Sidangi , Sina Mazingira ya Kudanga :-Diana kimary

Mwanadada Diana Kimary ambae alitamba sana katika movies ya foolish age kipindi cha nyuma amefunguka na kusema kuwa watu wamekuwa wakishangaa na kumuambia kuwa amekuwa akidanga na ndio maana  maisha yake amekuwa mazuri kwa sasa lakini swala hilo sio kweli.

Diana anasema kuwa swala hilo sio kweli kwa sababu kwa malezi anayoishi nyumbani kwao ni vigumu sana kufanya hivyo kwa sababu ,malezi na mazingira ya kwao hayaruhusu kufanya hivyo hata kidogo.

Diana anasema “mimi sidangi kwa sababu sina mazingira ya  kunifanya niwezi kudanga, kwetu mimi ni mdogo kabisa”

Diana Kimary Agoma Kumuacha Wema Sepetu

Muigizaji wa Bongo movie Diana Kimary ameibuka na kudai kamwe hawezi kuacha kuwa na ukaribu na na staa wa Bongo movie Wema Sepetu kwa sababu tu watu wanataka iwe hivyo.

Kutokana na skendo iliyompata Wema siku za Hivi karibuni Baada ya kuachia video za utupu kwenye ukurasa wake wa Instagram, wadau kadhaa walimtaka Wema kubadilika na hata kubadili aina ya marafiki aliokuwa nao ikiwemo Diana.

Kwenye mahojiano aliyofanya na Gazeti la Risasi Jumamosi, Diana amesema hawezi kupelekeshwa na maneno ya watu wanaomtaka asiwe na ukaribu na Wema.

Wanaodhani na mimi nimewekwa mbali na Wema na ndiyo maana simposti kwenye ukurasa wangu wa Insta kama ilivyokuwa huko nyuma, wanachekesha.

Niwafahamishe tu kwamba hakuna wa kunitenganisha na Wema, yule ni rafiki, ni kama dada yangu, tumegandana, manenomaneno sitaki, waniache na maisha yangu”.

Tangu sakata lake la kuvujisha picha za faragha Wema amekuwa kimya na kuonekana mahakamani ambapo amekuwa akifuatilia kesi yake hiyo.

Ukaribu na Wema Sepetu Wamponza Diana Kimary

Msanii wa fialmu za Bongo movie mrembo Diana Kimary amefunguka na kuweka wazi kuwa hajali manneo ya watu ambayo yamekuwa yakusemwa kuhusu yeye kuwa na ukaribu na Wema Sepetu ambapo amedai hajali na acha waendelee kumnanga lakini hawajui maisha yake halisi.

Diana Kimary ameonekana kuwa karibu sana na Wema Sepetu ambapo amekuwa akimuita dada lakini ukaribu huo umekuwa ukiibua maneno mengi sana  kwenye mitandao ya kijamii na kupelekea kusemwa sana na mashabiki.

Kwenye mahojiano aliyofanya na gazeti la Ijumaa, Diana alisema kuwa watu wengi kwenye mitandao ya kijamii hawajui kabisa maisha halisi ya mtu zaidi ya kukisia na kumsema vyovyote wawezavyo ndio maana hawafuatilii.

Unajua ni hivi wamenisema sana hapa katikati lakini hawajui kamwe maisha yangu na uzuri najitambua havinisumbui kabisa najua nini nataka maishani mwangu kwa hiyo hata kama wakinitukana ni sawa kwa vile siwalipii bando”.

Diana amekuwa na ukaribu na Wema kwa kipindi sasa ambapo ukaribu huo umemfanya hadi kujichora tattoo yenye jina la Wema.

 

“Sina Bifu na Mobetto Lakini Nampenda Wema”-Diana Kimary

Muigizaji wa Bongo movie Diana Kimary amefunguka na kudai hana bifu wala hamchukii Hamisa Mobetto ila tu anampenda sana Wema Sepetu.

Diana Kimary ambaye siku za hivi karibuni ameonekana kuwa na Ukaribu sana na Wema ameweka wazi kuwa watu wengi wanadhani yeye ana bifu na Mobetto kwa sababu yuko na Wema jambo hilo sio la kweli.

