Kim Nana Amwaga Povu Kisa Penzi la Diamond na Tanasha

Video vixen na mwanamitindo Lilian Kessy  maarufu kama Kim Nana amejikuta akimwaga Povu zito Baada ya kuulizwa kuhusu Ex Wake staa wa Bongo fleva Diamond Platnumz na Mpenzi Wake Mpya Tanasha Donna Oketh.

Kim Nana alikuwa kwenye mahusiano ya kimapenzi na Diamond kwa muda kabla ya kumwagwa chini miezi michache iliyopita na Diamond kuanza mahusiano na Tanasha.

Kim Nana ameibuka na kulitolea povu penzi jipya la Diamond na Tanasha baada ya Gazeti la Amani kumtaka azungumzie penzi jipya la Diamond ambaye awali iliaminika kuwa ndiye mumewe mtarajiwa kabla jamaa huyo hajaibuka na Tanasha.

Akimzungumzia zilipendwa wake huyo, Kim alisema mambo ya Diamond na Tanasha hayamhusu huku akielekeza lawama zote kwa mitandao ya kijamii.

 Hivi mnajua kiasi gani nimetukanwa kwenye mitandao ya kijamii? Na pia watu wa mitandao hawajui kabisa kufuatilia vitu kwa kina wanachojua ni kutukana watu lakini nashangazwa sana mimi kuhusishwa na Diamond, naomba kuweka wazi leo siko kwenye mapenzi na Diamond kwa sasa mimi nina maisha yangu na yeye hivyohivyo ndiyo maana amemuweka wazi mpenzi wake mpya kama ningekuwa ni mimi si angewaambia mashabiki zake kuwa ni mimi?”.

Kim Nana Adaiwa Kubadili Dini Kisa Diamond

Video vixen anayetrend sana kwenye mitandao ya kijamii Lilian Kessy maarufu kama Kim Nana ambaye pia ni mpenzi wa staa wa Bongo fleva Diamond Platnumz anasemekana kubadilisha dini kutoka kuwa Mkristo mpaka muislamu kwa ajili ya ndoa na Diamond.

Gazeti la Amani linaripoti stori hiyo ambapo ndugu wa karibu na msanii huyo ambaye aliomba hifadhi ya jina, alisema kuwa Diamond kwa sasa yupo na uhusiano ambao upo ‘siriasi’ kwani amefikia hatua ya kumbadili dini mpenzi wake huyo ili waingie naye kwenye ndoa.

Nyie hamjui, wanaosema eti Kim Nana ametupiwa virago vyake nje huko Madale nyumbani kwa Diamond na mama yake, wamepitwa na habari, mwenzao Diamond kambadili dini anataka kumuoa kwani hata muda mwingi yupo na mama mkwe wake pale Madale”.

Wiki iliyopita kuna stori ilisambaa kuwa penzi la Diamond na Kim Nana lilifika mwisho mara baada ya mrembo huyo kutimuliwa nyumbani kwa Diamond Madale na Mama Diamond baada ya kutibuana.

Mama mzazi wa Diamond Bi. Sandra amefungukia tetesi hizo na kusema Kim Nana hajatimuliwa Madale bali yupo pale Kim yupo nyumbani kwake na sasa amebadilishwa dini na mwanaye ambapo anafundishwa kusoma Kuruani na mumewe Maisala Shamte ‘Anko’ na ndio maana wako karibu muda wote.

Kwa taarifa yenu Kim nipo naye muda mwingi na sasa amebadili dini, anafundishwa Kuruani na mume wangu kwa hiyo watu watasubiri sana kama wanadhani ataachwa leo wala kesho, hilo halitatokea”.

Mwanzoni mwa mwaka huu Diamond alimuahidi mama yake hatamaliza mwaka 2018 bila kuoa labda huu ndio muda muafaka wa kumuoa mpenzi wake huyo.