Diamond Kuwakutanisha Wema na Zari Nchini South Africa

Ikiwa siku zinakaribia kuelekea birthday party ya mtoto wa staa wa Bongo fleva Diamond Platnumz na Bosslady Zarinah Hassan, Diamond anatarajiwa kuwakutanisha Zari na Wema nchini Afrika ya Kusini.

Diamond Kupitia uongozi wa label yake ya WCB imetangaza kusafiri na Wema Sepetu ambaye ametajwa kuwa mmoja wa wanakamati wa birthday party ya Tiffah Dangote.

WCB wamesema wataisafirisha kamati hiyo kwa kuwa wameipenda na wanaona ni jambo zuri kwenda kushiriki nao kwenye shughuli hiyo. Mastaa wengine ambao wanaunda kamati hiyo ni Shamsa Ford, Shilole, Irene Paul, Irene Uwoya, Lamata, Kajala Masanja pamoja na wengine wengi.

Wema pamoja na wanakamati wengine ambao siku ya jana walikuwa wanakamati katika arobaini ya mtoto wa Zamaradi wamepokea mualiko huo uliowasilishwa na Meneja wa Diamond Babu Tale.

Diamond ameitaja Birthday party ya Tiffah  kama  sherehe ya mwaka ambapo pia amehaidi kuwalipia mashabiki kadhaa kwa ajili ya kwenda kuhudhuria.

Kifesi Adai Diamond Amepoteza Kitu Cha Thamani Maishani Kwa Kumpoteza Zari

Aliyekuwa mpiga picha wa staa wa Bongo fleva na CEO wa WCB Diamond Platnumz, Kifesi amevunja ukimya na kufunguka kuhusu kuvunjika kwa Penzi la Diamond na Zari.

Kifesi aliacha kazi WCB Miezi michache iliyopita lakini ilisemekana kuwa amefukuzwa kazi na Diamond baada ya kuingilia kati Penzi la Diamond na Zari.

Kwenye mahojiano na Bongo 5, Kifesi amefunguka na kuweka wazi kuwa Diamond amefanya makosa kuachana na Zari kwa sababu ni mwanamke anayejielewa sana.

Mimi naamini Diamond amefanya makosa sana kuachana na Zari kwa sababu Mwanaume yoyote mwenye akili na Basara atamuona Zari kama aina ya mwanamke ambaye anatamani awe naye kujenga maisha na kujenga familia.

Kwaiyo Diamond atakuwa ni wa ajabu kama akisema eti hajapoteza kitu cha thamani kwa kumpoteza Zari nitamshangaa halafu hata yeye anaelewa umuhimu wake ukilinganisha na wanawake ambao ameshawahi kuwa nao na hata alionao huwezi ukawalinganisha na Zari”.

Kifesi pia amekiri kuwa hana mawasiliano yoyote na Diamond tangu aache kazi WCB Miezi michache iliyopita lakini bado ana ukaribu na urafiki na Zari na anaongea naye kila siku.

Kifesi-Tangu Nimeacha Kazi WCB Diamond Hajawahi Kunitafuta

Aliyekuwa mpiga picha wa Staa wa Bongo fleva Diamond Platnumz, Kifesi amefunguka na kudai tangu ameacha kazi WCB, Diamond hajawahi kutafuta zaidi alim-block Instagram.

Miezi michache iliyopita Kifesi alitangaza kuwa anaacha kazi WCB baada ya kufanya kazi kwa muda mrefu ambapo alidai sababu kubwa ilikuwa ni kutaka kufungua biashara zake na kujikita Kwenye mambo yake kidini.

Baadae kuna taarifa zilisambaa kuwa Kifesi hajaacha kazi WCB bali alifukuzwa kazi na Diamond  kwa utovu wa nidhamu baada ya kudaiwa kuingilia mapenzi ya bosi wake (Diamond na Zari).

Kwenye mahojiano aliyofanya na Bongo 5, Kifesi amefunguka na kuweka wazi kuwa tangu ameacha kazi WCB, Hajawahi kuwasiliana na Diamond na pia kukiri kuwa Diamond amemblock Instagram.

Lakini pia Kifesi amesema yeye binafsi hana beef na Diamond na hawezi kuongelea mabaya yake kwa sababu tu hayupo naye karibu na kudai yeye ni mtu mwaminifu na anampenda Diamond kama shabiki.

