“Bongo Kinabalu Mastaa Kibao Wanafanya Vitendo Vichafu R. Kelly Nyuma”- Diva

Mtangazaji wa Clouds Fm mrembo Loveness Malinzi maarufu kama Diva The Bawse amefungukia Sakata la Msanii mkubwa wa RnB Kutoka Marekani R.Kelly.

R. Kelly anatuhumiwa kwa kufanya vitendo vya unyanyasaji dhidi ya wanawake na ubakaji wa wasichana kuanzia umri wa miaka 12, 13 na kuendelea ambapo madhambi yake yalianikwa kwenye documentary ya ‘Surviving R. Kelly’.

Diva amepima uzito Suala hilo na kusema vitendo hivyo pia vinafanywa na wasanii wakubwa hapa Tanzania ambapo kupitia ukurasa wake wa Instagram, ameandika:

Nimeangalia #SurvivingR.Kelly toka juzi sijashangaa sana kiukweli zaidi ya kuumia. Tatizo liko kote. Kwa wazazi hasa. watu wengi ambao ni wanaitwa role model duniani watu maarufu wengi ni wachafu sana. Sana sana sana. Hata hapa Tanzania wapo zikiruhusiwa docuseries kama hizi tutasikia mengi sana na kuna hata watasema mtu anasingiziwa ili achafuliwe sababu pia fans hawa nao bendera fata upepo sana. Kwanza ndio wanapenda mambo ya ajabu .. So mejiuliza all the time ilikuwaje wakawa kimya? Na wasichana nao wakiona watu maarufu shobo nyingi sana zinakuwa … ndio matokeo kama haya . Very sad … as a woman i was truely hurt kwakweli. Tena hakunaga role model jaman watu hawako kama mnavyowafikiria. Huwa nakaa mbali sana na mwanaume anaenyanyasa mwanamke kwa njia yoyote ile .. awe rafik awe nani nakaa mbali …very heartless. Huwa i distance myself kabisa. The Love i have for Rkelly and his Music … im in pain . Na mauzo yake yameongezeka to 15% unaambiwa …. yan he is on top right now after the docu series. Smh …. wish hizi nazo zitokee Tanzania wanawake wawe free kuelezea wanavyoface kwa so called Role model mnaweza choka mshangae.. shame man!! The fact that uchunguzi umeanza na system ya america ime take action ngoja tuone ukweli ni upi. Ila wanaume jaman .. hii jamii . Watu kama hawa wamejaa …ila wuld luv to hear his side of the story kwakwel duh! Sad Gosh”.

 

Diva Akana Kuwa Kwenye Mahusiano na Mo J Wa Gigy

Mtangazaji wa kipindi cha Ala za Roho cha Clouds FM Loveness Malinzi maarufu Kama Diva The Bawse ameibuka na kukana tetesi kuwa yupo kwenye mahusiano ya kimapenzi na Mo j.

Mo J ambaye pia ni mtangazaji wa Choice Fm amezaa Mtoto mmoja na video vixens na msanii wa Bongo fleva Gigy Money ambaye Mtoto wao anaitwa Mayra.

Wiki chache zilizopita kuna taariza zilisambaa kuwa Baada ya Gigy na Mo J kuachana Diva ameanzisha mahusiano na Mo j ambapo taarifa hizo zilichochewa na video iliyosambaa kwenye mitandao ya kijamii iliyomuonyesha Diva na Mo J pamoja.

