Man Walter Achochea Bifu La Diamond na Ali Kiba Liendelee

Mtayarishaji wa muziki wa Bongo fleva Man Walter ameibuka na kusema kuwa anatamani Bifu kati ya wasanii wa Bongo fleva Diamond Platnumz na Ali Kiba lisiishe kabisa.

Man Walter amedai kuwa kuisha kwa bifu kati ya Ali Kiba na Diamond ni sawa na kuua timu za Simba na Yanga na hivyo kusababisha Kulia kaisa upinzani.

Kwenye mahojiano aliyofanya na Gazeti la Mwananchi, Man Walter ambaye ameshafanya kazi na wasanii hao wote wawili katika nyakati tofauti amesema Bifu hilo ndio Linapeleekea muziki kuwa mtamu.

Yaani Hawa wasanii wakipatana ni sawa na kutokuwepo kwa simba na Yanga, hivyo waacheni waendelee hivyo hivyo kwani ndio burudani yenye we”.

Pia Man Walter amefika mbali zaidi na kusema anahisi kabisa kama Bifu hilo litaisha kwa njia moja au nyingine basi ni wazi kabisa muziki wa Bongo fleva utadorora kabisa.

 

“Rayvanny Alivyofungiwa Nilikuwa Napata Mawazo Sana”- Fahyma

Mpenzi na mama Watoto wa staa wa Bongo fleva kutoka katika label ya WCB Rayvanny, Fahyma ‘ Fahyvanny’ amefunguka na kuweka wazi Furaha yake Baada ya Rayvanny kufunguliwa na BASATA.

Fahyma amekiri kufurahishwa na kitendo cha baba mtoto wake huyo kusamehewa na Baraza la Sanaa la Taifa (Basata) kwani ishu hiyo ilikuwa inamnyima usingizi.

Kwenye mahojiano aliyofanya na Gazeti la Ijumaa, Fahyma alisema katika kitu kilichokuwa kinampa mawazo na kukosa kabisa usingizi ni kufungiwa kwa baba mtoto wake huyo lakini kwa sasa anaishukuru Basata kwa kuwahurumia na kuwafungulia kuendelea na kazi kama kawaida.

Kufungiwa kwa Rayvanny kulikuwa kunanipa mawazo sana maana nilikuwa nawaza maisha yetu yatakuwaje na tulikuwa hatujui msamaha utatoka lini lakini tunashukuru Mungu wamesamehewa na mwisho wa siku maisha mengine yanaendelea, nitaendelea kumhimiza asirudie kosa tena”.

Rayvanny na Diamond Platnumz walifungiwa na BASATA Baada ya kupandishwa stejini na kuperfom wimbo wao wa ‘Mwanza’ ambao ulikuwa umepigwa stop kwa kukiuka maadili ya Kitanzania.

Diamond Aweka Wazi Mkwanja Mrefu Aliotaka Tyga Kwajili Ya Kolabo

Msanii wa muziki wa Bongo fleva nchini na CEO wa Music Label ya WCB, Naseeb Abdul maarufu kama Diamond Platnumz amefunguka na kuanika mkwanja mrefu aliotaka Msanii Tuga kwajili ya kolabo naye.

Diamond Platnumz ameanika gharama za kufanya kazi na rapa mkubwa wa Marekani wa lebo ya Young Money, Micheal Ray Stevenson,  maarufu kama ‘Tyga’.

Diamond alifunguka hayo kwenye  mkutano baina ya wasanii na Mamlaka ya Kudhibiti Mawasiliano nchini (TCRA) ambao ulihusu suala la asilimia ya malipo kwenye nyimbo za wasanii, Diamond alisema alitaka kufanya kolabo na mwanamuziki  Tyga ambaye alitaka  Dola 150,000 (Tsh.Milioni 300.7).

Rapa Tyga anatoka katika lebo kubwa nchini Marekani inayomilikiwa na Lil Wayne, ‘Young Money’. Lebo nyingine ni Last Kings Records, Def Jam Records, Republic Records, Empire Distribution, Cash Money, Universal Motown Records, Decaydance na Good Music.

