Vj Penny Afunguka Jinsi Alivyokwepa Matusi Kwenye Mitandao Ya Kijamii

Mtangazaji wa Magic Swahili, Penniel Mungilwa maarufu kama VJ Penny amefunguka na kueleza jinsi alivyoweza kuukimbia kabisa umaarufu kwenye mitandao ya kijamii na kuwa kimya.

Kwenye mahojiano aliyofanya na Global Publishers, Penny alifunguka kuwa kuna kipindi alikuwa gumzo sana midomoni mwa watu kila kukicha ambapo aliamua kujificha ili wamsahau na kweli alifanikiwa na hiyo ilimsaidia kufanya mambo yake mengine ya maendeleo zaidi.

Unajua kuna wakati watu wanaweza kukuzungumzia mpaka ukaogopa kabisa kukatiza mitaani na ndiyo iliyonitokea nikaamua kujificha na kuachana na maisha ya kujiachia klabu au sehemu za starehe, hii imenisaidia kwani wamenisahau na siku hizi wanajadili mambo mengine”.

Miaka minne iliyopita Penny alikuwa maarufu sana kwenye mitandao ya kijamii ambapo hiyo ilikuwa Baada ya kuwa kwenye mahusiano ya kimapenzi na Diamond Platnumz.

Lakini Penny alitoka kabisa midomoni kwa watu Mara Baada ya kuachana na Diamond na kuamua kukaa mbali na mitandao ya kijamii na hivyo kutoongelewa sana na mashabiki.

Diamond Awaomba BASATA Waruhusu Wimbo Wao Upigwe Muda Wa Usiku Watoto Wakiwa Wamelala

Msanii wa muziki wa Bongo fleva Diamond Platnumz ameibuka na kuliangukia Baraza la Sanaa Tanzania (BASATA) liruhusu japo wimbo wao na Rayvanny upigwe usiku watoto wakiwa wamelala.

Siku ya jana Baraza la Sanaa Tanzania (BASATA) lilitangaza kuufungia wimbo huo kwa madai ya kukiuka maadili ya Kitanzania kutokana na maneno yaliyoimbwa kwenye nyimbo hiyo.

Diamond ameibuka na kulalamikia uamuzi huo wa BASATA na kuwaomba wafikirie na kutafuta njia ya kuiacha nyimbo hiyo kuendelea kupigwa kwenye kumbi za starehe na ipigwe mida ya usiku watoto wakiwa wamelala Lakini pia ameomba wimbo huo urudishwe kwenye mtandao wa YouTube.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Diamond ameandika:

https://www.instagram.com/p/BqHLwGaFvfE/?utm_source=ig_share_sheet&igshid=1j577yw2ugopk

https://www.instagram.com/p/BqHM7WhlEou/?utm_source=ig_share_sheet&igshid=retbexv8i8mf

 

Rayvanny Afunguka Baada Ya Wimbo Wake na Diamond Kufungiwa na BASATA

Msanii wa muziki wa Bongo fleva kutoka katika label ya WCB Rayvanny amefunguka kwa Mara ya kwanza tangu wimbo wake wa ‘Mwanza’ aliomshirikisha Diamond Platnumz kufungiwa.

Siku ya jana Baraza la Sanaa Tanzania (BASATA) lilitangaza kuufungia wimbo huo kwa madai ya kukiuka maadili ya Kitanzania kutokana na maneno yaliyoimbwa kwenye nyimbo hiyo.

Rayvanny ameibuka na kulalamikia uamuzi huo wa BASATA na kusisitiza kuwa haikuwa maana yao kuimba matusi katika wimbo huo Bali ni Sanaa iliyotumika na kupelekea watu mawazo yao kufika huko.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Rayvanny ameandika:

https://www.instagram.com/p/BqG9rwonTtl/?utm_source=ig_share_sheet&igshid=mo32cxhbwmsv

https://www.instagram.com/p/BqG-WAGHFKG/?utm_source=ig_share_sheet&igshid=109chbj8a1coh

Diamond Amtupia Dongo Hamisa Baada Ya Kumuanika Mpenzi Wake

Msanii wa muziki wa Bongo fleva Diamond Platnumz amemtupia dongo zito aliyekuwa Mpenzi Wake na mzazi mwenzake Hamisa Mobetto Baada ya kumuanika mpenzi wake.