Kwenye Interview hiyo Kifesi aliongelea Tetesi za yeye kufukuzwa kazi ambapo amedai kama kweli angekuwa amefukuzwa basi watu wangemuona amempigia magoti Diamond amrudishe kazini na kama haitoshi angemtumia Zari ambaye amekiri Diamond hapindui kwa Zari.

Kifesi ameongelea biashara zake mpya ambapo amefungua studio ya upigaji picha na yupo mbioni kuanza kipindi chake cha mapenzi redioni lakini pia anafungua kampuni yake ya kuuza chakula.

Diamond Awajia Juu Wanaomuita Shoga Kisa Kuvaa Kikuku

Staa wa Muziki wa Bongo fleva Diamond Platnumz amemwaga povu zito na kuwajia juu watu wote wanaomkosoa na kumuita shoga baada ya kuonekana akiwa amevaa kikuku.

Wiki iliyopita Kuna picha zilisambaa Kwenye mitandao ya kijamii zilizomuonyesha Msanii huyo akiwa amevaa Kikuu Kwenye miguu yake, skendo ambayo ilikamata vilivyo hasa kwenye mitandao ya kijamii na kumjengea picha tofauti kwa ajili mashabiki wake.

Baadhi ya mashabiki hao kwenye mitandao hiyo walikasirishwa na kitendo hicho hivyo kummwagia matusi ya nguoni kutokana na kuchukizwa na kitendo hicho. Hoja kuu kutoka kwa mashabiki hao ilikuwa kwamba, jambo hilo haliendani na utamaduni wa Kitanzania na kwamba wanaofanya hivyo ni mashoga na lengo lake ni kuharibu vijana wadogo wa Kitanzania.

Baada ya povu hilo la mashabiki, Global Publishers lilimsaka Diamond ili Kupata kumfikia anajiteteaje juu ya skendo hiyo ya ushoga:

Kwanza sijui kama kile ni kikuku, nilivaa kama ninavyovaa mikufu au cheni. Niliona ni urembo kama urembo mwingine na kwamba haiwezi kuwa ishu kubwa kama ilivyotokea”.

Diamond aliwakemea wanaomuita Shoga na kuwataka waache mara moja kwani yeye mwenyewe anachukizwa na tabia za mashoga:

Ninawaomba chondechonde waache kunihusisha na jambo hilo baya, ujue nyuma yangu kuna watu wengi mno wanatamani kuwa kama mimi hasa vijana wadogo.

Sasa wakiona ninahusishwa na jambo ambalo linapigwa vita nchini mwetu, wataacha kunifuatilia kama mtu wanayetamani kuwa kama yeye, alisema Diamond na kuongeza: Lakini unajua imekuwa ni kasumba kwa watu maarufu kuhusishwa na jambo hilo ili kuwajengea picha fulani kwa mashabikia”.

 

Wema Sepetu na Diamond Platnumz Wang’ara Tuzo Za Kimataifa

Staa wa muziki wa Bongo fleva Diamond Platnumz na Muigizaji wa Bongo movie Wema Sepetu wamezidi kuipeperusha Bendera ya taifa baada ya kuchaguliwa kuwania tuzo za IARA Awards.

Wema Sepetu ambaye tayari ni Muigizaji bora wa kike katika tuzo za SZIFF amefanikiwa kuchaguliwa kuwania tuzo za International Achievement Recognition Awards (IARA) Kupitia Movie yake ya Heaven Sent.

Wema amechagulia kushindana katika kipengele cha Best International Actress huku akichuana na wasanii wengine wanne kutoka Africa ambao ni Joselyn Dumas kutoka Ghana, Amal Bouchoucha kutoka Algeria, Omotola Jalade kutoka Nigeria, Pearl Thusi kutoka South Africa na Tatiana Manslay kutoka Canada.

Kupitia page yake ya instagram Wema ameshukuru kwa kuweza kupata nafasi hiyo na kuwapa ujumbe mashabiki zake waendelee kumpigia kura kwa wingi  ili aweze kubeba tuzo hiyo:

And We are Nominated again…. Heaven Sent is still going places my loves…let’s keep on voting nawapenda nawajua Kwenye sekta ya kupiga kura tupo vizuri, tuseme INshalllah”.

Lakini pia Staa wa Bongo fleva Diamond Platnumz amekuwa nominated katika kipengele cha Best Male  International Artist huku akiwa anachuana na wasanii kama vile Davido, MOhamed Abbas, LA Foune, Mr. P, Medikal, Black Coffee pamoja na Casper nyovest.

