Dudubaya Apigiliwa Msumari Mwingine Baada Ya Kuwekwa Ndani

Msanii mkongwe wa muziki wa Bongo fleva Godfrey Tumaini maarufu kama Dudubaya amejikuta akikumbwa na Janga jingine Baada ya kuswekwa rumande.

Siku chache zilizopita Dudubaya aliwekwa ndani katika kituo cha Oysterbay Baada ya kumtolea maneno ya kejeli Marehemu Ruge Mutahaba.

Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) limetangaza kufuta usajili wa Msanii, Godfrey Tumaini maarufu kama Dudubaya kuanzia  Februari 28, kutokana na utovu wa nidhamu.

Barua hiyo iliyosainiwa na Katibu Mtendaji wa Baraza hilo, Godfrey Mngereza amesema kuwa baraza limechukua hatua hizo baada ya msanii huyo kukamatwa na jeshi la polisi kutokana na kauli zake kwenye mitandao ya kijamii.

Kwa sasa Dudu Baya anashikiliwa na Jeshi la Polisi katika kituo cha Oyster-bay jijini Dar es salaam kwa kosa la uhalifu mtandaoni.

Jeshi La Polisi Lathibitisha Msanii Dudubaya Kutiwa Mbaroni

Jeshi la Polisi nchini Kupitia Kamanda wa Polisi Kinondoni, Mussa Taibu amesema msanii, Godfrey Tumaini ‘Dudu Baya’anashikiliwa na Jeshi la Polisi katika Kituo cha Polisi Oyster Bay jijini Dar es Salaam.

Dudubaya amefikishwa kituono kwa mahojiano kutokana na tuhuma za kukashifu na kutoa lugha za kejeli kwa aliyekuwa Mkurugenzi wa Vipindi na Uzalishaji wa Clouds Media, marehemu Ruge Mutahaba.

Jana Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt Harrison Mwakyembe alilielekeza Baraza la Sanaa Taifa (Basata) kwa kushirikiana na Jeshi la Polisi nchini kumchukulia hatua Dudu Baya kwa kumdhihaki Ruge ambaye alifariki jana nchini Afrika Kusini.

Lakini baadaye kupitia akaunti yake ya Instagram, Dudu Baya alimjibu waziri huyo na kusema asisumbuke kuwaagiza polisi wamsake kwani watapoteza mafuta bure, badala yake wamuelekeze ni kituo gani cha polisi akaripoti.

Steve Nyerere: Dudubaya Aombe Msamaha na Atengwe

Msanii wa Bongo movie Steve Nyerere ameibuka na kumtolea Povu zito Msanii wa Bongo fleva Godfrey Tumaini maarufu kama Dudubaya Baada ya kutoa maneno na Chafu dhidi ya Marehemu Ruge Mutahaba.

Steve Nyerere, amesema kama kuna msanii anamzungumzia vibaya marehemu Ruge Mutahaba kwa sasa jkama anavyofanya Rapa Dudu Baya basi anapaswa kutengwa kwani hakuna binadamu aliye mkamilifu.

Steve amesema Ruge amefungua milango kwa vijana wengi na kutoa fursa waweze kufanikiwa huku akiweka wazi kuwa atamkumbuka milele.

Kwenye mahojiano aliyofanya na Bongo 5, Steve ameongea haya:

 

Dudubaya Adhamiria Kumtembezea Kichapo Harmo Rapa

Msanii mkongwe wa muziki wa Bongo fleva Godfrey Tumaini maarufu kama Dudubaya ameibuka na kusema wazi wazi kuwa mipango yake ya kumpiga Harmo rapa ipo pale pale.

Kama utakumbuka mwaka jana Dudubaya alisema hadharani kuwa endapo atakuwatana macho kwa macho live na msanii mwenzake Harmo Rapa basi atamtembezea kichapo kitakatifu.

Kwenye mahojiano aliyofanya na kituo kimoja cha habari Dudubaya aliulizwa kuhusu Bifu lake na Harmo rapa na kama ameamua kumsamehe Baada ya kuona kipindi kifupi kimepita ndipo Dudubaya alipojibu:

Hakuna nilichobadilisha, adhabu yako ipo pale pale”.

Dudubaya ni mmoja kati ya wasanii ambaye  ametajwa kuwa ni mkorofi tangu zamani ambapo siku za nyuma ameshawahi kuingia kwenye Bifu na Dudubaya na mwishowe aliishia kumpa kichapo cha maaana.

