“Wema Sepetu Hajanifundisha Tabia Mbaya”- Diana Kimari

Muigizaji wa Bongo movie Diana Kimari amefunguka na kuweka wazi kuwa Msanii mwenzake Wema Sepetu hajambadilisha tabia kama wengi wanavyodai.

Siku za nyuma Wema na Diana walikuwa na ukaribu uliopitiliza na kusababisha maneno Mengi kuzungumzwa kwenye Mitandao ya kijamii ikiwemo tetesi za wawili hao kuwa kwenye mahusiano ya jinsia moja.

Katika Mahojiano aliyofanya na Global Publishers, Diana alisema watu wengi wanahoji kuhusu ule ukaribu wake na Wema kuwa haukuwa wa kawaida, huku wengine wakiongeza kwamba alikuwa anasali lakini tangu alipoanza kuwa karibu na staa huyo ameacha kitu ambacho amesema hakina ukweli.

Unajua zamani nilikuwa naposti sana mambo ya kanisani kwenye akaunti yangu, lakini mambo yalikuja kubadilika baadaye nikaona hakuna umuhimu tena wa mimi kuendelea kuposti kila kitu changu mtandaoni, hivyo watu wakadhani nimeacha kusali kitu ambacho si kweli, kutoposti hivyo vitu haimaanishi kwamba nimeacha ulokole wangu.

Pia mimi ni mdogo sio mkubwa kihivyo kwa hiyo mpaka sasa bado nipo chini ya uangalizi wa wazazi wangu hata kipindi naishi kwa Wema wazazi wangu walikuwa wanajua, kwa hiyo hawatakubali wanione naharibikiwa wakati wao wapo hai, wananichunga sana yaani sijui nisemaje“.

 

Mapenzi Hayana Nafasi kwa Diana

Mwanadada Diana Kimari amefunguka na kusema kuwa moja kati ya vitu ambavyo kwake sio muhimu sana ni kufanya mapenzi kuwa sehemu ya maisha yake  hata kama yuko katika mahusiano .

Diana anasema kuwa kitedno cha kuwa katika mahusiano na kuyaweka mbele sana kunaweza kufanya kushindwa kufanya vitu vingine  vya maana ambavyo anahisi vinaweza kumpa faida zaidi kuliko kile anachokifanya.

siyo kwamba sina mapenzi, ni kwamba sijamchukulia kihivyo huyo mwanaume kwa sababu naona kuna vitu vingine ninaona nina vitu vingi sana vya kufanya kwa sababu  nikijikita huko naona nitaharibu mambo mengi sana,  na ndio maana sitaki kumuonyesha mahali popote kwa sasa.