Joh Makini Adai Haoni Tatizo Kwa Wasanii Wa Kiume Kuvaa Vikuku

Msanii wa muziki wa Bongo fleva anayetamba kwa staili ya kuchana kutoka katika kundi la Weusi Joh Makini au Mwamba wa kaskazini amedai haoni tatizo kwa wasanii wa kiume kuvaa vikuku kama wanataka kufanya hivyo.

Joh Makini wameweka wazi kuwa wasanii wa kiume kuvaa vikuku miguuni sio kitu cha ajabu kama watu wengi wanavyodhani kwani anaamini ni fasheni kama fasheni nyingine.

Kwenye mahojiano na Bongo 5, amesema kuwa wasanii ni watu ambao wanaishi na fasheni na style mbalimbali hivyo msanii kuvaa kikuku ni maamuzi yake na yeye anachukulia kawaida kabisa suala hilo;

Sijui kesho lakini mimi nachukulia kama style yake kama mimi nilivyoamua kuweka Rasta kuna wengine wameamua kuvaa vikuku wengine kutoboa pia na masikio lakini Sioni tatizo lolote kama mtu ameamua kuchagua aina ya maisha anayoishi”.

Wiki iliyopita msanii  wa muziki Diamond Platnumz aliposti picha kwenye ukurasa wake wa Instagram akionekana mguuni akiwa amevalia cheni maarufu kwa jina la kikuku jambo ambalo lilisababisha ashambuliwe na mashabiki wake mitandaoni.

Amber Lulu Aomba Msaada WCB na Kumtupia Dongo Diamond

Video Vixen na Msanii maarufu wa muziki wa Bongo fleva Amber Lulu amezua gumzo kwenye mtandao wa Instagram baada ya kumtupia Dongo staa wa Bongo fleva Diamond Platnumz.

Siku chache zilizopita Diamond alizua gumzo baada ya kuposti picha akiwa amevaa cheni ya mguuni ‘kikuku’ ambacho kimezoeleka kuonekana kimevaliwa na wanawake.

Amber Lulu aliposti picha ya Diamond akiwa amevaa kikuku na kuomba nafasi ya kusainiwa ndani ya WCB lakini alisindikiza na maneno ya kejeli kuhusu kuvaa kikuku.

Amber alitumia picha hiyo kumuomba Diamond kumpa nafasi ya kuwa Bosi wake na kumuomba ampe mkataba wa kuwa mmoja kati ya wasanii walio chini ya lebo ya Wasafi Classic Baby (WCB)

https://www.instagram.com/p/BlQ6eHthODV/?utm_source=ig_share_sheet&igshid=1isnpb8nfnavt

Diamond ni CEO wa WCB na katika label hiyo kuna wasanii kadhaa wa kiume lakini kuna msanii mmoja tu wa kike ambaye nidada yake na Diamond, Queen Darleen kwaiyo itakuwa ni vema kupata msanii mwingine wa kike ingawa Diamond

Sheikh Kipozeo Amwaga Povu Baada Ya Diamond Kuonekana Kavaa Kikuku

Sheikh Kipozeo ambaye amekuwa akitoa mawaidha katika mambo ya maadili, amefunguka ishu ya wanaume kuvaa cheni miguu ambapo amedai wanaume wanaojifanisha na wanawake kwa kuvaa cheni wamelaaniwa na Mwenyezi Mungu.

Wikiend iliyopita Diamond alizua gumzo Kwenye mitandao ya kijamii baada ya kuonekana akiwa amevaa cheni ya mguuni ‘kikuku’ ambacho mara nyingi kinavaliwa na wanawake.

Kwenye mahojiano na Bongo 5, Sheikh Kipozeo amefunguka na kusema sio kwa Diamond tu wanaume hawaruhusiwi kuvaa vitu ambavyo vinavaliwa na wanawake.

Mwanaume harusiwi kuvaa cheni halafu sio miguuni tu hata shingoni haruhusiwi kwa sababu cheni ni pambo la kike na Mungu amewalaani wanaume wanaojifananisha na wanawake na wanawake wanaojifanisha na wanaume.

Mtu yoyote tu mwanaume sio Diamond peke yake atakayevaa vazi la kike basi atalaaniwa na Mwenyezi Mungu”.

Kwa maadili ya Kiafrika cheni ya mguu yaani kikuku kimekuwa kikivaliwa na wanawake lakini kwa nchi za wenzetu ni jambo la kawaida kwa wanaume kuvaa wasanii wakubwa kama Chris Brown wameonekana wamevaa vikuku.

