Babu Tale- Sijaenda South Africa Kurudisha Penzi la Diamond na Zari

Meneja wa staa wa Bongo fleva Diamond Platnumz, Babu Tale amefunguka na kudai hakuenda nchini South Africa Kurudisha Penzi la Diamond na Zari.

Wikiendi iliyopita habari ya mjini ilikuwa Zari na Diamond baada ya video ya wimbo wa iyena kutoka ukiwaonyesha wawili wakifunga ndoa mwaka jana wakati bado wapenzi.

Babu Tale alitengeneza headlines baada ya kutangaza anaenda nchini South Africa kwa ajili ya kwenda Kurudisha Penzi la Diamond na Zari baada ya kutengana kwa zaidi ya Miezi minne sasa.

Lakini baada ya kufika nchini humo ambako ndipo Zari anaishi na watoto wake Babu Tale ameweka wazi kuwa hajaenda Kurudisha Penzi lao bali ameenda kuwapatanisha wawili hao ili waweze kulea watoto wao.

Kwenye mahojiano na Wasafi Tv, Babu Tale amesema ameona ni vyema wawili hao wakaelewana kwa manufaa ya watoto wao:

Kilichonileta  huku ni kuwasuluhisha matatizo yao wayaweke pembeni ili waweze kulea watoto wao, of course nimeongea sana na Zari nikamwambia kama mnataka kurudiana kimapenzi it’s up to you lakini mimi ningependa kuona wewe na Diamond mnapatana ili  watoto waweze kuwa karibu na nyinyi na ikitokea tupo South Africa ni rahisi kupita kusalimia watoto na kama watoto wamemiss Baba unampigia simu”.

Diamond na Zari wamekuwa na uadui fulani tangu wawili hao walipoachana Miezi michache iliyopita ambapo Zari alimtuhumu Diamond kwa kutowaona watoto wake kwa miezi mitano kutokana na wao kukosa maelewano.

Wema Sepetu Yupo Tayari Kushuhudia Ndoa Ya Diamond na Zari

Muigizaji wa Bongo movie Wema Sepetu ameshangaza watu wengi baada ya kufunguka kuwa anatamani a Ex wake Diamond Platnumz na Baby mama wake Zarinah Hassan wafunge Ndoa.

Wema alifunguka hayo baada ya video ya wimbo wa Iyena wa Diamond kutoka siku ya Ijumaa ambapo ndani yake yupo Zari kama video queen ambapo ndani ya video hiyo wanafunga ndoa.

Wema alimtaka Diamond kufanya kweli na kumuoa mama watoto wake huyo ambapo aliandika maneno haya Kupitia ukurasa wake wa Instagram:

New Track Alert Ila kama ingekuwa Pambe ingekuwa Kweli. Just thinking out Loud, Diamond Chibudeeee Fanya kweli bwana. Inshallah mwaka huu hata mwakani. Tuje kucheza Baikoko sie, Rayvanny Kazi nzuri”.

Hili suala limewaacha watu vinywa wazi kidogo k sababu hasa ukiangalia kuwa Zari aliweka wazi kuwa alimtosa Diamond baada ya video kusambaa zilizomuonyesha Diamond na Wema wakikumbatiana Kwenye kumbi za starehe Miezi minne iliyopita.

“Naenda South Africa Kama Kazi Hawezi Kunikataza Mtu”- Mama Diamond

Mama mzazi wa msanii wa Bongo fleva Diamond Platnumz, Bi. Sandra ametoa povu zito na kusema anaweza kwenda South Africa muda wowote akitaka kwenda kuwaona wajukuu zake na hawezi kukatazwa na mtu.

Mapema mwaka huu Zari the Bosslady alimpiga kibuti cha maana aliyekuwa mpenzi wake na  Baba watoto wake supastaa wa Bongo fleva Diamond siku ya Valentine’s baada ya kuchoshwa na tabia zake za kupenda michepuko.

Baada ya kuachana Diamond alienda South Africa kwa ajili ya maandalizi ya Albamu yake lakini cha ajabu ni kwamba hakufika kwenye nyumba aliyonunua aliyokuwa anaishi na Zari na watoto na Tena hakufika hata kwenda kuwaangalia watoto wake.

Baada ya sakata hilo kutokea habari zilianza kusikika kuwa Diamond na familia yake na mama yake mzazi hawatakaribishwa tena kwenye nyumba ya South Africa hasa kwa sababu wamejenga ukaribu na adui namba moja wa Zari, Wema Sepetu.