Dudubaya Akiri Kumkubali Gigy Money

Msanii mkongwe wa Muziki wa Bongo fleva Tumaini Godfrey maarufu kama Dudubaya ameibuka na kuweka kuwa anamkubali msanii mwenzake Gigy Money.

Dudu Baya amesema kuwa msichana anayeweza kumuoa na anampenda ni Gigy Money na Lady Jaydee. Japo kuwa ameeleza kuwa Gigy anatabia ambazo bado haweki kumfanya awe mke labda aziache.

Mwanamke ninayempenda ni Gigy Money, Gigy huwa nampenda ila tabia zake ambapo bado siwezi kumfanya kuwa mke yaani mpaka aache zile tabia, tulishazungumza ila hawezi kuacha zile tabia, Gigy mnaweza mkawa sehemu akaanza kucheza akiwa uchi kwahiyo kama mama watoto siwezi.

Lakini tukija mabinti wengine wakike kwenye hustle anajiamini ni Lady Jaydee, kwasababu ni mwanamke mwenye akili timamu kwasababu mimi nampenda mwanamke mbishi kwasababu mimi ni Konki”.

Dudubaya na Gigy Money waliwahi kuibua Tetesi Za kuwa pamoja Baada ya kuonekana karibu kuliko kawaida walipokuwa pamoja kwenye ziara ya Wasafi Festival.

 

Dudubaya Amtolea Povu Zito Nay Wa Mitego

Msanii mkongwe wa muziki wa Bongo fleva nchini Godfrey Tumaini maarufu kama Dudubaya ameibuka na kumtolea Povu zito msanii mwenzake Nay wa Mitego.

Dudubaya amerudi kwa kasi ya ajabu kwenye headlines Baada ya kuwa kimya kwa miaka mingi tangu alipoacha kufanya muziki miaka michache iliyopita lakini tangu arudi kwenye ramani na Wasafi Festival Dudubaya amekuwa akitrend Sana.

Dudubaya ameibuka na kumjia juu msanii mwenzake Nay wa Mitego ambaye Hivi karibuni ametajwa kuwa na bifu na msanii mwenzake Diamond Platnumz ambaye hapo nyuma alikuwa mshkaji Wake pia.

Baada ya Nay wa Mitego kuwaponda wasanii wa Wasafi, Dudubaya amemtolea Povu hilo Kwenye mahojiano aliyofanya na kituo kimoja cha habari:

Unamuona msanii kama Nay wa Mitego anasema wit wasanii wa Wasafi hawana amsha amsha hivi ana akili timamu? Nay wa Mitego alitumwa na Clouds kuandika wimbo wamepanda wameshuka kunitukana mimi na P-funk   Anawatukana malegendary waliozaa Bongo fleva”.

Lakini pia Dudubaya aliendelea kumtolea maneno Nay wa Mitego ikiwemo kudai kuwa amebuma na muziki wake umebuma:

Nilimwambia mdogo wangu Nay wa mitego siku zako zinakuja na chamoto utakiona, cha moto anakiona sasa amegombana na T. touch na sasa kila akitoa nyimbo inabuma na wale waliomwambia tunga wimbo uwaponde wakina Dudubaya siku hizi hawapigi nyimbo zake”.

 

Gigy Money Adaiwa Kushushiwa Kipigo Kizito na Dudubaya

Msanii wa Bongo fleva Gift Stanford maarufu kama Gigy Money anadaiwa kutembezewa kipigo cha haja  na msanii mwenzake mkongwe Godfrey Tumaini maarufu kama Dudubaya.

Global Publishers wanaripoti kuwa Tukio hilo lilitokea usiku wa kuamkia Jumapili iliyopita jijini Mwanza ambapo inaelezwa ugomvi ulianza kama utani wawili hao wakiwa nyuma ya jukwaa wakati Tamasha la Wasafi Festival likiendelea.

Shuhuda wa tukio hilo alidai Gigy ambaye mara nyingi ameonekana akiwa karibu na Dudu Baya alikuwa akiongea sana na kutaja mambo ambayo ni matusi mbele za watu huku Dudu Baya naye akiwa na mwanaye.Wakati Gigy akiendelea kumwaga maneno ya chumbani akijihusisha na Dudu Baya, msanii huyo mwenye asili ya utata alikuwa kimya kwa aibu akiwa na binti yake, Maria.

Kukaa kimya kwa Dudu Baya hakukusaidia kitu kwani Gigy aliendelea kutoa maneno makali lakini yalipozidi mwanamuziki huyo aliwaomba waungwana wakamtulize mwanamama huyo.