Wiki iliyopita Hamisa alimtambulisha rasmi Mpenzi Wake mpya anajulikana Kama Josh Adeyeye ambaye amekutana naye nchini Marekani alikoenda kwa ajili ya kupiga shoo.

Diamond ameibuka na kumtupia dongo zito Hamisa Baada ya Stori za Hamisa na Josh kupamba moto kola kona kwenye mitandao ya kijamii.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Diamond ameandika:

Najua mwili wangu ni mtamu, na najua bado unanitamani, ila usije ukadanganyika, hauwezi kuhimili stress“.

Hamisa na Diamond waliachana miezi michache iliyopita Baada ya kukiri kuwa kwenye mahusiano kwa miaka kumi ambapo Hamisa alikiri kumuacha Diamond Baada ya kuona hana muelekeo naye.

Mume wa Mama Diamond Afunguka Kuishi Madale Kwa Diamond

Mume wa Mama mzazi wa Diamond Bi. Sandra aitwaye Shamte Maisala ambaye kwa sasa ndiye baba wa kambo wa msanii Diamond Platnumz, amefungukia tuhuma za kuishi Madale.

Katika mahojiano yake na Global Publishers, Shamte amesema kuwa, anashangazwa na maneno hayo kwani ana kwake lakini anaishi Madale kwa kuwa kote ni nyumbani kwake. Amesema, kikubwa anachokitaka kutoka kwa mkewe ni heshima ya mume na anaipata hivyo suala la kuishi kwake siyo ishu.

Unajua watu wamekuwa wakihoji sana sababu ya mimi kumuoa mama Diamond na kuishi kwake lakini wanasahau kuwa zote ni nyumba, siku tukiamua kukaa Bunju (kwake) tutakaa na siku tukiamua kukaa Madale tutakaa kama tunavyokaa sasa, ishu si makazi bali ni heshima ya mume kwani napikiwa, nafuliwa na huduma zote napata”.

Baada ya Diamond kununua Jumba la kifahari maeneo ya Mbezi beach mapema mwaka huu aliamua kuhama Madale na kumuachia Nyumba mama yake na baba yake wa kufikia.

Queen Darleen Ajibu Tetesi Za Mama Yake Kufungwa China Kisa Madawa

Msanii wa muziki wa Bongo fleva na First Lady wa WCB Mwanahawa Abdul maarufu kama Queen Darlene amefunguka na kukana tetesi za mama yake kuwa kifungoni nchini China.

Miezi michache iliyopita kuna tetesi zilisambaa kwenye mitandao ya kijamii kuwa mama yake Mzazi na Queen Darlene amekamatwa nchini China Baada ya kukutwa na madawa ya kulevya na hivyo yupo jela akisota.

Katika mahojiano aliyofanya na Global Publishers juu ya ishu hiyo, Darleeen aliweka wazi kuwa, aliposikia hata yeye alishtuka na kwamba ni uvumi tu kwani mama’ke yupo hapa nchini na hapendi mambo ya mitandao.

Mama yangu kafungwa China? Niliposikia nilishangaa sana kwani mama yangu yupo na mtu akitaka anione nimpeleke nyumbani”.

Licha ya Queen Darlene kuwa na mama tofauti na msanii mwenzake na kaka yake Diamond Platnumz lakini Wana baba mmoja ambaye ni Mzee Abdul Juma.

“Nafarijika Kuona Unatabasamu Sasa”-Diamond Platnumz

Msanii wa Bongo fleva na Mkurugenzi wa WCB Abdul Naseb maarufu kama Diamond Platnumz amefunguka kuhusu matibabu ya msanii mwenzake Hawa Said.

Mwezi uliopita Diamond alitangaza kumpeleka Hawa nchini India kwa ajili ya matibabu ambapo alipofika alikutwa na ugonjwa wa moyo na kufanyiwa upasuaji.