Lakini sasa Diva amekana tetesi hizo na kuweka wazi kuwa hana mahusiano ya kimapenzi na Mo j zadi ya mahusiano ya kikazi ambapo kupitia ukurasa wake wa Instagram, Diva ameandika:

Naomba kwa heshima na taadhima nitoe tamko… Leo Ngoja nijibu..sababu nimejisikia afu pia mechefukwa tu yan na baadhi ya vitu na watu . . oky ni hivi Apa juzi kati niliona sana Picha Zangu na @moj360 kwamba tuna mahusiano. Nilipata simu nyingi za waandishi na nahisi niliwajibu sana short n clear sababu pia sikutaka mahojiano na mtu yan…… Yan mechoka kujielezea nilikuwa yan naona fresh whatever…. Truth is sijawahi kuwa na mahusiano na @moj360 yan ata kutongozana hatujawahi tunaheshimiana sana. Ni vile mliona mtu anaefanana nae tukiwa katika video ya Pamoja. Thought i said this once n im saying this again. Sina plan ya kumpost mtu apa uso ata niwe nae vipi. I prefer privacy siku hizi mekuwa. Kwanza medate watu wachache sana in the undustry kiukweli kweli Some zilikuwa stunts si zaid. kwanza nshakuwa mfanyabiashara nawaza hela zaid…and how to protect my brand na kutoka katika midomo ya watu kwa njia mbaya. Negativity stak.. Damn it work so hard to be here aisee. Living to the fullest livin ma life like happy n shit. Hard work y’all kno.. So ndugu jamaa na marafiki na mashabiki poleni kwa usumbufu. Xoxo Lovely Diva #temporarypost“.

 

Diva Nae Aibuka na Jina la Tanzania SweetHeart

Kwa muda mref warembo Wema Sepetu na Hamisa mobeto wamekuwa wakigombania jina la kuwa Tanzania Sweetheart jina ambalo alipewa Wema miaka ya nyuma na mashabiki zake kutokana na kupendwa sana na mashabiki zake na tanzania nzima kwa ujumla, hata hivyo jina hilo kwa sasa linaonekana kulegalega baada ya mashabiki wa Hamisa pia kutoka kumkabidhi jina hilo msanii wao hamisa.

Vita hii ya jina imekuwepo kwa muda mrefu mpaka kufikia hatua ya baadhi ya mastaa kuingilia kati na kila mmoja kusema msimamo wake huku wengi wakitaka libaki kwa mwenyewe Wema , hata hivyo baadhi ya watu hao ni pamoja Diva the bawse ambae ameibuka lakini kwa kutaka kumtetea Hamisa.

Tanzania sweetheart, africa sweetheart, word sweetheart, asietaka anywe panadol extra,  ndo nishasema point blank period, mi sipendi kabisa tabia ya kupindisha  maneno nimeyaweka wazi kabisa kuwa my baby @hamisa mobeto  came through dripping, we nyoosha tu baby,..hakuna namna we damshi tu kote , am so proud of hard working mama….jamani you all know kuwa mimi sina matatizo na mtu maana mapovu kama yote.

Diva anasema kuwa watu watamshangaa kuona akimtete Hamisa lakini wakae wakijua kuwa yeye na hamisa ni marafiki wa muda mrefu sana na kwamba ushoga wao umekuwa prvate kila siku kwa sababu sio lazima kila mtu ajue.

 

Diva Alia Kukosa Mtoto, Awaomba Watanzania Wamchangie Milioni15

Mtangazaji wa Clouds Fm Loveness Malinzi maarufu kama Diva The Bawse amefunguka na kueleza kuwa anahitaji mchango wa kiasi cha dola $7,000 ambazo ni sawa na milioni 15 za Kitanzania, kwa ajili ya matibabu ya kumsaidia kushika mimba.

Diva amefunguka hayo kupitia ukurasa wake wa Instagram ambapo amesema kuwa mwezi uliopita alienda Hospitali ya TMJ kufanya vipimo na aliambiwa kuwa mirija yake ya uzazi ina hitilafu (blockage) hivyo hawezi kutunga mimba kwa njia ya kawaida mpaka kwa mfumo wa kisasa wa kupandikiza mbegu wa IVF Treatment.

