Chid Benz Amwaga Povu Baada Ya Kukosekana Kwenye Listi Ya Wasafi Festival

Msanii mkongwe wa muziki wa Hip hop nchini Chid Benz amefunguka na kuwamwagia Povu zito timu nzima ya WCB Baada ya kukosa mwaliko wa kufanya shoo kwenye Wasafi Festival.

Chid Benz amefungukia ishu ya Diamond Platnumz na Timu yake nzima ya WCB kutumia wanamuziki Kama Dudubaya ambaye anaamini amechaguliwa kwa sababu ya umaarufu wa jina lake Konki Konki konki Master.

Kwenye mahojiano na kituo kimoja cha habari, Chid Benz amedai amesikiyishwa kuwa Msanii Kama yeye Anayeimba vitu vya maana hajachaguliwa kwa madai kuwa anatumia madawa ya kulevya ilhali ameshaacha.

Sisi wasanii tunaoimba nyimbo ambazo zinabeba ujumbe na maana hatupati nafasi kabisa utasikia wanasema achana na hao wakina Chidi Benz wanakula unga ila Dudubaya kisa anasema konki konki anajaza watu basi nasibu anampa tour kwenye Wasafi Festival”.

Diamond na timu nzima ya WCB ilimchagua Dudubaya Kama mmoja wa wasanii watakaoshiriki katika tamasha la WCB Baada ya umaarufu alioupata kupitia jina lake la utani la Konki Master.

 

“Wema ni Zaidi Ya Dada Kwangu, Nampenda Sana”-Diamond Platnumz

Msanii wa muziki wa Bongo fleva nchini na CEO wa WCB Diamond Platnumz amevunja ukimya juu ya sakata la picha chafu za Msanii wa Bongo movie Wema Sepetu.

Mwezi uliopita Staa Wema Sepetu alipatwa na Janga la mwaka Baada ya kuvujisha picha zake za utupu kwenye mitandao ya kijamii na kuishia kuburuzwa Mahakamani ambako kesi yake inaendelea kuunguruma.

Kwenye mahojiano aliyofanya na Dizzim Online, Kwa Mara ya kwanza Diamond amefunguka kuhusu sakata hilo la Wema na kuweka wazi kuwa anamheshimu na kuwa alifanya makosa Kama binadamu yoyote.

Wema ni zaidi ya Dada yangu namheshimu na kumpenda sana tulipotokaga Mimi na Wema ni mbali sana na hata Kama hatuna mahusiano lakini urafiki wetu upo na ninaami kila mwanadamu kuna vitu vinatokea ambavyo hatukupangaa vitokee kwaiyo inawezekana walikuwa wamekaa sehemu na hawakupenda vitokee lakini kwa bahati mbaya ikawa hivyo”.

Lakini pia Diamond amemshauri Wema kuwa makini na mambo Kama hayo yasijeyakatokea tena kwani kwa kufanya hivyo atakuwa anawaangusha mashabiki zake wanaompenda Lakini pia anaiangusha serikali inayomtegemea yeye kuwa kioo cha jamii.

Ali Kiba Ndiye Msanii Pekee Asiyehitaji Kiki Wala Matusi Kujaza Shoo-Mange Kimambi

Mwanaharakati wa mambo ya siasa mtandaoni Mwanamama Mange Kimambi ameibuka na kumpigia  saluti staa wa Bongo fleva Ali Kiba na kudai kuwa hakuna Kama yeye Bongo nzima.

Mange ameongea hayo Baada ya shoo iliyofanyika Wiki iliyopita mjini Kahama kujaza nyomi la ajabu pamoja na kwamba Ali Kiba hakuipigia promo shoo Ile Kama ilivyokuwa kwa Wasafi Festival na Fiesta.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Mange Kimambi ameandika maneno haya:

Ujumbe huo umeonekana Kama Dongo kwa mpinzani wa Ali Kiba Diamond Platnumz na tamasha lake la Wasafi Festival ambao walionekana kutoa promo ya nguvu Lakini pia Fiesta ambayo ilikuwa katika majobizano na Wasafi.