Siku ya jana Bi. Sandra alitoleana povu na shabiki baada ya kumuuliza kwanini hapendi kumposti mjukuu wake wa Hamisa au anamuogopa Zari kwa sababu hataruhusiwa tena kwenda South Africa kuwaona wajukuu wake? Basi bwana povu la Mama Diamond lilikuwa hivi:

South Africa naenda kama kazi kwa taarifa yako na siwezi kukatazwa na mtu yoyote”.

Zari alishasema Kwenye Interview aliyofanya na BBC Swahili kuwa hana tatizo na familia ya Diamond kwani muda wowote wakitaka kuona watoto wao wanakaribishwa hata Diamond akitaka kuona wanaye.

“Sitaki Kusikia Kuhusu Diamond Wala Mama Yake”. Amesisitiza Zari Kuwa Amemuacha Diamond Kweli Sio Kiki

Zari amerudi tena Kwenye headlines za mitandao ya kijamii baada ya kutoa povu zito baada kuulizwa kuhusu uhusiano wake na Baba watoto wake Diamond Platnumz.

Uhusiano wa Zari na Diamond umekuwa gumzo kila kona tangu wiki iliyopita siku ya Valentine’s ambapo Zari alitangaza kuwa amemuacha Diamond kwa sababu ya kuendekeza michepuko.

Siku ya jana kupitia Instalive ya Instagram Zari alitoa povu kali pale alipoulizwa swali kuhusu Diamond na shabiki wake.

Zari alizungumza haya kuhusu Diamond na familia yake:

Kuna mtu kaniuliza kuwa kosa gani la mwisho ambalo Diamond alikufanyia mpaka ukaamua kumuacha? Naomba niseme mara ya mwisho kuanzia sahivi huu ukurasa ni wangu na nitaongelea kuhusu mambo yangu binafsi yaani mambo ya Zari haihusiani na Diamond wala Mama yake wala sitaongelea alichokifanya au wanawake wake malaya wake waliochoka hapana kwaiyo hapa mnaniongelea mimi na watoto wangu”.

Lakini pia Zari amefunguka na kusisitiza ni kweli amemuacha Diamond na taarifa zote kuwa ni Kiki zinazoendelea kusambaa mtandaoni sio za kweli.

Mange Kimambi: Diamond Ndio Alimuacha Zari

Tangu jana stori kubwa inayotawala kwenye mitandao ya kijamii ni kuvunjika kwa mahusiano ya Supastaa wa Bongo fleva na President wa WCB, Diamond Platnumz na mama watoto wake Mfanyabiashara Zari The Bosslady.

Siku ya Wapendanao Zari alitumia ukurasa wake wa Instagram kujulisha mashabiki zake kuwa yeye na Diamond wameachana lakini kikubwa zaidi alichoweka wazi Zari ni kuwa sio tu yeye na Diamond hawako wote bali yeye ndio amemwacha Diamond sababu ya kuchepuka ambapo aliandika:

There have been multiple rumors some with evidence floating around in all sorts of media in regards to Diamond constant cheating and sadly I have decided to end my relationship with Diamond..”.

Zari amejaribu kuweka wazi ijulikane wazi kabisa na  umma kuwa yeye ndio aliyemuacha Diamond kitu ambacho Mange ameibuka na kudai kuwa sio kweli na kudai Diamond ndio alikuwa wa kwanza kumuacha Zari kwa sababu alikuwa ameshamchoka.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram Mange aliandika maneno haya akimtuhumu Zari kwa kudanganya:

No no no honey, you didn’t leave Diamond, Diamond ndio alikuacha, mara ngapi Dogo alikuwa anakuonyesha kuwa hakutaki wewe ndio ulikuwa unamng’ang’ania? Ulivhotakiwa kusema leo ni kwamba umekubaliana na hali halisi kuwa dogo hatokaa kutulia kwa ajili yako. Wewe usituchezee akili eti umemuacha. Nyambaafu ulijua kuzaa fasta ndio kumkamata mwanaume! Umenyooooshwa”.

 

Zari Amefunguka Mazito Kuhusu Usaliti Wa Diamond , Adai Kilichomkera Yeye Kulala na Hamisa Kitandani Kwao Bila Kinga

Mfanyabiashara maarufu na mama watoto wa Diamond Platnumz, Zari the Boss lady amefunguka kuhusiana matatizo waliyopitia yeye na mpenzi wake Nasibu Abdul ‘Diamond’ miezi michache iliyopita baada ya Diamond kuzaa na Hamisa.

