Dully Sykes Afunguka Kukopiwa na Harmonize

Msanii mkongwe wa muziki wa Bongo fleva Abdul Sykes maarufu kama Dully Sykes amefunguka na kuweka wazi kuwa amefurahi Baada ya Msanii Harmonize kukopi nyimbo yake.

Harmonize ametumia melody ya wimbo Dully Sykes wa muda mrefu unaofahamika kama ‘Handsome’ katika wimbo wake mpya alioutoa wa Kainama na kusema amefurahi kwa sababu ameona kama amemuenzi.

Kwenye mahojiano aliyofanya na Global Publishers, Dully alisema kabla Harmonize hajaweka maneno katika wimbo huo, alimshirikisha kwanza na hata wakati anarekodi alikuwepo studio na akamshauri baadhi ya vitu.

Wala sijachukulia kama kaniibia melody yangu ila nimechukulia kama hali ya kunienzi f’lani hivi kwa nilichokifanya huko nyuma nilifurahi sana alipotoa wazo la kuchukua melody hiyo ambayo nilitumia katika wimbo wangu wa zamani uliokuwa unafahamika kama Handsome, na ameutendea haki vilivyo nimefurahi sana”.

 

Dully Sykes Ataja Sababu Za Kumficha Mpenzi Wake

Msanii mkpngwe wa muziki wa Bongo fleva nchini Dully Sykes amefunguka na kuweka wazi kuwa kamwe hawezi kumuanika hadharani mwanamke ambaye yupo naye kwenye mahusiano kutokana na somo alilolipata siku za nyuma.

Dully amesema kamwe hawezi kumuonyesha mwanamke ambaye hajamuoa kwenye jamii kwa sababu ameshajifunza mengi sana kupitia wasanii wenzake waliothubutu kuonesha wanawake walio nao kwenye uhusiano.

Kwenye mahojiano aliyofanya na kituo kimoja cha habari nchini, Dully amesema kuwa kwanza kabisa hana mwanamke kwa sasa lakini kama akimpata atafaidi sana kwani mambo ya kidunia mengi kayaacha kwa sababu hakuna ambalo hajalifanya.

Hakuna kitu kibaya kama unatoka na mwanamke unaachana naye anaenda kutembea na rafiki yako ni kitu kibaya mno na cha fedhea sana, hivyo nitamuweka wazi mke wangu, sio msichana tu ambaye wakati wowote unaweza kuachana naye”.

 

 

Sina Mpango Wa Kuoa- Dully Sykes

Msanii mkongwe wa Bongo fleva Dully Sykes amefunguka na kuacha watu vinywa wazi baada ya kuweka wazi kuwa hana mpango wa kufunga ndoa pamoja na kuwa na watoto kadhaa.

Kauli hiyo iliyotolewa na Dully iliwashangaza mashabiki zake kwani ilitolewa mbele ya kadamnasi ya mashabiki.

Dully alifunguka suala hilo wakati akiwa jukwaani akikamua kwenye Tamasha la Komaa, lililofanyika kwenye Viwanja vya Tanganyika Packers, ambapo akiwa katikati ya shoo alisema kwa nguvu.

Dar es Salaam…hatupoi… hatuboi na wala hatuoiii…”.

Baada ya kauli hiyo swangwe ziliibuka kila kona na baadhi ya mashabiki walianza kuzungumza chini kwa chini juu ya kauli hiyo kwamba huenda Dully hana mpango wa kuoa kweli ndiyo maana kasema juu ya kauli hiyo.

Dully amekuwa akiulizwa kuhusu kufunga ndoa kwa miaka mingi sasa ambapo amekuwa akidai muda ukifika ataoa lakini mpaka leo bado hajaoa licha ya kuwa na watoto kadhaa.

Harmonize Kupita Tena na Dully Sykes

Msanii wa muziki wa Bongo fleva kutoka katika label ya WCB Harmonize, ameweka wazi nia yake ya kupita tena na kufanya kazi na Msanii mwenzake Dully Sykes.

