Dr.Shika Akana Kuwajua Babu Seya na Mwanae

Dr.Luis Shika ambae amepata umaarufu mkubwa baada ya kuvuruga ununuzi wa nyumba za tajiri lugumyi, dr.shika  amekuwa akishika vichwa vya habari vya magazeti na vyombo mbalimbali vya habari amesema kuwa hawajui kabisa Babu Seya na mtoto wake Nguza Viking  kwa sababu kipindi watu hao wanakuja nchini yeye alikuwa nje ya nchi.

Babu Seya na Nguza Viking walikuwa wasanii waliofanya vizuri  sana nchini lakini hadithi yao ya muziki ilikuja kukwama baada ya wasanii hao ambao ni Baba na mtoto kukutwa na hatia baada ya kufunguliwa kesi iliyohusu kulawiti watoto.Hata hivyo wasanii hao wametoka baada ya kupewa msamaha na raisi mwezi huu wa December tahere 9 siku ya Uhuru baada ya raisi huyo kutoa msahama kwa wafungwa zaidi ya elfu nane.

Hata hivyo baada ya kutoka kwa wasanii hao, watu katika mitandao walianza kusema kuwa kile kipindi cha Dr .Shik kueendelea kupata kiki kimeisha kwa sababu wasanii hao wawili wameweza kukamata sana mitandao ya kijamii kwa sasa.

Simfahamu babu Seya kipindi yeye anaingia nchini tayari nilishaondoka nchini muda mrefu , lakini nafahamu nyimbo zake  ile aliyoimba baba na mwana  wanaimba na kucheza hasa ndio naifahamu vizuri.-    Alisema Dr. Shika 

Lakini pia dr.shika anasema kuwa anampongeza sana  magufuli kwa hatua na maaamuzi aliyoyachukua  kwa kuwa watu hao sasa wanaenda kuanza maisha mapya wakiwa huru kabisa.

Nampongeza sana Mh.Raisi Magufuli kwa tukio ilo la kuwatoa wafungwa na kuwapa uhuru wao ili wakanze maisha mapya.

Wametolewa wafungwa wengi siku ya msamaha wa raisi lakini  wasanii hao walipata ku-trend katika mitandao kutokana na kuwa kifungo chao kiliwagusa watu wengi nawatu wengi walitamani sana kuachiwa kwao.

 

Mrembo Sanchoka Aweka Hisia Zake Juu Ya Dr. Shika Hadharani

Mrembo anayetingisha mitandao ya Kijamii kama Instagram kwa umbo lake matata Sanchoka au maarufu kama Sancho World amefunguka nakudai kuwa yuko tayari kuolewa na Dr. Shika ‘900 Itapendeza’.

Dr. Shika alipata umaarufu wiki chache zilizopita baada ya kwenda kwenye mnada wa nyumba za Lugumi na kuhaidi kuzinunua kwa mabilioni ya pesa lakini mara baada ya mnada kuisha Dr. Shika alishindwa kuzilipia na hivyo kuishia kupelekwa polisi. Baada ya kuachiwa huru Dr. Shika aliishia kupata umaarufu baada yakupata attention kubwa kutoka kwa waandishi wa habari iliyopelekea kupata nafasi mbalimbali za kushiriki kwenye matangazo ya kampuni nyingi ambayo yanamuingizia pesa nyingi.

Mrembo Sanchoka amejizolea umaarufu baada ya kuzoea kuweka picha za utupu ambaxo zinaonekana kuwavutia hasa wanaume kutokana na umbo lake la kuvutia.

Sanchi amemtolea macho Dr. Shika amefunguka na kudai kuwa anautamani sana umaarufu waDr. Shika kwasababu hajatumia ngumu kubwa. Sambamba na hilo Sanchi amesema kama Dr. Shika mzee wa 900 Itapendeza Kama atanunua kweli nyumba za Lugumi basi atakubali hata kufunga naye ndoa kwani Dr. Shia naye ni mwanaume, Sanchi ameyafunguka hayo baada ya kuulizwa kama yuko tayari kuolewa na Dr. Shika.

Sanchi aliweka wazi tangu mwanzoni kuwa anataka kuolewa na mwanaume mwenye hela kwani bila mahari ya miliobi kumi basi hataolewa.

 

 

Kala: Watanzania Wamemchukulia Dr. Shika Kama Kituko

Msanii wa Bongo fleva anayefanya mziki wake kwa miondoko ya hip hop, Kala Jeremiah amedai kuwa Watanzania wengi wanamchukulia Dr. Shika kama kituko Fulani.

Dr. Shika aliyepata umaarufu wiki chache zilizopita baada ya kununua nyumba za mnada za Lugumi kisha kushindwa kuzilipia amezidi kupata umaarufu huku watu wakiwa na maoni mbali mbali juu ya nini hasa ilikuwa nia ya Dr. Shika.

Mapema wiki hii mwanamuziki Kala aliibuka na kuwaomba watu wasimdharau Dr. Shika, lakini pia kwenye mahojiano aliyoyafanya na Millard Ayo, Kala amedai kuwa mpaka hivi sasa bado kuna Watanzania ambao bado wanamuona Dr. Shika kama kituko:

Mara ya kwanza nilipoona habari yake kusema kweli sikuielewa lakini baadae nilijaribu kuifatilia na mahojiano yalivyozidi kuendelea nikaona huyu jamaa hayupo kama watu wengi wanavyomchukulia kiwepesi lakini ukiangalia yule jamaa kapitia mambo magumu sana kwa hiyo lenfo language la kupaza sauti ni kuomba Watanzania wamuonee huruma kwanza na wampende kwasababu niliona kama wanamchukulia kama kituko lakini huwezi kuja yaliyomsibu mpaka kufika pale ni yapi kwa kusikiliza mahojiano yake na anvyoeleza kuwa alitekwa inaonekana sio uongo na kwa jinsi alivyotekwa na mate so aliyopata anaonekana kabisa kuwa kisaikolojia imemuathiri kwaiyo kwa kujua hilo watu lazima wampende wamuweke karibu kama mtu aliyepata matatizo kwaiyo asipuuzwe kwasababu ni mtu anayeonekana anaweza akawa na mchango mkubwa kwa taifa letu”.

 

Dr. Shika ‘900 Itapendeza’ Azidi Kuukwaa Ustaa

Dr. Louis Shika amezidi kuuvaa ustaa kwa nguvu na kwa kasi ya ajabu, hivi sasa utamuona Dr. Shika au wengi hupendelea kumuita 900 Itapendeza kwenye matangazo ya bidhaa mbali mbali utamuona amepozi na warembo wakali lakini pia amepiga picha na mastaa mbalimbali.

Dr. Shika alipata umaarufu kwa spidi ya 4g wiki chache zilizopita baada ya kuenda kwenye mnada wa nyumba za Lugumi na kununua nyumba tatu zenye thamani ya mabilioni kisha kushindwa kuzilipia hivyo kusababishwa kupelekwa polisi lakini hata baada ya kuachiwa Dr. Shika amezidi kusisitiza kuwa atalipia nyumba zile.

Siku ya juzi kuna picha ilienea ikimuonyesha mwanamuziki wa Bongo fleva Dogo Janja akiwa na Dr. Shika huku wengi wakidhani kuwa labda ataonekana kwenye moja ya video za Dogo Janja.

 

Huzi ni baadhi ya picha navudeo zinazo muonyesha jinsi Dr. Shika anavyokula bata hivi sasa na warembo kumkubali baada ya umaarufu wake:

Dr. Shika akiwaakiwa viwanja amezungukwa na warembo