Esma Ashabikia Ndoa Ya Diamond na Tanasha

Dada wa staa wa Bongo fleva Diamond Platnumz, Esma Platnumz ameibuka  na kuweka wazi mapenzi yake kwa wifi yake mpya Tanasha na kuweka wazi kuwa kama kaka’ke huyo atachukua uamuzi wa kumuoa kwake yeye anabariki kwa sababu ni chaguo lake.

Kwenye mahojiano aliyofanya na Gazeti la Ijumaa Esma hadhani kama ni vyema kumchagulia kaka yake huyo mke, bali macho yake ndiyo yanaona wapi ni bora aangukie hapo na atakapopachagua na kumuonesha atampokea tu.

Unajua hata leo Diamond  akimtambulisha rasmi Tanasha kuwa anataka kumuoa, mimi kama dada, nitaona ni jambo la heri kwenye familia yetu ambayo kila kukicha tunamuombea apate mke bora”.

Diamond alianzisha mapenzi na binti huyo wa Kikenya Wiki chache  zilizopita  Lakini wamekwisha tangaza ndoa yao ambayo itafanyika mwezi wa pili mwakani.

“Nampenda Sana Wifi Yangu Tanasha”-Esma Platnumz

Dada wa staa wa Bongo fleva Naseeb Abdul maarufu kama Diamond Platnumz, Esma Platnumz ameibuka na kusema hana neno na wifi yake mpya Tanasha Donna Oketh.

Wiki iliyopita Diamond alimtambulisha Mpenzi Wake Mpya na mara moja kutangaza kuwa ana mpango wa Kumuoa itakapofika mwakani tarehe 14 February.

Kwenye mahojiano na Gazeti la Risasi, Esma ambaye alikuwa beneti na Tanasha alifunguka kuwa kwa upande wake alimpokea wifi yake mpya kwa mikono miwili.Esma ambaye amepachikwa jina la Yuda mitandaoni kutokana na kuwageuka warembo ambao huwa wanakuwa na Diamond kisha kupigwa kibuti alisema:

Wala sina shida, nimemkubali wifi yangu na kwa sababu Nasibu (Diamond) mwenyewe ndiye amesema anamuoa na ameridhiana naye, mimi ni nani nikatae?

Kikubwa ninawaombea heri tu asiwe kama wengine ili na mimi nipate wifi wa halali, niache uyuda”.

Mashabiki wameituhumu familia ya Diamond kwa unafiki kwani Wiki mbili tu zilizopita walionekana na Kim Nana na hata Mama Diamond alisema mume Wake anamfundisha dini ili aweze kubadilisha dini na kuolewa na Diamond.

Mama Diamond Avunja Ukimya Kuhusu Mpenzi Mpya Wa Diamond

Mama wa staa wa Bongo fleva Diamond Platnumz   Bi. Sandrah amefunguka na kumuongelea Mpenzi mpya wa Diamond anayejulikana kama Tanasha Donna Oketh mwenye ajili ya Kenya.

Wiki iliyopita Diamond alishangaza watu wengi Baada ya kutangaza ndoa na Mpenzi Wake Mpya Tanasha itakayofungwa 14 February 2019 ilihali alikuwa anadaiwa kuwa kwenye mahusiano na Kimnana.

Gazeti la Risasi Mchanganyiko linaripoti kuwa kumekuwa na taarifa za chini chini kuwa Mama Diamond hamtaki kabisa Tanasha kwa sababu alikuwa anamkubali Kim Nana ambaye alikuwa tayari kubadilisha dini na alikuwa kashaanza kufundishwa Quran tayari kwa ajili ya ndoa na Diamond.

Kwenye mahojiano na Gazeti la Risasi, Mama Diamond alianza kwa kukanusha habari kuwa alimkataa mrembo huyo na kwamba alikuwa anamtaka Kim Nana. Mama Diamond alisema anamkubali Tanasha kwa moyo mmoja wala hana kipingamizi naye na ikitokea mwanaye kweli anataka kumuoa, basi yupo radhi wala hana shida.

Sasa nimkatae amenikosea nini mtoto wa watu? Nani amesema nimemkataa mkwe wangu? Kama  mwanangu amemuona anamfaa basi nipo radhi amuoe maana umri Wake unaenda na umri wa kumuoa ndio huu”.

 

 

Diamond Atangaza Kumuoa Mrembo Kutoka Kenya

Msanii wa muziki wa Bongo fleva kutoka WCB Diamond Platnumz ametangaza kufunga ndoa na mrembo ambaye ni mwanamitindo kutoka Kenya Anayejulikana Kama Tanasha Donna Barbier.

Diamond ametangaza ndoa na mrembo huyo Kwenye mahojiano aliyofanya na Gazeti la Ijumaa ambapo Alikiri kuwa kwenye mahusiano na mrembo huyo ambaye ni mtangazaji wa Radio NRG ya jijini Mombasa nchini Kenya.

Diamond alisema kuwa, mara baada ya kuachana na mzazi mwenzake ambaye alizaa naye watoto wawili, Princess Tiffah na Prince Nillan, Zarinah Hassan ‘Zari The Boss Lady’, wasichana wengi ‘aliowatokea’ na hata Zari mwenyewe hawakulichukulia jambo la ndoa kwa uzito kama alivyofanya Tanasha.

Tanasha ndiye mwanamke pekee aliyeonesha kujali na uzito juu ya jambo hilo hivyo rasmi natangaza kumuoa huyu.

Lakini nimejiridhisha kwamba mbali na umbo na mvuto wa kipekee pia ni mwanamke mwenye tabia nzuri.”

Alipoulizwa juu ya uwepo wa Tanasha kwenye ufunguzi wa Tamasha la Wasafi Festival mjini Mtwara, Diamond alifunguka kuwa ni kweli alikuwepo, lakini watu wengi hawakumjua kutokana na usiri uliokuwepo wa kumuonesha kabla ya yeye mwenyewe kumtambulisha alipokuwa stejini.

Nitakuwa na shoo kesho nchini Kenya katika Mji wa Thika ambapo Tanasha atanitambulisha rasmi kwa wakwe zangu“.

Diamond amesisitiza kuwa Tanasha ndiye mwanamke pekee ambaye amejikuta kweli ana vigezo vyote vya kuwa mke wake pamoja nakwamba siku za Nyumba alishawahi kutangaza ndoa na maex  zake kama Zari, Wema, Penny na Jokate.