Lakini pia ameshamnunulia nyumba mzazi mwenzake Zari nchini South Africa.

Hamisa Mobetto Akiri Kuwa Katika Kipindi Kigumu

Muigizaji wa Bongo movie na mfanyabiashara maarufu Hamisa Mobetto ameanika undani juu ya mambo anayopitia kwa hivi sasa na kukiri kuwa katika kipindi kigumu.

Hamisa amekuwa Kwenye headlines tangu alipotangaza kuzaa mtoto wa Diamond mwaka jana lakini siku chache hizi mambo yamekuwa mazito kidogo kwa upande wake.

Familia nzima ya Diamond kuanzia mama yake mpaka Dada zake mpaka mameneja wa Diamond wameonekana kumkataa kata kata Hamisa huku wakionyesha wazi kumpenda zaidi Ex wa Diamond Zari.

Hamisa amekuwa akirushiwa vijembe na Familia ya Diamond ambayo imedai kuwa ni mchafu na hata kusambaa kwa Tetesi kuwa amechezea kipigo cha mbwa koko kutoka kwa Mama Diamond.

Kupitia ukurasa wake wa Snapchat Hamisa amefunguka magumu hayo anayopitia kwa hivi sasa ambapo amesema licha ya magumu anayokabiliana nayo kwa sasa bado anaamini Mwenyenzi Mungu atamvusha:

Bado sijafika Mw/Mungu aliponipangia na kama mnavyoona barabara yangu ni mbovu, ina mashimo, mabonde na pia matope mengi kwa hiyo safari yangu inakuwa ngumu kidogo.

Lakini naimani sana na M/Mungu alonileta kwenye dunia hii, naimani ipo siku nitafika na Naimani barabara yangu hii nii mbovu ipo siku ataisawazisha na kuiweka rasmi.

Nina kushukuru sana Mungu, naimani kuna vibaya vingi umeniepusha navyo na pia naimani kuna vikubwa vizuri vyaja. Na naimani hivi vyote visingenipata mimi kama ningekuwa sina u-special wowote ndani yangu”.

 

 

Hamisa Amtaka Diamond Aongee na Familia Waache Kumuandama

Hamisa Mobetto alijikuta katika wakati mgumu mwishoni mwa wiki iliyopita baada ya familia nzima ya Mzazi mwenzake Diamond kumuandama.

Tangu ijulikane kwamba Diamond amerudisha majeshi kwa Hamisa baada ya kumwagwa na Zari, familia yake imeweka wazi kuwa haimkubali Hamisa na hawamtaki.

Lakini juzi mambo yalimfika shingoni Hamisa baada ya Mama Diamond na wifi yake Esma kumpa kichambo cha maana kwa kudai kuwa ni mchafu na hajui hata kusafisha chumba.

Baada ya povu hilo kuendelea kwa muda mrefu huku familia hiyo ikionyesha wazi kabisa kuwa wanamtaka Diamond arudiane na Zari, Hamisa alishindwa kuvumilia.

Hamisa alienda Kwenye ukurasa wa Instagram wa Diamond na kumtolea povu huku akitaka awaambie familia yake waache kumsema kwani wamemsimanga sana:

Hamisa alitoa povu hilo baada ya kuona familia ya Diamond inazidi kumuandama mtandaoni na Diamond haonyeshi jitihada zozote katika kumtetea yeye kama mama watoto wake dhidi ya familia yake mwenyewe.

Harmonize Amkingia Kifua Mobetto Baada Ya Kugeukwa na Kila Mtu

Staa wa muziki wa Bongo fleva Harmonize ameonekana kuwa upande wa Hamisa Mobetto na kumkingia kifua baada ya kila mtu kumtolea povu.

Sakata hili lilianza siku ya Ijumaa baada ya  Diamond kuachia wimbo na video yake mpya ya wimbo unaoitwa Iyena aliomshirikisha Rayvanny ambapo ndani ya wimbo huo Video Queen ni Zari.

Baada ya video hiyo kutoka karibia kila mtu kuanzia familia ya Diamond mpaka WCB wote walianza kumposti Zari huku wakimtaka arudi kwa Diamond na kumponda kabisa Hamisa.
Harmonize pekee alionekana kuwa upande wa Hamisa kwani baada ya kila mtu kwenda upande wa Zari Harmonize alimpa moyo Hamisa ambapo aliandika ujumbe huu:

Lakini pia hata Kwenye mahojiano aliyofanya na WAsafi Tv Harmonize alipoulizwa kwanini peke yake ameamua kuwa uapnde wa Hamisa alijibu kuwa yeye ni kama bendera fuata upepo kwani Diamond alisema yupo na Hamisa basi atakuwa upande huo na alisema kwa MObetto na yeye atakuwepo huko.

Pretty Kind Ahaidi Kumpindua Mobetto Kwa Diamond

Msanii wa Bongo fleva Suzan Michael maarufu kama Pretty Kind amefungukia azma yake ya kumpindua Hamisa Mobetto na kumchukua Diamond.

Pretty Kind amefunguka na kudai ameamua kusema hayo hadharani kwani Diamond amekuwa akimnyima usingizi siku nyingi kwa mapenzi aliyonayo kwake.

Kwenye Interview aliyofanya hivi karibuni na Global Publishers Pretty Kind alifunguka na kusema:

Nitamn’goa tu Diamond kwa Mobetto kwa sababu nampenda sana, ananikosesha usingizi huyu Mobetto asidhani amefika. Kuna wakati niliona ilikuwa ni ngumu kumpata Diamond kwa kuwa Mama yake alikuwa akimpenda sana Mobetto lakini sasa naona njia nyeupe baada ya Mobetto kuchezea kichapo”.