Diamond ameshafanya kolabo kadhaa na wasanii wakubwa kutoka nje ya nchi ikiwemo Rick Ross na Hivi karibuni Omarion.

Diamond Afungukia Hatma Ya Wasafi Festival

Msanii wa muziki wa Bongo fleva na CEO wa WCB Diamond Platnumz amefunguka na kuzungumzia mipango ya Wasafi Festival mara Baada ya kuachwa huru na BASATA.

Katika mazungumzo yake na Waandishi wa habari siku ya leo, Diamond amewataka mashabiki zake waendelee kuwa wavumilivu  kuhusu tamasha lao la Wasafi Festival kwani bado wanafikiria kama walianzishe upya au waendelee kufanya shoo mikoa iliyobakia, lakini kwakuwa tayari wameshafunguliwa basi hakuna shaka juu ya hilo watawajulisha kitachoendelea.

Namshukuru  mwenyezi Mungu kwakuniweka hai na salama mpaka nafika hapa, lakini pia kabla yakuanza chochote pia niishukuru serikali yangu pendwa kwakunifungulia kifungo ambacho nilikuwa nacho, maana kifungo kinafunguliwa tu na neema hizo zinakuja.

Niwashukuru watu wote ambao wameisapoti Wasafi Festival, nawashukuru sana kwa sababu mapokezi yalikuwa makubwa hatukuyategemea, lakini mimi na menejimenti yangu tulikuwa tunajadili tumalizie ile mikoa iliyobaki au tuanze na upya mwaka 2019, japo mzani unaelemea mwaka 2019 ili watu waliokuwa bado hususani mikoa ambayo hatujenda wawe na hamasa zaidi, hivyo tunawaomba mashabiki zetu wasichoke kutusapoti na kuendelea kuzifatilia kazi zetu nzuri“.

Diamond na Rayvanny walifungiwa na BASATA mwishoni mwa mwaka jana baada ya ku-perform wimbo wao wa Mwanza Nyegezi kwenye Tamasha lao la Wasafi Festival jijini Mwanza, wimbo ambao umefungiwa na Baraza hilo. Lakini juzi Baraza hilo lilitangaza kuwafungulia baada ya kuomba radhi.

Diamond Platnumz Asaini Dili Jipya na Pepsi

Msanii wa muziki wa Bongo fleva Naseeb abdul maarufu kama Diamond Platnumz ameweka wazi dili lake jipya alilosaini na kampuni ya Vinywaji baridi ya Pepsi Tanzania.

Diamond alisaini mkataba wa kwanza na kampuni hiyo kupitia kinywaji cha Mirinda ambapo walikuwa  wadhamini wakubwa wa tamasha la Wasafi Festival.

Siku ya Leo Diamond amezungumza na waandishi wa habari leo katika Ukumbi wa Serena Hotel uliopo Posta jijini Dar, wakati wa utambulisho wa kinywaji kipya cha Mkubwa Wao ambacho kilizinduliwa tangu Januari 21.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Diamond ameandika maneno haya juu ya dili lake jipya na Pepsi:

https://www.instagram.com/p/BtBdYGehoJA/?utm_source=ig_share_sheet&igshid=1jvnys135k9fy

Nampenda Sana Tanasha – Esma Platnumz

Dada wa staa wa Bongo fleva Diamond Platnumz, Esma Platnumz amefunguka na kudai kuwa anamkubali sana wifi yake mpya Tanasha kwa muda mfupi ambao amemjua.

Esma ambaye amekutana rasmi na Tanasha siku chache zilizopita amedai kuwa ameshaanza kumpenda ‘kumoyo’ wifi yake mpya Tanasha Donna kiasi cha kujiuliza kwamba, mwana­dada huyo alikuwa wapi siku zote hizo.