Yaani maneno ya Gigy yalikuwa yanamfadhaisha sana Dudu Baya na mwanaye  ambapo licha ya kumtaka aache hakusikia, aliendelea tu“.

Kutokana na kuendelea kutoa maneno machafu Dudu Baya alimvaa Gigy na kumshushia kipigo cha ambapo aliokolewa na mabaunsa waliokuwa karibu. Katika varangati hilo Gigy aliangua kilio kutokana na maumivu huku akilalama kupoteza simu yake ya kisasa.

Kwenye mahojiano aliyofanya na Gazeti la Risasi Mchanganyiko Dudu Baya ili kueleza sababu za kumshushia kipigo Gigy na kufunguka;

Huyu Gigy hana akili, nilishamwambia muda mrefu kwamba sitaki utani wake yeye hanielewi, yule ni mwanamke wa ajabu sana”.

 

Mrembo Aliye Kwenye Penzi na Dudubaya Ajitokeza (+picha)

Mrembo anayejulikana kwa jina la Khadijah Ziota kutoka mkoani Mwanza amejitokeza na kukiri kuwa katika penzi zito na Msanii huyo mkongwe siku chache Baada ya picha zao kusambaa mtandaoni.

Wiki iliyopita Msanii Godfrey Tumaini maarufu kama Dudubaya ‘Konki Master’ alihudhuria tamasha la Wasafi Festival mkoani Mwanza na mara moja alionekana akiwa karibuni sana na mwanamke huyo.

 

Kwenye mahojiano aliyofanya na Global Publishers, Khadija amesema kwa kawaida yeye anapenda wanaume wa type ya Dudu Baya, hivyo amemzimia hata Dudu a,empenda kwa sana huku akitamba kuwa wana mpango wa kuoana na kuwa mke na mume.

Kwa sababu picha zimesambaa na watu wameona, kama umeona picha inajitosheleza, kama huwezi kusoma hata picha ushindwe kuelewa? Konki Master ameniona akanielewa, amenipenda na mimi ninampenda, hapo baadaye nonatarajia kuwa mama watoto wake”.

 

“Dudubaya Hana Malinda, Nimeshawahi Kulala Naye”-Chiddi Benz

Msanii mkongwe wa muziki wa Bongo fleva Chiddi Benz ameibuka na kumtupia maneno ya kashfa msanii mwenzake Dudubaya na kudai kuwa hana malinda.

Kwa muda sasa kumekuwa na tetesi za kuwa msanii huyo mkongwe Dudubaya amesemwa kuwa anashiriki mapenzi ya Jinsia moja tetesi ambazo mwenyewe ameshazikataa na kuzipuuza.

Lakini sasa msanii mwenzake Chiddi Benz ameibuka na kutoa tuhuma kali kuwa Dudubaya hana malinda na ana uhakika kwa sababu yeye alishawahi kumgonga.

Kwenye mahojiano aliyofanya na na kituo kimoja cha habari, Chiddi Benz alifunguka haya Kuhusiana na tuhuma hizo:

Mimi naamini kwamba Dudubaya hana Malinda kwa sababu nilimkaza nilikuwa nalala naye na aliniomba nikae naye chumba kimoja”.

Chiddi Benz na Dudubaya wameshawahi kuwa na Bifu siku za nyuma na Hivi sasa bifu hilo limeibuka tena Baada ya Dudubaya kuonekana kushiriki katika tamasha Lao Wasafi festival na Chiddi Benz Kutoswa.

Chid Benz Amwaga Povu Baada Ya Kukosekana Kwenye Listi Ya Wasafi Festival

Msanii mkongwe wa muziki wa Hip hop nchini Chid Benz amefunguka na kuwamwagia Povu zito timu nzima ya WCB Baada ya kukosa mwaliko wa kufanya shoo kwenye Wasafi Festival.

Chid Benz amefungukia ishu ya Diamond Platnumz na Timu yake nzima ya WCB kutumia wanamuziki Kama Dudubaya ambaye anaamini amechaguliwa kwa sababu ya umaarufu wa jina lake Konki Konki konki Master.

Kwenye mahojiano na kituo kimoja cha habari, Chid Benz amedai amesikiyishwa kuwa Msanii Kama yeye Anayeimba vitu vya maana hajachaguliwa kwa madai kuwa anatumia madawa ya kulevya ilhali ameshaacha.

Sisi wasanii tunaoimba nyimbo ambazo zinabeba ujumbe na maana hatupati nafasi kabisa utasikia wanasema achana na hao wakina Chidi Benz wanakula unga ila Dudubaya kisa anasema konki konki anajaza watu basi nasibu anampa tour kwenye Wasafi Festival”.