Kwenye mahojiano na gazeti la  Ijumaa Wikienda, Diana ambaye hivi sasa yupo karibu na Wema alisema watu wengi wanajua ana bifu na Mobeto, lakini wanashindwa kuelewa anapoweka vitu vyake kwenye mtandao wake wa kijamii wa Instagram havilengi kumsema mtu.

Simchukii na wala sina tatizo na Hamisa (Mobeto)kama watu wanavyotengeneza kwenye mitandao, bali wakiona namuweka Wema ni kwa vile nina mapenzi kama yote kwake pia hata nikiandika ujumbe simsemi mtu”.

Wema na Mobetto wametajwa kuingia katika bifu zito kwa sababu ya Jina la ‘Tanzania Sweetheart’ ambapo mashabiki wamedai wamemvua Jina hilo Wema na kumvalisha Mobetto jambo ambalo Wema amepingana nalo.

Diana Kimary Adaiwa Kutimuliwa Kanisani Baada Ya Kufaidi Penzi La Mchungaji

Msanii wa filamu za Bongo Movie Diana Kimary ameingia Kwenye headlines kwa skendo ya mwaka baada ya kudaiwa kutimuliwa kanisani alipokuwa anasali baada ya skendo ya Kimapenzi na Mchungaji.

Global Publishers wanaripoti kuwa Diana amelikacha kanisa alilokuwa akisali awali la Nabii Mwamposa lililopo Mwenge jijini Dar. Mwigizaji huyo anadaiwa kukacha baada ya kuibuka kwa skendo kuwa anatoka na mmoja wa wachungaji wa kanisa hilo.

Inadaiwa kuwa taarufa zilianza kusambaa kanisani hapo kwa waumini mbalimbali na hata wa nje ya kanisa hilo, jambo ambalo lilikuwa chukizo kubwa kwa Diana na kuamua kukata mguu kidogokidogo hadi akapotea kabisa, pamoja na kwamba alikuwa mhudhuriaji mzuri wa kanisa hilo.

Baada ya skendo hiyo nzito kuzuka juu yake gazeti hilo lilimsaka ili kupata ukweli wa mambo ambapo alifunguka kuwa:

 Kwanza ngoja niliweke wazi hili jambo. Ieleweke kwamba mimi sijawahi kufukuzwa kanisani kama wanavyosema, bali niliamua mwenyewe kuhama na kusali kanisa lingine, na kilichonifanya nikahama Unajua pale kulizuka maneno mengi sana ya kuwa mimi natembea na mchungaji, jambo ambalo sikulipenda, ndipo nikaamua kuhama hapo kanisani”.

Diana aliendelea kufunguka na kutaja sababu ya waumini Wenzake kumzushia uzushi huo:

Unajua mtu anaweza kukuona msichana mdogo labda akajua una mafanikio au ukivaa ukapendeza watu wanakuchukulia tofauti na kingine nafikiri ni wivu tu”.

 

Mrembo Aliyechora Tattoo Ya Jina La Wema Afunguka

Msanii wa Bongo movie anayejulikana kama Diana Kimary amefunguka na kueleza sababu hasa za kuchora Tattoo ya Jina la Msanii Wema Sepetu Kwenye mwili wake.

Siku ya jana Diana alitengeneza headlines baada ya video iliyomuonyesha akiwa amechora tattoo hiyo kusambaa Kwenye mitandao ya kijamii na kupelekea gumzo.

Kwenye mahojiano na Sam Misago Tv, Diana amefunguka kuhusu Tattoo hiyo na kusema ameamua kumchora Wema kwa sababu mbali na urafiki Lakini pia ni dada yake na anampenda Sana.

Nampenda sana Wema kwa sababu amekuwa dada mzuri kwenye Maisha Yangu”.

Hii siyo mara ya kwanza kwa Tanzania sweetheart Wema Sepetu kuchorwa Kwenye mwili wa mtu kwani miaka ya nyuma Kajala Masanja alishwahi kuchora Tattoo kubwa yenye Jina la Wema lakini baada ya ushoga kuisha aliifuta.