“Nimechoshwa na Kuhusishwa na Kila Mwanamke”-Diamond Platnumz

Msanii w muziki wa kuzaliwa kimya staa Diamond Platnumz ameibuka na kumwaga Povu zito kwa watu wanamuhusisja kimapenzi na kila mwanamke ambaye anaonekna naye hadharani.

Sakata hilo limekuja siku chache Baada ya Diamond na familia yake kuonekana na mrembo mpya anayejulikana Kama Christina nchini Dubai walipoenda for vacation. We

Kwenye mahojiano na Global Publishers? Diamond alianza kwa kusema kuwa amechoshwa na kuhusishwa na kila mwanamke anayeonekana kuwa na mama yake au kuwa naye karibu tu watu wanasema ni mtu wake.

 

Diamond aliweka wazi msichana huyo wa Kibongo mwenye maskani yake Dubai, alikutana naye kama mwenyeji aliyekuwa akiwatembeza maeneo mbalimbali kama watu wengine ambavyo wanaweza kwenda nje na kupokelewa na marafiki zao.

Mimi na msichana huyo tunafahamiana ameonekana kweli na mama yangu na wamejiachia kwenye picha tofautitofauti lakini ifahamike kuwa alikuwa akitupa kampani tu kama mwenyeji na si mapenzi,”

Mimi na msichana huyo tunafahamiana ameonekana kweli na mama yangu na wamejiachia kwenye picha tofautitofauti lakini ifahamike kuwa alikuwa akitupa kampani tu kama mwenyeji na si mapenzi,”

Huko niliteketeza fedha nyingi ambazo nisingependa kuzitaja lakini nilifanya kwa ajili ya familia yangu kwani mafanikio niliyonayo ni kwa dua wanazoniombea mama yangu na ndugu zangu pia sikufanya kwa ajili ya mwanamke na nisingekataa kuongozana na mrembo huyo kwani alikuwa kama mwenyeji”.

Mrembo huyo alizua gumzo mtandaoni mara Baada ya kuonekana katika picha kadhaa za mjini Dubai akiwa na Mama Diamond na hata Diamond na familia yake.

Diamond Ampangishia Hawa Hoteli Baada Ya Matibabu

Msanii aliyewahi kutamba kwenye kibao cha ‘Ntarejea’ Hawa Said amedaiwa kukaa kwenye hoteli aliyopangishiwa na staa wa Bongo fleva Diamond Platnumz.

Wiki chache zilizopita Diamond alitoa  zaidi ya milioni 400 kwa ajili ya matibabu ya mrembo Hawa ambaye alikuwa anasumbuliwa na maradhi ya ugonjwa wa moyo.

Baada ya kumaliza matibabu na Kurudi nchini Tanzania, Hawa amepangishiwa hoteli ambapo atakaa kwa muda wa miezi mutate ili kuepusha usumbufu.  

Kwenye mahojiano aliyofanya na Gazeti la Risasi Jumamosi, mama wa Hawa, Ndagina Kapera alithibitisha mtoto wake kurejea salama kutoka nchini India alikokuwa kimatibabu akiwa na afya ambapo baada ya kutua amepangishiwa chumba hotelini kwa ajili ya kuepusha usumbufu wa kelele.

Hawa amepewa masharti ya kukaa sehemu iliyotulia, isiyo na kelele kutokana na tatizo lake la moyo hivyo amepangishiwa hoteli moja hapa jijini Dar (jina linahifadhiwa) na meneja wa Wasafi (Hamis Taletale ‘Babu Tale’) kwa muda wa miezi mitatu mpaka afya yake itakapotengamaa“.

Mama huyo ameweka wazi shukrani zake za dhati kwa Msanii Diamond Platnumz kwa Kuokoa maisha ya Mtoto Wake.