Kwenye mahojiano aliyofanya na Gazeti la Ijumaa Wikienda Esma alisema amekuwa na ukaribu kwa muda mfupi na wifi yake huyo lakini ametokea kumkubali na sasa ame­kaa kwenye moyo wake tofauti na alivyotarajia mwanzo kwani mtu akiwa mpya kumzoea inahitaji moyo kuridhia.

Huwezi amini Tanasha tayari ameshakaa ndani ya moyo wangu, nampenda sana na kuna muda najiuliza alikuwa wapi muda wote? Kwa nini hakutokea mapema kwenye familia yetu? Hayo mambo ya kuniita Yuda hata siyajali kabisa, wata­jua wenyewe kwani mimi maisha yanasonga”.

Diamond alimtambulisha Tanasha kwa Familia yake aliweka mama yake mzazi Mama Dangote siku chache zilizopita.

 

Zari Ampiga Kufuli Diamond na Familia Yake

Mfanyabiashara maarufuu na mzazi mwenzake na staa wa Bongo fleva Diamond Platnumz, Zarinah Hassan ‘Zari’  amedaiwa kuingia kufuli familia nzima ya Diamond.

Gazeti la Ijumaa linaripoti kuwa, Zari alianza kukata mawasiliano na Diamond, lakini alikuwa akiendelea kuwasiliana na ‘mkwewe’, Sanura Kassim ‘Bi Sandra’ na wifi yake, Esma Khan kabla ya kuwa-block wote.

Unajua Zari ni mtu mwenye misimamo sana. Baada tu ya kutangaza kummwaga Mondi Februari 14, mwaka jana, alisema penzi lake na Mondi limekufa, lakini hawezi kukata mawasiliano na familia yake maana wao hawana makosa yoyote.

Ndiyo maana ulikuwa unaona akaunti ya mama Diamond anayotumia jina la mama Dangote kwenye Insta ilikuwa inaendelea kupendeza na picha za wajukuu zake, Tiffah na Nillan kwa sababu Zari alikuwa vizuri na mama Dangote (mama Diamond), lakini baadaye walivyoanza kumletea mapichapicha ya wanawake wengine, Zari akaona isiwe shida, acha awafyekelee mbali”.

Baada ya tetesi hizo kusambaa Gazeti lilimsaka Esma Platnumz  ambaye alikiri kupigwa block muda mrefu, lakini akasema haoni tatizo kwani hayo ni mambo yao binafsi, lakini zaidi ni kwamba wao wanamuunga mkono ndugu yao pale anapokuwa kwenye uhusiano wake.

Sisi hatuwezi kuingia sana kwenye uhusiano wa Nasibu (Mondi), lakini huwa tunamsapoti pale anapokuwa. Kwa sasa yupo na Tanasha, basi tunamuunga mkono“.

Siku za Hivi karibuni Zari ameonekana kuwa mbali na Familia ya Diamond na kuonekana akiwa bize na maisha yake na Watoto Wake nchini Afrika ya Kusini.

 

Diamond Atangaza Ujio Wa Msanii Mpya Wa Kike WCB

Msanii wa muziki wa Bongo fleva na Mkurugenzi wa Music Label ya WCB Diamond Platnumz ametangaza rasmi kumsaini Msanii wa pili katika label ya WCB.

Diamond alitangaza habari hiyo njema siku ya Ijumaa kwani kwa muda mrefu Label hiyo imekuwa na utaratibu wa kudai ni wasanii wa kiume tu bil kuwapa nafasi wasanii wa kike.

Kupitia ukurasa wake wa Twitter, Diamond ameandika ujumbe huu:

About to introduce a FEMALE Artist….. Coz i believe Women they can, if you Empower them….” (Nipo mbioni kumtambulisha msanii wa kike (WCB), kwa sababu naamini wanawake wanaweza, wakiwezeshwa)“.

Mpaka sasa haijajulikana ni Msanii gani wa kike ambaye atatambilishwa ingawa Baadhi ya mashabiki wamekuwa wakihisi nafasi hiyo huenda akaipata mwanadada Nandy ila Diamond mwenyewe hajathibitisha hilo.