Harmonize ametangaza ujio wa  ngoma yake inayokuja hivi karibuni aliyomshirikisha Msanii mkongwe wa Bongo fleva Prince Dully Sykes.

Harmonize ameweka wazi kuwa mashabiki wajiandae mkao wa kul kwa sababu ngoma hiyo itakuwa kali kupita maelezo.

Kipitia ukurasa wake wa Instagram, Harmonize ameandika posti hii kuhusu ujio wa ngoma hiyo:

Lakini ngoma hii mpya haitakuwa Kolabo ya kwanza kati ya Harmonize na Dully Sykes kwani siku za nyuma walishawahi kutoa wimbo wa ‘Inde’ uliofanya vizuri kabisa.

Mimi ni Legend Kwenye Bongo fleva- Dully Sykes

Msanii mkongwe wa muziki wa Bongo fleva Dully Sykes amefunguka na kuweka wazi kuwa katika muziki wa Bongo fleva yeye ndio Legend.

Dully Sykes ameshawahi kutengeneza nyimbo kali kama Salome, Julietha, Hi na nyinginezo nyingi ambazo zilimpa umaarufu mkubwa sana kuanzia miaka ya 90 mpaka leo hii.

Kwa ajili ya uwezo wake wa kukaa kwenye gemu kwa karibia miaka 20 sasa, Dully amekuwa akiwnda kwa jina la Legendari katika muziki huu wa Bongo fleva.

Kwenye mahojiano na Sam Misago Tv, Dully amesisitiza kuwa yeye kweli ni legendary Kwenye muziki wa Bongo fleva ingawa Kwenye aina nyingine ya muziki kutakuwa na malegendari wengine:

Nisipoitwa mimi legend ataitwa legend nani? Tukija Kwenye muziki wa Bongo fleva mimi ndio legend lakini Kwenye Muziki wa dansi Gurumo na Bi. Chuka na wengine ndio malegend”.

Dully ni msanii mkongwe ambaye ameweza kukaa Kwenye gemu kwa zaidi ya miaka ishirini huku akiwa hapotei kabisa kwani amekuwa na uwezo wa kutoa nyimbo na kuhit kwa miaka kadhaa.

Dully Sykes Ataja Siri Ya Kutochuja Kwenye Muziki

Msanii mkongwe legendari wa muziki wa Bongo fleva Dully Sykes amefunguka na kutaja siri ya mafanikio yake ya kukaa kwenye muziki kwa miaka karibia ishirini bila kuchuja.

Dully amefunguka na kudai siri yake kubwa ya kukaa kwenye muziki kwa miaka yote hii bila kuchuja kwanza kabisa ni uvumilivu na pili kutoa nyimbo kutoka na mazingira na kubadilika kulingana na muda/wakati.

Kwenye mahojiano na Global Publishers, Dully amesema kuwa ili kuendelea kudumu kwenye gemu lazima uendane na mashabiki zako na kuangalia wanataka nini kwa wakati huo.

Kwanza ujue mashabiki wanataka nini na kwa wakati gani ukifanya hivyo lazima udumu kwenye gemu“.

Dully Sykes ameongelea wasanii wengi wakongwe waliopotea na wanaojaribu kurudi lakini wanakwama Lakini pia wasanii wapya ambao wameishia kuchuja mapema sana.

 

Msanii Kuwa na Baunsa ni Kulinda Status Yako:-Dully syskes

Msanii wa siku nyingi Dully Sykes amefunguka na kusema kuwa kuna umuhimu mkubwa kwa msanii kuwa na mlinzi wa kutembea nae kwa sababu kuna mambo mengi yanayotoka mitaani na kwa sababu za kiusalama ni bora kuwa na mtu wa kukusaidia kwa hilo.