Siku ya Leo meneja wa Diamond, Babu Tale aliweka wazi kuwa Mpaka sasa Hawa anaendelea vizuri na Ana afya njema kabisa Baada ya kufanyiwa upasuaji wa moyo.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Diamond ameweka wazi furaha yake Baada ya kuona afya ya Hawa imeimarika Lakini pia ameweka wazi hatomuacha mikono mitupu akisharudi Tanzania kwani amemtaka atafute biashara ya kufanya na yeye atamsaidia mtaji.

 

Babu Tale Aweka Wazi Hali Ya Kiafya Ya Hawa Kwa Sasa

Meneja wa staa wa Bongo fleva nchini Diamond Platnumz, Babu Tale ameweka wazi kuwa Mwanadada Hawa Saidi ambaye alikuwa anatibiwa nchini India anaendelea vizuri.

Hawa alikuwa na tatizo la ini ila ni moyo ndio uliokua unapelekea mgonjwa kujaa maji mwilini na Babu Tale ndio alipewa jukumu la kusimamia matibabu yake nchini India kwa kuwa gharama zote za matibabu alizitoa Diamond Platnumz.

Hawa alikuwa na tatizo la ini ila ni moyo ndio uliokua unapelekea mgonjwa kujaa maji mwilini na Babu Tale ndio alipewa jukumu la kusimamia matibabu yake nchini India kwa kuwa gharama zote za matibabu alizitoa Diamond Platnumz.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Babu Tale amesema wazi kabisa kwa sasa Hali ya Hawa inaridhisha kabisa tofauti na siku chache zilizopita kabla ya kupata matibabu:

Diamond aliweka wazi kuwa ametumia zaidi ya milioni 490 kumtibia Hawa ambaye miezi michache iliyopita alikuwa hoi kitandani nchini Tanzania.

Diamond Ampa Ali Kiba Ruksa Ya Kudhamini Wasafi Festival

Msanii wa muziki wa Bongo fleva Diamond Platnumz na msanii mwenzake Ali Kiba wameonekana kuelekea katika njia sahihi Baada ya Ali Kiba kuomba kuwa mdhamini kwenye Wasafi Festival na Diamond kukubali.

Kupitia, ukurasa wake wa Instagram, King Kiba ameshukuru kupokea mwaliko huo kutoka WCB na kudai kuwa hatoshiriki kwenye Tamasha hilo kwa sasa kutokana na kuwa na ratiba zake za uzinduzi wa kinywaji chake cha MoFaya na hivyo kusema atashiriki Tamasha hilo kwa kudhamini kupitia kinywaji chake hicho cha MoFaya.

Baada ya majibu hayo ya Kiba, Diamond Platnumz Baada ya kukutana na posti hiyo ya kiba aliamua kukomenti palepale kwa kumueleza kuwa uongozi wa WCB unaendelea kuwasiliana na uongozi wa RockyStar ili kuweka mambo sawa na kwamba tayari jambo hilo limeshapitishwa.

Limepita hilo Ally K@sallam_sk anamcheki Seven now… #DiamondKaranga#MoFaya#WasafiFestival2018 #NewBongofleva #BongoFlevaToTheWorld?@WasafiFM@WasafiFestival???????? “.

Baada ya Bifu la miaka Minho hatimaye Ali Kiba na Diamond wanaonekana kuelekea katika njia iliyonyoooka na kumaliza Bifu Lao.

Jibu la Ali Kiba Baada Ya Kualikwa na Diamond Lazua Utata

Siku mbili  zilizopita Staa wa Bongo fleva na mkurugenzi wa WCB Diamond Platnumz alimualika hasimu wake Ali Kiba kuperfom kwenye tamasha la Wasafi Festival litakaloanza siku za karibuni.

Lakini Ali Kiba amedaiwa kumjibu Diamond kimagumashi kwa kupost picha ya mchekeshaji maarufu duniani, Mr. Bean na kuandika maneno kadhaa.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Kiba amepost picha hiyo yenye maneno; ‘Thank you for listening, To my presentation’, halafu chini ya post hiyo akaandika “Your welcome”.