Diva amesema kuwa anajua kuna wanawake wengi wenye matatizo kama yake hivyo kufanya hivyo kutawafanya na hao wapate nafuu na kutambua kuwa tatizo hilo ni kubwa kwenye jamii Lakini pia ameomba kuchangiwa kupitia akaunti yake ya Go Fund me na akaunti ya benki.

https://www.instagram.com/p/Bmro7lBlMzA/?utm_source=ig_share_sheet&igshid=eeg3cvxfu0ss

 

https://www.instagram.com/p/BmrqMyVluqP/?utm_source=ig_share_sheet&igshid=1hqz5l0xipo0r

 

https://www.instagram.com/p/Bmrq7EylF5p/?utm_source=ig_share_sheet&igshid=17w1bkawga15d

 

https://www.instagram.com/p/BmsCnu2F1vl/?utm_source=ig_share_sheet&igshid=12klthh8hclxk

 

Diva Aweka Wazi Ugonjwa Unaomfnaya Asipate Mtoto, Aomba msaada wa Matibabu

Mwanadada Diva the bawse amefunguka na kueleze maumivu yake anayoyapitia kwa sasa kutokana na ukweli kwamba ameambiwa kwake itakuwa ngumu sana kupata mtoto kwa sasa kutokana na blockage kubwa iliyopo katika mirija yake ya uzazi.

Diva ambae anasimulia sababu kubwa iliyomfanya kuchunguza ili kujua kama anaweza kupata mtoto ni tamaa kubwa aliyonayo sasa hivi kuhusu kupata mtoto na ndipo alijiuliza kwa muda mrefu kwanini amekuwa akinywa dawa nyingi sana lakini hawezi kushika mimba.

Diva ambae anasema kuwa katika maisha yake aliwahi kupata mimba lakini haikukaa miezi minne , mimba hiyo liharibika na hiyo ndio ikawa kama mwisho ya ndoto zake kubwa za kuzaa tena katika maisha yake.

Hata hivyo diva anasema kuwa kwa madatari waliomshauri na kumpima katika hospitali aliyokuwa amekwenda, wamemwambia anaweza kupata matibabu ya tatizo lake nje ya nchi lakini ndio inacost pesa nyingi sana.

Kwa sasa diva amewaomba mashabiki na watu wake wa karibu , kumuombea na kama kuna atakaeguswa na hali yake basi anaweza kumsaidia kwa chochote ili aweze kupata pesa kwa ajili ya matibabu yake nje ya nchi.

Pia Diva amewashukuru na kwataja baadhi ya marafiki zake ambao wamekuwa karibu nae hasa katika kipindi hiki cha masikitiko na maumivu makubwa akiwemo mtangazaji mwenzie wa kipindi cha shilawadu Soudy Brown .

Diva the Bawse Achafua hali ya Hewa Instagram kwa Masaa.

Mwanadada kutoka clouds media Diva the bawse, amejikuta akichafua hali ya hewa huko instagram kutokana na attentio kubwa aliitengeneza baada ya kutangaza kuwa ana tamko kali anataka kulitoa na kuwafanya watu wakae wakisubiri ni kitu gani anataka kukisema lakini mwisho wa siku aliishia kusema kuwa amepigiwa simu na watu mbalimbali wakimuomba aache kufany hivyo.

Diva alianza kuwa kumsema mtu anayetaka kumtolea tamko kwa kusema kuwa mtu huyo ni mwembemba , kimbao kimbao na kufanya watu kupata hamu ya kutaka kumjua sana lakini mwisho  wa siku aliishia juu juu tu.

Nimevumilia na nimeshimdwa, hasira iko kali juu sana,itaneni kama kuna mtu nikakuwa nimemkwaza atanisamehee, mwisho wa ubaya ni aibu leo nimesema nitavua mtu nguo.-Aliandika Diva katika ukurasa wake wa instagram.