 

Msanii Tekno Adaiwa Kumuiga Diamond Kwa Hili

Msanii wa muziki kutoka Nchini Nigeria anayefanya vizuri kabisa maarufu kama Tekno Miles amedaiwa kufuata nyendo Msanii wa Bongo fleva Diamond Platnumz kwa kufungua Music Label yake.

Tekno ameingia Kwenye Listi ya wasanii wengi wa Afrika ambao wanafanya vyema kama vile Wizkid, Davido, Patoranking kwa kumiliki Music Label yake inayokwenda kwa jina la Cartel Music.

Meneja wa msanii huyo, ‘John Peace’ amethibitisha taarifa hizo katika mtandao wa burudani nchini  Nigeria kwamba Tekno ameondoka katika lebo yake ya awali  ya Triple MG na kuelekea kwenye lebo yake aliyofungua ya Cartel Records.

Msanii huyo pia amejitambulisha kuwa yeye ni mmiliki kamili wa lebo hiyo kwenye akaunti yake ya instagram kwa kuweka picha yenye jina la lebo yake ikiwa na maelezo yanayosomeka ‘CEO’.

Zari: Kamwe Siwezi Kumuanika Mwanaume Wangu Mtandaoni

Mzazi mwenzake na staa wa Bongo fleva Diamond Platnumz, Zarinah Hassan ‘Zari’ amefunguka na kuweka wazi kuwa kamwe hatakuja kumuanika tena Mpenzi wake kwenye mtandao.

Baada ya kuachana na Diamond mwaka mmoja uliopita Zari hajawahi kumuweka wazi mwanaume ambaye yupo naye kwenye mahusiano ingawa ameshawahi kusema yupo kwenye mahusiano.

Zari

Zari alifikia hatua ya kuweka wazi hayo alipoulizwa kama kweli hana mpango wa kuolewa na Diamond na atamuanika lini mwanaume anayempenda am­bapo alieleza kuwa mwanaume wake si wa mitandao ya kijamii.

Mume wangu siyo wa social media, ni mume wangu siyo wetu“.

Zari ambaye ana watoto watano wawili kati yao amezaa na Diamond baada ya kuachana na Mbongo Fleva huyo amewahi kuhusishwa kimapen­zi na mwanaume anayeitwa Brian wa nchini Uganda ambapo mara mbili to­fauti alionekana kupiga naye picha za ukaribu lakini mwenyewe alidai kuwa ukaribu wao huo ni wa kikazi tu.

Tangu Diamond aachane na Zari ameshawahi kuwa kwenye mahusiano na wanawake kadhaa ikiwemo mama Watoto Wake Hamisa Mobetto Lakini pia Kim Nana na Sasa mrembo kutoka Kenya Tanasha.

Raisi Mstaafu Kikwete Ampa Onyo Kali Diamond Platnumz

Raisi mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Jakarta Kikwete amempa wosia mzito Msanii ambaye ni staa wa Bongo fleva Diamond Platnumz.

Gazeti la Ijumaa linaripoti kuwa Raisi Kikwete alimuita Diamond nyumbani kwake jijini Dar na kumpa wosia mzito ambao uligeuka gumzo huku staa huyo akikomaliwa juu ya mambo matatu ndani yake.

Diamond ambaye ni Mkurugenzi Mtendaji wa Lebo ya Wasafi Classic Baby (WCB) alifunguka juu ya wosia huo kama ifuatavyo; “Nilipokuwa Mwanza (kwa ajili ya Tamasha la Wasafi), Rais mstaafu Jakaya Kikwete alinipigia simu na kunitaka niende nikamuone haraka”.