“Natamani BASATA Waniruhusu Kuperfom Mwanza”- Rayvanny

Msanii wa muziki wa Bongo fleva kutoka katika label ya WCB Rayvanny ameibuka na kuwaomba tena BASATA wampe ruhusa ya kuperfom wimbo wa Mwanza stejini.

Wiki chache ziliopita Baraza la Sanaa Tanzania (BASATA) liliufungia rasmi wimbo wa ‘Mwanza’ wa Rayvanny aliomshirikisha Diamond Platnumz kwa madai ya kukiuka maadili ya Kitanzania kwa kuimba matusi.

Kwenye mahojiano aliyofanya na Gazeti la Ijumaa, Rayvanny alisema angetamani sana kwa mara ya kwanza apafomu Wimbo wa Mwanza katika jukwaa la Wasafi Festival lakini anashindwa kutokana na adhabu ya Basata ya kuufungia wimbo huo ambao yeye anakiri kuwa hakuutunga kwa nia ya kupotosha watu bali kuburudisha.

Kiukweli natamani sana wangeniruhusu tu japo nipafomu katika shoo zangu maana mapokezi ya huu wimbo ni makubwa mno mpaka yananifanya nitamani kuupafomu katika jukwaa la Wasafi Festival Jumamosi hii”.

WCB wanategemea kupigwa bonge la shoo kwenye tamasha Lao la Wasafi Festival linalotarajiwa kufunguliwa rasmi Jumamosi hii tarehe 24 mkoani Mtwara.

“Wasafi Festival ni Tamasha Kubwa Halijawahi Tokea Tanzania”-Afande Sele

Msanii mkongwe wa Muziki wa Bongo fleva nchini Afanse Sele ameibuka na kuweka wazi kuwa hivi sasa hakuna msanii mkubwa Kama alivyokuwa Diamond na hivyo tamasha lake la Wasafi Festival ndio litafunika.

Suala hili limekuja kutokana na sakata linaloendelea kupamba moto hivi sasa la mabishano ya Nani zaidi kati ya Wasafi Festival na Tamasha la Clouds la Fiesta.

Kwenye mahojiano aliyofanya na kituo kimoja cha habari, Afande Sele ameibuka na kusema hivi sasa Tamasha kubwa sana Tanzania ni Wasafi Festival na halina mpinzani kumaanisha Fiesta linakalishwa na Wasafi.

Unajua hivi sasa Wasafi ndio Real Madrid ya Tanzania ndio tamasha bora  na linaonekana kuja kuwa kubwa kuliko yote kwaiyo kushiriki katika tamasha la Wasafi ni fahari na pia naunga mkono juhudi za wadogo zetu ambao wameamua kukata minyororo ya watu waliokuwa wanatufanya watumwa na kutunyanyasa kwaiyo Wasafi ndio mapinduzi ya burudani kwanza inaongozwa na wasanii wenyewe”.

Lakini pia Afande Sele amewatolea Povu zito Clouds Fm na kuwatolea tuhuma za kutumia nguvu zao na cheo chao kuwanyanyasa wasanii na kuwataka wafanye vile wanavyotaka wao.

“Wasanii Kuweni na Misimamo na Hata Mnapotakiwa Tajeni Dau Manalolitaka”-Diamond Platnumz

Msanii wa muziki wa Bongo fleva na CEO wa WCB Diamond Platnumz ameibuka na kuwataka wasanii kuwa na msimamo na kuchagua malipo yanayoweza kuwafaidisha wao na familia zao.

Maneno hayo yamekuja ikiwa ni muendelezo wa mivutano kati ya Wasafi na Clouds Fm ambapo Diamond na timu yake nzima wamekuwa wakimtuhumu Ruge ambaye ni Mkurugenzi wa Clouds kwa kuwanyonya na kuwaonea wasanii.