Diva Awananga Wanaume Aliowahi Kuwa Nao Kwenye Mahusiano

Mtangazaji wa Clouds Fm Loveness Malinzi maarufu kama Diva amewarushia madongo wanaume ambao amewahi kuwa nao Kwenye Mahusiano ya kimapenzi siku za nyuma.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram Diva amedaiwa wanaume wote aliokuwa nao Kwenye Mahusiano walipata umaarufu Kupitia Jina lake na sasa baada ya kuwaacha hawana kitu tena;

Wanaume wote niliowahi kuwa nao ni watu waliopata sana jina katika tasnia kwa kutumia jina la Diva kama mpenzi wao lakini baada ya kuwaacha Keisha habari yao hawana jipya hamna anayewaongelea hawana tena so called kiki tena so who made them famous”.

Lakini pia Diva aliendelea kujitapa kuwa ana nyota ya umaarufu ndio maana wanaume wote aliowahi kuwa nao walipata umaarufu Kupitia na yeye:

Mimi ndio niliwapa unaarufu hai watu ndio ujue watu na nyota zetu, Love me or hate me Ima star and I always shine…dear exes mshakuwa underground anzeni Tena hamjachelewa ila ndio hivyo pambaneni na hali zenu “.

Lakini Diva aliendelea kuwapa makavu na kuwa kuwataka wamuheshimu maana lawama jina mjini na walijulikana kwa sababu yake Ilan sasahivi kawaacha wanamiss kuandikwa.

Diva ameshawahi kuwa Kwenye Mahusiano na watu kadhaa maarufu kama vile Msanii mkongwe wa Bongo fleva Crazy GK, Heri Muziki, MO Racka na Mwanasiasa

Kisa Msiba wa Patrick, Diva Asema “Waandishi wa Habari Watapelekwa motoni

Mtangazaji wa Clouds tv, Diva the bawse amefunguka na kutoa lake la moyoni kuhusu waandishi wa habari wanavyosema maneno mengi kuhusu msiba wa mtoto wa Muna ambae amefariki siku mbili zilizopita .

Diva ansema kuwa kwa jinsi waandishi wa habari wanavyokuwa wakisema vibaya kuhusu msiba wa mtoto huyo, mungu atawachoma moto na kuwa kumekuwa na maneno mengi ya kuvunja na kuumiza moyo wafiwa .

ila waandishi wa habari sometimes sijui hawana mioyo,tuwe na mioyo jamana hizi views, likes na comments zitawapelka motoni, muda mwingine muwe na kumjua mungu.sio unafunga tu safari na kwenda kumhoji mtu eti mtoto wa nani.sijui hivi ebu kuwni na mioyo.

Ndani ya siku 14, Diva Atakiwa Kulipa Faini ya Mil.50 kwa Michael Lukindo

Msanii na mtangazaji wa Clouds Dadio, Diva Giselle ametakiwa kulipa fidia ya shilingili milion 50 kwa msanii na aiyewahi kuwa msanii mwenzie Michael Lukindo baada ya kumtukana matusi makubwa katika mtandao wa kijamii wa instagram.

Diva amepewa agizo hilo na kampuni ya wanasheria ya East Wood Attonery kwamba anatakiwa akamilishe jukumu hilo ndani ya siku 14 baada ya hapo hatu akali za kisheria zinaweza kufanyika.

Ikumbukwe kuwa , wiki iliyopita, michael lukindo alipokuwa akitambulisha wimbo wake mpya , alifanyiwa mahojiano ambapo alikiri kuwa alikuwa na mahusiano na Diva lakini Diva alitaka mahussiano hayo yawe ya siri na kweli waliamau kufanya hivyo,

Baada ya maohojiano hayo,  Diva aliamua kufunguka katika mtandao wa instagram na kutukana sana huku akikanusha taarifa za kuwa na mahusiano na mwanadada huyo hivyo baada ya matusi hayo, Michael Lukindo aliamua kupeleka mashtaka yake kwa mwanasheria kutokana na kutukanwa katika mtandao kwa kitu amabcho ni cha kweli na amekuwa na ushaidi nacho.