Miezi michache iliyopita habari hii ilienea kama moto wa kifuu na kusababisha tafrani kwenye mitandao ya kijamii pale Diamond alipoebda Clouds Fm na kukiri kuzaa na Hamisa na kumsaliti mpenzi wake Zari aliyezaa naye watoto wawili.

Baada ya sakata hilo Diamond na Zari walisameheana na kurudiana lakini tangu siku ile Zari hajawahi kuongelea ishu hiyo wala kueleza chochote kuhusu alivyojisikia mpaka juzi alipofanya mahojiano nchini Uganda.

Zari yupo nchini Uganda sasa hivi akijiandaa na tamasha lake analofanyaga la Zari All White Party litakalofanyika tarehe 21 nchini Uganda. Katika jitihada za kuitangaza shughuli hiyo anaputa kufanya interview na vituo mbali mbali vya redio.

Kwenye interview aliyofanya na ‘Celeb select’ Zari alifunguka mengi kuhusu uhusiano wake Diamond moja kati ya vitu alivyoongelea ni Diamond kuzaa na Hamisa na kumsaliti:

Diamond kutembea na kuzaa na mwanamke mwingine ni usaliti mkubwa sijapata kuona na kwa muda mrefu nilifikiri sitakuja kukaa na kuiongelea hii ishu lakini kwa kuwa ilishapita na nimeshapata amani kwaiyo haina shida. Unajua wanaume wengi wana-cheat lakini mimi kilichonitatiza ni kwa nini ulete mwanamke wako kitandani kwetu tunakolala wote? Kwanini utembee na mwanamke ambaye haeleweki wala hana thamani? Alafu kikubwa kwa nini haukuvaa kondomu na unajua kabisa tuna watoto wadogo na unaweza kupata ukimwi? Kusema kweli nilimuuliza maswali mengi na majibu yake yakawa na visingizio kibao mara ooh unajua wewe uko mbali ikatokea Bahati mbaya akabeba ujauzito wangu, nikasema sawa kwanini sasa ulimleta kitandani kwetu? Akasema unajua mimi ni maarufu sana ningeenda hotelini watu wangeniona kwaiyo inabidi aje usiku sana na kuondoka asubuhi sana ili watu wasimuone”.

Lakini Zari amesisitiza kuwa hawezi kumkataza Diamond kumuona mtoto wake aliyezaa na Hamisa kwani mtoto hana kosa lolote ni malaika tu. Pia amesema yeye na Diamond wako vizuri na amebadilika sana.

Hili Ndio Jambo Diamond na Zari Watafanya Kwaajili ya Birthday ya Mtoto Wao Nillan (picha)

Superstaa Diamond Platnumz na mpenzi wake Zarinah Hassan ‘Zari’ siku ya Leo wanasherekea sherehe ya kuzaliwa kwa mtoto wao wa kiume Prince Nillan Abdul anayefikisha mwaka mmoja.

Diamond kupitia ukurasa wake wa Instagram amefunguka kuhusu mpango wake wa kwenda nchini Uingereza ambapo atakuwa na shoo mji wa London ambapo ameeleza nia yake ya kwenda kufanya sherehe upya nchini humo kwenye steji atakapo kuwa anapafomu kama wafanyavyo mastaa wengi nchini Marekani.

Poppin belaire for my son Prince Nillan first years birthday and I am thinking with Prince Nillan in London so that we can re-celebrate his birthday again live during my performance out there #Nillansbirthday #Selfmade #AboyFromTandale”.

Zari na yeye amefunguka na kumtakia mwanae birthday njema huku akimsifia kuwa anakua haraka na kudai kuwa anazidi kuwa handsome na kuwatahadharisha watu jinsi atakavyo vunja mioyo ya wadada akiwa mkubwa kwa uzuri wake.

Ladies and gentlemen help me wish my hanshaaaam skwiiiiish a happy birthday you surely are growing up fast, I see you breaking up girls hearts soon because this cuteness is overload! Happy birthday my toto Prince Nillan”.

Hizi ni baadhi ya picha za baby Nillan kwa ajili ya birthday yake :

 

 

 

Tazama Picha na Video za Diamond na Zari Kwenye Mahaba Mazito Wiki Moja Baada ya Kumuita ‘Player’

Mwanamuziki machachari wa Bongo fleva nchini Diamond Platnumz anayetamba na vibao vyake alivyovitoa kwa mpigo redio amerudi katika vichwa vya habari na mpenzi wake mrembo azarinah Hassan.