Diamond na timu nzima ya WCB ilimchagua Dudubaya Kama mmoja wa wasanii watakaoshiriki katika tamasha la WCB Baada ya umaarufu alioupata kupitia jina lake la utani la Konki Master.

 

Dudubaya Hakulizishwa na Majibu ya Alikiba kwa Diamond

Siku chache zilizopita , msanii kutoka wcb alitangaza na kuomba kuwa katika tamsha kubwa linaloenda kufanyika mwezi huu la Wasafi Festival basi msanii mwenzao mkubwa ambae mara kadhaa imekuwa ikisikika kuwa wamekuwa na ugomvi  kuudhulia tamasha hilo ili kuwafurahisha mashabiki zao.

Lakini katika majibu yake , Alikiba alisema kuwa kwa sasa hawezi kufanya hivyo kwa sababua mekuwa na majukumu mengi sana kiais kwamba hatoweza kuwepo katika tamasha hilo lakini alisema kuwa angeweza kuwapa udhamini  kupitia kinywaji chake cha MO FAYA.

Baada ya kukaa na kuongea na uongzi wa pande zote mbili waliweza kukualiana juu ya hilo, hata hivyo kukutana kwa wasanii hawa ilikuwa ndoto ya mashabiki wengi sana

Msanii Dudubaya alimaaruf kama konki master amefunguka na kusema kuwa hajafurahishwa kabisa na majibu ya msanii alikiba kwa sababu kujibu hivyo ni kama kuonyesha dharau kuwa tamasha hilo sio muhimu kuliko mambo yake.

Dudubaya anaonekana ku-mind majibu hayo na  kumseama alikiba kuwa amekuwa msanii mwenye dharau kwa wasanii wengine, hata hivyo Dudu baya nae ni mmoja wa wasanii watakao tokea katika tamasha hilo.

Dudubaya Atoa Siri ya Kumpa Kipondo Mr Nice

Msanii mkongwe katika gamela muziki Dudubaya amefunguka sababu kubwa iliwahi kufanya katika histora ya muziki kuwepo na bifu kubwa kati yake na msanii mwenzake mr nice baada ya kumpiga sana msanii huyo.

Dudubabya anaelezea kuwa sababu kubwa ya yeye kuwa na ugomvi wa milelle na mr nice ni baada ya kukutana club ambapo sanii huyo alimletea dharau na ndipo alipoamua kumpiga ili kumuadabisha na kuanza kwa ugomvi wao.

Akielezea  kwa ujasiri msanii huyo ambae kwa sasa amejizolea umaarufu na jina lake la kibabe la konki master anasema ‘tualikutana club billcanass siku moja na akaniletea dharau na ndio nikaamua kumbabua  kwa sabbu mimi sipendi dharau na kweli aliumi na alivunjika kiuno, tangu hapo ndipo ugomvi wetu ulioanzia.

Ikumbukwe kuwa kwa muda mrefu tangu Dudababa hampige msanii huyo, waliingia katika ugomvi mkubwa kwa muda mrefu na hatasasa wasanii hao hawako katika mahusiano mazuri na kipindi walipokuwa wameshika sana nafasi ya muziki walikuwa hata wakiimbiana nyimbo za kupigana vijembe.

Aliyesemwa Kuwa Mke wa Dudu baya Afunguka Mazito

Mwana mama aliyesemwa kuwa Aliwahi kuwa  mke wa msanii Dudubabya amefunguka mazito mbele ya waandisi wa habari baada ya mume wake huyo kwenda katika maitandao ya kijamii na kusema kuwa anawajua wote wanaofanya biashara ya ngono haramu ya kinyue cha maumbile.

Mwanamama huyo anasema kuwa liijua siri ya mwanaume huyo baada ya kuifuma simu yake usiku akiwa amelala na kuona sms zilizokuwa zikitoka kwa mtu kama mwanamke lakini akiangalia jina la namba hiyo alikuwa ni rafiki wa mume wake ambae ni mwanaume na alikuwa anamjua.

Mwanamama huyo anasema kuwa baada ya kuongea  kwa sms na mwanaume huo kwa muda alikuja kugundua kuwa wamekuwa wakiona akila mara na kwamba walikuwa wakifanya mambo hayo kwa siri.

hata hivyo mwanamama huyo anasema kuwa pamoja na hayo anamjua dudbaya kuwa kama anataka kufanya jambo kama hilo hawezi kushindwa kwa sababu ana uwezo wa kumlazimisha mtu kufanya mapenzi kwa nguvu hata ama ni kwa kumpiga.