Mashabiki wengi walianza kuzungumza mitandaoni na kusema siyo rahisi kwa Alikiba kukubali kuungana na Diamond kwenye Wasafi Festival huku wengine wakisema Alikiba akubali tu, na hadi kufikia wengine kusema Alikiba atatoa jibu lake baya au la kizarau sana.

Mange pita aliweka wazi kuwa Ali Kiba hawezi kukubali kuperfom na Diamond kwani kwa kufanya hivyo itakuwa anajimaliza yeye kwani Bifu lake na Diamond likiisha tu basi na ndio mafanikio yake mwisho kwani anabebwa sana na Bifu na Diamond.

Mange Adai Ali Kiba Atapotea Kimuziki Bila Bifu na Diamond

Mwanaharakati wa mambo ya siasa kwenye mitandao ya kijamii Mange Kimambi amefunguka na kudai Bifu linaloendelea kati ya Diamond Platnumz na Ali Kiba linamfaidisha zaidi Kiba.

Sakata hilo limekuja baada ya msanii Diamond kutaka kumaliza Bifu lake na Ali Kiba Siku ya Jana Baada ya kumualika kushiriki katika tamasha lake la Wasafi Festival.

Mange amepima uzito ishu hiyo na kusema kuwa Ali Kiba Hatakiwi kupatana na Diamond kwani year ndio anafaidishwa na Bifu hilo Babu bila Bifu hilo ana hatihati ya kupotea kimuziki.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Mange Kimambi ameandika:

Sio kama nachochea ugomvi ila nimeongea fact tu. Tujikumbushe Ray na Kanumba. Mnalikumba beef lao? Siku Kanumba alipokosekana na lile bifu lilipokosekana Ray si alishuka na umaarufu ukapungua vibaya mno mpaka akapotea. .
So lile beef ndio lilikuwa linaibeba career ya Ray. Kwenye situation kama hizi yule ambae ndio msanii mkubwa zaidi huwa ana gain kiki kwenye beef ila anae gain sana ni yule mwingine. Beef la Ray na Kanuamba aliegain sana ni Ray ndo maana Kanuamba kukosekana akafulia.

Sasa naomba mu-ally hii concept to Diamond and Kiba. Then mtaelewa kwanini nasema hao wakipatana Diamond will win Kiba will loose. Diamond ndio ana benefit kwenye hili beef ila ana benefit kidogo mnoo anae benefit zaidi ni Kiba na ukijumlisha na dharau anazomfanyia ndio anazidi kupanda hata bila kutoa nyimbo ??. Ila wakipatana Diamond will gain everything and Kiba will loose everything. Wakipatana hao ndio utakuwa confirmation ya Diamond as the ONLY main artist wa Tz. Na Diamond is very strategic amelijua hili, keshajua kugombana na Kiba kuna faida ndogo sana kwake na faida kubwa sana kwa Kiba.Amestuka kuwa anamfaidisha Kiba. Na anajua akipatana na Kiba ni faida kubwa mnooo kwake na Kiba atapata faida ndogo. Ndo maana mnamuona Dai anahangaika staili izote ili mradi aelewane na Kiba. Anajua akielewana nae anampoteza mazima. Diamond sio mtu wa kujishusha kwa mtu kiasi hiki. He is very smart. Ana mahesabu yake. Ila na Kiba nae keshausoma mchezo ndo maana anampotezea tu ??. Na Diamond naamini amerealize hiki kitu kwenye seduce Me, maana alivyoleta ushindani ndio nyimbo ya Kiba ilinoga mara 1000 na watu waliisapoti kwa ushabiki na hasira ili wamkomeshe Dai. So So kaona bora amsogeze karibu ili ammalize kabisa abakie yeye ndio Konki Masta pekee wa bongo flava. .

Diamond Ampa Shavu Dudu Baya Kwenye Wasafi Festival

Msanii mahiri wa muziki wa Bongo fleva nchini Diamond Platnumz amempa shavu Nono msanii mkongwe  wa Bongo fleva Dudubaya baada kumtaja kuwa miongoni mwa wasanii watakaotumbuiza kwenye taamasha la Wasafi Festival 2018.

