Hakukuwa na Ndoa Kati ya Irene na Dogo Janja, Kilikuwa Kivuli :-Mwijaku

Mwigizaji msemaji sana Mwijaku amefunguka na kuongelea swala la ndoa ya Irene na ndogo janja kuvunjika na kusema kuwa tangu hapo awali aliwahi kusema swala hilo kuwa hakuna ndoa kati ya Irene na dogo janja kwa sababu irene hakuwa na aiba ya kuwa mke wa mtu.

Akisiistiza maneno yake , mwijaku anasema kuwa kati ya wawili hao waliofunga ndoa mwaka uliopita na ndoa hiyo kuvunjika mwaka huo huo , hakukuwa na ndoa kati yao zaidi ya kuwa walikuwa wakitaka kutengeneza matukio tu.

Ikumbukwe kuwa wawili hao walifunga ndoa ambayo ili-trend sana katika mitandao na kila mmoja alikuwa akiwaongelea  kila wakati lakini ghafla wawili hao waliishia njiani na ndoa kuvunjika huku sababu kubwa ikiwa ni swala la michepuko.

Mwijaku anasema  swala kubwa lilikuwepo ni kuwa dogo janja alikuwa akiongozwa na Irene na ndio maana ndoa imeshindwa kudumu , lakini kule alipo sasa hivi wanaweza kudumu kwa sababu wanaonekana wapo katika level zinazofanana na kwamba inaonekana kuwa kule amempenda mwanamke kwa kufuata moyo wake.

Irene Uwoya Ampongeza Dogo Janja

Mwanadada Irene Uwoya amefunguka na kutoa pongezi nyingi sana kwa aliewahi kuwa mume wake wa ndoa msanii Dogo Janja kwa kitendo anachoendelea kukifanya kwa sasa cha kuwa akitoa pesa kwa ajili ya kutatua mataizo mbalimbali katika jamii huku akinza na lile kubwa la kumjengea mama yake nyumba lakini na kurudi katika shule anayosoma na kufanya ukarabati,

Irene anasema kuwa hilo ni jambo jema sana ambalo Dogo Janja amemaua kulichukua kwa sababu jamii inatka asana msaada wake katika kipindi cha shida.

Irene anasema kuwa dogo janja kufanya hivyo anakuwa akirudisha fadhila kwa mashabiki waliomfikisha pale alipo lakini pia anamuomba hasiache kufanya hivyo kila mara na kujisahau tena.

Irene Ataka Kulipwa na Dogo Janja.

Mwanadada Iren Uwoya amefunguka na kusema kuwa ikitokea msanii Dogo Janja akitaka kufanya nae kazi ya kutaka kutikea katika video yake yoyote basi  anaweza kufanya nae kazi hiyo endapo tu ataweza kulipa pesa ambayo  anataka yeye.

Dogo Janja na iIrene ambao walikuwa mke na mume  lakini wametengana hivi karibuni  kutokana naskendo za mwanaume huyo kuchepuka na wema sepetu wamekuwa kama maadui kwa sasa huku kila mmoja akikaa kimya kutokuongelea mahusiano yao.

Hata hivyo Irene anasema kuwa kikubwa kwake pesa tu ‘niko tayari kuwa video model katima video yoyote ya Dogo janja ilimradi tu  kamaatakuja na dau zuri la kueleweka, kwanini nishinde?

Irene anasisitiza kuwa kwa sasa kila kitu anachokifanya kinachoonekana katika mitandao kuhusu yeye kinasimamamiwa na uongozi wake na wala sio wanaume kama watu wanavyosema.

Mange Afichua Ugonjwa wa Dogo Janja, ni Stress za Kuachawa na Irene

Kama ilivyokuwa kawaida yake ni kuweka wazi yale ambayo yanakuwa chini ya kapeti na sasa mwanadada ambae almekuwa akitoa siri za watu wengi nchini ikiwa yeye mwenyewe hakiwa hana makzi nchini humu mange kimambi amefunguka na kuweka bayana ugonjwa unaomsumbua Dogo janja tangu alipoanza kusemwa kuwa ni mgonjwa na anaumwa amelazwa.

Wikiendi iliyiopita msanii Dogo Janja alisherekea siku yake ya kuzaliwa akiwa hospitalini huku ikisemwa kuwa anaumwa kifua pamoja na ukosefu wa maji mwilini mwake.

Lakin Mange kimabi ametuma salamu kwa waliwahi kumlea sana dogo janja kipindi bado mtoto na akiwa mgeni kabisa katika tasnia ya sanaa madee  na kumwambia uwa Dogo janja anahitaji sana msaada kwa sababu ya kuchwa na mwanamke huyu ingawa pia anamwambia doho janja kuwa alichokosea na kumuoa Irene  kwa sababu Irene hakuwa mwanamk wa kuoa bali wa starehe.

Mange kimabi anaandika “@madee msichukulie poa mapenzi yanauma na hasa kwa wanaume, mifano hai ipo huyo dogo anahitaji watu wa karibu kusmhauri ili kuaccept situation,ninaamini kuwa hata anachoumwa hapo ni pressure tu za mapenzi. @ireneuwoya anaweza kuwa na makosa pia kwa sababu kuna kipindi isis wanwake tunakuwa tunataka tu kupata mwanaume  who can just love us lakini kiindi kile kikipita basi unakuwa hata unajishangaa kwanini uliamua vile………ukimfatilia irene kipindi anaolewa na huyu jamaa alikuwa kama anastress hivi lakini hapa karibuni amekuwa happy and she is living her life……

Ukiwa Hauna Maamuzi Kwa Mkeo ni Jambo Jema.:-Dogo Janja

Mwanamuziki Dogo Janja ambae ni mume wa mwanadada Irene Uwoya amefunguka na kusema kuwa yeye ndio mwanaume katika ndoa yake na ana sauti kama mwanaume kuliko hata watu wanavyofikiria na kusema katika mtandao ya kijamii.