JAMBO LA KWANZA “Baadaye, nilikwenda nyumbani kwake (JK) jijini Dar. Pamoja na mambo mengine, nikiwa pale, kitu cha kwanza kabisa alinishauri nioe kwani umri unaruhusu (Diamond ana umri wa miaka 30 sasa). “Aliniambia ni muda muafaka kuoa na kutulia,” alisema Diamond na kuendelea:

JAMBO LA PILI “Pia alinionya juu ya kuposti video na picha kwenye mitandao ya kijamii zikionesha nikitandaza pesa mezani. “Hayo aliyasema baada ya mimi kuposti video kwenye Instagram ikimuonesha Tanasha (mpenzi mpya wa Diamond) na mimi tukiwa hotelini nikihesabu maburungutu ya pesa juu ya meza wakati Tanasha akipiga ‘selfie’ kwa kutumia simu janja.

“Rais huyo mstaafu aliniambia jambo hilo nililofanya halikuwa sahihi ukitegemea kwamba kuna watu hawana uwezo kabisa wa kimaisha ambao watajisikia vibaya kuniona mimi nikijionesha nina pes.

JAMBO LA TATU “Aliniambia niwe makini na mambo ninayoyafanya kwani mengine yanaweza kunijengea chuki kwa watu.

Aliniambia anaweza kuja mtu mbaya kunipongeza kwa mafanikio au jambo lolote, lakini siwezi kumjua kwani atakuwa anakuja mbele yangu akinichea usoni, lakini moyoni ana chuki.

Kwa upande mwingine aliniambia ninaweza kupata matatizo ya kipesa, nitakapomfuata mtu mwenye chuki na mimi ataishia kunipa pole tu usoni, lakini ndani ya moyo wake atakuwa na furaha, hapo nitakuwa nimepata matatizo kwenye maisha yangu”.

 

Nandy na Diamond Platnumz Wang’ara Tuzo za AEAUSA

Wasanii wa muziki wa Bongo fleva Diamond Platnumz kutoka WCB na Faustina  Charles maarufu kama Nandy na wasanii wengine kutoka Tanzania wameng’ara katika tuzo za African Entertainment Awards USA (AEAUSA).

Mbali na wasanii hao wa Kitanzania kushinda tuzo lakini pia kuna wasanii kutoka katika nchi za Afrika Mashariki waliofanikiwa kushinda tuzo.

Wasanii waliofanikiwa kushinda tuzo ni pamoja na Diamond Platnumz ambaye ameshinda tuzo mbili, ikiwemo tuzo ya Msanii bora wa mwaka ( Best artist of the year pamoja na Best Collaboration akishirikiana na Omarion kutoka nchini Marekani.

Msanii Nandy ameshinda katika kipengele cha Best Female Single kupitia wimbo wa Kivuruge, huku Rayvanny akishinda tuzo ya Best Vocalist na Dj wa Diamond Rom Jones akishinda tuzo ya best DJ in Africa.

 

BASATA Wakanusha Taarifa Za Kuwafungulia Diamond na Rayvanny

Baraza la Sanaa Tanzania (BASATA) limekanusha taarifa za kuwafungulia wasanii Diamond Platnumz na Rayvanny wanaotumikia adhabu ya kutojihusisha na muziki kwa muda usiojulikana baada ya kufanya makosa mbalimbali ndani ya kipindi cha miezi miwili.

Taarifa hiyo imekuja baada ya msanii Diamond kutangaza kwenye mkutano wa waandishi wa habari jana kuwa wameruhusiwa kufanya tamasha la muziki, Wasafi Festival’  nchini Kenya.

Siku chache zilizopita wasanii hao kupitia mtandao wa Instagram Walionekana wakifanya mkutano na waandishi wa habari nchini Kenya kutangaza maonyesho yao yanayoendelea, lakini alifajiri taarifa ya Basata ilisema kuwa hawajatoa ruhusa kwa wasanii hao.

Baada ya kauli hiyo kutoka kwa wasanii hao kutoka WCB, BASATA walitoa tamko lao na kusema:

Ikumbukwe kuwa Desemba 18 tuliwafungia kutojihusisha na sanaa kwa kipindi kisichojulikana kwa kuimba kwa makusudi wimbo Mwanza tulioufungia kwa sababu za kimaadili,

“Baraza linasisitiza kuwa halijawafungulia wasanii hao, pia linawaonya kuacha kutoa taarifa za uongo kabla halijawachukulia hatua kali zaidi,” imeeleza barua hiyo.