Shigongo Adai Diamond Hawezi Kuwa Staa Milele

Mkurugenzi wa Global Publishers na mwandishi maarufu wa vitani Erick Shigongo ameibuka na kudai kuwa staa wa muziki wa Bongo fleva Diamond Platnumz hawezi kukaa kwenye chati kwa muda mrefu.

Shigongo ameweka wazi kuwa katika sanaa kuna kubadilishana nafasi kwaiyo pamoja na kwamba Diamond yuko juu kwa sasa lakini atakuja kuondoka na wataakaa wasanii wengine.

Kauli hiyo ya Shigongo ilikuja baada ya kuulizwa swali wakati akifanya mahojiano na Global TV Online iwapo alishawahi kumsaidia jambo lolote Diamond kwani staa huyo amemtaja Shigongo kama mmoja wa ‘role model’ (mtu aliyempa hamasa ya mafanikio) wake.

Sikumbuki kama nilishawahi kumsaidia, watu wananiambia lakini mimi sina kumbukumbu, labda kuandikwa magazetini kwa ajili ya promosheni za kazi zake za muziki, pengine kutokana na nasaha zangu ambazo huwa nazitoa kuwashauri Watanzania wenzangu na kuwapa mbinu za kujikwamua kwenye umaskini.

Ninachoweza kumwambia tu ni kwamba apambane.  Unajua ukifanikiwa unapata marafiki wengi, na wengi wao wanakuwa wanataka pesa zako au cheo chako, siku pesa zikiisha hutowaona tena. Ametoka kwenye umaskini, asisahau alikotoka.

Walikuwepo akina Mohamed Ali, wakaondoka, wakaja kina Tyson, wakaondoka, sasa hivi yupo Maywether, ataondoka atakuja mwingine. Mimi nipo, nitaondoka.   Je, nikiondoka watoto wangu wataendelea kula chakula kilekile? Watasoma shule zilezile? Lakini pia tulikuwa nao akina Mr. Nice, waliondoka, sasa hivi yupo Diamond, itafika wakati ataondoka, watakuja wengine, hatakuwa championi milele.

Ninachoweza kumwambia ni kwamba  awekeze kwa ajili ya baadaye, ukiwapelekea watu chakula sehemu uliyotoka, Tandale,  watasema unatafuta kiki, ukila peke yako Madale watasema huyu jamaa mbinafsi, mimi namshauri asisikilize watu wanasema nini, aendelee kupambana hadi mwisho”.

Zari Ampa Pole Hamisa Baada Ya Kukanwa na Diamond Hadharani

Zarinah Hassan ‘Zari’ amerudi Kwenye headlines tena baada ya kumuandikia ujumbe adui yake namba moja Hamisa Mobetto baada ya kukanwa na Diamond hadharani.

Sakata hilo lilianza siku ya leo baada ya Diamond kuachia video yake mpya ya wimbo wake wa ‘Baila’ ambapo aliposti Kwenye ukurasa wake wa Instagram na kuandika kuwa hajapata mwanamke wa kuwa naye lakini siku akimpata atamsikilizisha Baila:

Kwa machache niliyojifunza Kwenye Mahusiano nilisema siku nikikutana na mwanamke mpya nitakayetaka kuwa naye kabla ya kuianza Safari sitamwambia neno bali nitamuwekea huu wimbo wa Baila”.

Baada ya Diamond kuweka wazi kuwa hayupo kwenye mahusiano moja kwa moja Zari alianza kumnanga Hamisa na kumpa pole baada ya kukataliwa na mwanaume ambaye amekuwa akijitangaza kuwa Kwenye Mahusiano naye.

Kwenye ukurasa wake wa Snapchat Zari aliandika maneno ambayo directly alikuwa anampiga vijembe Hamisa na kumcheka kuwa amekaa Kwenye Mahusiano na mwanaume kwa miaka kumi lakini bado anamkana hadharani kuwa hana uhusiano naye:

Bifu la Zari na Hamisa lilianza baada ya Diamond kuchepuka Kwenye Mahusiano Yake na Zari na kuzaa mtoto na Hamisa Mobetto tangia hapo Zari na Mobetto hawaivi chungu kimoja ni majungu kwenda mbele na kujibizana mitandaoni.

Mwarabu Fighter Athibitisha Bado Yupo WCB Hajafukuzwa Kazi

Bodyguard wa staa wa Bongo fleva na CEO wa WCB, Diamond Platnumz, Mwarabu Fighter ameibuka na kuweka wazi kuwa taarifa zilizosambaa kuwa amefukuzwa kazi sio za kweli.