Baada ya mvutano wa muda mrefu na majibizano yao ya siku mbili hizi kuchochewa na shoo zao zitakazofanyika jumamosi ambapo Fiesta mwaka huu imeweka wasanii wengi ambao ni wakongwe na Wasafi wanaamini wamefanya hivyo Baada ya kuwapa changamoto.

Kupitia ukurasa wake wa Twitter, Diamond amewndelea kuwatupia vijembe Clouds na kuandika haya:

Miriam Odemba Akiri Kutamani Kuzaa na Diamond

Mwanamitindo na mlimbwende Miriam Odemba anefunguka na kuanika mapenzi yake kwa staa wa Bongo fleva Diamond Platnumz na kukiri kuwa anatamani kumzalia Mtoto wa nne.

Ijumaa Wikienda linaripoti kuwa Miriam Odemba alifunguka hayo kwenye mahojiano waliyofanya naye kwa njia ya simu kutokea nchini Ufaransa anapoishi sasa.

Kwenye mahojiano hayo Miriam alijikuta akimfungukia Diamond kwa kusema amekuwa akiangalia mwenendo wake na kumuona ni ‘baba bora’ hivyo si vibaya akimzalia mtoto mmoja.

Odemba alisema anafuatilia watoto wa Diamond, wale wawili aliozaa na mwanamama mjasiriamali wa Kiganda, Zarinah Hassan ‘Zari The Boss Lady’ na yule wa mwanamitindo Hamisa Mobeto na kugundua anawalea vizuri, kitu ambacho kinamshawishi na yeye awe tayari ‘kumtunuku’.

Diamond nampendaga pia anavyojua kuangalia watoto wake mpaka kuna wakati natamani mimi ningezaa naye mtoto mmoja pia ni  kijana mdogo, lakini anaweza kujali familia yake na watoto wake japokuwa hayupo vizuri na mama wa watoto hao (Zari na Mobeto), hapo ndipo anaponikosha sana”.

Alipoambiwa afafanue kwa njia gani anaona Diamond anawajali watoto wake, Diamond alifunguka:

Unajua mara nyingi naweza kumuona anatoka Tanzania na kwenda Sauz (Afrika Kusini), kwa ajili ya kuona watoto wake japokuwa hayuko tena kwenye mapenzi na mzazi mwenzake”.

 

Diamond Awatupia Kijembe Clouds Fm Baada Ya Kumgeukia RC Makonda

Msanii wa muziki wa Bongo fleva na Mkurugenzi wa  WCB Diamond Platnumz ameibuka na kuwatupia kijembe Clouds Fm Mara Baada ya kumgeukia RC Makonda.

Sakata la Wasafi Festival na Fiesta limeendelea kupamba moto ambapo inaonekana live kwamba kila mmoja anataka apige tamasha kubwa kuliko mwenzake.

Kwa muda mrefu kumekuwa hakuna maelewano kati ya pande hizo mbili kwaiyo ilivyotokea uwezekano wa kuwepo tamasha kwa siku moja lakini katika Mikoa tofauti.

Diamond Platnumz amewarushia kijembe Clouds Fm kwa kusema wameomba poo kwa mlezi wao akimaanisha Paul Makonda Baada ya kuonekana akilitangaza tamasha hilo na kuwataka watu wajae siku ya tukio.

Inafahamika kwamba mlezi wa Wasafi ni mkuu wa mkoa wa Dar Es Salaam Paul Mkonda hivyo baada ya jana Clouds kumtumia Makonda katika moja ya video akiongelea inshu ya Ruge na kwamba yeye mwenye atakuwepo Fiesta imekuwa habari nyingine tena.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Diamond ameandika:

Diamond Aiangukia BASATA Aomba Japo Kuperfom ‘Mwanza’ Stejini

Msanii wa muziki wa Bongo fleva na CEO wa WCB Diamond Platnumz ameibuka na kuiomba ruhusa Baraza la Sanaa kutumia wimbo wake walioufungia wa Mwanza kuperfom stejini.