Kwa mujibu wa Diva, Michael ametangaza kuwa na mahusiano nae wakati sio kweli hivyo kwake ilikuwa imemkera.

 

 

Diva Amwagia Mvua Ya Matusi Ya Nguoni Michael Lukindo

Msanii na mtangazaji wa kipindi cha Ala za roho cha Clouds Fm Loveness Malinzi ‘Diva The bawse’ amemtolea povu zito msanii mwenzake wa Bongo fleva Michael Lukindo ‘ML’ baada ya kudai ni wapenzi.

Siku chache zilizopita Michael Lukindo alifanya mahojiano na XXL ya Clouds Fm na alikuwa anatambulisha ngoma yake mpya lakini Kwenye mahojiano hayo alifunguka kuwa yupo Kwenye Mahusiano na Diva.

Baada ya kusikia taarifa hizo Diva alitumia ukurasa wake wa Instagram na kumwaga povu zito na kukataa kata kata kama yupo Kwenye Mahusiano ya kimapenzi na Michael Lukindo.

Baada ya Tetesi hizo kusambaa Soudy Brown alimsaka Michael ambaye alikiri kuwa alikuwepo Kwenye Mahusiano na Diva lakini walifanya siri na mpaka sasa Diva hayupo tayari kuzungumzia hayo mahusiano.

Baada ya kusikia maneno hayo Diva ambaye kwa muda huo alikuwa studio alimtolea matusi mazito Michael Lukindo:

Wewe mata** unikome shika adabu yako umeshawahi kuwa na Mahusiano na mimi lini na wapi?na nilikwambia kabisa kwamba nimekushtaki I have defamation letter for you utajifunza kufunga huo mdomo wako sitaki mambo ya kise*** k*** la mama ako umeenda umemzungumzia Jokate on the same same thing haukutosheka ukamuandika Miriam Odemba kuwa una Mahusiano naye sasahivi unataka kwangu mimi kunitafutia kiki sasa mimi ntakukomesha nimeshakushtaki”.

 

Diva Amefunguka Haya Kuhusu Mpenzi Wake

Mtangazaji wa kipindi cha Ala za roho cha Clouds FM Loveness Malinzi au maarufua kama Diva The Bawse amefunguka kuhusu mahusiano yake mapya.

Ikiwa ni miezi michache imepita tangu Diva na aliyekuwa mpenzi wake msanii wa Bongo fleva Heri Muziki waachane  hatimaye Diva ameweka wazi kuwa yupo na mpenzi wake mpya.

Wiki chache zilizopita Diva alishangaza watu wengi baada ya kutangaza kuwa hatakubali kuolewa kwa mahari isiyopungua milioni  500 kiasi cha fedha ambacho kimeonekana kingi kwa wengi.

Lakini pia Diva alitangaza kwa kupitia ukurasa wake wa Twitter kuwa mwaka huu hata iweje lazima atahakikisha anazaa mtoto ingawa swali la watu wengi lilikuwa kama kaachana na mpenzi wake anazaa na nani?.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram Diva amewajulisha mashabiki zake kuwa tangu ameachana na Heri Muziki amepata mpenzi mpya na hiki ndicho alichoandika kuhusu mpenzi wake:

Mpenzi wangu mpya sio mtu maarufu wala sio mtu wa media wala movies..He is living in a cooperate world na kama nilivyosema sitaki mapenzi ya mtandao wala public Tena”.

 

Baada ya Kuachana na Heri muziki, Diva Akiri Kupata Usumbufu Mwingi.

Mwandada asiyeishiwa kuwa na drama katika mitandao ya kijamii , Diva the Bawse amefunguka na kusema kuwa tangu alipoachana na mpenzi wake aliekuwa nae katika mahusiano hivi karibuni, Diva the bawse amekuwa akipata usumbufu sana kutoka kwa wanaume mbalimbali.