Katika mkutano wake na waandishi wa habari, Diamond ameweka wazi kuwa kuna wasanii wengi wakubwa ambao hawapati nafasi ya kutumbuiza kwenye matamasha makubwa kwa kisingizio kuwa hawajatoa nyimbo mpya.

Kaka yetu Dudu Baya muda mrefu watu hawajamuona kwenye show ya steji, sasa nawambia kwamba nitafurahi sana akiwepo kwenye show ya Wasafi Festival. Unajua sio tu Dudu Baya peke yake unajua kuna wasanii wengi wana sauti kubwa lakini sometimes hawapewi nafasi kwenye matamasha kwa sababu tu hawajatoa wimbo mwaka huu lakini kuna watu wanawapenda.

so wanaoandaa Wasafi Festival nitaongea nao na Dudu Baya pia wamuweke kwenye tamasha, nitafurahi kwa sababu nilikuwa tu namuonaga kipindi kabla sijatoka namuona anaimba”.

Dudu Baya au maarufu Kama Konki Konki Konki master amejizolea umaarufu Baada ya kendo yake inayoendelea kusambaa ya ushoga na bifu lake na Mange Kimambi.

Babu Tale-Tumeshaanza Kuwasiliana na Uongozi Wa Ali Kiba

Meneja wa msanii wa Bongo fleva Diamond Platnumz, Babu Tale amefunguka na kuweka wazi mipango yao ya kumpata msanii wa Bongo fleva Ali Kiba ili aweze kuperfom kwenye tamasha la Wasafi Festival.

Siku ya Jana kwenye mkutano na waandishi wa Habari Mkurugenzi wa WCB, Diamond Platnumz aliweka wazi mipango yao  ya kumpata Ali Kiba ili aweze kuperfom kwenye shoo yao.

Lakini sasa Meneja wa Diamond Babu Tale anafunguka kuhusu jitihada zao za kuwasiliana na Kiba ambapo amekiri kuwa hana mawasiliano na Kiba lakini anaelewana sana na meneja wake anayeitwa Seven.

Siongeagi na Alikiba kivile, mimi naongeaga na meneja wake maana alishawahi kunisaidia sana, lakini kuhusu inshu ya Wasafi Festival Sallam ameshaanza kuwasiliana na uongozi wa Alikiba”.

Baby Tale ameweka wazi kuwa siku ya uzinduzi wa Wasafi festival pamoja na wasafi fm mbali ya kuwepo kwa mipango ya kumpata Ali Kiba lakini pjs atakuwepo msanii Konki konki konki master Dudu baya katika tamasha hilo ambalo limeandaliwa na Wasafi media.

Mama Diamond Afungukia Uhusiano Wa Ommy Dimpoz na Zari

Mama mzazi wa staa wa Bongo fleva Diamond Platnumz, Bi. Sandra Kassim maarufu kama Mama Diamond amefunguka na kuongelea uhusiano na kinachoendelea kati ya Zari na Ommy Dimpoz.

Siku chache zilizopita msanii wa Bongo fleva Omary Nyembo ‘Ommy Dimpoz’ na mzazi mwenzake na Diamond Zari the Bosslady walitengeneza headlines baada ya picha zao wakiwa pamoja nchini South Africa kusambaa kwenye mitandao ya kijamii.

Kwenye mahojiano na gazeti la Risasi Jumamosi, Mama Diamond amesema kuwa ukaribu wa Zari na Dimpoz ni wa kawaida kama watu wengine na kuwataka watu waache maneno maneno yasiyo na msingi.

Kwani kuna ubaya gani? Hivyo ni vitu vya kawaida kwa mtu kukumbatiana na mtu aliyekutana naye Mimi sijaona hiyo picha ambayo kamshika pajani lakini bado nasema hayo ni mambo ya kawaida tu. Ina maana Zari asiongee na watu? Watu wanasema Nasibu na Ommy wana ugomvi, mimi sijaona wakipigana, najua wanaongea na wala mimi sina ugomvi na mtu”.