Wiki chache zilizopita wimbo wa ‘Mwanza’ ulitoka lakini mara moja BASATA waliufungia wimbo huo kwa madai ya kukiuka maadili ya Kitanzania kwa kubeba ujumbe wenye lugha ya matusi.

Lakini Diamond Platnumz amefunguka na kuwaomba Basata kuutumia wimbo wao ba Rayvanny wa Mwanza kwenye tamasha lao la Wasafi Festival 2018.

Kupitia ukurusa wake wa Instagram Diamond ameandika hayo.

Wasafi Festival Kuwashusha Wizkid na Mr. Eazi

Mkurugenzi wa WCB Diamond Platnumz amethibitisha ujio wa staa wa muziki kutoka Nigeria  Wizkid kwa ajili ya kuperfom katika tamasha la Wasafi Festival.

Diamond Platnumz  amethibitisha hilo kupitia ukurasa wa Instagram baada ya ku-comment kwenye post ya Rayvanny ambayo alipost video fupi ikiwaoyesha Diamond na Wizkid muda mfupi baada ya kumalizika kwa tamasha kubwa la muziki la One African Music Festival lililofanyika Dubai wikiendi iliyopita.

Kwenye video hiyo Diamond alithibitisha kuwa atamshusha msanii huyo mkubwa Afrika kwenye tamasha hilo litakalofanyika Dar Es Salaam baada ya kuzunguka mikoa mingine.

Lakini pia na msanii Harmonize ameamua kuweka wazi meseji zake alizokuwa anawasiliana na msanii kutoka Nigeria akiomba kuja kushiriki angalau katika moja ya tamasha la Wasafi Festival Tanzania.

Mama Mobetto Atoa Masharti Mazito Kwa Mkwe Wake

Mama mzazi wa Msanii wa Bongo fleva na mwanamitindo Hamisa Mobetto, Shufaa Rutiginga maarufu kama Mama Mobetto ameibuka na kutoa masharti kwa Mpenzi wa mwanaye.

Mama Mobetto amefunguka hayo Baada ya picha kusambaa kwenye mitandaoni ya kijamii zilizomuonyesha Hamisa na Mpenzi Wake Josh Adeyeye nchini Marekani.

Kwenye mahojiano na Global Publishers, Mama Mobetto alipoulizwa kuhusu picha hizo alisema, msimamo wake ni kwamba, hata kama picha hizo zinaonekana na yeye kuziona kwenye mitandao lakini bado anamtambua tu kama hawara.

Mama Mobeto alisema, kama kweli jamaa huyo anamhitaji mwanaye basi masharti anayompa ni kufika nyumbani kwanza nyumbani kwake kujitambulisha ili amjue vizuri yeye pamoja na ndugu zake.

Hivi jamani umeona wapi mzazi ambaye anajua maadili amuongelee hawara wa mtoto wake ambaye hajatambulika rasmi? Aje nyumbani, ajitambulishe, hapo sasa nitakuwa free kumuongelea, lakini habari za kwenye mitandao siwezi kuzizungumzia”.

Mobetto alimuanika Mpenzi Wake huyo siku chache zilizopita baada ya kuisha kwa mahusiano na aliyekuwa Mpenzi na baba mtoto Wake Diamond Platnumz.

WCB Watangaza Mdhamini Wa Wasafi Festival, Ali Kiba Atupwa Kule

Msanii wa Bongo fleva na CEO wa WCB Diamond Platnumz ametangaza kinywaji rasmi kitakacho dhamini Tamasha la Wasafi Festival linalotegemewa kuanza tarehe 24 November.

Mpaka siku ya jana ilikuwa inaaminika kwamba Ali Kiba kupitia kinywaji chake cha Mo Faya ndio watakuwa wadhamini rasmi wa Wasafi Festival hii ni Baada ya Diamond kukubali mwaliko wa Ali Kiba kudhamini tamasha hilo.