Dogo Janja anasema kuwa ni bora kutokuwa na sauti kwa mkeo kuliko kutokwa na sauti kwa hawara maana hiyo haileti maana yoyote.

Ukiwa hauna sauti na maamuzi kwa mke wake ni halali kuliko kutokwa na sauti kwa hawara, mimi nina mtii mke wangu na yeye anafanya hivyo hivyo, kwenye familia yngu mimi ninasimama kama baba.-Aliongea Dogo janja akiwa katika kipindi cha FNL Kinachorushwa na EATV kila ijumaa na Sam Misago.

Baada ya sakata la irene kuweka katika mtandao picha iliyokuwa ikimuonyesha sehemu kubwa ya mwili wake nje , watu walizuka na kusema kuwa mwanamke huyo anafanya hivy kwa sababu mme wake hana sauti kwa mkewe.

Na Kimvua Hiki Uniambie Ratiba, Atadodondoka Mtu:-Dogo Janja.

Msanii Dogo Janja ametolea ufafanuzi wa ratiba iliyosambaa katika mitandao ya kijamii baada ya msanii huyo kuipiga picha na kuiweka katika ukureasa wake wa snapchat na kusemekana kuwa ilikuwa ni ratiba aliyokuwa amepangiwa na mke wake juu ya kufanya tendo a ndoa.

Dogo Janja anasema kuwa ni kweli alikuwa amelala na kuamka alikutana naratiba hiyo lakini irene ni mke wanke na mara nyingi amekuwa akipenda utani na ndio maana hata yeye aliamauakuiweka katika snap kwa sasa ilikuwa ni utani.

Nilikuwa nimelala nimekuja kuamka nikakuta na ratiba ya ukutani ,nikaiangalia nikaipiga picha nikaiweka kwenye mitandao ya kijamii.unajua yule ni mshikaji wangu sana na alikuwa akinitania sana, na hta hivyo yeye ndio alikua wa kwanza kuipost, na kimvua hiki uniambie ratiba!atadondoka mtu.

Siku za nyuma kidogo kulisambaa kwa picha ikionyesha karatasi inayomtaka Dogo Janja kufata ratiba ya kupewa tendo la ndoa na mke wake Irene Uwoya.

Dogo janja na irene uwoya tangu wamefunga ndoa na kuwa pamoja wamekuwa na drama nyingi sana katika mitandao ya kijamii ambapo kwa upande wao wanaona ni kitu cha kawaida na maisha yanaendelea.

 

Dogo Janja Atoa Siri za Ndani za Ndoa Yake.

Wasanii wa muziki na bongo movies irene uwoya na Dogo Janja wamewaacha mashabiki wao wazi baada ya Dogo Janja kuanika hadharani ratiba ya kupewa unyumba na mkewe Irene Uwoya wanapokuwa chumbani.

Ingawa watu wamekuwa wakishaangaa kwa kitendo hicho cha Dogo Janja lakini bado wapo waliolawashauri wawili hao kuwa wanajitahidi kuweka  maisha yao ya ndoa kuwa na usiri kwa sababu wao  tayari ni wanandoa.

Latika ukurasa wake wa snapchat dogo janja altumapicha ya karatasi ambayo chini imeandikwa jina la mkewe  irene uwoya huku kicha cha habari cha karatasi hiyo ikisema “RATIBA YA KUKUPA MME WANGU”

                                                          

Ndoa ya Dogo Janja na Irene Uwoya imekuwa ni moja ya mahussiano yaliyotawaliawa na drama nyingi tangu  kufungwa kwa ndoa hiyo.

Dogo Janja Na Uwoya Kupata Mtoto Mwakani

Ikiwa jana ni siku ya kuzaliwa kwa mwanadada mrembo Irene Uwoya ambae ni mke halali wa ndoa wa msanii wa muziki Dogo Janja, aliamua kumuandikia kumtakia kheri katika siku hiyo ya kuzaliwa , lakini pia Dogo Janja alitumia fursa hiyo kutangaza kuwa wawili hao mwakani wanategemea kuwa wazazi. Hii inaweza kuwa ni moja ya njia ya Dogo Janja kutuambia kuwa Irene sasa ni mjamzito ukizingatia wametoka kufunga ndoa hivi karibuni.

Akianza n kumshukuru kwa jinsi alivyoweza kubadilisha maisha yake tangu alipokutana nae,dogo jnaja aliandika kuwa watu watambue kuwa mwakani wanatgema kuwa wazazi.

umebadilisha maisha yangu kutoka nanii kwenda nanii.umenifanya nacheka muda wote hata nikiw ausingizini.wewe ni mke wangu wa kwanzana mke wangu wa mwisho.tuipeleke Dunia kwenye mwangaza wa ajabu na tuwamulike wasioamini kuwa sisi ni wazazi mwakani,wengi wameoana ila sisi tumefunga ndoa.happy birthday mke wangu….#MrsAbdul

Mapema November mwaka huu Dogo Janja na Irene Uwoya walifuga ndoa ambayo iliibua maswali na maneno mengi kutoka kwa watu mbalimbali huku kigezo kikubwa ikiwa ni umri wa  Dogo Janja.