Diamond Athibitisha Kuzama Kwenye Penzi Zito na Tanasha

Staa wa muziki wa Bongo fleva na CEO wa WCB Naseeb Abdul maarufu kama Diamond Platnumz amethibitisha kuwa amezama vibaya  kwenye Penzi na Mpenzi Wake Mpya Tanasha Donna Oketh.

Diamond alitangaza kuanzisha uhusiano wa kimapenzi na mrembo kutoka Kenya Tanasha ambaye ni video vixen na Mtangazaji wa redio.

Lakini pamoja na kuwa pamoja kwa muda mfupi tu Diamond ameweka wazi ni Jinsi gani anavyomzimia  mrembo huyo kwani amekuwa akimuanika kwenye mtandao wa kijamii.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Diamond Platnumz ameweka video yake na Tanasha inayomuonyesha akimtengeneza nywele Mpenzi Wake huyo na kuweka wazi Jinsi anavyomzimia.

Basi na Mie nikiingiaga kwenye mapenzi nazama mzima mzima kama boya….Matokeo yake nikizinguliwa naanza kutoa Povu…”.

https://www.instagram.com/p/BrsWX0MFzNh/?utm_source=ig_share_sheet&igshid=1t7cbpa4u9y9e

Tanasha Awatumia Ujumbe Huu Maadui Zake

Mpenzi wa staa wa Bongo fleva Diamond Platnumz, Tanasha Donna Oketh mrembo kutoka Kenya ameibuka na kuwatolea Povu zito watu ambao wamekuwa wakimfanyia ubaya.

Tangu Diamond na Tanasha waweke wazi mahusiano yao wiki chache zilizopita mrembo huyo amekuwa akilalamika na watu ambao wamekuwa wakimponda  kila kukicha.

Wiki iliyopita tu Tanasha aliwatolea Povu zito watu ambao walikuwa wanamponda shepu yake na kudai ana shepu mbaya na miguu mibaya ambapo alisema hata Kama mbaya ndio hivyo Diamond ameshampenda na atamuoa.

Siku ya jana tena Tanasha aliwatolea Povu mashabiki wa Instagram ambapo aliwatumia ujumbe wabaya wake kuwataka kuwa wavumilivu kwani kuna mengi makubwa anakuja nayo ambayo yatazidi kuwakera.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Tanasha aliandika:

Tanasha Avunja Ukimya Kuhusu Kupambanishwa na Zari

Mpenzi mpya wa staa wa Bongo fleva Diamond Platnumz, Tanasha Donna Oketh mrembo kutoka Kenya amefunguka kuhusu kupambanishwa na Baby mama wa Mpenzi Wake Zari The Bosslady.

Tangu Diamond aweke hadharani kuwa ana mahusiano ya kimapenzi na Tanasha Baada ya kuachana na Zari kumekuwa na mgongano katika ya timu hizo mbili za ushabiki wa Zari na Tanasha.

Lakini Tanasha ameibuka na kuzima tetesi zote za kuwepo na Bifu kati yake na Zari na kuweka wazi kuwa yeye una tatizo binafsi na mwanamama huyo na kuwataka watu wasiwachokonoe.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Shabiki mmoja alimuuliza Tanasha kama anamfahamu Zari na yeye moja kwa moja alijibu:

Hapana simfahamu Zari lakini naamini ni mama wa Watoto wawili ambaye ni mchapakazi na watu tafadhali was he kutupambanisha na kuanza kututengenezea maugomvi yasiyokuwa na maana badala yake watuinue wote kwa pamoja”.

 

“Diamond Ruksa Amuoe Tanasha”- Lynn

Video vixen na msanii wa muziki wa Bongo fleva Irene Godfrey Louis amefunguka na kumpa baraka zote aliyekuwa mpenzi wake Staa wa Bongo fleva Diamond Platnumz  kumuoa Mpenzi wake mpya Tanasha Donna Oketh.

Kwenye mahojiano aliyofanya na  Global PublishersLynn ambaye aliwahi kutajwa kuwa mbioni kuolewa na Diamond alisema anawashangaa wanaosema anaumia juu ya kitendo cha Diamond kutangaza kumuoa Tanasha, jambo ambalo si kweli.

Sina kinyongo, Diamond amuoe Tanasha hata kesho maana ni jambo la heri. Ninafurahi sana kwa sababu Diamond ni mshkaji wangu sana na si vinginevyo”.

Diamond aliweka wazi mahusiano yake na mrembo Tanasha kutoka Kenya na kutangaza ndoa yao mara moja hali iliyopelekea taarifa kusambaa kuwa Lynn amemwaga na msanii huyo aliyekuwa kwenye mahusiano naye.

“Tanasha Ndiye Mwanamke Pekee Mwenye Sifa Za Kuoa”- Diamond Platnumz

Msanii wa muziki wa Bongo fleva nchini na Mkurugenzi wa WCB Diamond Platnumz ameibukana na kumwagia sifa lukuki Mpenzi Wake Tanasha Donna Oketh mwenye asili ya Kenya.

Diamond ameonekana kuzidi kunogewa na Penzi la Tanasha kwani amedai kuwa yuko tofauti na wanawake wote aliowahi kuwa nao hapo nyuma na kudai yeye ni ‘Wife material zaidi’.

Zikiwa ni Wiki mbili tu zimepita tangu Diamond atangaze rasmi ndoa na Tanasha Diamond anaonekana hakuwa na masihara kuhusu jambo hilo kwani kwenye interview yake na kituo kimoja cha habari nchini Kenya Diamond alisema haya:

Tanasha ndiye mwanamke pekee aliyeonesha kujali na uzito juu ya jambo hilo hivyo rasmi natangaza kumuoa huyu. Ana sifa zote za mwanamke wa kuoa, lakini unajua sisi wanaume wengi huwa tunaangalia sura, umbo na vingine vya mwilini kisha ndiyo inafuata tabia. Lakini nimejiridhisha kwamba mbali na umbo na mvuto wa kipekee pia ni mwanamke mwenye tabia nzuri”.