 

 

Diamond Akapimwe Akili na Kufanyiwa Maombi-Dudubaya

Msanii mkongwe wa Muziki wa Bongo fleva DuduBaya amemwagia povu zito msanii mwenzake Diamond Platnumz baada ya kuvaa kikuku na kumtaka akapimwe akili.

Wiki chache zilizopita Diamond alizua gumzo Kwenye mitandao ya kijamii baada ya kuposti picha yake aliyomuonyesha akiwa amevaa cheni ya mguuni (kikuku) ambayo inavaliwa mara nyingi na wanawake tu.

Dudubaya amefunguka n kumtolea povu zito Diamond ambapo Kwenye Interview yake na kipindi cha Refresh cha Wasafi Tv, amedai kitendo alichofanya Diamond ni cha kutia aibu kwa wanabongo fleva wote:

Kwa mdogo wangu Diamond kuvaa kikuku siwezi kujua anatangaza biashara gani hasa labda na yeye anatangaza biashara sawa sawa na wanawake wanaojiuza wanavyojitangaza kwa kuvaa kikuku kwaiyo kwa mimi ni aibu na  kaitia aibu Bongo fleva na hata familia yake na hata mademu zake anaolala nao hawana akili kwa nini wasimshauri asivae kikuku”.

Lakini pia Dudubaya aliendelea kumwaga povu na kumtaka Msanii huyo akapimwe akili:

Mimi naona akapimwe akili yake na pia akae chini na viongozi wa dini ili waweze kumpa ushauri”.

Dudubaya Atoa Tamko Kwa Vyombo Vya Habari Kuhusu Mwanaye Wille

Msanii mkongwe wa Bongo fleva Dudubaya aliyewahi kutamba na vibao vyake kama Mpenzi na Nakupenda amemwaga povu zito kwa vyombo vya habari kuhusu Mahusiano Yake na mwanaye Wille.

Kwa muda mrefu sasa Dudubaya amekuwa hana uhusiano mzuri na mtoto wake Wille ambapo imedaiwa kuwa aliamua kumtelekeza mtoto huyo kwa kama yake baaada ya kuacha shule na kuamua kufanya Muziki.

Lakini sasa baada ya mgogoro wa muda mrefu na mvutano Kwenye mitandao ya kijamii Dudubaya ameweka wazi kuwa hataki tena kuulizwa na vyombo vya habari kuhusu mtoto wao wake.

Kwenye mahojiano na Kipindi cha Refresh cha Wasafi Tv, Dudubaya ametangaza rai hii:

Leo tarehe 18 mwezi wa 6 mwaka 2018 natangaza kauli yangu kwenye vyombo vya habari kuwa sitaki Dj yoyote, mtangazaji yoyote aniulize kuhusu mtoto wangu Wille kwa sababu toka ameacha shule hayuko mikononi mwangu yuko kwa mama yake na kila kitu atakachofanya huko mimi sitahusika”.

Siku za hivi karibuni kuna picha zilisambaa Kwenye vyombo vya habari zilizomuonyesha Wille akiwa anavuta bhangi na kunywa pombe.

Dudubaya Amwagia Povu Zito Mwanaye Wille

Msanii mkongwe wa Bongo fleva aliyewahi kutamba na vibao vyake kama vile Nakupenda, ameweka wazi kuwa yeye na mwanaye Willy bado hawana maelewano mazuri.

Kama utakumbuka miaka ya nyuma Dudubaya ameshawahi sana kumuimba mwanaye Wille katika nyimbo mbali mbali na hata ameonekana kwenye baadhi ya video zake.

Lakini tangu hapo Dudubaya na mwanaye Wille ambaye sasahivi amekuwa na ana miaka kumi na nane wamekuwa wakikosa maelewano hasa kwa sababu aliacha shule na kuingia kwenye muziki mwaka jana.

Lakini hivi sasa Dudubaya amefunguka Kwenye mahojiano na Clouds Tv na kuweka wazi kutofurahishwa na kitendo cha mwanaye kutoa wimbo bila hata kumshirikisha.

Mimi ni mwanamuziki, yeye ni mwanamuziki na mimi ni baba yake hajawahi kunisikilizisha ngoma ina maana kawasilizisha baba zake wengine.

Kwa hiyo mama yake yeye ndio anajua baba zake wengine ndio maana kawasikilizisha wale, hajaja kuniimbia mimi hata freestyle”.