Dully anasema kuwa sio kila mtu ana kuwa na nia nzuri na wewe hivyo ni lazimakuwa na mlinzi wa kutembea nae, kwa sababu hata yeye amekuwa na mlinzi kwa muda mrefu na amemsaidia sana kwa maswala ya ulinzi.

msanii kuwa na mlizni hiyo ni moja ya kulinda status yako, na pia sio kila mtu ambae unakutana nae basi  anakuwa na lengo zuri na wewe,mimi niliamua kutembea na mlinzi ili awe ananilinda  kwa sababu sio kila sehemu ni nzuri.

Wasanii wengi sana kwa sasa wameamua kuwa wanatembea na walinzi, moja wapo akiwa ni Diamond Platinum huku sababu kubwa ilikuwa ni sababu za kiulinzi.

Dully Sykes Awakingia Kifua Wasanii Wa Kileo Awaponda Wakongwe

Msanii mkongwe wa muziki wa Bongo fleva Dully Sykes ameibuka na kuwakingia kifua wasanii wa kileo wanaofanya muziki wa Bongo fleva na kuwaponda wasanii wakongwe.

Dully Sykes amewamwagia Sifa kibao wasanii wa kileo ana kudai wanaubunifu mkubwa katika kazi zao tofauti na walivyokuwa wasanii wakongwe wa Kwenye tasnia hii.

Kwenye mahojiano na Tv E msanii huyo anayetamba na ngoma yake mpya ‘Zoom’ amefunguka kudai kuwa sababu kubwa ya wasanii hao kuwachukia wenzao ni kutokana na kukosa ubunifu.

Nachukia sana wasanii wa zamani wanaoponda wasanii wa kileo, kwa sababu ukileta upendo wa wasanii wa kileo, unaweza kujenga kitu kimoja kikubwa sana. Wengi wanapotea kwa sababu wanachukia wasanii wa kileo.

Wasanii wa zamani hawanaga ubunifu, bado wanataka kuwasema wasanii wa kileo. Kiukweli mimi muziki wangu unakua kila siku kwa sababu ya wasanii wa kileo“.

Hivi karibuni alisikika msanii mkongwe wa Bongo fleva Sister P akiwaponda vibaya mno wasanii wapya na kudai wanafanya muziki  biashara lakini wao walikuwa wanafanya Muziki kazi.

Naheshimu Ndoa Kama Ninavyoheshimu Dini Yangu.;-Dully Sykes

Mwanamuzii Dully Sykes amefunguka na kusema kuwa kwa sasa hana mpango wa kufunga ndoa kwa sababu hataki kukurupuka kama wat wengine kwa sababu kitendo cha kuoa ni kuongeza mtu na kama inatokea mnagombana mkashindwa kuelewana ni kuongeza mawazo.

kwa upande wangu mimi ninaheshimu ndoa kama ninavyoheshimu dini yangu,siwezi tu nikaoa na kukurupuka kumuweka ndani mwanamke alafu baadae tunagombana , unakuwa tayari ulishamuweka moyoni unajikuta unaongeza stress tu.

Hata hivyo alipokuwa akiongea na Shadee wa Clouds e aliulizwa kuhusu swala la umri wake  kuwa unaenda na miaka hairudi nyuma hivyo anavyochelewa kuoa inakuwaje, Dully alisema kuwa kwake swala la umri sio shida kama watoto tayari anao.

najua umri una kwenda lakini tayari nina watoto kwa sababu unaweza kuwa na ndoa lakini huna watoto na pia nina shukuru sana kwa sababu watoto wangu pamoja na kwamba wote sikai nao lakini ninawapa malezi bora na kitu kikubwa nashukuru Mungu nimelelewa katika maadili ya dini sana ya kiislamu kutoka kariakoo mpaka ninapokaa sasa , nina ishi maisha tulivu kulivyo vile watu wanavyodhani.

Dully Sykes Alalamika Kutopewa Heshima Kwenye Mziki

Mwanamuziki mkongwe wa muziki wa Bongo fleva Prince Dully Sykes amemwaga povu zito na kudai kuwa hapewi heshima anayostahili katika mziki huu Bongo fleva.