 

Diamond Athibitisha Kuzama Kwenye Penzi Zito na Tanasha

Staa wa muziki wa Bongo fleva na CEO wa WCB Naseeb Abdul maarufu kama Diamond Platnumz amethibitisha kuwa amezama vibaya  kwenye Penzi na Mpenzi Wake Mpya Tanasha Donna Oketh.

Diamond alitangaza kuanzisha uhusiano wa kimapenzi na mrembo kutoka Kenya Tanasha ambaye ni video vixen na Mtangazaji wa redio.

Lakini pamoja na kuwa pamoja kwa muda mfupi tu Diamond ameweka wazi ni Jinsi gani anavyomzimia  mrembo huyo kwani amekuwa akimuanika kwenye mtandao wa kijamii.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Diamond Platnumz ameweka video yake na Tanasha inayomuonyesha akimtengeneza nywele Mpenzi Wake huyo na kuweka wazi Jinsi anavyomzimia.

Basi na Mie nikiingiaga kwenye mapenzi nazama mzima mzima kama boya….Matokeo yake nikizinguliwa naanza kutoa Povu…”.

https://www.instagram.com/p/BrsWX0MFzNh/?utm_source=ig_share_sheet&igshid=1t7cbpa4u9y9e

Kim Nana Afungukia Tetesi Za Bifu na Lynn

Video vixen maarufu kama Lilian Kessy ‘Kimnana’ amefunguka na kudai kuwa yeye na video queen mwenzake Irene Louis ‘Lynn’ hawana Bifu kama inavyodaiwa.

Tetesi za kuwepo kwa Bifu kati ya warembo hao zilizuka Baada ya warembo hao wawili wote kudaiwa kuwa na uhusiano wa kimapenzi na staa wa Bongo fleva Diamond Platnumz.

Kwenye mahojiano aliyofanya na Global Publishers, Kim Nana amefunguka  kuwa watu wamekuwa wakizungumza mengi kuwa ana bifu na Lynn, lakini hawajawahi kuwa maadui hata siku moja na Lynn ni kama mdogo wake na hata wakikutana wanasalimiana vizuri na kuzungumza.

Lynn ni mshkaji wangu, hatuna bifu kabisa ndiyo maana hata hivi karibuni niliposti kipande cha video nikiwa naimba wimbo wake wa Chafu kwa lengo la kumsapoti hivyo wanaosema tuna bifu imekula kwao maana siyo kweli”.

 

Diamond na Rayvanny Waomba Msamaha BASATA na Serikali Baada Ya Kufungiwa

Wasanii wa muziki wa Bongo fleva kutoka Katika Label ya WCB Diamond Platnumz na Rayvanny ameibuka na kuomba Radhi kwa serikali na BASATA siku chache Baada ya kufungiwa.

Wiki iliyopita Baraza la Sanaa Tanzania (BASATA) walitangaza kuwafungia wasanii Diamond Platnumz na Rayvanny Baada ya kukaidi amri yao na Kuperfom wimbo wa Mwanza uliofungiwa kwenye tamasha lao la Wasafi Festival.

BASATA Walitangaza kulifungia tamasha la Wasafi Festival na pia kuwataka wasanii hao kutoperfom katika nchi nyingine yoyote pamoja na kwamba walishapanga kwenda Kuperfom Nchini Kenya.

Lakini Wasanii hao wameomba msamaha Kwa BASATA na Serikali kwa ujumla na kuomba wasemehewe adhabu yao waliyopewa.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Rayvanny ameposti kipande hiki cha video kinachoonyesha wasanii Hawa wakiomba radhi:

https://www.instagram.com/p/BroqbY3j9YE/?utm_source=ig_share_sheet&igshid=1uqh6m3umbdj1