Wiki iliyopita Zari ambaye makazi yake yapo nchini South Africa alitumia mtandao wa Snapchat kumpiga madongo baba watoto wake Diamond kwa kumuita player ‘kicheche’ kwa vitendo vya kuchepuka na wanawake wengine jambo lililofanya wengi waamini kuwa wapendanao hao wameachana.

Wikiendi iliyopita Zari alionekana kakanyaga ardhi ya Tanzania na moja kwa moja picha za wawili hao zilianza kusambaa zikiwaonyesha wakiwa katika mahaba mazito hasa pale waliposimamia harusi ya kaka yake  na Diamond, Rommy Jones na Kay.

Hizi ni baadhi ya picha zikiwaonyesha Diamond na Zari katika mahaba mazito:

 

 

 

 

 

 

 

 

Angalia Diamond Akijiachia Pamoja na Familia Yake

Mwanamuziki anayefanya vizuri kwenye ulimwengu wa Bongo fleva, Diamond Platnumz yupo nchini South Africa kwa ajili ya kuitembelea familia yake.

Diamond na mpenzi wake Zari ambao wamepitia kipindi kigumu kidogo miezi michache iliyopita baada ya Diamond kuzaa na Hamisa na skendo zisizoisha kila siku za yeye kutembea na wanawake wengine kibao.

Lakini Zari hakumuacha Diamond kwa ajili ya mapungufu yake alikubali kumsamehe na hivi sasa wako wote na furaha tele.

Siku ya Jumatano Diamond alisafiri kuelekea nchini South Africa kwa ajili ya kumsalimia Zari na watoto wao Prince Nillan na Princess Latifah, naomba niseme picha walizoweka mtandaoni zilikuwa nzuri na zilionyesha uhusiano mzuri alionao Diamond na watoto wake hasa Tifah. Baadhi ya picha hizo ni hizi;

Diamond na binti yake Tiffah.
Diamond na watoto wake Nillan na Tiffah.
Diamond, Zari na Watoto wao.
Diamond akicheza na watoto wake.

Diamond ameonekana akifurahi kuwa na familia yake lakini watu wengi wanajiuliza mbona hafanyi vitu hivyo na mtoto wake aliyezaa na Hamisa? Ingawa mpaka Leo haijajulikana nini hatma ya ile kesi waliyoipeleka mahakamani.

Tazama video inayowanyesha jinsi Diamond, Zari na watoto wanavyofurahi:

Diamond ameelekea South Africa kuisalimia familia yake lakini pia ameenda kutengeneza video kwani ameambatana na msanii mwenzake kutoka Wasafi, Rayvanny.

Diamond Aongelea Jinsi Alivyombembeleza Zari Asimuache

Mwanamuziki Diamond Platnumz amekuwa msanii aliyeshika vichwa vya habari kwa takribani miezi miwili mfululizo kuanzia skendo yake ya kuzaa na Hamisa mpaka kuachana na Zari na mengine Mengi yaliyozuka hivi kati.

Diamond aliongelea uhusiano wake na Zari alipokuwa jukwaani siku ya Jumamosi alipopiga shoo kwenye uwanja wa Amani, Zanzibar ambapo Diamond alisema:

Unajua hapa katikati palitokea mambo mambo mengi, shetani akaingia kati mara maneno ooh hivi na vile ebwana mambo yakawa mengi kweli unajua, nikaona enhee mtoto wa kiganda kacharuka, nikiangalia kushoto na kulia nikawa naona kabisa kama jiko nakaribia kulikosa moja kwa moja nikapanda ndege nikaenda mpaka Sauzi, kufika sauzi kabla hata sijaongea moja kwa moja mpaka chumbani kule tulifanya vitu vingi sana nikajua mambo yatakuwa yameisha, hee mambo yakaendelea nafika tu Tanzania yakazuka mengine, akanitupia dongo kwenye Instagram nikapiga simu takribani saa zima nabembeleza baby anisamehe nikamwambia baby sikia hivi vitu vinatokea mi nimeteleza nikamuimbisha mtoto mgumu hataki kusikia mpaka ilivyonijia nyimbo kwenye kichwa nikamwimbia mtoto ndo ameelewa”.

Pamoja na yote yaliyotokea baina yao Diamond amekiri kuwa Zari kamsamehe na wamerudiana na wanataka kuendelea kulea watoto wao na kutengeneza pesa.