Wiki chache zilizopita kuna taarifa zilisambaa kuwa Mwarabu Fighter amefukuzwa kazi na kudaiwa kuwa aliambiwa na Diamond akae nyumbani mpaka pale atakapopata taarifa.

Kwenye Interview na Global Publishers, Mwarabu amekanusha tetesi hizo na kusema kuwa bado yupo WCB na anaendelea kufanya kazi na Diamond kama kawaida, kutokumuona naye ni kwa sababu ya taratibu za kiofisi ambazo hawezi kuziweka wazi ila siku yoyote tutamuona naye.

Taarifa za Mwarabu kufukuzwa ziliaminika kwa sababu aliokuwa anaonekana yuko Tanzania Wakati Diamond yupo na timu yake nchini Marekani kwa ajili ya Tour yake ya ‘A Boy from Tandale’.

 

Hatimaye Mama Diamond Amkubali Mtoto wa Hamisa Kuwa Mjukuu Wake

Mama mzazi wa Staa wa Bongo fleva Diamond Platnumz, Bi Sandra au maarufu kama Mama Diamond amemkubali mjukuu wake Dylan kwa mara ya kwanza hadharani.

Dylan ni mtoto wa mwisho wa Diamond aliyezaa na Hamisa kipindi bado yupo Kwenye Mahusiano ya kimapenzi na mama watoto wake aliyezaa naye watoto wawili Zarinah Hassan.

Kwa muda mrefu imekuwa ikonekana kama Mama Diamond hana mapenzi kwa mjuukuu wake Dylan kutokana na kuwaposti watoto wa Zari Tiffah na Nillan tu Kwenye mitandao ya kijamii.

Mama Diamond aliwahi kuweka wazi kuwa anamchukia Mama Yake na Dylan Hamisa Mobetto na hata kusemekana kumtembezea kipigo kizito na sababu ni Hamisa kumuita Mama Diamond Shilawadu.

Wikiend iliyopita ilikuwa Birthday ya Mama Diamond ambapo Diamond alimuandikia Mama yake ujumbe mzito akimtaka amsamehe Hamisa na amkubali mjukui wake Dylan na ampende kama wajukuu zake wengine.

Maneno hayo ya Diamond yameonekana kumuingia mama yake kwani Kwenye clip ya birthday yake ameonekana akipokea Keki kutoka kwa Dylan na akimuita Dylan mume wake na Kukiri kuwa anampenda.

 

Diamond Amfungukia Mazito Mama Yake Siku Yake Ya Kuzaliwa

Staa wa Muziki wa Bongo fleva Naseeb Abdul maarufu kama Diamond Platnumz amemfungukia maneno mazito Mama yake mzazi Bi. Sandra alipomtumia salamu za Kheri siku yake ya kuzaliwa.

Diamond aliandika ujumbe huo wa kum-wish mama yake siku ya kuzaliwa kupitia ukurasa wake wa Instagram, Diamond amesema mama yake amepitia magumu mengi sana ikiwemo manyanyaso wakati akimlea hivyo hakuna mtu wa kumlinganisha na mama yake.

Nasikitikaga sana Wanapojaribu Kulinganisha Thamani yako kwangu na Mtu yoyote…Na kusahau kuwa pasipo wewe kunizaa na Kunilea kwa shida na tabu leo hii hakuna yoyote ambae angeniona wamaana….. Ikiwa wewe ndio Ulonifanya mie nikawa Duniani Basi you will always be My First priority then the rest will follow…Dharau na Manyanyaso Ulopitia kwenye kunilea Hakuna anayejua, Tabu na shida Ulizopitia kufanya hadi leo walau nionekane mtu mbele za watu.. eti mtu kirahisi tu anatokea na kukuringanisha na mtu… Mama MADALE is your House!!! na ikitokea kesho nimekufa pia NUSU ya Mali zangu zote ni zako”.

Diamond amekuwa muwazi juu ya mapenzi makubwa aliyonayo kwa mama yake, na Julai 7, 2018 Mama yake na Diamond Platnumz, Sandra anasherehekea siku yake ya kuzaliwa.

Zari: Diamond Ameniomba Sana Msamaha Baada Ya Kuchepuka

Zarinah Hassan maarufu kama Zari The Bosslady amefunguka na kuweka wazi kuwa mzazi mwenzake staa wa Bongo fleva Diamond Platnumz alimuomba sana msamaha baada ya kuchepuka.