Dully Sykes ni mmoja kati ya wasanii wachache walioanzisha Bongo fleva miaka hiyo ya nyuma na ukiambiwa utaje malegend wa mziki wa Bongo huwezi kumuacha Dully Sykes amekuwa kwenye gemu tangu miaka ya 90 mpaka leo hii bado anatoa nyimbo kama ‘Bombadier’ na bado anakimbiza.

Kwenye interview aliyofanya na Clouds TV Dully Sykes amesema anashangaa ni kwa nini mpaka leo bado hapewi heshima yake kama muanzilishi wa Bongo fleva ilihali watu wote wanajua wazi mchango wake ulivyo mkubwa:

Wadau pia wa muziki huu wananisahau sana kama juzi kuna sehemu niliona watu maarufu mia moja waliofanya mambo makubwa Tanzania nikaangali angalia jina langu pale lakini likawa halipo kusema ukweli nilishangaa sana wanasahau kwamba mimi ndio nilishwawishi mpaka huu mziki wa kuimba ukaingia Tanzania mimi nasahaulika sana unajua lakini najua siku nikifa watanikumbuka unajua wengine wananihofia na ndio maana hawataki kunipa nafasi unajua kwa muziki wangu mimi nilitakiwa niwe mbali sana”.

 

Dully Sykes:Ugomvi wa Alikiba na Diamond ni Biashara.

Msanii mkongwe wa muziki nchini Dully Sykes amefunguka na kuzungumzia swala la Ugomvi unaoendelea na usiotaka kuisha kila siku  kati ya Diamond na Alikiba na kusema kuwa wasanii hao wawili wamekuwa wakifanya biashara kwaio ugomvi wao hakuna aneweza kuingia au kutaka kuwaweka chini na kuwapatanisha kwa sababu kuna watu wanafanya biashara kupitia wao.

Dully amewafanisha Alikiba na Diamond kama team kubwa mbili za mpira nchini Simba na Yanga ambazo watu wamekuwa wakishabikia kwa mapenzi lakini kuna watu wanafanya biashara kupitia wao na haitaweza kupatanishwa kwa sababu watakuwa wanaua soka nchini na ndivyo ilivyo kwa Alikiba na Diamond.

Unajua sisi Tanzania tunapenda kufanya biashara , Alikiba na Diamond ni baishara ya watu kwaio sitaki kuingilia kwa sababu hiyo ni biashara ya watu. Utaingiliaje kitu ambacho ni biashara hiyo ni kama Simba na Yanga ulishawahi kuona Simba na Yanga zinapatana au kuwe na team nyingine zizidi hizo, watu wanazaliwa wanazikuta Simba na Yanga.Mimi sitaki hata kuingilia ugomvi wao ,Alikba ni mdogo wangu na Diamond ni mdogo wangu wote nawapenda na wala sioni kama kuna haja ya mimi kuingilia hapo.

Diamond na Alikiba  wamekuwa mahasimu wakubwa  kwa muda mrefu na kushindana sana huku mashabiki woa wakiwa ndio chachu ya kutokupatana kwao,hata hivyo hakuna anaetaka kuwapatanisha watu hao kwa sasa  kwa kuwa hata waliowahi kujaribu walishashindwa na kuona ni bora kuwaacha.

Kwa maoni ya watu wengi ,inasemekana kuwa wawili hao wanakuwa katika migogoro hiyo ili kuweka ushindani na kufanya biashara ya muziki wao kwa sababu hiyo ndio inaongeza mashabiki kwa pande zote mbili.Lakini pia hata wasanii hawa wenyewe wanapokuwa wakiulizwa kuhusu swala la beef lao hakuna anaetoa sababu ya msingi kwanini hawapatani zaidi ya kusema kuwa hayo ni maneno ya mashabiki katika mitandao.

Dully Sykes Amewatolea Povu na Kuwatangazia Vita Wasanii Wenzake wa Bongo Fleva

Mwanamuziki mkongwe wa Bongo fleva Dully Sykes amefunguka na kuwatolea povu wasanii wenzake wa bongo fleva na kudai kuwa wasanii hao wametumia ‘teaser’ za ngoma zake lakini hawajawahi hata kumshukuru.