Diva amesema kuwa kwa mwezi amaweza kubadili line ya simu hata mara saba kwa sababu tu wanaume wamekuwa ni wengi sana wanaomtaka kimaoezni na kumtumia sms ili waweze kuwa nae hivyo kwa kuepuka usumbufu muda mwingine inabidi aamue kubadilisha lin eya simu.

Maisha ya kuwa single ni mazuri, ingawaje kwa sasa nimekuwa nikipata usmbufu mkubwa sana,yani ninapata ssms hata 2000 na zote zinakuwa ni kutoka kwa wanaume,kitu ambacho kinnipa wakati mgumu sana na kunifanya nibadili line ya simu hata mara saba kwa mwezi.

Diva anasema kuwa ukiachana na upande wasimu lakini pia hata katika ukurasa wake wa instagram upande wa dm, lakini diva ameongezea na kusema kuwa maeshapata mwanaume ambae atakuwa baba wa mtoto wake kwa hivi karibuni ingawa amekataa kumuweka wazi mwanaume huyo kwa sasa na kusema kuwa bado mapema sana.

Diva: Kama Huna Milioni 500 Huwezi Kunioa

Mtangazaji wa Clouds Fm Loveness Malinzi maarufu kama Diva the bawse amefunguka na kuwa hawezi akaolewa na mwanaume yoyote bil kutokew mahari ya shilingi milioni 500.

Hii sio mara ya kwanza kwa Diva kuweka kigezo cha kuolewa na mwanaume mwenye pesa mbele kwani mara nyingi amekuwa akisema kuwa hawezi akaolewa kwa mahari ndogo.

Siku ya jana kupitia ukurasa wake wa Instagram Diva amekumbushia Tena vigezo vikubwa kwa mwanaume ambaye atakubali amuoe ambavyo ni awe tajiri kiasi ya kwamba aweze kutoa mahari ya milioni 500 lakini pia awe anajua kuongea kingereza:

Kunioa ni milioni 500….set that jokes aside am deadly serious….make sure uwe unaongea English yenyewe hasa… uwe smart uwe handsome…..uwe loaded…No broke niggas in 2018 tupendane kwa faida, you can say wheteves just heard worse, seen worse SMHFG Nothing mean to me…..harsh ain’t new to me I heard it all…..Mwenye povu hana hela ruksa na povu lako nina Omo na jiki plus toothbrush na Colgate jus there for you dummy”.

Diva ametangaza ruksa mwenye hizo sifa ajitokeze hii imekuja baada ya kuachana na mpenzi wake msanii wa Bongo fleva Heri Muziki baada ya kutoswa hewani.

Dalili ya Kwanza ya Superstar Hapokei Simu:Divva.

Mwanadada anaetamba na kazi yake ya utangazaji wa kipindi pendwa kwa vijana cha ala za roho,Divva the Bawse amefunguka na kuongelea kwa undani kitu kikubwa ambacho hakipendi kwa wasanii wa bongo.Diva anasema kuwa wasanii wengi wa bongo wamekuwa wakijidai sana baada ya kupata jina na kuridhika kabisa  na kitu hicho.

Sipendi kuona wasanii wengi wanaojiona kuwa wamefika , wakishapata jina kidogo tu wanajiona wakubwa na wamefika wanapopataka.

lazima mtu akubali kujifunza kila siku.lazima kila siku u-focus kufanya kitu bora na bora zaidi, kwaio usijione umefika.

kuna wasanii ukimtafuta kwa simu hapokei kabisa,unamtafuta ili kufanya nae press kwa faida yae lakini hapokei wala hakujulishi.sasa wasanii wa hivyo akija baadae akinitafuta au kunipigia na mimi sipokei.akinitext siwajibu,muda mwingi unafanya hayo kwa ajili yake mimi tayari nishapata followers wengii, kwaio nfanya kwa ajili ya kukunufaisha wewe mwenyewe.Wanasemaga kuwa dalili kubwa ya superstar hapokei simu.