Katika Interview yake na Global Publishers, Zari amekiri kuwa tangu Diamond amsaliti na kuzaa na Hamisa Mobetto mwaka jana amemuomba sana msamaha na hata Babu Tale kuenda South Africa juzi juzi ilikuwa ni kuomba radhi.

Babu Tale alikuja Pretoria, alitaka turudiane na Diamond kwa ajili ya watoto, sikuona ubaya katika hilo, lakini mambo ya mapenzi hapana tena, watu haohao wa karibu walipaswa kumuonya Diamond wakati anafanya mambo yake kwa sababu anaamini walifahamu kila kitu.

Wangemwambia Diamond aache mambo aliyokuwa anayafanya. Kufufua penzi kwa sasa ni vigumu sana, wameshachelewa. Mimi nawaheshimu sana, na ndiyo maana hata Babu Tale alipokuja nilimkaribisha vizuri. Sina ubaya na mtu yeyote, hata ndugu zake Diamond“.

Lakini Zari amesisitiza kuwa taarifa zilizoenea kuwa wawili hao walirudiana Diamond alipoenda Sauzi sio za kweli kwani hawakulala hata chumba kimoja:

Diamond alikuja kuwaona wanawe. Alilala chumba kingine na mimi nikalala chumbani kwangu. Tuliongea kuhusu kuwa karibu lakini ni kwa ajili ya watoto tu. Kwa sasa sina uhusiano wowote.  Nimeyaweka kando mambo hayo, nachoangalia ni kulea watoto wangu”.

 

Diamond- Mtoto Wa Hamisa ni Mtoto Wangu Kama Walivyo Watoto Wa Zari

Staa wa muziki wa Bongo fleva Diamond Platnumz amemwaga povu zito kwa mashabiki waliokuwa wanamnanga mtoto mmoja ale aliyezaa na Hamisa wakidai sio mtoto wake.

Siku ya jana Diamond aliachia trailer mpya ya shoo yake ya ‘The real Life of Wasafi’ itakayoonyesha maisha halisi ya familia ya Diamond itakayorushwa Kwenye Wasafi Tv.

Kwenye trailer hiyo kuna kipande kinachomuonyesha Diamond akiwataka anazungumzia watoto wake lakini watoto wanaoonekana ni wawili tu ambao amezaa na Zari huku mtoto wake aliyezaa na Hamisa hakuonekana.

Kuona hivyo mashabiki wa Zari wakaanza kumnanga mtoto wa Hamisa kuwa sio mtoto wa Diamond ndio maaan hajaonekana kwenye trailer ya shoo ile na hapendwi kama watoto wa Zari wanavyopendwa.

Baada ya maneno mengi sana Diamond alishindwa kujizuia na kuandika kwenye ukurasa wake wa Instagram kuwa Dylan ni mtoto wake kama walivyo watoto aliozaa na Zari walionekana kwenye trailer ile sababu pekee ambayo ilisababisha mpaka Dyalan hakuonekana ni kwa sababu hakuwa na clip yake:

 

Nuh Mziwanda- Sina Bifu na Diamond Ila Sina Ukaribu Naye Pia

Mwanamuziki wa Bongo fleva Nuh Mziwanda amefunguka na kudai jana bifu na staa wa Bongo fleva Diamond Platnumz.

Nuh ambaye ameshafanya ngoma na Ali Kiba aliomshirikisha katika wimbo wake wa Jike Shupa amefunguka na kusema hata kama hajawahi kufanya ngoma na Diamond haimaanishi wana bifu.

Mziwanda alifunguka hayo Kwenye mahojiano aliyofanya na Dizzim Online pale alipotakiwa kujibu tetesi kama ana tatizo lolote na Diamond:

Mimi sina bifu na Msanii yoyote na wala sina bifu na Diamond wala sina ugomvi naye unajua yule mchizi sana na tulishawahi kufanya vitu vingi sana lakini muda nakumbuka Times hafanyi shoo zake tulikutana Dodoma tukafanya shoo yake kwaiyo ni mtu ambaye yuko Poa lakini hatuna mawasiliano wala ukaribu wowote.

Lakini pia Mziwanda ameweka wazi kuwa kama ikitokea nafasi ya kufanya kazi na Diamond basi atafuata taratibu za kwenda Kwenye uongozi wake na kuomba Kolabo.

Kutokana na Bifu lililopo kati ya Diamond na Ali Kiba, wasanii wanaofanya kazi na wasanii hao hujikuta wakichagua upande wa kuwa na hivyo Mziwanda baada ya kufanya Kolabo na Ali Kiba alidaiwa kuwa na bifu na Diamond.