Hivi karibuni imesekana kuwa hali si shwari kati ya Hamisa Mobetto na Mama mzazi wa Diamond Bi. Sandra baada ya kudaiwa alimpa kipigo cha mbwa mwizi baada ya kumkuta nyumbani kwake Madale.

Diamond alirudisha majeshi yake kwa Hamisa mapema mwaka huu baada ya kumwagwa na kama watoto wake Zari.

Baada Ya Kupewa Kichapo na Mama Diamond, Hamisa Afunguka

Muigizaji wa Bongo movie na mfanyabiashara Hamisa Mobetto amefungukia skendo ambayo imekuwa ikimzunguka kwa siku kadhaa sasa ile ya kupewa kichapo na Mama Diamond.

Kuna habari zilisambaa siku chache zilizopita ambazo zilikuwa zinadai kuwa Mama Diamond alimpa kipigo cha mbwa koko Hamisa baada ya kumkuta nyumbani kwa Diamond Madale.

Mama Diamond alithibitisha taarifa hizo Baada kuwaambia Global Publishers kuwa hampendi Hamisa na kila atakapokutana naye basi atampiga tena kwa kudai amekosa adabu na hataki mtoto wake awe naye.

Kwenye mahojiano na waandishi wa habari, Hamisa alikataa kuliongelea  jambo hilo na kudai ni  binafsi zaidi ila kugombana kwa binadamu ni kitu cha kawaida.

Hilo siwezi kuliongelea, yeah!. is too person, is too private, is too family. Hata vikombe kwenye kabati vinagong’ana, so sisi binadamu vinaweza kutokea”.

Lakini pia Hamisa aliulizwa nini Mahusiano Yake na Mama Diamond ambaye yeye alisema kabisa kuwa hampendi, alifunguka;

Sina kinyongo na mtu, sina bifu na mtu, mimi am just fine, may be yeye mwenyewe sio upande wangu wa kuweza kuelezea”.

Sakata hilo linasemekana kuleta sintofahamu kati ya Diamond na mama yake kwani kwa hivi sasa Diamond yupo Kwenye Mahusiano na Hamisa.

Hamisa Mobetto Awachana Wasiopenda Penzi Lake na Diamond

Muigizaji wa Bongo movie na video vixen maarufu Hamisa Mobetto amewachana watu wote wasiopenda Mahusiano Yake na staa wa Bongo fleva Diamond Platnumz.

Hamisa na Diamond wamerudiana penzi lao rasmi na inaonekana wazi kabisa hivi sasa mambo ni moto kwani Diamond ameonekana ana ukaribu sana na mtoto wao Dylan tofauti na ilivyokuwa siku za nyuma.

Lakini tangu wamerudiana Kumekuwa na maneno mengi yanayosemwa ikiwemo na Mama Diamond kumkataa Hamisa na hata baadhi ya mashabiki kumtolea maneno ya kejeli Hamisa na Diamond.

Hamisa amewapa za Uso watu wote wasiopenda Mahusiano yao ambapo Kwenye mahojiano na Dizzim Online, Hamisa amesema maneno hayawssumbui kwani ndio wapo wote hivyo:

Unajua huwezi kumlazimisha mtu apende pilau wakati alishazoea biriani kwaiyo ni hivyo ni maisha yangu na ni maisha ya watu wengine kwaiyo utakachoona wewe kinakufaa haimaanishi na mimi kitanifaa kwaiyo kila mtu aangalie maisha yake waniache na mimi na maisha yangu.

Mimi sio mtu wa kumridhisha kila mtu maana mimi sio Mungu kwaiyo kama hutaki acha sio lazima what you see is what you get and what you don’t see is what you don’t get”.

 

Mama Diamond Athibitisha Kumpa Kipigo Cha Mbwa Mwizi Hamisa Mobetto

Mama mzazi wa staa wa Bongo fleva Diamond Platnumz, Bi. Sandra au maarufu kama Mara Diamond amethibitisha kumpa kipigo cha mbwa mwizi mkwe wake Hamisa Mobetto.

Mwanzoni mwa wiki hii kuna stori ilisambaa kuwa Mama Diamond kampa kipigo kizito Hamisa baada ya Kumekuwa nyumbani kwa Diamond Madale hadi kuacha wigi lake.

Mama Diamond amethibitisha habari hizo kwenye mahojiano aliyofanya na Globa Publishers ambapo ameweka wazi kuwa hampendi na hataki hata kumuona nyumbani kwake:

Ni kweli nilimpiga na wigi nikamvua na hayo  mambo ya kumfuata mzazi mwenzie ni huko, pale Madale ni kwangu na simtaki nyumbani kwangu kabisa.

Mama Diamond aliulizwa sababu gani hasa ilimfanya amchukie Mobetto na alifunguka haya:

Kitendo cha kuniitia mimi Shilawadu (kipindi cha udaku cha Televisheni ya Clouds) kilinikera sana halafu nikaanza kutukanwa kwenye mitandao ya kijamii.

Lakini pia Mama Diamond aliweka wazi kuwa baada ya kumtembezea kipigo Hamisa alimvua wigi ndipo Diamond alikuja kumuamulia:

Mama Diamond ameweka wazi hamtaki Mobetto na  kama mwanaye atakuwa na Mahusiano naye basi hawataelewana:

Kwanza tu siyo mwanamke wa kuoa (wife material) hajui kutandika hata kitanda wala kufanya tu usafi ni shida.

Yaani atajua yeye mwenyewe maana mimi ndiyo nimemzaa Diamond na siyo yeye sasa sijui nani ana nguvu hapo.

Siwezi kukanyaga kwenye  harusi yao hata siku moja watasherekea wenyewe”.

Mama Diamond ameweka wazi kuwa anataka Mwanayr amletee mwanamke mwingine anayejiheshimu na sio Mobetto.