Diamond afungua ofisi mpya ya Wasafi nchini Rwanda

Msanii Diamond Platnumz amazindua ofisi mpya ya label yake ya Wasafi. Hit maker huyo wa ‘Marry Me’ alisafiri kuelekea Rwanda baada ya kurejea kutoka nchini Oman alipoenda kutumbwiza mashabiki wake.

Diamond alitangaza kuwa tawi mpya la Wasafi nchini Rwanda utafunguliwa rasmi hivi punde, alisema kuwa ataka wasanii nchini Rwanda kuuza muziki wake kwa tovuti ya Wasafi.

“Mapema baada ya kukamilisha kikao na Makubaliano na kampuni itayokuwa tawi letu ama agent wa Wasafidotcom nchini RWANDA… Muda si Mwingi nitawatangazia Wasanii wote wa Rwanda ni namna gani mnaweza kuwa na Acount za kuuza nyimbo zenu Wasafidotcom,” Diamond alisema.

Tiffah Dangote amependeza zaidi na mavazi ya kiume ya kakake Nillan?

Mtoto wa kwanza wa Diamond Platnumz, Tiffah Dangote, wikendi hii aliwafurahisha wengi alipovalia nguo za mdogo wake, Nillan na kuposti picha kuwaonyesha mashibiki wake.

Kupitia mtandao wa Instagram, mamake Tiffah aliposti picha za Tiffah akiwa amevalia mavazi ya kiume na kwenye caption akaandika alikuwa ameazima nguo za Nillan alizozivaa wakati wa #40 photoshoot.

Rocking @princenillan shirt and hat from his #40 photoshoot. Everything from #BABYSHOP

Mashabiki wengi walimpongeza mtoto huyu kwa fashion sense yake huku wakisema kuwa amependeza sana na nguo hizi. Tiffah Dangote ambaye atafikisha miaka miwili mwezi wa Agosti ameonekana kuwa mtoto ambaye anataste nzuri ya mavazi na inaweza kuwa mamake, Zari Hassan, ndiye anayemfunza mtot huyu kuwa a fashion icon wa watoto maarufu Tanzania.

Kwenye picha hizi mpya, Tee pia amaonekana pia kufanana na baba yake sana. Angalia picha za Tee kama amevalia nguo za mdogo wake hapa.

Tiffah's tomboy look
Tiffah’s tomboy look
Tiffah apendeza na mavazi yake ya tomboy
Tiffah apendeza na mavazi yake ya tomboy

‘DNA ifanyike kuweka wazi,Nillan ni mtoto wa nani?’ Zari Hassan na Diamond Platnumz au Ivan!

Maisha ya Diamond Platnumz na baby mama wake Zari Hassan,yamekua kama vile bongo movie,kila wakati lazima usikie mastori kuhusu hili na lile,ni kero wanasema.

Babake Diamond Platnumz,mzee Abdul Juma amefunguka kuhusu tuhuma kuwa, mtoto Nillan sio mwanawe,na Zari Hassan.

Stori zilitamba kwenye mitandao eti Nillan amefanana sana na Ivan,mpenzi wa zamani wa Zari ambaye pia ni baba ya watoto wake.

Mzee Abdul anasema,’ili kuwazima wale wenye dhana potofu kwamba mtoto si wa Diamond ni lazima vipimo vya DNA vifanyike.’

Anaendelea kusema,’Mimi kama mzazi namshauri Diamond akapime DNA ili apate uhakika zaidi japokuwa tunaamini hao wajukuu wetu ni watoto wake lakini kwa kuwa maneno yamekuwa mengi kila kukicha ni lazima afanye hivyo, naamini na maneno ya watu kumsimanga yataisha.’

 

Cha kuumiza zaidi amekiri,’Katika maisha ya kawaida kwa mwanaume ni aibu kulea watoto ambao unajua kabisa si wako lakini unasema ni wako. Mpaka Diamond anaamini ni watoto wake na sisi ndugu tunaamini hivyo, kwa nini wengine wasikubaliane na ukweli huo.’

Habari hii imezua gumzo kwenye mitandao ya jamii,baada ya kutokea kwenye ukurasa wa kwanza wa gazeti.

 

Msanii Barnaba adai kuwa ni bora fedha zao za muziki ziibiwe na Diamond

Hitmaker  wa ‘Lover Boy’ anadai kuwa ni bora wasanii waibiwe na Diamond Platnumz kuliko kuibiwa na mtu binafsi ambaye si mwanamziki.

Barnaba amemsifu Diamond kwa kuanzisha tovuti yake ya kuuza muziki ya Wasafi.com. Msanii huyu alikutana na Diamond alipomtembelea katika ofisini kwake.

Barnaba na Diamond

“Tumeibiwa sana wasanii, tumedhulumiwa sana. Mungu anisamehe kidogo, bora atuibie msanii mwenzetu, tunajua msanii mwenzetu anakula yupo kwenye soko letu kuliko atuibie mtu binafsi.”

““Na yeye akiwa kama CEO [Diamond] alichukua uamuzi wa busara kama heshima kutupigia simu wasanii wenzake mwenyewe kuliko kuwatuma menejimenti. Mimi naona jambo zuri la bahati alilolifanya na nilienda nikachukuwa contract yangu na kiukweli nimeusaini lakini bado kuurudisha,” Barnaba aliambia Dizzim Online.

“Si mtegemia mtu mimi” Diamond Platnumz awaambia wandiishi wa habari wanaomharibia sifa

Inaonekana kuwa Mwimbaji Diamond Platnumz amechoshwa na wanatangazali na waandishi ambao wamekuwa wakimsema vibaya. Kupitia interview aliyoifanya na Kings FM Diamond alisema kuwa wanajiharibia wakati.

Diamond Platnumz aliendelea kusemakuwa hapo alipofika, hategemei Redio wala TV kumpa push anapotoa nyimbo zake. Hivi sasa yeye ni big fish na anaamini kuwa mashabiki wake wapo kumsaidia kupromote projects zake.

“Unajua kwamba kuna kiwango unapofikia,unapokuwa na mashabiki wengi,lazima uongeze ufanisi wako wa usambazaji wa kazi zako.Tuna redio tuna TV, lakini pia lazima tuongeze namna zingine za kupromote kazi zako,” amesema Diamond.

Akizungumza exclusively na Prince Ramalove kupitia Kings FM, Diamond aliendelea kusema kuwa waandishi na wanahabari hupenda kutengeza controversy kupitia wanachoandika kumfanya mtu kukakaa vibaya mbele ya watu.

“Wasanii wanatakiwa wajiongeze, sasa naona kuna watu wameichukua tofauti na kuipindua kumtengenezea mtu baya,lakini wanapoteza muda.”

Hata hivyo, Diamond Platnumz aliongeza kusema anaheshimu media ata wanapomchomea picha, bado yeye anaamini kuwa hiyo ni part of their wrok.