Dully Sykes aliyerudi kwenye gemu na ngoma yake mpya ya ‘Bombardier’ amewatolea povu hilo wasanii hao kwenye mahohiano aliyofanya na Lilommy ambapo alifunguka yafuatayo:

Wasanii wengi siku hizi wamekuwa na roho mbaya sio wote lakini wengi wao lakini ninapoweza kutuma teaser za cover zangu nikategemea vijana ndio wanisapoti lakini wanashindwa kushoo love, wasanii wa leo wamekuwa na roho mbaya sana baadhi yao lakini maana wapo ambao wamenisapoti nasema asante ila hao wenye roho mbaya naomba niwashauri kuwa mziki unataka mapenzi tubaliane wenyewe kwa wenyewe ndio japo ni vita”.

Pia Dully aliendelea kuwafungukia wasanii hao wenye roho mbaya japo hakuwataja kwa majina:

Wasanii wengine wanakataa kuposti na kusapoti kazi zangu kwasababu wanaona kama huyu mzee anataka kutuletea vita lakini kiasi ya kwamba mimi ninachojua ni vita tu hakuna cha ukaka wala undugu na ninawaambia wanisikie sasahivi hapa vita tu tufanye kama  mnavyotaka kwa sababu mimi nilikuwa nawachukulia kama wadogo zangu alafu wao wananichukulia mimi kawaida sana yaani heshima hakuna kabisa wengine wanadiriki kusema kuwa hawajui kama nimetoa nyimbo yote hiyo mbaya, Mimi nawashauri wasanii wa kileo wapunguze roho mbaya wazidishe Upendo”.

 

Dully Sykes atoa siri yake ya muziki wake kufanya vyema

Msanii wa Bongo Dully Sykes ni mmoja wa wasanii ambao wanaendelea kufanya vizuri kwenye muziki ilhali ya wasanii wengi wenye sauti nzuri kujitokeza.

Dully Sykes ameweza kuachia nyimbo kwa miaka mingi sasa na bado nyota yake inang’aa. Akizungumza kwenye mahojiano na Bongo5 katika tamasha la Heshima ya Bongo Flava, Dully alifunguka kusema huyo kuwa yeye kuwepo katika mzuki kipindi hiki chote hicho ni kwa sababu anawaelewa wanachotaka mashabiki na pia yeye kujitambua kama msanii….alisema,

“Mimi najitunza najielewa kama msanii, kutengeneza status yako na kujitambua, wasanii wengi hawajitambui. Mimi ninajitambua na ninajua mimi ni nani,”

Mkali huyu ‘Yono’ anaendelea kutisha kupitia nyimbo zake na collabos anazozifanya na wasanii wakubwa kama Harmonize na wengine Bongo.

Tazama interview yake hapa:

Dully Sykes aeleza kwanini anaegemea upande wa Diamond badala ya Ali Kiba

Dully Sykes ameshawahi kushirikiana na Ali Kiba na Diamond kuachia nyimbo; ‘Kuteseka Nimechoka’ (na Ali Kiba) na ‘Utamu’ (na Dianond na Ommy Dimpoz).

Sykes pia amejaribu mara nyingi kuwapatanisha Diamond na Ali Kiba lakini kila mara alipojaribu juhudi zake ziliambulia patupu.

Dully Sykes na Diamond

Akiongea kwenye kipindi cha 180 Power cha Sibuka FM, Dully Sykes alifunguka na kusema kuwa anaegemea upande ya Diamond kuliko upande wa Ali Kiba.

Mwimbaji huyo alieleza kuwa upande wa Ali Kiba hawataki kuwa karibu lakini upande wa Diamond wanamuonyesha upendo

“Upande wa Alikiba hawataki kuwa karibu na mimi ila upande wa Diamond wapo karibu na mimi, sababu hao wapo karibu na mimi na wao wananionyesha upendo ndio maana nipo karibu nao na sina tatizo na Ali Kiba wala Diamond,” alisema Dully Sykes.