Siku mbili zilizopita Diamond alitangaza kuwa kinywaji Fulani ndio kitadhimini kinywaji hiko ambapo kupitia ukurasa wake wa Twitter aliandika:

Management imenambia kuna Kinywaji kesho kinaingia Rasmi onboard kama Mdhamini Mkuu wa #WasafiFestival2018 …Labda nikitaarifu tu kuwa kijiandae kutengeneza Storck za kutosha maana sio tu kunywewa, bali hata wengine watataka kukiogea kwa promo ntayokipa…. “.

Lakini jambo hilo limekuwa tofauti kwani usiku wa jana Diamond ametangaza kuwa kinywaji rasmi kutakacho dhamini Tamasha la Wasafi Festival ni Pepsi ambapo kupitia ukurasa wake wa Instagram ameandika:

https://www.instagram.com/p/BqNo1pehxso/?utm_source=ig_share_sheet&igshid=irbye9kwk5xm

Mpaka sasa bado haijajulikana Kama Ali Kiba Kupitia Mo Faya bado atadhamini tamasha hilo au ndio basi katupwa kule lakini hawajatoa mrejesho wowote.

“Kukua Kwa Sanaa Haimaanishi Lazima Wasanii Waimbe Matusi, Tubadilike”-Mwana FA

Msanii mkongwe wa muziki wa Bongo fleva anayetamba kwa miondoko yake ya kuchana Mwana FA amesema kuwa kukua kwa sanaa nchini sio lazima wasanii watunge nyimbo zenye maudhui machafu au video zenye muonekano mbaya kwenye jamii, bali ni kufanya kazi kwa bidii na kwa kufuata kanuni na sheria.

Mwana FA amefunguka hayo alipokuwa anaongelea sakata linalokamata headlines hivi sasa la Wimbo wa Rayvanny na Diamond kufungiwa kutokana na kudaiwa kukiuka maadili ya Kitanzania.

Kwenye mahojiano aliyofanya na Bongo 5, Mwana FA alifunguka haya zaidi:

Mimi napenda kuwashauri wasanii kuwa wanapotoa kazi zao wahakikishe wanatoa nyimbo ambazo zitaburudisha Lakini pia zisivuke mipaka ya kuharibu jamii kwasababu ukuaji wa Sanaa sio lazima wasanii watukane kwenye nyimbo au wawe uchi kwenye video zao hapana tubadilike kuna njia nyingi sana zilizo kwenye maadili”.

Mwana FA amesema hayo jana Novemba 14, 2018 muda mfupi baada ya kutoka BASATA ambako alienda kuwaombea msamaha wasanii wa WCB, Diamond na Rayvanny kuhusu kufungiwa wimbo wao wa Mwanza

Hawa Atoa Shukrani Zake Kwa Diamond na WCB Baada Ya Kumaliza Matibabu

Msanii wa Bongo fleva Hawa Said maarufu kama Hawa ntarejea wa Diamond amevunja ukimya Mara Baada ya kumaliza matibabu nchini India na kumshukuru Diamond na WCB.

Msanii Diamond Platnumz na timu nzima ya WCB ndio ilisimamia matibabu yote ya Hawa mpaka anapiga kabisa Baada ya kuugua mpaka kutaka kufa miezi michache iliyopita.

Mrembo huyo amemshukuru Mungu pamoja na Watanzania kwa dua zao kwani mpaka sasa anaendelea vizuri na uvimbe wa tumbo umeondoka kwa asilimia kubwa.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Babu Tale ameweka wazi salamu kutoka kwa Hawa:

https://www.instagram.com/p/BqM4FSDlEiw/?utm_source=ig_share_sheet&igshid=1ex61xjcr1qbp

Awali msanii huyo wa kike aliripotiwa kuumwa ugonjwa wa ini lakini alipofanyiwa vipimo nchini India walimkuta na ugonjwa wa moyo.