Siku za nyuma Diamond aliwahi kuingia kwenye ugomvi mzito na Ommy Dimpoz uliopelekea kutukanana matusi ya nguoni hadi Ommy kumkashifu Mama Dimoand lakini tangu alipougua kuna tetesi kuwa bifu hilo limeisha na wasanii hao wamesahameana.

 

Kim Nana Adaiwa Kubadili Dini Kisa Diamond

Video vixen anayetrend sana kwenye mitandao ya kijamii Lilian Kessy maarufu kama Kim Nana ambaye pia ni mpenzi wa staa wa Bongo fleva Diamond Platnumz anasemekana kubadilisha dini kutoka kuwa Mkristo mpaka muislamu kwa ajili ya ndoa na Diamond.

Gazeti la Amani linaripoti stori hiyo ambapo ndugu wa karibu na msanii huyo ambaye aliomba hifadhi ya jina, alisema kuwa Diamond kwa sasa yupo na uhusiano ambao upo ‘siriasi’ kwani amefikia hatua ya kumbadili dini mpenzi wake huyo ili waingie naye kwenye ndoa.

Nyie hamjui, wanaosema eti Kim Nana ametupiwa virago vyake nje huko Madale nyumbani kwa Diamond na mama yake, wamepitwa na habari, mwenzao Diamond kambadili dini anataka kumuoa kwani hata muda mwingi yupo na mama mkwe wake pale Madale”.

Wiki iliyopita kuna stori ilisambaa kuwa penzi la Diamond na Kim Nana lilifika mwisho mara baada ya mrembo huyo kutimuliwa nyumbani kwa Diamond Madale na Mama Diamond baada ya kutibuana.

Mama mzazi wa Diamond Bi. Sandra amefungukia tetesi hizo na kusema Kim Nana hajatimuliwa Madale bali yupo pale Kim yupo nyumbani kwake na sasa amebadilishwa dini na mwanaye ambapo anafundishwa kusoma Kuruani na mumewe Maisala Shamte ‘Anko’ na ndio maana wako karibu muda wote.

Kwa taarifa yenu Kim nipo naye muda mwingi na sasa amebadili dini, anafundishwa Kuruani na mume wangu kwa hiyo watu watasubiri sana kama wanadhani ataachwa leo wala kesho, hilo halitatokea”.

Mwanzoni mwa mwaka huu Diamond alimuahidi mama yake hatamaliza mwaka 2018 bila kuoa labda huu ndio muda muafaka wa kumuoa mpenzi wake huyo.

Mama Diamond Adai Kusubiri Kwa Hamu Harusi Ya Mwanaye

Mama mzazi wa msanii wa Bongo fleva Diamond Platnumz. Bi. Sandra Kassimu au maarufu kama Mama Diamond ameibuka na kudai kuwa anasubiri kwa hamu harusi ya mwanaye huyo licha ya kwamba hana taarifa itafungwa lini.

Mama Diamond amefunguka na kuweka wazi kuwa licha ya kwamba anasubiri kwa hamu harusi hiyo lakini hajui tarehe ya mwananye kuoa na wala hajui ataoa mwanamke gani.

Kwenye mahojiano aliyofanya na gazeti la Risasi Vibes, mama Diamond alisema licha ya kwamba Diamond ni mwanaye, lakini hawezi kumchagulia mwanamke wa kuoa kwani hata yeye hakuchaguliwa mwanaume wa kuwa naye hivyo kikubwa anachosubiri ni kusherehekea tu siku hiyo.

Unajua siwezi kumchagulia Diamond  mwanamke wa kuoa bali yeye mwenyewe ndiye atakayechagua maana hata kama watu wanavyosema amuoe Zari (mzazi mwenza wa Diamond) wakati wanakutana na kuanzisha uhusiano wao mpaka wakapata watoto mimi sikuwepo hivyo mambo ya kuoa ni uamuzi wa mtu mwenyewe”.

Diamond ameshazaa watoto watatu na wanawake wawili tofauti lakini mpaka hivi sasa hajamuweka wazi mpenzi wake na kudai yupo single licha ya kuonekana na wanawake kadhaa na hata wanawake hao kumgombania hadharani.