Hata hivyo Diva alisema kuwa yeye ni fan mkubwa wa Aslay kwa sababu ya nyimbo zake zimekuwa zikimvutia sana.

Diva:Siwezi ku-date na Bongo Movies Hawajui Kingereza

Mwanadada mtangazaji wa Clouds Tv asieishiwa na vituko kila siku kutokana na mambo anayoyafanya Diva the Bawse amefunguka na kuongelea mahusiano yake alipokuwa akiongea na televisheni moja online na kusema kuwa kamwe hawezi kuthubutu kutoka kimapenzi na wasanii wa bongo movies.

Akiongea na Jonij0, Diva aliulizwa kama anaweza kudate na msanii wa bongo movie  na kama anaweza amtaje mmoja ambae angeweza kudate nae ndio alipojibu kamwe hawezi kufanya hivyo.

siwezi hata mara moj kwa sababu bongo movies hawajui kingereza,siwezi hata kwa fimbo.napenda sana mwanaume mwenye akili hata kidogo anaejua kingerza.but am sorry guys.

Diva aliendelea kusema kuwa kwa upande wake sasa yupo single kwaio hana mpango wa kuzaa kwa sababu bado anaugulia maumivu a mtoto wake aliyefariki hivi karibuni , baada ya mimba yake kutoka akiwa katika mahusiano na msanii wa bongo fleva Heri Muziki.

mtoto wa kwanza bado namuwaza sana , huyo akinitoka nitawaza kuzaa tena nakwa sasa nipo single lakini nilikuwa napenda sana mwanaume ambae ni  sperm donor tu,

Diva Adhamiria Kushika Ujauzito Mwaka Huu Kwa Njia Yoyote

Mtangazaji machachari wa kipindi cha Ala za roho kinachoruka Clouds Fm Loveness Malinzi maarufu kama Diva the Bawse ameibuka na kuwaambia mashabiki zake kuwa amedhamiria kushika mimba mwaka huu kwa njia yoyote ile.

Diva amekuwa kwenye headlines sana kwenye mitandao ya kijamii tangu mwaka umeanza hii ilitokea baada ya yeye na mpenzi wake wa zamani Heri Muziki kukorofishana ndani ya studio za Clouds Fm kwenye kipindi cha Leo Tena.

Wawili hao walienda studio hapo kwa ajili ya mahojiano kuhusu mziki wa Heri Muziki na mapenzi yao kwa ujumla lakini walipofika studio mule Heri hakutaka kuongelea mapenzi yake na Diva bali alitaka kuongelea mziki na kuishia kusema  yeye na Diva hawana mahusiano.

Bifu lile lilikuwa kubwa na Diva alionekana ku-mind sana kwani baada ya ugomvi huo wawili hao walitangaza kuachana na Heri Muziki alikuwa wa kwanza kusema kuwa yeye ndiye aliyemuacha Diva.

Diva ni moja kati ya mastaa ambao wanapenda sana kuweka mambo yao hadharani hasa kwenye mitandao ya  kijamii huku hilo likiwa ni jambo la kawaida sana kwake sasa jana amewaacha hoi mashabiki zake kwenye mtandao wa Twitter baada ya kutangaza anahitaji kushika mimba mwaka huu kwa njia yoyote na kuwataka mashabiki zake waanze kuhesabu siku:

Kupitia ukurasa wake wa Twitter Diva aliandika maneno haya:

Tangazo mwaka huu lazima niwe na ujauzito By any means…. Anzeni count down”.

Baada ya kutoa tangazo hili la kushika ujauzito mashabiki zake wengi walionekana kushangazwa na yeye kuwataka waanze kumuhesabia siku za kushika mimba.